Wednesday, February 15, 2012
Makaya's Forum: SAUTI KALI...
Makaya's Forum: SAUTI KALI...: Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imet...
SAUTI KALI...
Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni
kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje
kihalisi imetimia,labda upate mawaidha,yaani utiwe moyo,unaweza kuleta
usikivu na ikiwa hivyo ukakaa chini na kufikiria,lakini isiwe hadi kufika
kilele,maana hapo nguvu zinapungua,uwezo wa kufikiri unatokana na nguvu pia,na
hapa ikaeleweke sio wazee wanawasemea,ni vijana mkaweze kukaa na kuweza
tazamia,milango usifunge,makelele yatakuzidia,ingawa ulikuwa hujui ya
mwanzo yaliyokufikia,usingeliyafahamu hata kwa nguvu kupayukia,vile sauti kuwafikia,labda ufikirie na kwa makini kusikilizia,tunavutiana kwa
namna isiyowezekana,na hii itatupelekea kukaa kimya sana,hata ukaweka utamu wa
lugha kwa jinsi zinavyojulikana,haita leta msingi zaidi ya watu kupigana,ikiwa
wengi wanasoma shule yale ya mtaani yamekuwa hayana maana,ingawa ni yetu ya leo
na wala siyo ya jana,tumekuwa wazembe wenyewe haina haja wa zamani
kuwatukana,hata ukatembea mbali kutafuta nyama,majani yatakuotea karibu na
kuchafua bila hiyana,unahangaika kwa pesa na zimekuwa hazina dhamana.ikawekwe
barabara iliyo jaa rami kama mkeka,faida ya nani kama siyo ya malaika?maana
imekuwa ikipita siku chache na kubomoka,sijui ni raslimali au ujuzi wa
kutokujali,ntaongelea machache yasiyo kuwa na hali,siyo yale ya wanaume wasio
lijali,ni wazi kwa mwenye vichache apaswe kuongezewa,maana ni anavyo vichache
kweli,ile ya mwenye nacho kuongezewa ni ya watu hai,wafu lao kaburi,na maombezi
ndiyo nyongeza yao,nao wafike salama mahala pema mbinguni.
Mambo yanapozidi
kuwa magumu ndiyo mwanzo hasa wa yale maraisi,ni kile alichonacho mwanaadamu,ingelikuwa kila
mtu anazaliwa anaambiwa nenda kaendeshe baiskeli sidhani kama angetoka mtu na
kusema ni rahisi,tena bila kufundishwa..kwani hata hiyo baiskeli yenyewe
ingelikuwa ngumu kuitaja bila ya kuiendesha,mbadala wa matembezi
yanayotoa sugu miguuni ni mapumziko ya viungo hivyo,hawakuchoka hawa
wanaotengeneza baiskeli tangia mwanzo,wakarahisisha mpaka wakaweza kusafiri nazo,sio
uwezo ni namna ya kuweza na kigezo,inapochakaa baiskeli makelele
huanza,ukapita mikoa mbalimbali kama mbeya na mwanza,baiskeli zinapokuwa kitu
cha kwanza,ni maendeleo haya kwani hakuna aliyeyakataza,barabara zikaonekane
hazina maana kwani hata mijini ukawawekea bado ni mtafaruku kwa wao kupita
yapitapo magari,na ikiwa ni mmoja wapo watakupigia kelele ya kuwa unaleta
foleni.mambo ya mjini ni mengi,lakini mji huo huo ndiyo kijiji,sasa uchague
moja kati ya kijiji au mji,maana unaona watu wanatoka morogoro wanakuja
kutibiwa hospitali ya mkoa dare s salaam,wale wa dar na wenyewe wanafanya hivyo,mshangao
kwa wale wanaosafiria nje magonjwa yao,kenda rudi ni maralia na baada ya hapo
ni mapumziko..kule hakuna kelele tatizo
hapa ni pale unapopumzikia kodi za watu huku wenyewe wakiwa hawazijui hata
haki za kwenda hospitali,sauti kali huleta ugomvi kwa kutokuelewana,na baadaye
ni vita.
Macho yasitoboke,masikio yameziba sasa wanaopiga kelele
waendelee,maana hata ukikataa sauti zenu hazipayuki na haipiti siku,pigeni
kelele wanafunzi na mwalimu akija mwambieni ni kwa sababu hakuwepo,maana
hujifanya kuelewa yao mara nyingine,hata hivyo ikiwa ni namna ya kutaka kujua
ni nini kifanyike mda huo.
By:Benson G.Makaya
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com
Tuesday, February 14, 2012
Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.
Makaya's Forum: MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.: Makubwa ni neno linalosifia kitu,kitu yaweza kuwa ni kitendo,kifaa,mawazo,nafsi ya mwanadamu mwenyewe na mengineyo mengi yanayomzun...
MAKUBWA ZAIDI YA FIKRA.
Makubwa ni neno linalosifia kitu,kitu yaweza kuwa
ni kitendo,kifaa,mawazo,nafsi ya mwanadamu mwenyewe na mengineyo mengi
yanayomzunguka mwanadamu,likiwa leo limetajwa basi litaenda kwa maana yake,hiyo
hiyo ya ukubwa,ukubwa wa kitu sio uzuri,na ubaya sio udogo pia,yote
yanawezekana,ikiwa tu mlengwa amejua kitu,ameujua ukubwa unaozungumziwa.
Makubwa ni mengi ya kutosha,zaidi umilikisha ukubwa
kukua.ikiwa ni katenda basi ni lazima kufikiri,iwe ni kufikiri vizuri ama
vibaya,bila kujali umri maana na udogo upo hapo,yule anayetenda anafikiri kitu
katika yale aliyonayo,ikiwa ni mara nyingine huwa tunasema mtu amefanya makubwa
baada ya kuona mafanikio,lakini katika kipindi cha kuyaona hayo matendo makubwa
kisiwepo,ikawe ni hali tu iliyokuja na kuweza kuitwa ni kubwa.tulingel bahatisha
kuishi kama tungelikuwa tunayaona makubwa ya wazazi wetu,maana tungelikuwa sawa
sasa,kwani ule ukubwa wao usingekuwa kama udogo wetu na tukasema enzi hizi
zimeharibika sana,vijana wanatembea uchi barabarani ikiwa hawana heshima,na
yule mkubwa aliyefikiria kutokea hayo anahisi mafanikio,kwani alifikiri hivyo.
Ndani ya jamii zetu binadamu wengi tupo sawa,labda
niseme kwa sababu hatuna uhakika ya kuwa tuna utofauti zaidi ya ile ya kike na
uume,maana akiwazacho mtu ndio huleta usawa,ikaja kutokea siku labda tutaulizwa
wale wote wanaofikiria chochote watoke mbele,yule atakaye baki atakuwa lazima
hajasikia,maana kama atakuwa amesikia na amezidi kubaki ni lazima
atajiuliza,asipojiuliza huyo aamshwe,maana amelala,na tuangalie tusije ruhusu
akakoloma zaidi kwani watoto wao wataamka zaidi,watakuwa wamezidishiwa kipimo
cha dawa,na madhara yanaweza kutokea,labda yametokea tayari.
Fikra zetu
zimekuwa zikifananisha mengi sana,ikiwa yule mkubwa akafanye ya kitoto,sio
lazima mkubwa kufanya makubwa lakini kila aliye na umri afanye yake yale yanayo
au yaliyo endana na huo umri wake.,kama ni yalikuwa ya akiba basi ayamalizie
kwani ni maisha yake,maisha,mtu inabidi aishi yeye,sio tuishi kwa sababu ya
binadamu mwingine,na endapo inatokea hivyo basi awe ni mungu pekee,muda uliopo
ni ule uliotengwa,labda tufahamu kwa mitihani yetu tulikuwa tunafanyaje,maana
wengine walianza na maswali magumu na wengine ikawa walijibu wao
wanavyojua.,tena isiwe tukachelewa katika kujibu yale tulioyaona tuna uwezo
nayo,maana itafika kipindi muda ukiisha kila mwenye chake atabaki nacho,haina
haja ya kubebeshana mizigo ikiwa dhambi,na tutakapo zeeka labda tuseme hilo
hatukulifahamu..sijui tufahamu vipi kabla ya uzee,au ndio makubwa zaidi ya
fikra.
Wengi tunafikiria mengi,wengi wakubwa tunafikiria
hadhi yetu ya kuwa wakubwa,wengi watoto wakatamani kuwa wakubwa,ikiwezekana
kama sisi,au wale Fulani wanofanya vitu Fulani,yanayotuletea ukubwa ndio
yanayotusumbua ukubwani,ikiwa na tabia za utotoni hazikuachwa au kutiliwa maanani wakati wa ukuaji,kwani
yaeza kuwa mtu katamani kuwa mkubwa na asielewe kama pale ndio anakuwa,wakubwa
tuliitwa hivyo ni kwa sababu inaeleweka tunafanya nini,mambo wayafanyayo ni
kama yale ya msingi wanayofanya watoto nao wakaitwa watoto.tusiwaumize watoto
kwa kuangalia mawazo ya ukubwa wetu,yanayotatuliwa ndio huwa na mwongozo,ni
fikra zinazohitaji kuwa na uwezo tusije pita mahala palipo na uozo tujijali na
kuyaangalia yetu matendo.
IKIWA ATAKUA MDOGO BASI UKUBWA UTAMFATIA,MWANADAMU
YAANI.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255714
33 66 57.
Sunday, February 12, 2012
WATU WANAENDA MAHALA PA KUABUDIA NA HAWAJUI WANAENDA KUFANYA NINI..!
!
Ingalikuwa tumezidiana sana utofauti basi pangekuwa si
mahala pale pa heshima kama inavyojulikana,tokea ilipoanza tulijua ni mahala pa
kuabudia ikaja hii leo kila mtu akaelewa lake,na hii inatokana na kuwa wote
tuna matatizo,tena ndiyo yanayotupelekea kufika mahala pale,ikiwa lengo sio
kubishana kama ilivyoeleweka basi na wengine tuelewe tunavyoelewa,ikiwa si
lazima kuelewa hivi,vile ambavyo havieleweki.mwanadamu asipokuwa anaeleweka
ndiyo mwanzo wa kueleweka,kwani hata tukafikiri kuelewa ni nini tutabaki
hatuelewi na wachache wakawa viongozi wa wasio elewa.
Siku ya sita ni ipi ili ya saba nikapumzika?yamebaki
mabishano kwa wale wote kuonekana hawana uhakika,mawazo ni yetu ndiyo maana
tunayafuata mahala yalipo,kama ni kuyatoa ni pale tulipo,hata tukasema hakuna
asiye na mawazo hapo tutakuwa tunayataka,kwani yajapo mengine ya kuyafikiri
hatutaelewa hasa zaidi kwa lile lililopo,inakuwa ni rahisi kumwamishia mbwa
ujuzi wa binadamu bila ya mwanadamu mwenyewe kujua kama anao huo wa mbwa,kwani
ingalikuwa naye mbwa anajua kusema tungaliamuliwa kila mara hata tuwakutapo
majalalani,na wao wangechagua cha kula hata kugoma pale kinapokuwa
hakiwapendezi,hapa nikiwa na imani kwa Yule mfugaji anao uwezo wa kula zaidi
mbwa wake,na kama mbwa huyo kazidi basi jua hayo ni mawazo,tena epuka karibuni
waeza kuwa mbwa.
10 Ways to Make Chores Fun
for Kids
http://www.findananny.net/blog/10-ways-to-make-chores-fun-for-kids/
http://www.findananny.net/blog/10-ways-to-make-chores-fun-for-kids/
Shetani asemi kwa sauti tukatenda,yupo kimya akisubiri tutende,si
anajaribisha?maana anaweza kutumia nguvu zake bure wakati tupo katika upande
wake,mahala pengine pana maana zake,maana nyengine zina mahala pake,hata ikawa
hatuja maanisha kuwa mahala hapo tutaleta maana zetu,vingi vipo ili kuijaza
maana,na maana hukamilika pale inapojazwa,hujazwa pale kitu kinapokuwepo,ni
kama pale mahala pa kujisaidia,na hata huwa ni lugha au ni mahala penyewe,maana
kama ingalikuwa ni kumfuata na kumwomba mungu kuhusu wokovu inatupasa kufahamu
tumeyaacha mengi sana,tunakimbilia matokeo yetu ya yakitutokea tunasema maisha
ni magumu,ni sawa na Yule aliyamua kwenda kusomea udaktari hapaswi kugoma kwani
hata mhasibu anayempa huo mshahala mdogo akigoma sijui ataupata wapi.na
ingalikuwa ni udaktari wake angelibaki huko akijitibu.
Tuheshimu mahala pa kazi,watu wanafanya kazi ili wale,wale
wasio fanya na wasile maana hawajatoa taarifa ya kuwepo kwao mahala
hapo,tusijichague kwa kwenda na kuongea maneno ya mungu,eti tukajiita tukasema
tunajifahamu sisi ni watoto wa mungu,bila kujua kama ametukubari,eti tukabisha tukisema ni mara ya
kwanza,hapa tutakuwa hatuna fikra za nyuma,wale wenye mawazo wanajua nini maana
ya mahala walipo.unaweza kuwa mtoto ki umri au rika lakini si vile kwa
baba,hapa nazungumzia nyumba hizo..maana wamekuwa wakipiga makelele sana kuwakaribisha
watu..bila wageni kujua tuangalie mlangoni wametuandikia kabisa..mgeni njoo
mwenyeji apone..sasa anayeponywa sijui ni yupi hapo,lengo hapa sio
kukataza,bali ni kujua la kufanya uwapo mahala husika.
By:Benson G.Makaya
Email:bensonsmakaya@gmail.com
Saturday, February 11, 2012
WALIO BORA..
Ubora ni kama uzuri,uzuri ni sifa ikiwa inaelekea kuzidi
ni budi kuwa nzuri sana,au bora sana ikiwa ina maana ya kudumu na thamani
iliyopo,kwa hiyo ubora unaweza ukawa katika kitu chochote kile kisicholenga
jinsia,aina,wala namna,ubora huwa hauulizwi ikiwa unaonekana pale unapokuwa kwa
mtu au kitu husika,ikiwa mmoja anafahamu juu ya ubora wa mwingine anaweza naye
huyohuyo akawa haelewi nini juu ya ubora
wake yeye mwenyewe,maana tunaweza kuona tu na tusijifunze kitu,au tukajifunza
na tusielewe,maana wengi walio bora nao hujifanya ubora ule ni wao,yaani
wameutengeneza wao,ingawa si ya kushangaa kama vile ilivyo kwa mtengeneza wino
katika peni,naye yu bora lakini siye aliyetengeneza peni.yu bora katika wino.
Moja iliyo kuu linalohitajika ni lile linalokuwepo ndani ya
moyo wa mtu,ikiwamo nia ya kufanya na malengo yaliyothabiti,uthabiti wa kitu
ndiyo ubora wake,ubora haulazimishwi na hasa pale mwanadamu anapohitaji,ubora unaendana
na matendo ya mtu,watu au kitu.Vingi vilivyopo huwa vinatakiwa kufanyika tena
ikiwa ni kwa ubora ule utokao ndani ya mtu mwenyewe,kwani yale yasiyo bora kwa
kutokana na mawazo ya mtu hayo yanatokana na mtu mwenyewe pia,aliyoiwazia.hauwezi
kuupata ubora kwa kuiga,kwani unaweza kuiga ule wa chini,
Kuna ubora mwingine
wa kuonekana tu,ikiwa sifa nyingi zinatokana na ubora basi ni wazi na sifa
zieleweke ya kuwa zinakuja zenyewe,hazilazimishwi,ni sawa na kuulazimisha
ubora,ni sawa na kulazimisha mapendo,na tuelewe pale tunapolazimisha sio kwamba
ni hali imekuwa ngumu bali tunafanya vile hasa visivyo vya muhimu kwetu,hii
yote inatokana na watu halisia,nao wakidhani hata pale tulipo ni tumeenda
kuonyesha ubora wetu,labda tuseme wa kushangilia maana wanacheza wengine,ingawa
ni kweli lakini ubora wa mtu upo kwa mtu mwenyewe,ikiwa ni wachache tunaweza
tusielewe na kwa muda mwingine tukajutia kwa yale tuliyonayo.
Ubora huja mahara popote,hata pale katika ukuaji kwani
kila Yule anayekuwa atataka kuonyesha ni kwa namna gani ameweza jambo,tendo
linapaswa kusifiwa na aliyetenda pia,kwani kama kuiba ni kosa basi na tujue ni
haki kweli kumkamata mwizi na kumpeleka mahakamani,ikiwa anaenda kushtakiwa kwa
sifa zake,’maana amekuwa bora sana katika kukwapua mali za watu’.unaweza
kusema unyooshe njia ili uishi vyema katika maisha yako,ikaja na wengine
wasielewe nini na wapi njia hiyo ilipo,
tutashindwa kabisa endapo tutadhania
njia,kwani nazo zimewekwa zikiwa na ubora wake,na ili zionyeshe ubora ni lazima
kupoteza ubora,wa mtu mwenyewe,ubora wa mpita njia hiyo kwa maana.Maisha na
sehemu zake ndizo zinazofanya usiweze kuonekana bora,maisha yakiwa mazuri au
mabaya,au yakawe mazuri lakini katika upande mmoja,yaani ikawe ni mtu mwenyewe
anajiona bila kuonwa na ubora,ikiwa sehemu zenye ubora ni chache kuliko watu
halisia,
unaweza kurekebisha visivyo bora na kuwa vile namna unavyohitaji
ikiwa utajiongoza wenyewe,ukijiamini kwamba unaweza na itafika kipindi utapewa sifa bora,kwani na huwa inafika kipindi hata mwizi huacha licha ya
kutamani kuiba kutokana na kwamba anataka ubora na siyo amekuwa bora,walio bora
wapo kama mimi,wewe na wengine tofauti ikiwa ubora wetu nao upo tofauti.
‘Ubora wetu upo pale
tutakapouonyesha.’
By:Benson
G.Makaya,
Tel:+255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
Friday, February 10, 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...