Ni kauli vile mchungaji akimwambia mwanafunzi
wake,maana sio kila mchungwaji anachungwa na mchungaji mwema,wengine si katika
maovu bali ikiwa bado kutokujua kuelekeza,yaani wewe ng’ombe usipite hapo ni
lazima na viboko?maana bora hata Ukamsukuma pengine mnaweza kusikia yaliyo
karibu naye akalalamika tu,mnachapa sana ngombe hawa hii ikiwa ni
historia ya kwamba ni bora akawa anachapwa chapwa hapo ukiwa unataka ngozi ,yeye yule sasa
akiwa ameumbwa kama mwanadamu,ya kuwa na kizazi,yaani wote ni
binadamu..sishangai pale unawaita watoto mbwa,ni mbwa pekee anayeweza kumzaa mbwa.
Labda utafute madawa ya kukaushia ngozi,maana ng’ombe
wameskika wakilalama sana,ingali na viboko hivyo imekuja hata
wanyonyaji,hata muda wa malishoni kwa ngombe imekuwa taabu,fikiri
mchungaji anapolala hulala na usingizi upi na Yule ngombe alotoka machungoni
kwa viboko?maana hilo la mchungaji sijui ndiyo kuendeleza nchi ama ni
kutengenezana baadaye wakapata maziwa ndani yake,hutajua
maana ya kiboko cha mgongo ni uelekeo wa wapi zaidi ya kutia maumivu.
Katika lile linalomuumiza mwanadamu ndiyo lile au yale
yaliyotukia na furaha,maana hata mwisho wa sukari ni uchungu,pengine mchungaji
utuulize kuhusu utamu wa viboko hivi,maana si kulalama,ila isemekanavyo maumivu
yakizidi umwone daktari,sasa kama daktari amegoma haya maumivu yanatokea wapi ikiwa yule daktari
ni mwanafunzi,angelikuwa mwalimu asingekubali kuikosa heshima yake uelekezani,maana ni wito huo na mchungaji punguza namna ya nguvu zitumikazo kuchapia
ng’ombe wako,maana kuna wale wenye vichaa,wakiruka kile cha kukanyaga ni kesi yako mwenyewe,maana utaelezea
imekuwaje hata viboko ukashindwa kuchapa,au vilichapwa kwa namna ya
utofauti yaani yakaanza maumivu na kichapo kikaja baaadaye.
No comments:
Post a Comment