Wengi wameonekana wakiishi maisha ya samahani hiyo ikiwa
hawajafikiria ni namna gani waweze kuishi,kwa bila ya kujua nini
wanachokifanya yaweza kuwa umefanya mengi lakini yakaonekana
machache,umegandamizwa na maumivu mengi maumivu ya maisha na bado upo na pengine
unapomaliza jambo uwe unafikiria kabla labda baada ya hili nini kitafanyika ili
kugeuza kuwa na kufanya kile mtu unachokihitaji ukiwa unahitaji kuishi
maisha yaliyo sababu yako.
Muda mwingine ushangae yale unayoyafanya pale yakaleta
mshtuko,ukiwa umeelewa cha kufanya na ukachagua hapo unaweza kujua ukweli wako
wa maisha na maisha ni kuishi tena vile unavyoweza ikiwezekana vile unavyopenda ,mafanikio yaweza kuwa hakufika ndiyo maana akaondoka ama kughairi hilo hutajua lakini Kile kinachokuja baaada ya muda unahaki kukijua na kukifauru maana
kimekuja muda wako,hapa usipofikiria hofu ya kuachwa na muda angalia usichague hivyo pengine
wengine watakula kichwani na wewe uanze mkiani ama mwingine atataka paja na mwenzake kidali,pengine ni kutokana na ilivyo ama vile waipendavyo baadhi ya kila mmoja wapo.
Ishi ukiamini unajituma na sio kutumwa,ishi ukiamini wewe ni bora Zaidi ya mwengine akuchukuliavyo,ulizaliwa peke yako sina hakika kama kua mtu mnagawana shida na raha,wengi wanaopenda na kuishi wanavyotaka hula raha zao na shida zao wenyewe na wewe ukifanya hivyo utakuwa umeishi vile unavyotaka na sio lazima iwe hivyo ila kuishi kutakuwa pale pale.
No comments:
Post a Comment