Mpira unapodunda sana,maana hata control zikakushinda,umekuwa
kitenesi hata katika namna ya kukidaka ikawa mzozo,pengine kwa ajili ya hawa unaowaona,hata ikawe hujui umeona nini namna gani ipi yaani mpaka ikaeleweka ile ni
kwa nguvu na nyenzake kwa akili,ikiwa hatujui imedunda ama imepaa maana nguvu ya juu hutegemea na ya
chini vile ilivyo kwa kipimo cha akili yakiwa yanashirikiana katika kuyasogeza marefu na mapana.
Vingi vinapaa lakini hatuelewi vinapaaje pengine ndiyo
vinavyotembea hivyo,vinadunda yaani,ilivyo muda usemekao zamani watu walikuwa
wakitembea miondoko Fulani ya mdundiko walionekana wahuni,muda huu imezoeleka
kwani unajidundia mwenyewe,wee dundaa na badaye utaeleweka maana
ndiyo itajulikana nguvu zako ulikuwa unazitumia katika upande gani,hakatazwi
mtu mara mbili asipoelewa ni aendelee na yanayompa nguvu kuyafanya kwa wakati
huo
Hata kumbe mipira mengine siyo yakuitumia hiyo wanasema
inachezeka hata mchangani,sijui kwa nini isingekuwa haiwezekani,kurudi ni
kufuta maana iliyopo ikiwa nguvu
iliyotumika katika kudunda kwa mara ya kwanza na kushindwa kufikia mara ya pili
kujaribu tena hapo unakuwa umefuta,sio adhabu ni mazoezi ya kuweza kumbe hata
mpira unapojaribu kudunda hutafuta mahala panapoleta maana,hapo utasikia ule
umetoboka,basi hapo ujue kuna mtu kakosa lengo.
Dunda ndugu usiogope uwanja wako,maana makelele tumeyasikia
na pengine yangekuwa kiburudisho hivyo vingine uviite kukua kwa lugha maana ukafikiri
yametokea kwenye nguvu ama pasipo tumia akili ,kwa sababu ya kudunda huanza chini ikiwa na lengo la kuelekea
juu au huanza juu ikiwa na lengo la kuelekea chini.Chagua namna unaweza,fanya vile unaweza.
No comments:
Post a Comment