Tuesday, February 28, 2012

SAFARI IMESAHAULIKA, TURUDI MWANZO..

Mwanzo ni mzuri,mwanzo ndiyo kina cha urembo,kina cha uwezo wa kufikiri kabla,mwanzo ndiyo muonekano wa kitu,ikiwa katika yote kuna mabaya na mazuri,tunaporudi mwanzo ni lazima tulienda mahala,tena sijui tunaweza kuwa tulifika mbali au ni karibu,mara nyingine tunarudi mwanzo baada ya kumaliza mwisho,vyote hivi ni katika yote yakiwa matendo na fikra,tujue kama ni mabovu,mema au ni yapi hayo.Safari inapofika ni lazima kuelekea,hapa huwa inakuwa haina mbele wala nyuma,safari sio kifo mpaka tukaseme tunaelekea kaburini,pale inapotulazimu inatubidi kufanya,pale inapobidi kufanya iwe na kusudi,kwa kukusudia pia tunaweza tusisahau mpaka tukarudi mwanzo,maana ikiwa tutakusudia kutokufanya hivyo.

Yale mapya yanaweza kustaajabisha ulimwengu kwa kiasi kikubwa sana,ikiwa kwa wengine walianza mwanzo mpaka kufika mwisho bila kujua kama kuna kitu kimesahaulika,wengine hata hawakuanza lakini walisema hivi ni nini kinachohitajika?eti ili mradi ikifika zamu ya kwao wengine wasisahau,kumbe walisahau walikuwa nje ya uwanja,yanaposemeka maneno kwa kila mmoja ajue ni yake,maana ingali inasemekana itasemeka tu,sio mtoto wala mkubwa anayeweza kumsahau mzazi wake,wala hata mzazi mwenyewe kumsahau mzazi wake,maana ndiyo mwanzo wake,kule mbali tunapofikiria ni zaidi ya kurudi nyuma,maana ikiwa ni sawa na kuangua korosho kwa kuukata mti  mzima,tena tukawa na tegemeo la kupata tena korosho hiz,ikaja tushikane mashati kwa kukosa korosho kwa muda uliotakikana 

Safari yetu sio ndefu sana,ila safari tuliyotoka hakika ilikuwa madhubuti,tukisema tuifikirie safari inayokuja na kuiita kwa jina yenyewe ni ndefu tutakuwa tumeelewa ule urefu wa mwanzo,tena mwanzo ukabadilika na usiwe madhubuti tena,kwa wengine watafikiria iweje iwe safari,nini ni  ndefu,au ipi ni madhubuti naye asipojua isemekane tunazungumzia maisha,sasa kuna wengine tunawaita watafsiri wao wakalinganishwa kilicho kuwa cha habari na habari yenyewe.mwanzo ni mgumu sana na imefika bora kusemea hivyo kwani wengi tunapenda vile virahisi,safari hizi za hapa na pale angalau kusiwe na foleni,ukisikia mwanaadamu anatamani bora kuishi MBWA akiwa nchi za ughaibuni kuliko kuwa yeye TANZANIA,AFRIKA huyo ndiye MBWA HASWA,maana ameufahamu uumbwa,jinsi ulivyo katika namna yake kwa kufanya  na kutamani.

Mwanzo unaoanza ndiyo mwisho unaokuja,kwa lolote jambo tukalifikiria ndiyo hasa likawe,maana linapokuwa ndiyo mwisho wake,tena mwisho wa jambo huwa haufikiriki kama mwanzo yakuwa ya mwanzo mengi yapo tofauti na mwisho,mwishoni ndiyo kuna majibu yote na hapo ndiyo tuone,haina haja ya kusema tutaona maana mwisho ndiyo huu,tuangalie tusirudi nyuma,vingine havina maana ya kusaidiana na vyenzake hapa mwishoni,vipo vingi vitu vinavyofanyika na kuonekana mwishoni ikiwa mwanzo vilisahaulika,hapa tunahitaji kuamini,tena tuamini katika namna tunavyoweza ili kuepusha mwingiliano wa IMANI,maana imani si kitu cha mchezo,nikiwa na maana haichezwi,imani si ya kuisahau na kuirudia,Kama ilisahaulika ni lazima tujue tunarudi nyuma kuifata imani ipi,maana ya hii iliyopo kutoweza kufanya kazi.

By:          Benson G. Makaya,
Tel:       +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...