Friday, August 17, 2012

MAISHA YAKO....

The purpose of life is not to be happy – but to matter, to be productive, to be useful, to have it make some difference that you have lived at all.
       
Leo Rosten, American teacher and humorist

Yaweza usitegemee yakuwa haijatokea katika maisha yako,usimtegemee mtu yoyote katika maisha yako hii ikiwa ni kauli ambayo inahitaji mtu kujiamini,kujipa nguvu na sio chuki ya kujitenga,kufikiri na kujua kama maisha unayoishi ni ya kwako peke yako,maana baadaye zisije kuwa lawama kwamba fulani anapenda pesa,hapo usipofikiri unataka mtu afe?maana na kweli njaa imekaba sana mtaani,watu wanapendeza,wanakunywa na kusaza lakini wana taabu mioyoni mwao,pengine ikiwa ni mapenzi ama ni namna ya maisha yalivyoandaliwa.

Katika maisha yako kuna mengi sana,itafika kipindi utasema sasa umekuwa,hata kama ulikuwa unajiona umekuwa,maana kuna wengine wakifanya maksudi na kuona hata aibu wa wakifanyacho,hata kama ikiwa sawa ni kutafuta pesa,lakini namna nyingine ni kutafuta pesa kwa ajili ya kuzikwa,naogopa kuwa Malaya wa maneno na mwisho wa siku wakaielewa wachache,kataa kupoteza muda wako,maana kwa lile lililopita liache liende,hakuna zuri moja katika dunia zaidi ya kile akionacho mtu,pengine wengine wakafikia hadi moyoni,unaweza kukutana na maneno mengi sana hata katika mitaa hiyo ni namna ya kukupanua ubongo,yaani experience,kwa vile mtoto alianza kusikia na atasema,wakubwa wakisikia huwa ni siri daima.

Pigana maisha ni magumu sana,napigana na ikiwa kwa kila namna,,pigana sana wanadamu hawana hiyana,maisha haya ya leo unaweza kuishi kesho na kusema unaishi maisha ya jana,yanakuja mengi sana mengine yatasemekana kumwachia maulana,tutaona mengi sana kwa kuwa bado sisi ni vijana,wazee wetu wametufundisha vile ilipofika,ni wakati wa kutumia kijiko kujaza pipa kipindi cha masika,utake usitake vyote vimekwekwa uvunguni sharti ya kufurahi ni kuinama.tukiwa kama wote vijana tuombeane kheri haya maisha yasije kutuendea mlama.

):-Benson G. Makaya

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...