Friday, February 10, 2012
Tuesday, February 7, 2012
OPT:-ONA, POKEA,TOA.
ONA ni vile kwa namna uliyoumbwa
ili kuweza kuvitambua vitu kwa urahisi,kwa kutumia macho yako umeweza
kuona vingi sana,na kila kimoja kikiwa katika maana yake ya utambuzi kutoka kwa
yule muonaji.Kutokana na utofauti wa maumbile ambao uko mbali na usawa wa
kusema kuwa wote binadamu tu sawa,kama wengine walivyopewa macho kwa pengine
wale wasioona mungu anawalinda kwa namna yao,na ndio maana maisha yakaendelea
na vitu vyote kuonekana kama vilivyo,kila jicho
litaona imeandikwa kwa namna iliyopo na itakayokuwepo,kwa yeyote anayeomba
msaada anakuwa ameshindwa,lakini kwa nguvu ya mpambanaji hata kuomba msaada ni
kupambana maana iliandikwa kwa yule atakayeomba atapata,
Hapa huwa inakuwa ni kama haujaona,kwani pale unapopata unashindwa kufanya na hatimaye kupotea,kwani wengine wanahitaji kuona pia,yule aliyekosa miguu atembelee mikono na ikishindikana atafute namna,unaendelea na safari,yule anayeomba,asirudi na kesho ya kuwa aliona jana,ikiwezekana kifichwe maana itazoeleka,ikiwa sio roho mbaya yule aambiwe nenda katafute,vipo pale hata kama havipo basi aelekezwe njia.Ubishi ndio huleta upofu,maana mbishi hataki kuonekana ameshindwa,zaidi ni kwa namna ya yeye atakavyojifanya HAONI..
Hapa huwa inakuwa ni kama haujaona,kwani pale unapopata unashindwa kufanya na hatimaye kupotea,kwani wengine wanahitaji kuona pia,yule aliyekosa miguu atembelee mikono na ikishindikana atafute namna,unaendelea na safari,yule anayeomba,asirudi na kesho ya kuwa aliona jana,ikiwezekana kifichwe maana itazoeleka,ikiwa sio roho mbaya yule aambiwe nenda katafute,vipo pale hata kama havipo basi aelekezwe njia.Ubishi ndio huleta upofu,maana mbishi hataki kuonekana ameshindwa,zaidi ni kwa namna ya yeye atakavyojifanya HAONI..
Kuna mengine sio lazima kuyaona,maana yatabaki kwenye mboni za macho
yako na kwenda ndani ya mwili,kwani hata wachache utasikia “yale mambo yamemwingia damuni” ,hapo
watasema wao na unahitaji kuya POKEA,ikiwa kwa kuona yatakuwepo mpaka katika vidole vya mguu kwani kule
ndio mwanzo kuliko mwisho.Viungo vya mwili sio vya kutufanya ushindwe
maisha,ikiwa ni kichwa kwa ujumla,mikono,na vinginevyo,ikiwa mtu hasikii ndio maana
ya kujua kusikia,kwani hata umuulizapo mtu asiye sikia anatamani nini naye
aseme ‘kusikia’maana hata akawa ametamani kusikia vizuri ni nini hasa
ulichomuuliza.
Ni kweli sio wote tunaosikia,na hapa ieleweke sio wote tunaoweza kupokea katika muda muafaka,kwani ikiwa sauti imetoka watakaosikia ni wale waliohitaji kuipokea sauti hiyo,iwe wanasikia au hawasikii.Wale wanaosikia lakini wanaweza wasisikie endapo pale mtu ameongea na kama ni ililetwa zawadi basi watapata wachache kwani kuna wale walio iona zawadi,wengine walisikia lakini wasijue ni zawadi gani na kuna wale walioitiwa zawadi ikiwa kila mmoja na yake,wale watakao pokea si tu ndio wale walio itiwa zawadi kwa maana ni za kwao.endapo mtu amekosa zawadi na aliitwa basi ajue ni huwa inatokea hiyo,hata maisha ya kwako si ya kufananisha na mwenzio.
Ni kweli sio wote tunaosikia,na hapa ieleweke sio wote tunaoweza kupokea katika muda muafaka,kwani ikiwa sauti imetoka watakaosikia ni wale waliohitaji kuipokea sauti hiyo,iwe wanasikia au hawasikii.Wale wanaosikia lakini wanaweza wasisikie endapo pale mtu ameongea na kama ni ililetwa zawadi basi watapata wachache kwani kuna wale walio iona zawadi,wengine walisikia lakini wasijue ni zawadi gani na kuna wale walioitiwa zawadi ikiwa kila mmoja na yake,wale watakao pokea si tu ndio wale walio itiwa zawadi kwa maana ni za kwao.endapo mtu amekosa zawadi na aliitwa basi ajue ni huwa inatokea hiyo,hata maisha ya kwako si ya kufananisha na mwenzio.
unapopokea yakupasa upokea kwa shukrani,labda usiwe umezipenda zawadi
zenyewe,na hata iwe hivyo zitakuwa za kwako tu,kinachotoka machoni hupita na
moyoni kabla ya ruhusa ya kutoka nje,moyo unapopokea ni inapasa kuushirikisha
na ubongo ili kuweza kujua kama ni imetambulika pia ni haki,moyo wa mwanadamu
haufai kufuga uchafu labda uwe wa mtu wa namna hiyo.Mwisho ni matendo,yawe
yanatoka moyoni,ikiwa moyo wako utajulikana kutokana na matendo yako jua unapotenda ni kama pale unapoongea,unapoongea una TOA yaliyopo moyoni na
kuyaweka katika mazingira ya kawaida,ingawa hata ya moyoni ni ya kawaida kwa
wengine katika mazingira hayohayo ya kawaida,ikiwa haionekani kwa macho lakini
ni macho yaliyopelekea akilini,hivyo yapasa kupumzisha akili,kama vile unapopumua kwa kutoa na kupokea hewa ili uendelee kuishi,labda imekuwa nzuri kutoa kuliko kupokea
ya kuwa unaotoka ni uchafu.
'ona sahihi,pokea vyema na utoe kwa moyo mmoja'.
By: Benson G.Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com
Monday, February 6, 2012
MWISHO WA KUTENDA,NI MAAMUZI.
Asichekwe yule atayetenda bila ya kujua ni nini,ikiwa mtendaji anatakiwa kutenda zaidi
ya vile bila ya yeye kujua mwenyewe..basi aachwe hivyo.Maana katenda,ya hivyo
na yenyewe kaamua,na linalokuwa na msingi ni kuweza kuelewa pale vifanyikapo
vitu,kwani na mara nyingine visieleweke,yaweza kuwa ni nusu au nzima
iliyokuwepo katika matendo lakini msimamo wa jambo wenyewe umekuwa mgumu,mda
mwingine kwa yale ya kiswahili huwa ni mazuri zaidi lakini yanaharibu
yanapokuwa mengi,maamuzi ni zaidi ya mtu kutenda moja
kwani yamekuwa mengi sasa,hapa tukatenda hivi na baadae kumalizia mengine,pale
kwenye kumalizia si lazima yawe yalianza zamani mengine yakiwa ni marahisi,kama
maamuzi yako yataamua kubaki,muda hua
ni kwenda mbele,kwani nao umeamua,tena shikilio la amuzi moja tu,la kwenda
mbele.
Kipindi cha kujutia hakitakiwi endapo tu pale imetokea,kwani wengine
hukaa kabisa na bila kuyakataza mawazo yao,kama mtoto anakatazwa kuchezea wembe
ndio ije mtu mzima kwa mabovu?kama tutachukulia kila kitu kilivyo ndivyo
kitakavyo kuwa kwani kilivyokuwa ndio kilikuwa kinaelekea hapo,hatua
tusipoichukua ni tumetoa ruhusa kwani muda kazi yake ni lazima utumike,sio
lazima wewe kwani ndiyo nani?alieutengeneza alikaa kila mda huohuo
kuutengeneza,akijua itafika kipindi ataumaliza,tunapokimbilia kule tunamaana ya
kuwepo huko,
Hatuwezi kuamua au kuacha wengine waende bila yetu kuamua tubaki,
Ijulikane hakuna wa kuishi maisha ya mwenzake,tofauti isiwe sababu ya
kuishi tofauti,tena tusiamuliane,lile lililo la mmoja likafanyike katika
yeye,maana mda utapita,sio tunahofia ingawaje hatulazimishi kuelewa ndio maana
tukaamua tofauti,kuepuka ubishi na maamuzi yasiyo na msingi,ikiwa hatutaki
ubishani usio na maana,maana itafika kipindi tuwaze vilivyopotea na wakati
vizuri ndio hivyo vinajongea,ni ukaribu ambao katika moyo unaweza usikia,sio
kama ule wa kunyata na miguu ukaishtukia,maana mda mwingine tusiseme tu maneno
yasiyo na msingi,ikawe tutaelewana kila mmoja akawe na maana katika lake,akiwa
katika mahala pake ndipo atakapofika.mahala pake pale alipo yeye kimawazo,akili
na uhalisia wa mwili wake.
Ili matendo yapendeze ni kuna ulazima wa maamuzi sahihi kufanyika
sasa,isiwe lazima kwa wale wachache,maana hao watakuja na kusema wanataka baadae,yule
atakayebisha naomba nisiwe mimi kwani nitakuwa nje ya vile alivyoamua
yeye,ikaja yeye au wewe umeamua jinsi vile nilivyogoma mwisho waweza kuwa mbali
sana,kwani bado wengine tupo mwanzo na kinachosubirika hakieleweki kwani
hatukueleweshwa kama haya ya muda huu yanahitaji maamuzi yake,wakiwa kama wao
wanaogopa kutuambia kwani ni heli kumwacha nyani amalizie maembe katika mti
kuliko kumshtua,maana mpaka kapanda aliyatafutia,
sijui nani amesikika akiakataza.eti yale walipasa kula wao,sijui walikuepo wapi maana muda wote mpaka
yakaoza hawayakuona.binadamu tunalidhika na kile tunachokiona,wala
hatunashida na kuridhika na kile tunachokitafuta,machache yawe ni majina na wala sio watu
hapo tunaweza kupata hekima,maana tukijazana tutaonekana wazembe,ikiwa muda wote
huo tulikuwa wapi?itakuwa zamu ya wengine bila ya kuamua,tuangalie kipindi
maana huwa vinatofautiana dakika.
MAWAZO YASITUTENDESHE
MAOVU, MDA MWINGINE MWANA ADAMU ANAPOKUWA HAJIELEWI.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255714336657
Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...
Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...: Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameis...
WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJIFUNZA JINSI YA KUTOKA KATIKA MATATIZO.
Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameisibu jamii au mtu binafsi katika ufanisi wa kufanya mambo fulani,matatizo huwa hayaangalii hali halisi ya mtu husika endapo atakuwa na uwezo nayo ama la,matatizo ni maswali yanayoijia jamii,kwa upande mmoja ama mwingine matatizo huwa hayakaribishwi kwani yanaweza kuja magumu zaidi.Wakubwa ndiyo watu wanaoeleweka kuwa na matatizo ndani ya maisha ya mwanadamu kutokana na kile kitu tunachoweza kusema wao ndiyo watafutaji wa maisha kama inavyoeleweka,na matatizo yanaweza kuwepo ni kutokana na ugumu wa maisha katika mawazo ya klila mtu pale inapomtokea,tukitolea mbali ya kiafya,watoto wamekuwa wakihesabika kama ni watu wasio na maatatizo na hata kama wanayo ni si kwamba utofauti wa ukubwa na udogo..
Yale yaliyopita ndiyo haya yanayokuja,kwani ifikapo kipindi cha ukubwa,mtoto hufanya kile alichofanya kipindi cha utoto,kubaki kuwa mtoto kwa sababu umri ni unasogea.Wakaona tofauti ambayo hao ndiyo uliowatendea,ikiwa nikiwa litaendelea kusemeka kwa muda wote na ukawa mwingi bila hata ya mageuzi hapo kuna uwalakini wa mafunzo kutokupatikana kwa mtoto na hata kuendelea kukua na tabia kama hizo.Tabia chafu humnyima furaha mtu mwanadamu,Yule anayetenda uchafu ni sawa na mtoto maana haelewi lolote,akiwa anaelewa na kufanya maksudi basi tunaweza kukaa mbali na huyo mtu,kwani mwishowe atatufanyia maksudi na sisi wenyewe.
Wakubwa wengi wanaelewa ni kwa sababu ya kupita kwingi pia,watoto wakafundishwe na wakubwa,ikiwa wakubwa wanaofundisha na wao hawana uelewa basi hapa kwa mtoto itasemeka vile ya namna 'umleavyo ndiyo vile atakavyokuwa',ikawe sio ni makosa zaidi ya lawama,na hii huwa haiji kwa mzazi kwani 'chanda chema'..!,hata kama tunalifahamu hilo lakini hatujui la kufanya,kwani akili inaweza kumfanya akafanya kitu kama ni mtoto ndiyo naye akatambue yake,maana matendo sio ya kuchaguliana,zaidi tutaumizana kwa dhana za kwenda katika vifungo vya maisha,hata kupelekea vifo bila hali kukaa sawa,maana vinakuja vizazi sasa,vizazi vinavyoelewa yale ya kwao,maana hata nimesema yale ya kuwa ni vigumu ya kuyafahamu.
Yanayotushinda ni ya kufikiri na sio kutumia 'nguvu',ikiwa hivi hata kabla ya kutenda tungelikuwa tunajifikiria na kama yangetokea basi yangekua na upungufu kidogo wa makali,ingawa kila mtu ana matatizo yake na ule uchungu anaufahamu yeye muhusika,ni sawa na pale inapokuwa mbaya kwa mwenzako mwengine naye akapata kuchekelea,si ya kwamba tu ni rahisi bali ni yametokea katika upande ambao yeye haumuhusu,na hata kama ulipita vibaya wao watataka kujua hilo, mtoto anapokuwa haelewi ni haki kumrekebisha ikiwa nawe mzazi umeelewa jambo,mtoto anapofanya kitu sio kama mtu mzima,mtoto ni kama mashine,mara nyingine ikaende yenyewe itakavyo au vile mzazi akaendesha,ikiwa ni kwa pupa bila uhangalifu basi mali hiyo si ya kukaa muda mrefu,hakuna kinachodumu kwa mateso zaidi ya kuteseka.
Bila ya kusahau maisha ya mtu anayatengeneza mwenyewe,ikiwa kama vile tukajenga nyumba,kununua magari na kusema tumefanikiwa,tukiwa na msingi ulio bora,msingi wa maendeleo kutoka kwa jamii na wakubwa wengine,mtoto anapaswa kuelewa pale anapoelekezwa,mtoto mwenye kiburi na sio usikivu ni Yule aliyefundishwa hivyo,akazembewa na akakua,tabia ni kama samaki,haswaa samaki aliyekauka ndiyo hatakiwi hata kukunjwa,maana atavunjika na baadaye kuwa hasara.
"Mali ni mali tu hata ikiwa mbovu ili mradi uwe na umiliki nayo".
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
Saturday, February 4, 2012
UZURI.
Katika kila kitu kuna sifa,ili kitu kiweze kujisikia kwamba
ni kitu kinahitaji sifa,sio kila sifa ni nzuri,wala sio kila uzuri ni
uzuri,inaweza ikawa ni hivyo kimaandishi na maneno yalivyo lakini katika maana
ikatoka tofauti na uzuri ulivyo,uzuri ni
kwa uzuri tu.Katika yote mazuri huwa juu ya watu,kwa watu haipendezi kukawa na
uzuri bila ya watu kuwa wazuri,ikiwa watu tunatakiwa kuendana na vile
tuvifanyavyo au tunavyoweza kuvimiliki,ikiwa mtu ana chake tunaweza
kutofautisha uzuri ikiwa na watu pia tuko tofauti,ikiwa katika mavazi na undani
wetu zaidi,kwani sio wote wanaovaa vizuri kuonyesha vyao,ieleweke kuvaa vizuri
sio kupendeza kwani wengine hufurahisha maumbile na mioyo kwa kuvaa wawezavyo
ikiwa ni tofauti na uzuri,mavazi ndiyo yanayomfanya mtu aonekane katika namna
inayompendeza yeye,mavazi ndio humtambulisha mwanaadam,tena tusifike mbali kwa
kuulizia jinsia maana mavazi tunayaona wenyewe.
Wanaocheka sasa baadae wanaweza kutafuta wao,kama lengo ni
kuuelewa uzuri.tukiwa tunajifahamu ni sisi tusitake na wengine watujue tusijifanye
tupo juu wakati ni chini tusipopajua,tutaumia tukiwaza mazuri yamepita bila
kuonekana wakati ni sisi wenyewe tulikuwa katika mabaya,ingawaje haikupendeza
kwa mabaya kuongeleka pengine yangekuwa ni sawa na yale mazuri,labda
utofautishaji tu,ni kama pale tunapoimba na kusoma na ifike kipindi tusielewe
kama tulikuwa tunaimba ama tunasoma,kwani muda mzuri wa kufikiri yote hayo
ungekuwa ule wakati hasa kabla ya kutenda,ingawaje sio kosa,na hakuna wa kumpa
mwenzake lawama kwani kila mtu ni mzuri katika upande wake.
Lugha huwa zinachanganya sana,tatizo sio kusikika,tatizo sio
njia ya mawasiliano,tatizo ni kusikia,kivingine tumeweza kusikika tofauti na
vile maana ya mtu inavyoweza kumjia ikiwa tunasikia kwa lugha nzuri na
safi,kama ni mbaya basi inapaswa kubadilishwa,maana hata sasa tumekuwa
tukijitahidi kufahamu lugha nyingine,na hapa tuone uzuri,ya kuwa sio ile ya
kwanza haifai bali na ya pili imekuwa bora,na ya tatu mwishowe tutakuja
kugundua zote ni nzuri ila utofauti ni pale katika matumizi ya lugha hizo,ikiwa
wengine wanatumia lugha chafu haimaanishi ni wachafu,labda lugha chafu
ilitumika kumwambia mtu aache uchafu wake,lugha ile inaweza kuonekana ni nzuri
kwa mchafu,yakuwa ni yake.
Nguvu haibadilishi rangi,kile kinachokuwa kibaya baada ya
kupungua basi ni kizuri maana ni kimepungua tu,kumbe itafika kipindi tunaweza
kujaza uzuri wetu hadi mioyoni,maana imekuwa kama ni sura
tunazibadilisha,maumbile tunayaweka vile tunavyotaka wabaya waone vizuri,yaweza
kuwa nasi ni wabaya na tunatenda ili
tuonekane tumefanya vizuri,lakini katika yote ni heli tumefanya,maana tusiogope
kujifunza,ikiwa watu wanajenga madaraja sio kwa ajili wapiti peke yao,na kwa
kile chochote kilicho kibaya kimetendeka nasisi tukajifunze juu ya hicho,tusije kunywa sumu na haya maisha
yalivyo magumu,maana siku hizi tunapona,tatizo linakuja katika kuendelea kuishi
kwani mtu aliyekata tama anastaili falaja,lakini hawa wa kutoa faraja nao
wamekuwa wafanyakazi,wanatafuta mshahara ingawaje mwanzo waliweza,na ndiyo
maana ya kufika mpaka muda huu
Tuiache imani ibaki kama dhamana,ikiwa ni lazima turudi na kufanya yale
mazuri ya maana.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66
57.
Friday, February 3, 2012
TUNAWAZA KUKOSA,TUSIPOJUA NI VIPI TUMEPATA..
Mawazo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,katika kupitia na kufanya vile au kile ilivyotakiwa.Kuna mengi ambayo mwanadamu anaweza kuwaza ikiwa ya furaha,kejeli,chuki,upweke,na ya ki kawaida kabisa,mawazo huweza kurudisha na kukamilisha mipango au malengo ya mwanadamu ikiwa sahihi pale anapokuwa na utambuzi zaidi.
Kweli
inapasa utofauti,ikiwa wengine wako kawaida basi na sisi tuwe,ili ikaonekane tofauti
kwa wengin,labda tuseme tumepata ikiwa ni mvuto wa kupata na vingine,vile
ambavyo yeyote yule anavyo kwa miliki ya uhalisia wowote,ikawe na maana ya
maamuzi kwani yeyote anayeishi anayo mawazo,katika yote na hata yale
asiyoyaomba,juzi hapa tulifanikiwa kama mvua isingeendelea kunyesha,kumbe
hatukufanikiwa ila ilipasa kwa mwelekeo wa mienendo na shughuri zilizokuwa
zikifanywa ziliashiria jambo,ikiwa kila mwanaadamu anaukaribu na yaliyobora
yake,na sio kwamba tulifeli sasa,labda tumefauru tofauti,mda mwingine uhakika
tunakuwa hatuna ni kwa sababu mengine mambo yanakuwa ni ya wengine,hatutaweza
kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,hapa tutajiongezea mawazo,labda
tuseme tumeweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,haya mengi
sana yamechanganyika na ya watu..na hii ndio hufanya kushindwa,au hata kufauru
ikiwa lengo,asiyependa upumbavu ndiyo yule anayetaka maana,kile kinachoingia
hakiingii hivi hivi ni lazima kiwe na njia,na kama walisema tusikie na tukaziba
masikio yetu basi hatutaelewa vizuri kwani yaliyosikika si yale yaliyoonekana
mdomoni.
Katika kufanya ni kunatokea na kile unachokitaka
kitokee,kama hatutajua ni namna gani tumevifanya basi hata tunapovipata
tusiseme ni sisi tumefanya,maana wapo waliofanya ndio wakasema tugawane,kwa
yule aliyegawa..ikiwa anaye gawa anagawa chochote kilichomzidia,ikiwa tumemwita
mwenzetu mmoja na kibri ni lazima tuelewe kimetoka wapi,isije ikawa ni chetu
maana chuki hugawika kwa upendo,tukawapa wengine wasiwe na hatia na kwa uzito
tu ikawe kujibu kwa mitetemo,yule akaonekana muongo kwa kutetemeka,tuache
kufanya kufahamu herufi kabla ya maneno,maana hayo yakiunganika yatatuangamiza
zaidi.mwanadamu amependa basi amepata ikiwa alitafuta,tutafikiria yaliyo sahihi
na mabovu yataendelea kuharibika,kwani malengo yapo,na nani anaweza
kuyafuatilia,kwa kutokujua idadi maana tungesema ni mengi,au machache endapo
yangehesabika,hivyi vyote hata ikawa hakuna lolote yaani hakuna cha kuhesabu hata
vingi vikawa idadi,mwanzo ukigundulika mwishowe hueleweka,mtu anaposema pole sio
kaumia yeye,
Yale yaliyopatikana sasa ndio yaliyokosekana mwanzo,yakiwa
na ukosekanaji pale palipo na uhitaji,haya mengi sio ya kuyasumbukia labda iwe
imeeleweka hayo ni mengi kiasi gani,tutasaidiana sana lakini tutafikia tofauti
ikiwa usaidizi mwingine haufanyiki baada ya kusikilizwa,na ndio baadae tusiseme
yale ni ya Fulani na haya ni ya nani,vichwa vitauma endapo dawa zitaonekana,maana
bila hivyo tena wanaadamu watahitaji kula nyama ya mwanadamu mwenzao,tunaweza tengeneza njia ya
msitu wa miba,,haiwezi kuonekana njia ikiwa wale wengine walikataa
kusikia,hatutaweza kuyafikia ikiwa tu tumekaa na kushindwa kutembea,yule anaye tembea
anajua mengi,maana atakuja hata nyumbani akikwambia ana njaa,njaa haijatokana
na kazi za huko ya kuwa mwanadamu ni lazima ale.labda iwe na awe ameelelewa
hivyo.
Yawepo,yasiwepo yatatafutwa.
Lengo ni kuyapata!!
By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...