Friday, April 19, 2019

KATAA


Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika  hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofauti na vile inavyoweza kusukumika,upepo  unaweza vuma kuelekea kusini na yenyewe maisha  yakataka uelekeo wa  magharibi  itakuwa na kueleweka vile inavyoonekana uelekeo ulivyo.

Unaweza ukawa umekatalika upande wa kushoto lakini kulia ukafanya kazi na kama vile ilivyo katika viungo vya mwanadamu,wengine wakatumie  kufanya mambo yao kwa upande wa kulia na wengineo  kushoto yaani pande zote na hiyo ikawe ni kulingana na mazingira ya jinsi ulivyoweza kuumbwa.

Unapokataa jambo ni lazima ujue kipindi cha kukubali pengine muda unaolikataa jambo ndiyo muda mdogo wa kusubiri na kupata jambo lingine likiwa ni lile lililokataa  uelekeo ama ni  jipya,yule aliyekataliwa jana na sasa anang'aa ni katika maisha ya mwanadamu huwa yanatokea,

Yote sio ya kumwachia Mungu Mengine hata yeye aliyakataa akaumba Amri ili uweze kujikataa katika nafasi uliyopo pengine ikiwa na mahitaji ya mabadiliko ama vinginevyo,ingawaje yaweza kupelekea kukataliwa na jamii na watu wanao kuzunguka lakini kataa kukataliwa kwa sababu ya maono ya watu,

Wengine wakadhani umejikataa lakini ni namna ya jinsi maisha yako umeyataka yawe,unapokaa chini ona waliokataliwa wakakata kutokukatalika,maana kuna vile vingine hukataliwa kwa sababu anafanya fulani.

Muda mwingine unaweza kudhani hata ulikosea kufanya kile unachokifanya au ulikosea kuoa,ulikosea kununua mashine fulani hata pengine ulikosea kumwambia mtu fulani jambo fulani na mengine mengi.Kile kinachosukuma mwelekeo kinatagemea uwiano wako na ukikataa kwenda kulia na msukumaji anasukuma kushoto basi jua utaenda kushoto tu.

Sio kila sikio linasikia kile chema kinachoweza kupitia mdomoni baadaye,midomo mingine hukataa kutoa tafsiri sahihi ya kile kilichokipokea kwa kuchelewa kufika taarifa ama kukataa kufikisha kile kilichotafsiliwa na kukifikisha kikiwa na maana tofauti inayoweza kukatalika.

Ingawaje hata kukataliwa kuna faida zake pia usijisikie wa chini pale unaposukumwa na mkatazo,kataa wewe kabla hujakataliwa,yule ajaye kakukataa atapata sababu baada ya wewe kujua kujikataa kwa faida.

Usijisikie hali yoyote katika kukataa,kukatalika,kujikataa ama kukataliwa pengine fikiria matokeo yake kwanza na ukajua leo yangu iliyokataliwa ni Nuru yangu kesho na hata kama kesho  yako inaonekana kukataliwa kataa mawazo ya kuona kukataliwa.


No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...