Friday, November 30, 2012

KUMBUKUMBU..

Ni miaka mitano tangu umetutoka,Tutazidi kukuombea Baba,japo haupo karibu Nasi kimwili lakini daima upo katika nafsi zetu,jina lako lieendelee na likawe jema mbinguni,kumbukumbu zako vichwani  mwetu hazitaweza kuisha kamwe katika maisha haya ya uhai,tunaomba na tutazidi kuomba kwa upendo uliotuachia.

umekuwa ni pengo kubwa kwetu,ulikuwa chuma kisichochakaa bali kuvunjika katika mipango ya mungu,nafsini tunakupenda sana,wake,watoto,wajukuu zako,wadogo na ndugu zako wakiwapo marafiki,majirani Pamoja na jamaa.

Mungu ilaze roho ya marehemu baba Col G.K Makaya,mahala pema

'AMIN'

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...