Ni wazi macho hutumika kwa kuangalia,kuona,kutazama yote
yakiwa kama ni matendo yake,na hii yote inatokana na namna tofauti ambazo zimefikirika,na
hata ukazifikia.macho ni moja kati ya viungo vya mwanadamu,NI macho!!
Pale mtu anapofahamu inapoelekea yeye mwenyewe katika
nafsi yake kuwa na utambuzi na wakati mwingine unaweza usiwe wa kiujumla mtu wa
kujielewa,unapoelekea ni mbali zaidi ya ulipotoka,ni kama pale umefika
mahala na kusahau yote uliyokuwa ukilalama nayo kwa mara ya mwanzo,yakiwa yale yamegeuka kuwa mazuri,na uzuri
wake haujaja tu baada ya kuacha kulalama,bali ni pale uliposifia vizuri,maana unaweza kushukuru mungu kwa kufika bila kujua mahala unapoelekea,ulipo.tumshukuru
mungu,tena kwa njia nyingine hazina waelekezaji…inahitaji nguvu kweli na
uvumilivu ili kujua pia kuelekeza,si watakuja na wengine,wao ndiyo wakiwa
hawajui kitu kabisaa,watatulilia pamoja na hata ukiwakataa utakuwa umezikataa nafsi zetu,maana ikiwa unakubari mifano hai isiyoonekana
,uangalie yasije timamu yasiyowezekana,yatatusumbua tu ingawa yanaonekana yasiyokuwa
na ufahamu,tena hata kuwa na ubishi,wakiamini wao ndiyo wameishi,au tuone labda
kama utasahau hata majina yetu maana ingali wote tungeitwa “SALUMU” ingelikuwa
haina haja ya kuhukumu,labda ubaki ukituhumu ingawaje wanaonekana lakini
ushaidi hautadumu,wanapoteza wao ili ieleweke wanayoitaka,maana ndiyo chaguzi
pekee litakalo baki.na hii pekee usizani kwamba ni ya kwao tu hata kwako
pia,yaani yangu ndiyo itabaki.maana kila mtu ataona ya kwake.
Yaliyopo yametoka mahala,yaliyopo sijui yametoka wapi,kwani
nasema hivyo ya kuwa siyo yote mwanadamu akayafahamu,mengine yapo katika miliki
na uwezo wa watu wengine,na endapo ukikubariana na hili basi lazima ujue kwamba
lile au yale uliyoyashindwa ndiyo yetu,maana yangelikuwa si yetu usingeyafanya,au useme kweli sio yetu basi uangalie mara ya pili,maana wakati unavyosema si
vile unavyomaanisha,ikiwezekana ujue wakati ni mwanadamu mwenyewe,kama kijana
wa kiume akaota ndevu na asinyoe huo utakuwa ni wakati wake,amemaanika hivyo.na
hata ikawe siyo mara ya pili ila ni tendo lililoonekana,maana kama tendo
linaloeleweka ni litatimia kwa kitendo ni lazima ujue chanzo,ili yakija mafuriko usilalame,maana ulijua
yatakuja na kutuzomba,tena kwa walio mbali wafahamu..MAFURIKO!!.shida za
kuonekana hazipaswi kumwinua na kumtuma
mwanadamu,anayeona na kutenda katika utatuzi ni mwana adamu mwenyewe,isifike
kipindi ukalazimishwa kuishi,tena ikawe ni amri kwamba sasa ni “LAZIMA” ,ingawa usipoitumia lugha hii katika mambo yetu utashika mitutu,watoto wataona baba
zao wanachokifanya na kwa sababu wao wamekuja kujifunza,wamekuja kukua,wamekuja
ili wawe wakaitwe watu wazima na wakajue,watashika mitutu yenye technolojia ya
kizazi chao,hapo vita itakuwa haina heshima..watoto wataonekana wakubwa,na kwa
wakubwa labda uwasikilizie,ingawa wanasema vita haina baba.
Tunapoelekea hakutazamwi mtu ukaambiwa ona,sio kwa
macho.unapoelekea ni mbali lakini si kama kule ukasema ulipotoka,kwani
wengine watasema ni karibu kutokana na maisha yao kiujumla,unapoelekea ndiyo
kwa mungu.tunapokaribishana majumbani mwetu tunategemea HODI,kama kuna mgeni
ataingia bila hodi huyo atakuwa mwenyeji sema ni sababu ya mgeni aliyetangulia
hakumkuta mara ya kwanza.
UKITAKA KUJUA NI LAZIMA KUJUA UMEJUAJE?
By: Benson
G.Makaya,
Tel: +255714 33
66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
No comments:
Post a Comment