Saturday, June 16, 2012

PANAPO!!


Muda ukiwasili palipo inatakiwa kuelekea,
maana ikiwa ni kufanya hata kwa ilivyo kwa namna ya kuweza kuutenganisha muda ili uje kuleta maana,kauli ya kusema hapo ndipo palipo haikusemeka kana kwamba ndipo ilipo maana pale ukakamatana mashati na hata kushindwa kuelewa kwa yale yaliyopo na mengine yasiyozungumziwa,
pengine ikiwa hakuna aliye yafahamu kama mimi pia,au labda ukategemee ile  baadaye,
Ukaja kungoja nayo ikiwa  pameonekana pana uwepo,
maana watu kama wameamua tu kukaa hapo basi palipo kidogo au hata vile nafsi ikaridhika.

Mizunguko inatengeneza duara,
ya kuwa na maana ya kuacha kijiti na kukimbia sana kwanza  ukafika na kusema pale au hapa nimewahi,
hakuna gumu  lisilo tegemeka ikiwa kuzunguka imeamulika,hapo maana kuzunguka ni vigumu,
hivi pengine ndiyo watu wanaamua kupita njia zao.maana hizi zetu zimekuwa  za kuzunguka zaidi,
kwa kipimo cha uwingi unaweza kuleta maana ya umoja,
hii ikiwa unazunguka pamoja  na ukiwa hauna maana ya kujipa namba.
Muda huu  ulizungumziwa lakini kuna wale wapya,mapya yamekuja pia kwa ajili ya wale wa zamani,hii ikiwa wale wapya wamekuja na mapya na wale wa zamani wameendelea na yale ya zamani lakini yakionekana ni mapya,hapo ni matunzo sema sasa ukutane ubadilishane,japo sio kitu kikaonekana ila hata kimazingira kuonana,maana panapo kuwa na nyuki lazima asari kuwepo.

Pengine ukakutane pasipo nyuki wenyewe kuwa na asali,
hapa usilalamike na manundu,kwa wanaoweza kulala chini,isiwe walizoea na kuona raha,juu pia kuna raha,embu panapo fika na nyuki kuwasilli ubadilishane,hapo ujue aliye kuwa akilala kuwakwepa nyuki ni nani?maana palipo kwa zamani panaweza kujirudia tena.

KUWA(2)...


Mengine yanapokuwa yanakuwa sumu,
hapa kwa watoto na wenyewe wakaelewa,kwa vile imekuwa ni taarifa inayoonyesha kuwa kuna sumu hapo,na pale mtu anapotaka kukuwa zaidi ni pale anapoifatilia hiyo sumu,
pengine ni nini au pengine ikatumike kwa  matumizi yatakayoonekana ya kawaida ikiwa kabla ya matokeo,hiyo ikiwa sababu imetangulia au vile itakuja,
ni lazima tuwe na mategemeo,maana na yenyewe yanakuja kutokana na vile mtu anachofikiria,mtu anakuwa  kwa namna alivyojitambua yeye.

Tatizo linakuja pale furaha inapokuwepo,tena kwa vile ilivyo namna ya kuharibu hiyo furaha,labda tukajue tukuwe katika namna ipi,hata kama yale yanayonyanyuka ni kidogo lakini yapasa kuyafanya kila siku,kama inategemeka kwa  mtoto kuwa na tabia nzuri basi yapasa tuweze kumuheshimu,yaani hivyo navyo naye atakuwa na heshima ya namna hiyo,
Kila mara tunahitaji kukua katika jambo hata kidogo kidogo ikiwa kinachotakiwa ni kukua katika kila muda,muda mengine tukaeleweke hapa tumekuwa sana,maana yaweza kuwa ni haraka kwelikweli,lakini katika hilo furaha napo huwa kivyake,endapo kama akaulizwa kama ni nini kile mtu atapata ili ionekane amekuwa katika namna ya furaha.

Ikiwa imeonekana mtu hakui basi hapo italeta maana ya utegemezi na chuki ikiwa bado kukuwa hakujajulikana ni nini kinachohitajika,pengine mafanikio ndiyo yanayoleta furaha,lakini labda tukauliza kwa wale waliofanikiwa,endapo kama labda kunafuraha,hapo tutaielewa furaha,sio wote wenye furaha,sio wote wanaokuwa

Kama vile inavyosemeka kama unataka kukua katika namna unavyofikiri ni lazima kutumia pesa ya kuwa umeutaka utajiri,pengine katika kujua pesa ni nini maana mtu hawezi kuwa tajiri bila ya kujua hilo na thamani ya utajiri wake ni nini,pengine ikawe kwa kuuliza ni namna gani inaweza kufanyika vizuri,hapo tukiwa pia tunakuwa.

KUWA..


Hapa tunataka kukua,sio kutajirika bali kuwa na furaha,pengine inapasa kujua kama tunakuwa,haitaleta maana kwa mmoja kufanya kazi bila ya kuonekana na kukua,ingawaje tunaendelea kukua lakini  tusione kwa mengine tu kukua,pengine kama ilivyo kwa mfanyakazi anapoona kazi yake inakuwa,bila kujali ni imekuwaje,pengine kwa muonekano kwa vile unapoondoka uzuri basi iwe katika furaha,hapa ikiwa sio vyote vizuri vinauwezo wa kukua tena na furaha.

Katika kukua kuna  kuzoea,na endapo inafika wakati tunazoea yasiyo ya kuzoeleka hapo furaha itapotea,ikiwa kwa mmoja kama ni mke ndiyo wa kukupa furaha,ama ilivyo kwa biashara hapo tutakuwa,lakini katika kukuwa  haitokani na mtu zaidi ya mtu mwenywe,hata ikaonekana katika upande mmoja kwamba wachache au mtu Fulani amekuwa lakini japo kidogo hiyo nayo haimaanishi furaha zaidi kuwepo,zaidi tunaweza kusema katika mabadiliko ni lazima kufanyika kila siku,na hii ikiwa ni kuleta maendeleo katika kile chochote kinachofanyika.
Ikiwa kama ni kazi inatakiwa kukua katika mwonekano bora basi yapasa mtu kama mtu kukua  na kukuza yale unayoyafanya,hapa inawezekana watu wakataka kukua kwa haraka,hii ikiwa katika afya,kiakili,kimwili na mengineyo watu wayakuzayo,katika kujua kukua lazima kuelewa ni namna gani mtu anaweza kujikuza,sio ya kwamba Fulani amekuwa mnene basi ikaja na kueleweka kuwa amekua,kukua ni kubadilika,lakini  kukua ni kuwa katika namna ile mmoja anayoipenda,

Kwa mmoja anataka kuwa mwanamichezo na mwengine anataka kuwa mwanamichezo lakini hii ikiwa watakuwa wanamichezo wa michezo tofauti,na hapa ikaja maana ya kuweza kufundishana maana kwa wengine wametaka kukua lakini haijulikani ni namna gani ambayo inaweza kukamilika ya kufanya kama ilivyo kusudiwa,kazi yetu iwe ni kuingia na kutaka kukua zaidi katika ufanisi hasa kwa yale tuyafanyao.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS