Tatizo ni kwangu maana hata muda bado unazidi
kwenda,nimekosa leo nikitegemea kupata kesho,ikiwa kila mtu ana kipato
chake,kwa upande wangu sijapata na ikiwa kwa upande wangu ulio kwako umepata
basi uhaki kuisubiria ahadi yako kama vile ninavyoisubiri,matatizo ni namna ya
kuweza kutafuta,maana kama hautafuti kwa nini una matatizo?hapo ndiyo utasikia
wakisema lazima kuna mchawi hapa.maisha mchawi ni wewe,hakuna mlinzi mzuri wa
mwili wako zaidi ya wewe mwenyewe,hivyo ukishindwa utajiletea matatizo,tena
‘matatizo’ ni kama ‘maisha’ maana yenyewe yana mazuri na mabaya.
Duniani ndiyo mahala pa kuishi,utasikia ikisemeka
kwamba duniani maisha magumu sana ,sasa wapi rahisi,unapoona nyuki
wanakukimbilia na wewe kimbia,kwa mfano wa kuku anapotakwa kuchinjwa siku yake
inapofika,maana siku yako ikifika hapo utajua tatizo,tena yenyewe huwa hayana
hodi wala kalenda labda siku fulani yapasa kupumzika ili kusherehekea,maana
itakuwa imepatikana.pengine matatizo yako ikiwa kama ni raha ya mtu mwengine,wewe unacheka wengine wanalia.hapa ikiwa lazima ujue umekosa nini.
Tatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu ikiwa ameamua
kuishi,wengine wanakata tamaa kwa kuona maisha magumu,kama wale
wanoenda shule na kuacha,ya kuwa shule ngumu,na bila kugunndua baadaye itasemeka
ni kwa sababu shule haikuenda.maisha yenyewe ni shule,matatizo hasa ndiyo
yanayomfundisha mwanadamu,kuna mengine yale yanayokosekana yakaonekana kama na yenyewe
ni matatizo,sasa kama yakija na yenyewe kwa matatizo yake si utakata roho kabisa?labda ikiwa ni furaha..,maana
kama kile kilichokuwepo kimekuwa tatizo basi hata kisichokuwapo haina haja ya kukisumbukia maana
tutaongeza matatizo tu.
No comments:
Post a Comment