Tuesday, February 7, 2012

OPT:-ONA, POKEA,TOA.



ONA ni vile kwa namna uliyoumbwa  ili kuweza kuvitambua vitu kwa urahisi,kwa kutumia macho yako umeweza kuona vingi sana,na kila kimoja kikiwa katika maana yake ya utambuzi kutoka kwa yule muonaji.Kutokana na utofauti wa maumbile ambao uko mbali na usawa wa kusema kuwa wote binadamu tu sawa,kama wengine walivyopewa macho kwa pengine wale wasioona mungu anawalinda kwa namna yao,na ndio maana maisha yakaendelea na vitu vyote  kuonekana kama vilivyo,kila jicho litaona imeandikwa kwa namna iliyopo na itakayokuwepo,kwa yeyote anayeomba msaada anakuwa ameshindwa,lakini kwa nguvu ya mpambanaji hata kuomba msaada ni kupambana maana iliandikwa kwa yule atakayeomba atapata,

Hapa huwa inakuwa ni kama haujaona,kwani pale unapopata unashindwa kufanya na hatimaye kupotea,kwani wengine wanahitaji kuona pia,yule aliyekosa miguu atembelee mikono na ikishindikana atafute namna,unaendelea na safari,yule anayeomba,asirudi na kesho ya kuwa aliona jana,ikiwezekana kifichwe maana itazoeleka,ikiwa sio roho mbaya yule aambiwe nenda katafute,vipo pale hata kama havipo basi aelekezwe njia.Ubishi ndio huleta upofu,maana mbishi hataki kuonekana ameshindwa,zaidi ni kwa namna ya yeye atakavyojifanya HAONI..

Kuna mengine sio lazima kuyaona,maana yatabaki kwenye mboni za macho yako na kwenda ndani ya mwili,kwani hata wachache  utasikia “yale mambo yamemwingia damuni” ,hapo watasema wao na unahitaji kuya POKEA,ikiwa kwa kuona yatakuwepo mpaka katika vidole vya mguu kwani kule ndio mwanzo kuliko mwisho.Viungo vya mwili sio vya kutufanya ushindwe maisha,ikiwa ni kichwa kwa ujumla,mikono,na vinginevyo,ikiwa mtu hasikii ndio maana ya kujua kusikia,kwani hata umuulizapo mtu asiye sikia anatamani nini naye aseme ‘kusikia’maana hata akawa ametamani kusikia vizuri ni nini hasa ulichomuuliza.

Ni kweli sio wote tunaosikia,na hapa ieleweke sio wote tunaoweza kupokea katika muda muafaka,kwani ikiwa sauti  imetoka watakaosikia ni wale waliohitaji kuipokea sauti hiyo,iwe wanasikia au hawasikii.Wale wanaosikia lakini wanaweza wasisikie endapo pale mtu ameongea na kama ni ililetwa zawadi basi watapata wachache kwani kuna wale walio iona zawadi,wengine walisikia lakini wasijue ni zawadi gani na kuna wale walioitiwa zawadi ikiwa kila mmoja na yake,wale watakao pokea si tu ndio wale walio itiwa zawadi kwa maana ni za kwao.endapo mtu amekosa zawadi na aliitwa basi ajue ni huwa inatokea hiyo,hata maisha ya kwako si ya kufananisha na mwenzio.

unapopokea yakupasa upokea kwa shukrani,labda usiwe umezipenda zawadi zenyewe,na hata iwe hivyo zitakuwa za kwako tu,kinachotoka machoni hupita na moyoni kabla ya ruhusa ya kutoka nje,moyo unapopokea ni inapasa kuushirikisha na ubongo ili kuweza kujua kama ni imetambulika pia ni haki,moyo wa mwanadamu haufai kufuga uchafu labda uwe wa mtu wa namna hiyo.Mwisho ni matendo,yawe yanatoka moyoni,ikiwa moyo wako utajulikana kutokana na matendo yako jua unapotenda ni kama pale unapoongea,unapoongea una TOA yaliyopo moyoni na kuyaweka katika mazingira ya kawaida,ingawa hata ya moyoni ni ya kawaida kwa wengine katika mazingira hayohayo ya kawaida,ikiwa haionekani kwa macho lakini ni macho yaliyopelekea akilini,hivyo yapasa kupumzisha akili,kama vile unapopumua kwa kutoa na kupokea hewa ili uendelee kuishi,labda imekuwa nzuri kutoa kuliko kupokea ya kuwa unaotoka ni uchafu.

'ona sahihi,pokea vyema na utoe kwa moyo mmoja'.

By: Benson G.Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Monday, February 6, 2012

MWISHO WA KUTENDA,NI MAAMUZI.


Asichekwe yule atayetenda bila ya kujua  ni nini,ikiwa mtendaji anatakiwa kutenda zaidi ya vile bila ya yeye kujua mwenyewe..basi aachwe hivyo.Maana katenda,ya hivyo na yenyewe kaamua,na linalokuwa na msingi ni kuweza kuelewa pale vifanyikapo vitu,kwani na mara nyingine visieleweke,yaweza kuwa ni nusu au nzima iliyokuwepo katika matendo lakini msimamo wa jambo wenyewe umekuwa mgumu,mda mwingine kwa yale ya kiswahili huwa ni mazuri zaidi lakini yanaharibu yanapokuwa mengi,maamuzi ni zaidi ya mtu kutenda moja kwani yamekuwa mengi sasa,hapa tukatenda hivi na baadae kumalizia mengine,pale kwenye kumalizia si lazima yawe yalianza zamani mengine yakiwa ni marahisi,kama maamuzi yako yataamua kubaki,muda  hua ni kwenda mbele,kwani nao umeamua,tena shikilio la amuzi moja tu,la kwenda mbele.

Kipindi cha kujutia hakitakiwi endapo tu pale imetokea,kwani wengine hukaa kabisa na bila kuyakataza mawazo yao,kama mtoto anakatazwa kuchezea wembe ndio ije mtu mzima kwa mabovu?kama tutachukulia kila kitu kilivyo ndivyo kitakavyo kuwa kwani kilivyokuwa ndio kilikuwa kinaelekea hapo,hatua tusipoichukua ni tumetoa ruhusa kwani muda kazi yake ni lazima utumike,sio lazima wewe kwani ndiyo nani?alieutengeneza alikaa kila mda huohuo kuutengeneza,akijua itafika kipindi ataumaliza,tunapokimbilia kule tunamaana ya kuwepo huko,

Hatuwezi kuamua au kuacha wengine waende bila yetu kuamua tubaki,
Ijulikane hakuna wa kuishi maisha ya mwenzake,tofauti isiwe sababu ya kuishi tofauti,tena tusiamuliane,lile lililo la mmoja likafanyike katika yeye,maana mda utapita,sio tunahofia ingawaje hatulazimishi kuelewa ndio maana tukaamua tofauti,kuepuka ubishi na maamuzi yasiyo na msingi,ikiwa hatutaki ubishani usio na maana,maana itafika kipindi tuwaze vilivyopotea na wakati vizuri ndio hivyo vinajongea,ni ukaribu ambao katika moyo unaweza usikia,sio kama ule wa kunyata na miguu ukaishtukia,maana mda mwingine tusiseme tu maneno yasiyo na msingi,ikawe tutaelewana kila mmoja akawe na maana katika lake,akiwa katika mahala pake ndipo atakapofika.mahala pake pale alipo yeye kimawazo,akili na uhalisia wa mwili wake.

Ili matendo yapendeze ni kuna ulazima wa maamuzi sahihi kufanyika sasa,isiwe lazima kwa wale wachache,maana hao watakuja na kusema wanataka baadae,yule atakayebisha naomba nisiwe mimi kwani nitakuwa nje ya vile alivyoamua yeye,ikaja yeye au wewe umeamua jinsi vile nilivyogoma mwisho waweza kuwa mbali sana,kwani bado wengine tupo mwanzo na kinachosubirika hakieleweki kwani hatukueleweshwa kama haya ya muda huu yanahitaji maamuzi yake,wakiwa kama wao wanaogopa kutuambia kwani ni heli kumwacha nyani amalizie maembe katika mti kuliko kumshtua,maana mpaka kapanda aliyatafutia,

sijui nani amesikika akiakataza.eti yale walipasa kula wao,sijui walikuepo wapi maana muda wote mpaka yakaoza hawayakuona.binadamu tunalidhika na kile tunachokiona,wala hatunashida na kuridhika na kile tunachokitafuta,machache yawe ni majina na wala sio watu hapo tunaweza kupata hekima,maana tukijazana tutaonekana wazembe,ikiwa muda wote huo tulikuwa wapi?itakuwa zamu ya wengine bila ya kuamua,tuangalie kipindi maana huwa vinatofautiana dakika.

MAWAZO YASITUTENDESHE MAOVU, MDA MWINGINE MWANA ADAMU ANAPOKUWA HAJIELEWI.


By:          Benson G.  Makaya,

Tel:           +255714336657

Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...

Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...:  Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameis...

WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJIFUNZA JINSI YA KUTOKA KATIKA MATATIZO.


 Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameisibu jamii au mtu binafsi katika ufanisi wa kufanya mambo fulani,matatizo huwa hayaangalii hali halisi ya mtu husika endapo atakuwa na uwezo nayo ama la,matatizo ni maswali yanayoijia jamii,kwa upande mmoja ama mwingine matatizo huwa hayakaribishwi kwani yanaweza kuja magumu zaidi.Wakubwa ndiyo watu wanaoeleweka kuwa na matatizo ndani ya maisha ya mwanadamu kutokana na kile kitu tunachoweza kusema wao ndiyo watafutaji wa maisha kama inavyoeleweka,na  matatizo yanaweza kuwepo ni kutokana na ugumu wa maisha katika mawazo ya klila mtu pale inapomtokea,tukitolea mbali ya kiafya,watoto wamekuwa wakihesabika kama ni watu wasio na maatatizo na hata kama wanayo  ni si kwamba utofauti wa ukubwa na udogo..

Yale yaliyopita ndiyo haya yanayokuja,kwani ifikapo kipindi cha ukubwa,mtoto hufanya kile alichofanya kipindi cha utoto,kubaki kuwa mtoto kwa sababu umri ni unasogea.Wakaona tofauti ambayo hao ndiyo uliowatendea,ikiwa nikiwa litaendelea kusemeka kwa muda wote na ukawa mwingi bila hata ya mageuzi hapo kuna uwalakini wa mafunzo kutokupatikana kwa mtoto na hata kuendelea kukua na tabia kama hizo.Tabia chafu humnyima furaha mtu mwanadamu,Yule anayetenda uchafu ni sawa na mtoto maana haelewi lolote,akiwa anaelewa na kufanya maksudi basi tunaweza kukaa mbali na huyo mtu,kwani mwishowe atatufanyia maksudi na sisi wenyewe.

Wakubwa wengi wanaelewa ni kwa sababu ya kupita kwingi pia,watoto wakafundishwe na wakubwa,ikiwa wakubwa wanaofundisha na wao hawana uelewa basi hapa kwa mtoto itasemeka vile ya namna 'umleavyo ndiyo vile atakavyokuwa',ikawe sio ni  makosa zaidi ya lawama,na hii huwa haiji kwa mzazi kwani 'chanda chema'..!,hata kama tunalifahamu hilo lakini hatujui la kufanya,kwani akili  inaweza kumfanya akafanya kitu kama ni mtoto ndiyo naye akatambue yake,maana matendo sio ya kuchaguliana,zaidi tutaumizana kwa dhana za kwenda katika vifungo vya maisha,hata kupelekea vifo bila hali kukaa sawa,maana vinakuja vizazi sasa,vizazi vinavyoelewa yale ya kwao,maana hata nimesema yale ya kuwa ni vigumu ya kuyafahamu.

Yanayotushinda ni ya kufikiri na sio kutumia 'nguvu',ikiwa hivi hata kabla ya kutenda tungelikuwa tunajifikiria na kama yangetokea basi yangekua na upungufu kidogo  wa makali,ingawa kila mtu ana matatizo yake na ule uchungu anaufahamu yeye muhusika,ni sawa na pale inapokuwa mbaya kwa mwenzako mwengine naye akapata kuchekelea,si ya kwamba tu ni rahisi bali ni yametokea katika upande ambao yeye haumuhusu,na hata kama ulipita vibaya wao watataka kujua hilo, mtoto anapokuwa haelewi ni haki kumrekebisha ikiwa nawe mzazi umeelewa jambo,mtoto anapofanya kitu sio kama mtu mzima,mtoto ni kama mashine,mara nyingine ikaende yenyewe itakavyo au vile mzazi akaendesha,ikiwa ni kwa pupa bila uhangalifu basi mali hiyo si ya kukaa muda mrefu,hakuna kinachodumu kwa mateso zaidi ya kuteseka.

Bila ya kusahau maisha ya mtu anayatengeneza mwenyewe,ikiwa kama vile tukajenga nyumba,kununua magari na kusema tumefanikiwa,tukiwa na msingi ulio bora,msingi wa maendeleo kutoka kwa jamii na wakubwa wengine,mtoto anapaswa kuelewa pale anapoelekezwa,mtoto mwenye kiburi na sio usikivu ni Yule aliyefundishwa hivyo,akazembewa na akakua,tabia ni kama samaki,haswaa samaki  aliyekauka ndiyo hatakiwi hata kukunjwa,maana atavunjika na baadaye kuwa hasara.

"Mali ni mali tu hata ikiwa mbovu ili mradi uwe na umiliki nayo".


By:            Benson G. Makaya,
Tel:             +255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

Saturday, February 4, 2012

UZURI.



Katika kila kitu kuna sifa,ili kitu kiweze kujisikia kwamba ni kitu kinahitaji sifa,sio kila sifa ni nzuri,wala sio kila uzuri ni uzuri,inaweza ikawa ni hivyo kimaandishi na maneno yalivyo lakini katika maana ikatoka tofauti na uzuri ulivyo,uzuri  ni kwa uzuri tu.Katika yote mazuri huwa juu ya watu,kwa watu haipendezi kukawa na uzuri bila ya watu kuwa wazuri,ikiwa watu tunatakiwa kuendana na vile tuvifanyavyo au tunavyoweza kuvimiliki,ikiwa mtu ana chake tunaweza kutofautisha uzuri ikiwa na watu pia tuko tofauti,ikiwa katika mavazi na undani wetu zaidi,kwani sio wote wanaovaa vizuri kuonyesha vyao,ieleweke kuvaa vizuri sio kupendeza kwani wengine hufurahisha maumbile na mioyo kwa kuvaa wawezavyo ikiwa ni tofauti na uzuri,mavazi ndiyo yanayomfanya mtu aonekane katika namna inayompendeza yeye,mavazi ndio humtambulisha mwanaadam,tena tusifike mbali kwa kuulizia jinsia maana mavazi tunayaona wenyewe.

Wanaocheka sasa baadae wanaweza kutafuta wao,kama lengo ni kuuelewa uzuri.tukiwa tunajifahamu ni sisi tusitake na wengine watujue tusijifanye tupo juu wakati ni chini tusipopajua,tutaumia tukiwaza mazuri yamepita bila kuonekana wakati ni sisi wenyewe tulikuwa katika mabaya,ingawaje haikupendeza kwa mabaya kuongeleka pengine yangekuwa ni sawa na yale mazuri,labda utofautishaji tu,ni kama pale tunapoimba na kusoma na ifike kipindi tusielewe kama tulikuwa tunaimba ama tunasoma,kwani muda mzuri wa kufikiri yote hayo ungekuwa ule wakati hasa kabla ya kutenda,ingawaje sio kosa,na hakuna wa kumpa mwenzake lawama kwani kila mtu ni mzuri katika upande wake.

Lugha huwa zinachanganya sana,tatizo sio kusikika,tatizo sio njia ya mawasiliano,tatizo ni kusikia,kivingine tumeweza kusikika tofauti na vile maana ya mtu inavyoweza kumjia ikiwa tunasikia kwa lugha nzuri na safi,kama ni mbaya basi inapaswa kubadilishwa,maana hata sasa tumekuwa tukijitahidi kufahamu lugha nyingine,na hapa tuone uzuri,ya kuwa sio ile ya kwanza haifai bali na ya pili imekuwa bora,na ya tatu mwishowe tutakuja kugundua zote ni nzuri ila utofauti ni pale katika matumizi ya lugha hizo,ikiwa wengine wanatumia lugha chafu haimaanishi ni wachafu,labda lugha chafu ilitumika kumwambia mtu aache uchafu wake,lugha ile inaweza kuonekana ni nzuri kwa mchafu,yakuwa ni yake.

Nguvu haibadilishi rangi,kile kinachokuwa kibaya baada ya kupungua basi ni kizuri maana ni kimepungua tu,kumbe itafika kipindi tunaweza kujaza uzuri wetu hadi mioyoni,maana imekuwa kama ni sura tunazibadilisha,maumbile tunayaweka vile tunavyotaka wabaya waone vizuri,yaweza kuwa nasi ni wabaya  na tunatenda ili tuonekane tumefanya vizuri,lakini katika yote ni heli tumefanya,maana tusiogope kujifunza,ikiwa watu wanajenga madaraja sio kwa ajili wapiti peke yao,na kwa kile chochote kilicho kibaya kimetendeka nasisi tukajifunze juu  ya hicho,tusije kunywa sumu na haya maisha yalivyo magumu,maana siku hizi tunapona,tatizo linakuja katika kuendelea kuishi kwani mtu aliyekata tama anastaili falaja,lakini hawa wa kutoa faraja nao wamekuwa wafanyakazi,wanatafuta mshahara ingawaje mwanzo waliweza,na ndiyo maana ya kufika mpaka muda huu

Tuiache imani ibaki kama dhamana,ikiwa ni lazima turudi na kufanya yale mazuri ya maana.

By:      Benson G. Makaya,
Tel:     +255 714 33 66 57.

Friday, February 3, 2012

TUNAWAZA KUKOSA,TUSIPOJUA NI VIPI TUMEPATA..


Mawazo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,katika kupitia na kufanya vile au kile ilivyotakiwa.Kuna mengi ambayo mwanadamu anaweza kuwaza ikiwa  ya furaha,kejeli,chuki,upweke,na ya ki kawaida kabisa,mawazo huweza kurudisha na kukamilisha mipango au malengo ya mwanadamu ikiwa sahihi pale anapokuwa na utambuzi zaidi.

Kweli inapasa utofauti,ikiwa wengine wako kawaida basi na sisi tuwe,ili ikaonekane tofauti kwa wengin,labda tuseme tumepata ikiwa ni mvuto wa kupata na vingine,vile ambavyo yeyote yule anavyo kwa miliki ya uhalisia wowote,ikawe na maana ya maamuzi kwani yeyote anayeishi anayo mawazo,katika yote na hata yale asiyoyaomba,juzi hapa tulifanikiwa kama mvua isingeendelea kunyesha,kumbe hatukufanikiwa ila ilipasa kwa mwelekeo wa mienendo na shughuri zilizokuwa zikifanywa ziliashiria jambo,ikiwa kila mwanaadamu anaukaribu na yaliyobora yake,na sio kwamba tulifeli sasa,labda tumefauru tofauti,mda mwingine uhakika tunakuwa hatuna ni kwa sababu mengine mambo yanakuwa ni ya wengine,hatutaweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,hapa tutajiongezea mawazo,labda tuseme tumeweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,haya mengi sana yamechanganyika na ya watu..na hii ndio hufanya kushindwa,au hata kufauru ikiwa lengo,asiyependa upumbavu ndiyo yule anayetaka maana,kile kinachoingia hakiingii hivi hivi ni lazima kiwe na njia,na kama walisema tusikie na tukaziba masikio yetu basi hatutaelewa vizuri kwani yaliyosikika si yale yaliyoonekana mdomoni.

Katika kufanya ni kunatokea na kile unachokitaka kitokee,kama hatutajua ni namna gani tumevifanya basi hata tunapovipata tusiseme ni sisi tumefanya,maana wapo waliofanya ndio wakasema tugawane,kwa yule aliyegawa..ikiwa anaye gawa anagawa chochote kilichomzidia,ikiwa tumemwita mwenzetu mmoja na kibri ni lazima tuelewe kimetoka wapi,isije ikawa ni chetu maana chuki hugawika kwa upendo,tukawapa wengine wasiwe na hatia na kwa uzito tu ikawe kujibu kwa mitetemo,yule akaonekana muongo kwa kutetemeka,tuache kufanya kufahamu herufi kabla ya maneno,maana hayo yakiunganika yatatuangamiza zaidi.mwanadamu amependa basi amepata ikiwa alitafuta,tutafikiria yaliyo sahihi na mabovu yataendelea kuharibika,kwani malengo yapo,na nani anaweza kuyafuatilia,kwa kutokujua idadi maana tungesema ni mengi,au machache endapo yangehesabika,hivyi vyote hata ikawa hakuna lolote yaani hakuna cha kuhesabu hata vingi vikawa idadi,mwanzo ukigundulika mwishowe hueleweka,mtu anaposema pole sio kaumia yeye,

Yale yaliyopatikana sasa ndio yaliyokosekana mwanzo,yakiwa na ukosekanaji pale palipo na uhitaji,haya mengi sio ya kuyasumbukia labda iwe imeeleweka hayo ni mengi kiasi gani,tutasaidiana sana lakini tutafikia tofauti ikiwa usaidizi mwingine haufanyiki baada ya kusikilizwa,na ndio baadae tusiseme yale ni ya Fulani na haya ni ya nani,vichwa vitauma endapo dawa zitaonekana,maana bila hivyo tena wanaadamu watahitaji kula nyama ya  mwanadamu mwenzao,tunaweza tengeneza njia ya msitu wa miba,,haiwezi kuonekana njia ikiwa wale wengine walikataa kusikia,hatutaweza kuyafikia ikiwa tu tumekaa na kushindwa kutembea,yule anaye tembea anajua mengi,maana atakuja hata nyumbani akikwambia ana njaa,njaa haijatokana na kazi za huko ya kuwa mwanadamu ni lazima ale.labda iwe na awe ameelelewa hivyo.

Yawepo,yasiwepo yatatafutwa.
Lengo ni kuyapata!!

By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...