Saturday, February 18, 2012
Makaya's Forum: MACHO YANAONA SAHIHI..
Makaya's Forum: MACHO YANAONA SAHIHI..: Ni wazi macho hutumika kwa kuangalia,kuona,kutazama yote yakiwa kama ni matendo yake,na hii yote inatokana na namna tofauti ambazo zim...
MACHO YANAONA SAHIHI.
Ni wazi macho hutumika kwa kuangalia,kuona,kutazama yote
yakiwa kama ni matendo yake,na hii yote inatokana na namna tofauti ambazo zimefikirika,na
hata ukazifikia.macho ni moja kati ya viungo vya mwanadamu,NI macho!!
Pale mtu anapofahamu inapoelekea yeye mwenyewe katika
nafsi yake kuwa na utambuzi na wakati mwingine unaweza usiwe wa kiujumla mtu wa
kujielewa,unapoelekea ni mbali zaidi ya ulipotoka,ni kama pale umefika
mahala na kusahau yote uliyokuwa ukilalama nayo kwa mara ya mwanzo,yakiwa yale yamegeuka kuwa mazuri,na uzuri
wake haujaja tu baada ya kuacha kulalama,bali ni pale uliposifia vizuri,maana unaweza kushukuru mungu kwa kufika bila kujua mahala unapoelekea,ulipo.tumshukuru
mungu,tena kwa njia nyingine hazina waelekezaji…inahitaji nguvu kweli na
uvumilivu ili kujua pia kuelekeza,si watakuja na wengine,wao ndiyo wakiwa
hawajui kitu kabisaa,watatulilia pamoja na hata ukiwakataa utakuwa umezikataa nafsi zetu,maana ikiwa unakubari mifano hai isiyoonekana
,uangalie yasije timamu yasiyowezekana,yatatusumbua tu ingawa yanaonekana yasiyokuwa
na ufahamu,tena hata kuwa na ubishi,wakiamini wao ndiyo wameishi,au tuone labda
kama utasahau hata majina yetu maana ingali wote tungeitwa “SALUMU” ingelikuwa
haina haja ya kuhukumu,labda ubaki ukituhumu ingawaje wanaonekana lakini
ushaidi hautadumu,wanapoteza wao ili ieleweke wanayoitaka,maana ndiyo chaguzi
pekee litakalo baki.na hii pekee usizani kwamba ni ya kwao tu hata kwako
pia,yaani yangu ndiyo itabaki.maana kila mtu ataona ya kwake.
Yaliyopo yametoka mahala,yaliyopo sijui yametoka wapi,kwani
nasema hivyo ya kuwa siyo yote mwanadamu akayafahamu,mengine yapo katika miliki
na uwezo wa watu wengine,na endapo ukikubariana na hili basi lazima ujue kwamba
lile au yale uliyoyashindwa ndiyo yetu,maana yangelikuwa si yetu usingeyafanya,au useme kweli sio yetu basi uangalie mara ya pili,maana wakati unavyosema si
vile unavyomaanisha,ikiwezekana ujue wakati ni mwanadamu mwenyewe,kama kijana
wa kiume akaota ndevu na asinyoe huo utakuwa ni wakati wake,amemaanika hivyo.na
hata ikawe siyo mara ya pili ila ni tendo lililoonekana,maana kama tendo
linaloeleweka ni litatimia kwa kitendo ni lazima ujue chanzo,ili yakija mafuriko usilalame,maana ulijua
yatakuja na kutuzomba,tena kwa walio mbali wafahamu..MAFURIKO!!.shida za
kuonekana hazipaswi kumwinua na kumtuma
mwanadamu,anayeona na kutenda katika utatuzi ni mwana adamu mwenyewe,isifike
kipindi ukalazimishwa kuishi,tena ikawe ni amri kwamba sasa ni “LAZIMA” ,ingawa usipoitumia lugha hii katika mambo yetu utashika mitutu,watoto wataona baba
zao wanachokifanya na kwa sababu wao wamekuja kujifunza,wamekuja kukua,wamekuja
ili wawe wakaitwe watu wazima na wakajue,watashika mitutu yenye technolojia ya
kizazi chao,hapo vita itakuwa haina heshima..watoto wataonekana wakubwa,na kwa
wakubwa labda uwasikilizie,ingawa wanasema vita haina baba.
Tunapoelekea hakutazamwi mtu ukaambiwa ona,sio kwa
macho.unapoelekea ni mbali lakini si kama kule ukasema ulipotoka,kwani
wengine watasema ni karibu kutokana na maisha yao kiujumla,unapoelekea ndiyo
kwa mungu.tunapokaribishana majumbani mwetu tunategemea HODI,kama kuna mgeni
ataingia bila hodi huyo atakuwa mwenyeji sema ni sababu ya mgeni aliyetangulia
hakumkuta mara ya kwanza.
UKITAKA KUJUA NI LAZIMA KUJUA UMEJUAJE?
By: Benson
G.Makaya,
Tel: +255714 33
66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
Friday, February 17, 2012
Makaya's Forum: USHINDI…UNAHITAJI KUJIANDAA.
Makaya's Forum: USHINDI…UNAHITAJI KUJIANDAA.: Maandalizi ni malengo katika kutekeleza yale yanayotaka kufanyika,ikiwa katika mmoja mmoja hadi pale ikafikia kundi,hii yote hutokana ikiw...
USHINDI UNAHITAJI KUJIANDAA.
useme ni wangapi wanaojiandaa,na utakuta ni wote maana kila mtu ajiandaaye hujiandaa mwenyewe,yule anayeandaliwa ni lazima ajue kuandaa pia kwani endapo akishinda hataweza kuulinda ushindi ya kuwa hana maandalizi useme wale wanaoamka ndio wa kuweza kujiandaa kwani walikuwa wamelala,na wale walio lala ni kuwaamsha ili waweze kujiandaa ikiwa ushindi mtu anaupata pale hasa alipojiandaa mwenyewe,maana unaweza kuja kidogo ama ukazidi na kufanya karaha,kivingine ikawe ni ile bahati maana haukuwa wa maandalizi yale,ushindi wa bila kuongea unaweza usisikike,na mara nyingine ukiongea sana wanaweza kunyamazisha,maana wao hawamjui mungu na labda nisiseme hivyo zaidi iwe wanamjua mungu wao.pale unapokosa ndio pale majibu yalipo,ni kama pale unapopata ingawa haitaweza kulingana,ni tofauti ya kuwa moja ni ushindi nyingine ni kinyume yake.
Kile kinachoweza kuzuilika ni kile kisichopangika,maana kitakaaje?kama maji hupita kokote,hata yakaleta uharibu hata ikawe sio lengo kubomoa,pale yanapobomoa yenyewe ushinda ikiwa yalipotoka yalikuja na yakabomoa,labda yangeenda pengine ili ungejua kuwa haikuwa lengo,na iweje yangefanikiwa ungeeiita ni bahati yake,kwa yule anayejenga ukuta kwa ajili ya kuzuia maji hayo anajiandaa,kwa yule anayeyasubili yaingie mpaka ndani basi atafanikiwa,maana amesubiri hivyo,muda mwingine huwa inakuwa haiwezekani,ikiwa katika hali ya kawaida hasa mtanzania ikiwa wengi hatufahamu mazingira yetu,ikiwa ni miili pekee tunayoifahamu,tukisahau mazingira mengine tukataka afya bora,hii itakuja kwa kunenepa ikiwa ni bora basi itakuwa bahati,siwezi kusema sana hapa labda tungeulizana nani au na flani wanapenda nini,maana utofauti upo,na matokeo sio maandalizi,ikiwa yenyewe yakawe na kusudio la kuleta ushindi.
Vizuizi ni haki kuviweka pale unapojiandaa.lakini ni pale tu utakapo jua ni unazuia nini,Katika utofauti wa malengo tuseme yawe yanayofaa yote,yakitofautiana kwa mabaya na mazuri kwani tunaweza kuchanganyana kwa muda mbadala,endapo yale yasiyokuwa ni malengo kufanyika kama malengo wakati Fulani,yule anayejiandaa ndiye anayejua lengo hasa,labda na ije tofauti..hapo tunasema anapanga mungu.
mda mwingine lawama hazifai labda ujue nini unachokifanya,maana kama ni unajiandaa na imetoka kipindi maandalizi yakawa magumu unaweza kuyakimbia endapo haujafahamu unajiandaa na nini,
'tutaishia
kunawa maji ikiwa na chakula tumekiona mbele yetu'.
kwani hata meza zenyewe waligeuza kitambo!!
By:
Benson G, Makaya,
Tel:
+255 714 33 66 57.
email.
bensonsmakaya@gmail.com
Thursday, February 16, 2012
Makaya's Forum: BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!
Makaya's Forum: BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!: Binadamu anapotembea anaangalia wapi..?maswali mengine bwanaa!!tuseme ni kushoto ama kulia,wale wenye uwezo huangalia kote,hatuwezi kuan...
BINADAMU ANAPOTEMBEA..!!
Binadamu anapotembea anaangalia wapi..?maswali
mengine bwanaa!!tuseme ni kushoto ama kulia,wale wenye uwezo huangalia
kote,hatuwezi kuangalia kote bila kuwa
makini,yaani utambuzi kiujumla
kujielewa.
Hatuwezi kusema wote tunaangalia kote,kwani wote
sio wale tunaotembea,na hii haiwezekani,ni kweli tunatembea,na ni kweli sio
wote.muda wote tuseme sio haki kutendeka lakini ndio inatendeka,hakuna yule
atendaye lisilotendeka na likaitwa tendo
bora,matendo ni yale hasa tuyatendayo,ndiyo na yote sio mageni,sio yale ya
kushoto wala kulia,ya chini yatabaki huko maana hayana haja ya
kuyafikia,wengine watasema hawajawahi na kama kutenda ni kuwahi basi wote tumechelewa.
Sio yale tuliyonayo tukimaanisha tumeyatenda,hata
kama tumeyatenda si yale tunayoyasema tumeyaweza,yapo yote na
tuliyoyashindwa,tunapotembea sio miguu tu kwani hata akili nayo hufanya kazi
kubwa mikono nayo pia ikatembee,muda mwingine tutembeze na mioyo yetu.Wengi
watu hatuelewani,tumesahau kuwa hata wale wa zamani waliandika,ndiyo wale
waliotembea wamefika hadi hapa,waliacha akili zao zinatembea,sasa wengine wakiangalia
wanavyotembea wanapofika ni pale walipo,mahala na muda wanautaja kama ulivyo,ya
kuwa wapo hapo.Kama matembezi ya maelfu yameshindikana basi hatutaweza
yoyote,wataweza wachache,ni kama ilivyo shule kwani chochote kile sio cha
kusoma,cha kusoma huwa wanaambiwa soma hapa,elewa
pale unaposoma,jua unachokisoma sio kile unachokiona,macho hayadanganyi lakini
kwa dunia jinsi inavyotembea haiangalii mwanadamu amesimama ki namna gani.
Tusherehekee vyote na tujipongeze hasa pale
tunapoona tumeweza kukimbia,ikiwa ni wengi wanapenda kuwahi,labda tutembee
haraka tu tusikimbie,yakuwa hatujui tunakimbilia
wapi,tusije kimbilia bomu,bomu hufyatuka endapo pale kunakuwa hakuna
uangalizi na yule anayekimbia uangalizi wa sehemu aliyopo ni mdogo
sana,tukubari yote ya kuwa tunauwezo wa kukataa yote,kwani hata tukisema ni
kutaka ufikiriavyo wewe lazima wengine watakubari huku wengine watakataa,labda
tuseme haina haja ya vyote hivyo,watakao kataa na kukubari vyote kheri kwani
yule anayekataa njia hii anayo nyingine,yakuwa
anataka kupanua uelewa,ili asaidikike atakua ametembea.
TEMBEA UYAONE..
By: Benson G. Makaya,
Tel:
+255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com
Wednesday, February 15, 2012
Makaya's Forum: SAUTI KALI...
Makaya's Forum: SAUTI KALI...: Sauti zimezidi kuwa kubwa,zimejaa na chumba ni kidogo,ikabaki ikawa na sasa imekuwa ni mtafaruku,sio mda wake huu,ingawaje kihalisi imet...
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...