Asichekwe yule atayetenda bila ya kujua ni nini,ikiwa mtendaji anatakiwa kutenda zaidi
ya vile bila ya yeye kujua mwenyewe..basi aachwe hivyo.Maana katenda,ya hivyo
na yenyewe kaamua,na linalokuwa na msingi ni kuweza kuelewa pale vifanyikapo
vitu,kwani na mara nyingine visieleweke,yaweza kuwa ni nusu au nzima
iliyokuwepo katika matendo lakini msimamo wa jambo wenyewe umekuwa mgumu,mda
mwingine kwa yale ya kiswahili huwa ni mazuri zaidi lakini yanaharibu
yanapokuwa mengi,maamuzi ni zaidi ya mtu kutenda moja
kwani yamekuwa mengi sasa,hapa tukatenda hivi na baadae kumalizia mengine,pale
kwenye kumalizia si lazima yawe yalianza zamani mengine yakiwa ni marahisi,kama
maamuzi yako yataamua kubaki,muda hua
ni kwenda mbele,kwani nao umeamua,tena shikilio la amuzi moja tu,la kwenda
mbele.
Kipindi cha kujutia hakitakiwi endapo tu pale imetokea,kwani wengine
hukaa kabisa na bila kuyakataza mawazo yao,kama mtoto anakatazwa kuchezea wembe
ndio ije mtu mzima kwa mabovu?kama tutachukulia kila kitu kilivyo ndivyo
kitakavyo kuwa kwani kilivyokuwa ndio kilikuwa kinaelekea hapo,hatua
tusipoichukua ni tumetoa ruhusa kwani muda kazi yake ni lazima utumike,sio
lazima wewe kwani ndiyo nani?alieutengeneza alikaa kila mda huohuo
kuutengeneza,akijua itafika kipindi ataumaliza,tunapokimbilia kule tunamaana ya
kuwepo huko,
Hatuwezi kuamua au kuacha wengine waende bila yetu kuamua tubaki,
Ijulikane hakuna wa kuishi maisha ya mwenzake,tofauti isiwe sababu ya
kuishi tofauti,tena tusiamuliane,lile lililo la mmoja likafanyike katika
yeye,maana mda utapita,sio tunahofia ingawaje hatulazimishi kuelewa ndio maana
tukaamua tofauti,kuepuka ubishi na maamuzi yasiyo na msingi,ikiwa hatutaki
ubishani usio na maana,maana itafika kipindi tuwaze vilivyopotea na wakati
vizuri ndio hivyo vinajongea,ni ukaribu ambao katika moyo unaweza usikia,sio
kama ule wa kunyata na miguu ukaishtukia,maana mda mwingine tusiseme tu maneno
yasiyo na msingi,ikawe tutaelewana kila mmoja akawe na maana katika lake,akiwa
katika mahala pake ndipo atakapofika.mahala pake pale alipo yeye kimawazo,akili
na uhalisia wa mwili wake.
Ili matendo yapendeze ni kuna ulazima wa maamuzi sahihi kufanyika
sasa,isiwe lazima kwa wale wachache,maana hao watakuja na kusema wanataka baadae,yule
atakayebisha naomba nisiwe mimi kwani nitakuwa nje ya vile alivyoamua
yeye,ikaja yeye au wewe umeamua jinsi vile nilivyogoma mwisho waweza kuwa mbali
sana,kwani bado wengine tupo mwanzo na kinachosubirika hakieleweki kwani
hatukueleweshwa kama haya ya muda huu yanahitaji maamuzi yake,wakiwa kama wao
wanaogopa kutuambia kwani ni heli kumwacha nyani amalizie maembe katika mti
kuliko kumshtua,maana mpaka kapanda aliyatafutia,
sijui nani amesikika akiakataza.eti yale walipasa kula wao,sijui walikuepo wapi maana muda wote mpaka
yakaoza hawayakuona.binadamu tunalidhika na kile tunachokiona,wala
hatunashida na kuridhika na kile tunachokitafuta,machache yawe ni majina na wala sio watu
hapo tunaweza kupata hekima,maana tukijazana tutaonekana wazembe,ikiwa muda wote
huo tulikuwa wapi?itakuwa zamu ya wengine bila ya kuamua,tuangalie kipindi
maana huwa vinatofautiana dakika.
MAWAZO YASITUTENDESHE
MAOVU, MDA MWINGINE MWANA ADAMU ANAPOKUWA HAJIELEWI.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255714336657
No comments:
Post a Comment