Thursday, February 16, 2012

BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!



Binadamu anapotembea anaangalia wapi..?maswali mengine bwanaa!!tuseme ni kushoto ama kulia,wale wenye uwezo huangalia kote,hatuwezi kuangalia kote bila kuwa makini,yaani utambuzi kiujumla kujielewa.
Hatuwezi kusema wote tunaangalia kote,kwani wote sio wale tunaotembea,na hii haiwezekani,ni kweli tunatembea,na ni kweli sio wote.muda wote tuseme sio haki kutendeka lakini ndio inatendeka,hakuna yule atendaye lisilotendeka na likaitwa tendo bora,matendo ni yale hasa tuyatendayo,ndiyo na yote sio mageni,sio yale ya kushoto wala kulia,ya chini yatabaki huko maana hayana haja ya kuyafikia,wengine watasema hawajawahi na kama kutenda ni kuwahi basi wote tumechelewa.

Sio yale tuliyonayo tukimaanisha tumeyatenda,hata kama tumeyatenda si yale tunayoyasema tumeyaweza,yapo yote na tuliyoyashindwa,tunapotembea sio miguu tu kwani hata akili nayo hufanya kazi kubwa mikono nayo pia ikatembee,muda mwingine tutembeze na mioyo yetu.Wengi watu hatuelewani,tumesahau kuwa hata wale wa zamani waliandika,ndiyo wale waliotembea wamefika hadi hapa,waliacha akili zao zinatembea,sasa wengine wakiangalia wanavyotembea wanapofika ni pale walipo,mahala na muda wanautaja kama ulivyo,ya kuwa wapo hapo.Kama matembezi ya maelfu yameshindikana basi hatutaweza yoyote,wataweza wachache,ni kama ilivyo shule kwani chochote kile sio cha kusoma,cha kusoma huwa wanaambiwa soma hapa,elewa pale unaposoma,jua unachokisoma sio kile unachokiona,macho hayadanganyi lakini kwa dunia jinsi inavyotembea haiangalii mwanadamu amesimama ki namna gani.

Tusherehekee vyote na tujipongeze hasa pale tunapoona tumeweza kukimbia,ikiwa ni wengi wanapenda kuwahi,labda tutembee haraka tu tusikimbie,yakuwa hatujui tunakimbilia wapi,tusije kimbilia bomu,bomu hufyatuka endapo pale kunakuwa hakuna uangalizi na yule anayekimbia uangalizi wa sehemu aliyopo ni mdogo sana,tukubari yote ya kuwa tunauwezo wa kukataa yote,kwani hata tukisema ni kutaka ufikiriavyo wewe lazima wengine watakubari huku wengine watakataa,labda tuseme haina haja ya vyote hivyo,watakao kataa na kukubari vyote kheri kwani yule anayekataa njia hii anayo nyingine,yakuwa anataka kupanua uelewa,ili asaidikike atakua ametembea.

TEMBEA UYAONE..

By: Benson G. Makaya,
Tel:  +255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Wednesday, February 15, 2012

Makaya's Forum: SAUTI KALI...

Makaya's Forum: SAUTI KALI...: Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imet...

SAUTI KALI...



Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imetimia,labda upate mawaidha,yaani utiwe moyo,unaweza kuleta usikivu na ikiwa hivyo ukakaa chini na kufikiria,lakini isiwe hadi kufika kilele,maana hapo nguvu zinapungua,uwezo wa kufikiri unatokana na nguvu pia,na hapa ikaeleweke sio wazee wanawasemea,ni vijana mkaweze kukaa na kuweza tazamia,milango usifunge,makelele yatakuzidia,ingawa ulikuwa hujui ya mwanzo yaliyokufikia,usingeliyafahamu hata kwa nguvu kupayukia,vile sauti  kuwafikia,labda ufikirie  na kwa makini kusikilizia,tunavutiana kwa namna isiyowezekana,na hii itatupelekea kukaa kimya sana,hata ukaweka utamu wa lugha kwa jinsi zinavyojulikana,haita leta msingi zaidi ya watu kupigana,ikiwa wengi wanasoma shule yale ya mtaani yamekuwa hayana maana,ingawa ni yetu ya leo na wala siyo ya jana,tumekuwa wazembe wenyewe haina haja wa zamani kuwatukana,hata ukatembea mbali kutafuta nyama,majani yatakuotea karibu na kuchafua bila hiyana,unahangaika kwa pesa na zimekuwa hazina dhamana.ikawekwe barabara iliyo jaa rami kama mkeka,faida ya nani kama siyo ya malaika?maana imekuwa ikipita siku chache na kubomoka,sijui ni raslimali au ujuzi wa kutokujali,ntaongelea machache yasiyo kuwa na hali,siyo yale ya wanaume wasio lijali,ni wazi kwa mwenye vichache apaswe kuongezewa,maana ni anavyo vichache kweli,ile ya mwenye nacho kuongezewa ni ya watu hai,wafu lao kaburi,na maombezi ndiyo nyongeza yao,nao wafike salama mahala pema mbinguni.

Mambo yanapozidi kuwa magumu ndiyo mwanzo hasa wa yale maraisi,ni kile alichonacho mwanaadamu,ingelikuwa kila mtu anazaliwa anaambiwa nenda kaendeshe baiskeli sidhani kama angetoka mtu na kusema ni rahisi,tena bila kufundishwa..kwani hata hiyo baiskeli yenyewe ingelikuwa ngumu kuitaja bila ya kuiendesha,mbadala wa matembezi yanayotoa sugu miguuni ni mapumziko ya viungo hivyo,hawakuchoka hawa wanaotengeneza baiskeli tangia mwanzo,wakarahisisha mpaka wakaweza kusafiri nazo,sio uwezo ni namna ya kuweza na kigezo,inapochakaa baiskeli makelele huanza,ukapita mikoa mbalimbali kama mbeya na mwanza,baiskeli zinapokuwa kitu cha kwanza,ni maendeleo haya kwani hakuna aliyeyakataza,barabara zikaonekane hazina maana kwani hata mijini ukawawekea bado ni mtafaruku kwa wao kupita yapitapo magari,na ikiwa ni mmoja wapo watakupigia kelele ya kuwa unaleta foleni.mambo ya mjini ni mengi,lakini mji huo huo ndiyo kijiji,sasa uchague moja kati ya kijiji au mji,maana unaona watu wanatoka morogoro wanakuja kutibiwa hospitali ya mkoa dare s salaam,wale wa dar na wenyewe wanafanya hivyo,mshangao kwa wale wanaosafiria nje magonjwa yao,kenda rudi ni maralia na baada ya hapo ni mapumziko..kule hakuna kelele tatizo hapa ni pale unapopumzikia kodi za watu huku wenyewe wakiwa hawazijui hata haki za kwenda hospitali,sauti kali huleta ugomvi kwa kutokuelewana,na baadaye ni vita.

Macho yasitoboke,masikio yameziba sasa wanaopiga kelele waendelee,maana hata ukikataa sauti zenu hazipayuki na haipiti siku,pigeni kelele wanafunzi na mwalimu akija mwambieni ni kwa sababu hakuwepo,maana hujifanya kuelewa yao mara nyingine,hata hivyo ikiwa ni namna ya kutaka kujua ni nini kifanyike mda huo.

By:Benson G.Makaya
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com


Tuesday, February 14, 2012

Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.

Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.: Makubwa ni neno linalosifia kitu,kitu yaweza kuwa ni kitendo,kifaa,mawazo,nafsi ya mwanadamu mwenyewe na mengineyo mengi yanayomzun...

MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.


Makubwa ni neno linalosifia kitu,kitu yaweza kuwa ni kitendo,kifaa,mawazo,nafsi ya mwanadamu mwenyewe na mengineyo mengi yanayomzunguka mwanadamu,likiwa leo limetajwa basi litaenda kwa maana yake,hiyo hiyo ya ukubwa,ukubwa wa kitu sio uzuri,na ubaya sio udogo pia,yote yanawezekana,ikiwa tu mlengwa amejua kitu,ameujua ukubwa unaozungumziwa.

Makubwa ni mengi ya kutosha,zaidi umilikisha ukubwa kukua.ikiwa ni katenda basi ni lazima kufikiri,iwe ni kufikiri vizuri ama vibaya,bila kujali umri maana na udogo upo hapo,yule anayetenda anafikiri kitu katika yale aliyonayo,ikiwa ni mara nyingine huwa tunasema mtu amefanya makubwa baada ya kuona mafanikio,lakini katika kipindi cha kuyaona hayo matendo makubwa kisiwepo,ikawe ni hali tu iliyokuja na kuweza kuitwa ni kubwa.tulingel bahatisha kuishi kama tungelikuwa tunayaona makubwa ya wazazi wetu,maana tungelikuwa sawa sasa,kwani ule ukubwa wao usingekuwa kama udogo wetu na tukasema enzi hizi zimeharibika sana,vijana wanatembea uchi barabarani ikiwa hawana heshima,na yule mkubwa aliyefikiria kutokea hayo anahisi mafanikio,kwani alifikiri hivyo.

Ndani ya jamii zetu binadamu wengi tupo sawa,labda niseme kwa sababu hatuna uhakika ya kuwa tuna utofauti zaidi ya ile ya kike na uume,maana akiwazacho mtu ndio huleta usawa,ikaja kutokea siku labda tutaulizwa wale wote wanaofikiria chochote watoke mbele,yule atakaye baki atakuwa lazima hajasikia,maana kama atakuwa amesikia na amezidi kubaki ni lazima atajiuliza,asipojiuliza huyo aamshwe,maana amelala,na tuangalie tusije ruhusu akakoloma zaidi kwani watoto wao wataamka zaidi,watakuwa wamezidishiwa kipimo cha dawa,na madhara yanaweza kutokea,labda yametokea tayari.

Fikra  zetu zimekuwa zikifananisha mengi sana,ikiwa yule mkubwa akafanye ya kitoto,sio lazima mkubwa kufanya makubwa lakini kila aliye na umri afanye yake yale yanayo au yaliyo endana na huo umri wake.,kama ni yalikuwa ya akiba basi ayamalizie kwani ni maisha yake,maisha,mtu inabidi aishi yeye,sio tuishi kwa sababu ya binadamu mwingine,na endapo inatokea hivyo basi awe ni mungu pekee,muda uliopo ni ule uliotengwa,labda tufahamu kwa mitihani yetu tulikuwa tunafanyaje,maana wengine walianza na maswali magumu na wengine ikawa walijibu wao wanavyojua.,tena isiwe tukachelewa katika kujibu yale tulioyaona tuna uwezo nayo,maana itafika kipindi muda ukiisha kila mwenye chake atabaki nacho,haina haja ya kubebeshana mizigo ikiwa dhambi,na tutakapo zeeka labda tuseme hilo hatukulifahamu..sijui tufahamu vipi kabla ya uzee,au ndio makubwa zaidi ya fikra.

Wengi tunafikiria mengi,wengi wakubwa tunafikiria hadhi yetu ya kuwa wakubwa,wengi watoto wakatamani kuwa wakubwa,ikiwezekana kama sisi,au wale Fulani wanofanya vitu Fulani,yanayotuletea ukubwa ndio yanayotusumbua ukubwani,ikiwa na tabia za utotoni hazikuachwa  au kutiliwa maanani wakati wa ukuaji,kwani yaeza kuwa mtu katamani kuwa mkubwa na asielewe kama pale ndio anakuwa,wakubwa tuliitwa hivyo ni kwa sababu inaeleweka tunafanya nini,mambo wayafanyayo ni kama yale ya msingi wanayofanya watoto nao wakaitwa watoto.tusiwaumize watoto kwa kuangalia mawazo ya ukubwa wetu,yanayotatuliwa ndio huwa na mwongozo,ni fikra zinazohitaji kuwa na uwezo tusije pita mahala palipo na uozo tujijali na kuyaangalia yetu matendo.

IKIWA ATAKUA MDOGO BASI UKUBWA UTAMFATIA,MWANADAMU YAANI.

By:          Benson G. Makaya,

Tel:      +255714 33 66 57.

Sunday, February 12, 2012

WATU WANAENDA MAHALA PA KUABUDIA NA HAWAJUI WANAENDA KUFANYA NINI..!


!
Ingalikuwa tumezidiana sana utofauti basi pangekuwa si mahala pale pa heshima kama inavyojulikana,tokea ilipoanza tulijua ni mahala pa kuabudia ikaja hii leo kila mtu akaelewa lake,na hii inatokana na kuwa wote tuna matatizo,tena ndiyo yanayotupelekea kufika mahala pale,ikiwa lengo sio kubishana kama ilivyoeleweka basi na wengine tuelewe tunavyoelewa,ikiwa si lazima kuelewa hivi,vile ambavyo havieleweki.mwanadamu asipokuwa anaeleweka ndiyo mwanzo wa kueleweka,kwani hata tukafikiri kuelewa ni nini tutabaki hatuelewi na wachache wakawa viongozi wa wasio elewa.

Siku ya sita ni ipi ili ya saba nikapumzika?yamebaki mabishano kwa wale wote kuonekana hawana uhakika,mawazo ni yetu ndiyo maana tunayafuata mahala yalipo,kama ni kuyatoa ni pale tulipo,hata tukasema hakuna asiye na mawazo hapo tutakuwa tunayataka,kwani yajapo mengine ya kuyafikiri hatutaelewa hasa zaidi kwa lile lililopo,inakuwa ni rahisi kumwamishia mbwa ujuzi wa binadamu bila ya mwanadamu mwenyewe kujua kama anao huo wa mbwa,kwani ingalikuwa naye mbwa anajua kusema tungaliamuliwa kila mara hata tuwakutapo majalalani,na wao wangechagua cha kula hata kugoma pale kinapokuwa hakiwapendezi,hapa nikiwa na imani kwa Yule mfugaji anao uwezo wa kula zaidi mbwa wake,na kama mbwa huyo kazidi basi jua hayo ni mawazo,tena epuka karibuni waeza kuwa mbwa.


Shetani asemi kwa sauti tukatenda,yupo kimya akisubiri tutende,si anajaribisha?maana anaweza kutumia nguvu zake bure wakati tupo katika upande wake,mahala pengine pana maana zake,maana nyengine zina mahala pake,hata ikawa hatuja maanisha kuwa mahala hapo tutaleta maana zetu,vingi vipo ili kuijaza maana,na maana hukamilika pale inapojazwa,hujazwa pale kitu kinapokuwepo,ni kama pale mahala pa kujisaidia,na hata huwa ni lugha au ni mahala penyewe,maana kama ingalikuwa ni kumfuata na kumwomba mungu kuhusu wokovu inatupasa kufahamu tumeyaacha mengi sana,tunakimbilia matokeo yetu ya yakitutokea tunasema maisha ni magumu,ni sawa na Yule aliyamua kwenda kusomea udaktari hapaswi kugoma kwani hata mhasibu anayempa huo mshahala mdogo akigoma sijui ataupata wapi.na ingalikuwa ni udaktari wake angelibaki huko akijitibu.

Tuheshimu mahala pa kazi,watu wanafanya kazi ili wale,wale wasio fanya na wasile maana hawajatoa taarifa ya kuwepo kwao mahala hapo,tusijichague kwa kwenda na kuongea maneno ya mungu,eti tukajiita tukasema tunajifahamu sisi ni watoto wa mungu,bila kujua kama  ametukubari,eti tukabisha tukisema ni mara ya kwanza,hapa tutakuwa hatuna fikra za nyuma,wale wenye mawazo wanajua nini maana ya mahala walipo.unaweza kuwa mtoto ki umri au rika lakini si vile kwa baba,hapa nazungumzia nyumba hizo..maana wamekuwa wakipiga makelele sana kuwakaribisha watu..bila wageni kujua tuangalie mlangoni wametuandikia kabisa..mgeni njoo mwenyeji apone..sasa anayeponywa sijui ni yupi hapo,lengo hapa sio kukataza,bali ni kujua la kufanya uwapo mahala husika.

By:Benson G.Makaya
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Saturday, February 11, 2012

WALIO BORA..


Ubora ni kama uzuri,uzuri ni sifa ikiwa inaelekea kuzidi ni budi kuwa nzuri sana,au bora sana ikiwa ina maana ya kudumu na thamani iliyopo,kwa hiyo ubora unaweza ukawa katika kitu chochote kile kisicholenga jinsia,aina,wala namna,ubora huwa hauulizwi ikiwa unaonekana pale unapokuwa kwa mtu au kitu husika,ikiwa mmoja anafahamu juu ya ubora wa mwingine anaweza naye huyohuyo akawa haelewi  nini juu ya ubora wake yeye mwenyewe,maana tunaweza kuona tu na tusijifunze kitu,au tukajifunza na tusielewe,maana wengi walio bora nao hujifanya ubora ule ni wao,yaani wameutengeneza wao,ingawa si ya kushangaa kama vile ilivyo kwa mtengeneza wino katika peni,naye yu bora lakini siye aliyetengeneza peni.yu bora katika wino.

Moja iliyo kuu  linalohitajika ni lile linalokuwepo ndani ya moyo wa mtu,ikiwamo nia ya kufanya na malengo yaliyothabiti,uthabiti wa kitu ndiyo ubora wake,ubora haulazimishwi na hasa pale mwanadamu anapohitaji,ubora unaendana na matendo ya mtu,watu au kitu.Vingi vilivyopo huwa vinatakiwa kufanyika tena ikiwa ni kwa ubora ule utokao ndani ya mtu mwenyewe,kwani yale yasiyo bora kwa kutokana na mawazo ya mtu hayo yanatokana na mtu mwenyewe pia,aliyoiwazia.hauwezi kuupata ubora kwa kuiga,kwani unaweza kuiga ule wa chini,

Kuna ubora mwingine wa kuonekana tu,ikiwa sifa nyingi zinatokana na ubora basi ni wazi na sifa zieleweke ya kuwa zinakuja zenyewe,hazilazimishwi,ni sawa na kuulazimisha ubora,ni sawa na kulazimisha mapendo,na tuelewe pale tunapolazimisha sio kwamba ni hali imekuwa ngumu bali tunafanya vile hasa visivyo vya muhimu kwetu,hii yote inatokana na watu halisia,nao wakidhani hata pale tulipo ni tumeenda kuonyesha ubora wetu,labda tuseme wa kushangilia maana wanacheza wengine,ingawa ni kweli lakini ubora wa mtu upo kwa mtu mwenyewe,ikiwa ni wachache tunaweza tusielewe na kwa muda mwingine tukajutia kwa yale tuliyonayo.

Ubora huja mahara popote,hata pale katika ukuaji kwani kila Yule anayekuwa atataka kuonyesha ni kwa namna gani ameweza jambo,tendo linapaswa kusifiwa na aliyetenda pia,kwani kama kuiba ni kosa basi na tujue ni haki kweli kumkamata mwizi na kumpeleka mahakamani,ikiwa anaenda kushtakiwa kwa sifa zake,’maana amekuwa bora sana katika kukwapua mali za watu’.unaweza kusema unyooshe njia ili uishi vyema katika maisha yako,ikaja na wengine wasielewe nini na wapi njia hiyo ilipo,

tutashindwa kabisa endapo tutadhania njia,kwani nazo zimewekwa zikiwa na ubora wake,na ili zionyeshe ubora ni lazima kupoteza ubora,wa mtu mwenyewe,ubora wa mpita njia hiyo kwa maana.Maisha na sehemu zake ndizo zinazofanya usiweze kuonekana bora,maisha yakiwa mazuri au mabaya,au yakawe mazuri lakini katika upande mmoja,yaani ikawe ni mtu mwenyewe anajiona bila kuonwa na ubora,ikiwa sehemu zenye ubora ni chache kuliko watu halisia,

unaweza kurekebisha visivyo bora na kuwa vile namna unavyohitaji ikiwa utajiongoza wenyewe,ukijiamini kwamba unaweza na itafika kipindi utapewa sifa bora,kwani na huwa inafika kipindi hata mwizi huacha licha ya kutamani kuiba kutokana na kwamba anataka ubora na siyo amekuwa bora,walio bora wapo kama mimi,wewe na wengine tofauti ikiwa ubora wetu nao upo tofauti.
Ubora wetu upo pale tutakapouonyesha.’

By:Benson G.Makaya,
Tel:+255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...