Monday, February 6, 2012

WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJIFUNZA JINSI YA KUTOKA KATIKA MATATIZO.


 Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameisibu jamii au mtu binafsi katika ufanisi wa kufanya mambo fulani,matatizo huwa hayaangalii hali halisi ya mtu husika endapo atakuwa na uwezo nayo ama la,matatizo ni maswali yanayoijia jamii,kwa upande mmoja ama mwingine matatizo huwa hayakaribishwi kwani yanaweza kuja magumu zaidi.Wakubwa ndiyo watu wanaoeleweka kuwa na matatizo ndani ya maisha ya mwanadamu kutokana na kile kitu tunachoweza kusema wao ndiyo watafutaji wa maisha kama inavyoeleweka,na  matatizo yanaweza kuwepo ni kutokana na ugumu wa maisha katika mawazo ya klila mtu pale inapomtokea,tukitolea mbali ya kiafya,watoto wamekuwa wakihesabika kama ni watu wasio na maatatizo na hata kama wanayo  ni si kwamba utofauti wa ukubwa na udogo..

Yale yaliyopita ndiyo haya yanayokuja,kwani ifikapo kipindi cha ukubwa,mtoto hufanya kile alichofanya kipindi cha utoto,kubaki kuwa mtoto kwa sababu umri ni unasogea.Wakaona tofauti ambayo hao ndiyo uliowatendea,ikiwa nikiwa litaendelea kusemeka kwa muda wote na ukawa mwingi bila hata ya mageuzi hapo kuna uwalakini wa mafunzo kutokupatikana kwa mtoto na hata kuendelea kukua na tabia kama hizo.Tabia chafu humnyima furaha mtu mwanadamu,Yule anayetenda uchafu ni sawa na mtoto maana haelewi lolote,akiwa anaelewa na kufanya maksudi basi tunaweza kukaa mbali na huyo mtu,kwani mwishowe atatufanyia maksudi na sisi wenyewe.

Wakubwa wengi wanaelewa ni kwa sababu ya kupita kwingi pia,watoto wakafundishwe na wakubwa,ikiwa wakubwa wanaofundisha na wao hawana uelewa basi hapa kwa mtoto itasemeka vile ya namna 'umleavyo ndiyo vile atakavyokuwa',ikawe sio ni  makosa zaidi ya lawama,na hii huwa haiji kwa mzazi kwani 'chanda chema'..!,hata kama tunalifahamu hilo lakini hatujui la kufanya,kwani akili  inaweza kumfanya akafanya kitu kama ni mtoto ndiyo naye akatambue yake,maana matendo sio ya kuchaguliana,zaidi tutaumizana kwa dhana za kwenda katika vifungo vya maisha,hata kupelekea vifo bila hali kukaa sawa,maana vinakuja vizazi sasa,vizazi vinavyoelewa yale ya kwao,maana hata nimesema yale ya kuwa ni vigumu ya kuyafahamu.

Yanayotushinda ni ya kufikiri na sio kutumia 'nguvu',ikiwa hivi hata kabla ya kutenda tungelikuwa tunajifikiria na kama yangetokea basi yangekua na upungufu kidogo  wa makali,ingawa kila mtu ana matatizo yake na ule uchungu anaufahamu yeye muhusika,ni sawa na pale inapokuwa mbaya kwa mwenzako mwengine naye akapata kuchekelea,si ya kwamba tu ni rahisi bali ni yametokea katika upande ambao yeye haumuhusu,na hata kama ulipita vibaya wao watataka kujua hilo, mtoto anapokuwa haelewi ni haki kumrekebisha ikiwa nawe mzazi umeelewa jambo,mtoto anapofanya kitu sio kama mtu mzima,mtoto ni kama mashine,mara nyingine ikaende yenyewe itakavyo au vile mzazi akaendesha,ikiwa ni kwa pupa bila uhangalifu basi mali hiyo si ya kukaa muda mrefu,hakuna kinachodumu kwa mateso zaidi ya kuteseka.

Bila ya kusahau maisha ya mtu anayatengeneza mwenyewe,ikiwa kama vile tukajenga nyumba,kununua magari na kusema tumefanikiwa,tukiwa na msingi ulio bora,msingi wa maendeleo kutoka kwa jamii na wakubwa wengine,mtoto anapaswa kuelewa pale anapoelekezwa,mtoto mwenye kiburi na sio usikivu ni Yule aliyefundishwa hivyo,akazembewa na akakua,tabia ni kama samaki,haswaa samaki  aliyekauka ndiyo hatakiwi hata kukunjwa,maana atavunjika na baadaye kuwa hasara.

"Mali ni mali tu hata ikiwa mbovu ili mradi uwe na umiliki nayo".


By:            Benson G. Makaya,
Tel:             +255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...