Saturday, March 30, 2024

ELEWA 2

 

Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa kuelekezwa,kimfumo kumtafuta mtu kwenye kundi ni ngumu,ili kutofautisha kama kuna mwizi,malaya au mlevi ni kuangalia alipoiba aliekea wapi maana vyote vinaweza kuwa vya mtu mmoja.

Sifa mbovu inayotembea ni sawa na rungu la kichwa ukiwa usingizini, katika miliki matendo mabovu yamekuwa yakitendeka bila woga kuliko mawazo ya mazuri,anayekusifia mazuri hadharani anakusubiri utoke,yule asiyekusifia ana ubaya wake mwingine wa kuelezea.ukigeuka watakwambia hawajakuita na hata wakikuita hawana cha kukwambia.

Kuna namna ipo umefanana na wazazi wako,hata isipokuwa sura basi hasira,tabia wengi wametokea utotoni usimlaumu mtu kwa  kuwa malaya vile unavyojisikia kunywa pepsi mwingine coca,vingine vipo ndani ya damu hivyo tembo akinya sogea mbali pengine uchafu utakumwagikia alafu iabidi uelewe kufuata yako.

Kuna muda huelewi,yaani hata nilichokiandika hauelewi,tatizo lisije kwangu maana ulivyovijaza kichwani mwako vyaweza kuwa kinzani na hivi,nikawa naandika kwa kutumia wino mweupe.kuna mmoja alisema yanatoka popote bila kujua yametokea wapi,ukitaka kupaa kuwa na mahusiano ya karibu na ndege.Usipojua yanatoka wapi jaribu kuwaelewa ndege kwanza.

Watu ni zaidi ya chochote,yoyote yule umwonaye.hata sifa zangu hakuna nzuri imekuwa kwa mwengine,maana kila mtu ananjia yake mafanikio sio utu,ukitaka pesa watakutesa.unapotaka kunielewa isiwe kwa mlengo wako,mtu akitaka kukuelewa asikuelewe anavyokuelewa Ukiishi usimwambie na mwenzio baadaye atajiita kuwa mshauri.

ELEWA 1

Usidharau upendo unaoupata,sio kila kinalengwa kinalengeka,ukiona mchele umeota kwenye maji kuna ardhi chini ,haihitaji nguvu kupanda mbegu,itakuchosha mapema na utapoteza furaha yako vivo hivyo,asikwambie mtu kucheka wakati mrefu wa kununa ni nguvu tosha na ikakupa amani muda wote.

kama hakuna jibu kwanini uliingia kwenye mdomo wa mamba basi utakuwa unaishi nao,kujua kuogelea sio kuitii kiu ya maji ya kunywa,sehemu nyingine za kuogelea kuna mamba,wazee hupendelea sana swimming pool,sehemu za kuogelea ndogo ,vijana hujitupa maziwani na mabaharini na wakifika katikati hushituka na kujilaumu,na huo huwa msingi wa kubomoka.

Kuna maziwa na bahari nyingine zina ghasia sana,utaratibu mtu mmoja lakini wao huwapanga hata ishirini,mawimbi yanatoka popote kwenye mwelekeo,bora swiming pool mawimbi utayaleta wewe.wanasema saidia uendelee na safari,ni vile unatoa dhaka na mchungaji anaenda kununua shamba ili alime apate chakula cha kuuza na familia.

Elewa kwamba sio yote unayoyaona lazima uyaelewe,hata kama umeyasoma sio lazima uyaelewe,elewa wengine wa kuwaacha,kataza moyo wako kushikamana na matendo,Elewa duniani kuna watu watataka kwa lazima kufikiria tofauti ya wewe unavyofikiri ili wao kuonekana tofauti.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...