B inadamu,tunajua zaidi ya anaye jua’binadamu,tunabisha yale
tusiyoyajua,tunayasemea yale tusiyoyajua,tunajifanya tunajua yale
tusiyoyajua,mwanzo huu ni mbaya sana,mwanzo huu ni mrefu sana,maana tusipojali
muda hata nafasi zitachukulika,pengine tukasingizia kila kitu kina
sababu,huku ikiwa hata hizo sababu hatuzijui,tusibishe yakuwa tunayajua,kaa
kimya mengine ni kwa Yule asiyeyajua,sio wewe hata mimi sijayajua,ni mengi sana
yaliyopo chini ya hilo jua,kama mwenyezi mungu asingeyajua,kuona mapambo na ua tusingetambua,akili ya mkubwa
ni vigumu kwa mdogo kuijua,akili ya mkubwa ni nyepesi mdogo kuijua,akili ya
anayejua ni rahisi kwa anayejua,maana hata tukaandika upumbavu
tusioujua,pengine itakuwa ni chaguzi kati ya kama mvua na jua,machache
tunayasema bila ya kuyatambua,pengine ni hekima kwa nyani kula mabua,yataenda
wapi viwanda vilituumbua,wachache wakali wamekuja kuviibua,
Mwacheni mnyonge aje na mvua,maana wababe wamekaa na kuotea
jua,litakuja joto tutasema moto,tukikosea kusema kuwa kama watoto,simaanishi
hivyo mengine ni yangu wala sio ndoto,tunafundisha sana mashairi kama mrisho
mpoto,na tutaimba sana bila mtoko,ijazane dunia pasipo viroboto,iwepo dunia
palipo na watoto,nay a wakubwa yakabaki huko,mbali sana haina haja ya
kuitana,si karibu sana kwa vile mmoja kufikiria,ukubwa ndiyo ubinaadamu maana
tumekosa kwa mengi yaliyona uzuri na hata yasiyo na uzuri ndani yake,hapo
tukapoteza mitoko,hapo tukakamatwa na joto,hapo tutakanyaga moto,hakuna
anayesikia kama Yule anayeelewa,tusindikizane hivi kwa namna ilivyo..wala hata
tusijari na hiyo mioto.
Dunia inakwenda kule inapoelekea,dunia inajizungusha katika
njia zake,maana pasingekuwepo njia haina haja ya kutembea,pengine tutakimbia
wapi wakati njia yenyewe ni mbovu?tutengeneze njia na zenyewe zikatutengenezea
mahala pazuri,maana ule mti mkavu ndiyo wa kushukuliwa na kabati,hata vitanda
pia,ule mti mkavu ndiyo ule hasa usipate jema mwanzoni,kwa kuwa wenyewe unakuwa
mkavu,si kwamba hauna maji bali yale yaliyopo yametosheleza shina,ikiwa na
wenyewe unaweza kushika moto,baadaye ikawa ni heli kwetu pale tunapotaka
moto,pengine moshi utakuja kwa miti hii mibichi,tukiachana na moto kuna
moshi,hapo hatutaona,hapo hatutaonekana kana kwamba hata kuna njia,tutabaki
kutengeneza nyusi tusijue wapi macho kuona,tusielewe nini na wapi pa
kuelekea,tukabisha kwa kujifanya lakini kwa ukweli utaeleweka.
No comments:
Post a Comment