Monday, February 6, 2012
Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...
Makaya's Forum: WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJI...: Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameis...
WATOTO WANAHITAJI KUINGIA KATIKA MATATIZO ILI KUJIFUNZA JINSI YA KUTOKA KATIKA MATATIZO.
Matatizo ni sehemu ya maisha,matatizo ni sehemu ya yale magumu yaliyo machache yanayohitaji kufanyiwa marekebisho kupitia ya kwamba yameisibu jamii au mtu binafsi katika ufanisi wa kufanya mambo fulani,matatizo huwa hayaangalii hali halisi ya mtu husika endapo atakuwa na uwezo nayo ama la,matatizo ni maswali yanayoijia jamii,kwa upande mmoja ama mwingine matatizo huwa hayakaribishwi kwani yanaweza kuja magumu zaidi.Wakubwa ndiyo watu wanaoeleweka kuwa na matatizo ndani ya maisha ya mwanadamu kutokana na kile kitu tunachoweza kusema wao ndiyo watafutaji wa maisha kama inavyoeleweka,na matatizo yanaweza kuwepo ni kutokana na ugumu wa maisha katika mawazo ya klila mtu pale inapomtokea,tukitolea mbali ya kiafya,watoto wamekuwa wakihesabika kama ni watu wasio na maatatizo na hata kama wanayo ni si kwamba utofauti wa ukubwa na udogo..
Yale yaliyopita ndiyo haya yanayokuja,kwani ifikapo kipindi cha ukubwa,mtoto hufanya kile alichofanya kipindi cha utoto,kubaki kuwa mtoto kwa sababu umri ni unasogea.Wakaona tofauti ambayo hao ndiyo uliowatendea,ikiwa nikiwa litaendelea kusemeka kwa muda wote na ukawa mwingi bila hata ya mageuzi hapo kuna uwalakini wa mafunzo kutokupatikana kwa mtoto na hata kuendelea kukua na tabia kama hizo.Tabia chafu humnyima furaha mtu mwanadamu,Yule anayetenda uchafu ni sawa na mtoto maana haelewi lolote,akiwa anaelewa na kufanya maksudi basi tunaweza kukaa mbali na huyo mtu,kwani mwishowe atatufanyia maksudi na sisi wenyewe.
Wakubwa wengi wanaelewa ni kwa sababu ya kupita kwingi pia,watoto wakafundishwe na wakubwa,ikiwa wakubwa wanaofundisha na wao hawana uelewa basi hapa kwa mtoto itasemeka vile ya namna 'umleavyo ndiyo vile atakavyokuwa',ikawe sio ni makosa zaidi ya lawama,na hii huwa haiji kwa mzazi kwani 'chanda chema'..!,hata kama tunalifahamu hilo lakini hatujui la kufanya,kwani akili inaweza kumfanya akafanya kitu kama ni mtoto ndiyo naye akatambue yake,maana matendo sio ya kuchaguliana,zaidi tutaumizana kwa dhana za kwenda katika vifungo vya maisha,hata kupelekea vifo bila hali kukaa sawa,maana vinakuja vizazi sasa,vizazi vinavyoelewa yale ya kwao,maana hata nimesema yale ya kuwa ni vigumu ya kuyafahamu.
Yanayotushinda ni ya kufikiri na sio kutumia 'nguvu',ikiwa hivi hata kabla ya kutenda tungelikuwa tunajifikiria na kama yangetokea basi yangekua na upungufu kidogo wa makali,ingawa kila mtu ana matatizo yake na ule uchungu anaufahamu yeye muhusika,ni sawa na pale inapokuwa mbaya kwa mwenzako mwengine naye akapata kuchekelea,si ya kwamba tu ni rahisi bali ni yametokea katika upande ambao yeye haumuhusu,na hata kama ulipita vibaya wao watataka kujua hilo, mtoto anapokuwa haelewi ni haki kumrekebisha ikiwa nawe mzazi umeelewa jambo,mtoto anapofanya kitu sio kama mtu mzima,mtoto ni kama mashine,mara nyingine ikaende yenyewe itakavyo au vile mzazi akaendesha,ikiwa ni kwa pupa bila uhangalifu basi mali hiyo si ya kukaa muda mrefu,hakuna kinachodumu kwa mateso zaidi ya kuteseka.
Bila ya kusahau maisha ya mtu anayatengeneza mwenyewe,ikiwa kama vile tukajenga nyumba,kununua magari na kusema tumefanikiwa,tukiwa na msingi ulio bora,msingi wa maendeleo kutoka kwa jamii na wakubwa wengine,mtoto anapaswa kuelewa pale anapoelekezwa,mtoto mwenye kiburi na sio usikivu ni Yule aliyefundishwa hivyo,akazembewa na akakua,tabia ni kama samaki,haswaa samaki aliyekauka ndiyo hatakiwi hata kukunjwa,maana atavunjika na baadaye kuwa hasara.
"Mali ni mali tu hata ikiwa mbovu ili mradi uwe na umiliki nayo".
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com
Saturday, February 4, 2012
UZURI.
Katika kila kitu kuna sifa,ili kitu kiweze kujisikia kwamba
ni kitu kinahitaji sifa,sio kila sifa ni nzuri,wala sio kila uzuri ni
uzuri,inaweza ikawa ni hivyo kimaandishi na maneno yalivyo lakini katika maana
ikatoka tofauti na uzuri ulivyo,uzuri ni
kwa uzuri tu.Katika yote mazuri huwa juu ya watu,kwa watu haipendezi kukawa na
uzuri bila ya watu kuwa wazuri,ikiwa watu tunatakiwa kuendana na vile
tuvifanyavyo au tunavyoweza kuvimiliki,ikiwa mtu ana chake tunaweza
kutofautisha uzuri ikiwa na watu pia tuko tofauti,ikiwa katika mavazi na undani
wetu zaidi,kwani sio wote wanaovaa vizuri kuonyesha vyao,ieleweke kuvaa vizuri
sio kupendeza kwani wengine hufurahisha maumbile na mioyo kwa kuvaa wawezavyo
ikiwa ni tofauti na uzuri,mavazi ndiyo yanayomfanya mtu aonekane katika namna
inayompendeza yeye,mavazi ndio humtambulisha mwanaadam,tena tusifike mbali kwa
kuulizia jinsia maana mavazi tunayaona wenyewe.
Wanaocheka sasa baadae wanaweza kutafuta wao,kama lengo ni
kuuelewa uzuri.tukiwa tunajifahamu ni sisi tusitake na wengine watujue tusijifanye
tupo juu wakati ni chini tusipopajua,tutaumia tukiwaza mazuri yamepita bila
kuonekana wakati ni sisi wenyewe tulikuwa katika mabaya,ingawaje haikupendeza
kwa mabaya kuongeleka pengine yangekuwa ni sawa na yale mazuri,labda
utofautishaji tu,ni kama pale tunapoimba na kusoma na ifike kipindi tusielewe
kama tulikuwa tunaimba ama tunasoma,kwani muda mzuri wa kufikiri yote hayo
ungekuwa ule wakati hasa kabla ya kutenda,ingawaje sio kosa,na hakuna wa kumpa
mwenzake lawama kwani kila mtu ni mzuri katika upande wake.
Lugha huwa zinachanganya sana,tatizo sio kusikika,tatizo sio
njia ya mawasiliano,tatizo ni kusikia,kivingine tumeweza kusikika tofauti na
vile maana ya mtu inavyoweza kumjia ikiwa tunasikia kwa lugha nzuri na
safi,kama ni mbaya basi inapaswa kubadilishwa,maana hata sasa tumekuwa
tukijitahidi kufahamu lugha nyingine,na hapa tuone uzuri,ya kuwa sio ile ya
kwanza haifai bali na ya pili imekuwa bora,na ya tatu mwishowe tutakuja
kugundua zote ni nzuri ila utofauti ni pale katika matumizi ya lugha hizo,ikiwa
wengine wanatumia lugha chafu haimaanishi ni wachafu,labda lugha chafu
ilitumika kumwambia mtu aache uchafu wake,lugha ile inaweza kuonekana ni nzuri
kwa mchafu,yakuwa ni yake.
Nguvu haibadilishi rangi,kile kinachokuwa kibaya baada ya
kupungua basi ni kizuri maana ni kimepungua tu,kumbe itafika kipindi tunaweza
kujaza uzuri wetu hadi mioyoni,maana imekuwa kama ni sura
tunazibadilisha,maumbile tunayaweka vile tunavyotaka wabaya waone vizuri,yaweza
kuwa nasi ni wabaya na tunatenda ili
tuonekane tumefanya vizuri,lakini katika yote ni heli tumefanya,maana tusiogope
kujifunza,ikiwa watu wanajenga madaraja sio kwa ajili wapiti peke yao,na kwa
kile chochote kilicho kibaya kimetendeka nasisi tukajifunze juu ya hicho,tusije kunywa sumu na haya maisha
yalivyo magumu,maana siku hizi tunapona,tatizo linakuja katika kuendelea kuishi
kwani mtu aliyekata tama anastaili falaja,lakini hawa wa kutoa faraja nao
wamekuwa wafanyakazi,wanatafuta mshahara ingawaje mwanzo waliweza,na ndiyo
maana ya kufika mpaka muda huu
Tuiache imani ibaki kama dhamana,ikiwa ni lazima turudi na kufanya yale
mazuri ya maana.
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66
57.
Friday, February 3, 2012
TUNAWAZA KUKOSA,TUSIPOJUA NI VIPI TUMEPATA..
Mawazo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,katika kupitia na kufanya vile au kile ilivyotakiwa.Kuna mengi ambayo mwanadamu anaweza kuwaza ikiwa ya furaha,kejeli,chuki,upweke,na ya ki kawaida kabisa,mawazo huweza kurudisha na kukamilisha mipango au malengo ya mwanadamu ikiwa sahihi pale anapokuwa na utambuzi zaidi.
Kweli
inapasa utofauti,ikiwa wengine wako kawaida basi na sisi tuwe,ili ikaonekane tofauti
kwa wengin,labda tuseme tumepata ikiwa ni mvuto wa kupata na vingine,vile
ambavyo yeyote yule anavyo kwa miliki ya uhalisia wowote,ikawe na maana ya
maamuzi kwani yeyote anayeishi anayo mawazo,katika yote na hata yale
asiyoyaomba,juzi hapa tulifanikiwa kama mvua isingeendelea kunyesha,kumbe
hatukufanikiwa ila ilipasa kwa mwelekeo wa mienendo na shughuri zilizokuwa
zikifanywa ziliashiria jambo,ikiwa kila mwanaadamu anaukaribu na yaliyobora
yake,na sio kwamba tulifeli sasa,labda tumefauru tofauti,mda mwingine uhakika
tunakuwa hatuna ni kwa sababu mengine mambo yanakuwa ni ya wengine,hatutaweza
kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,hapa tutajiongezea mawazo,labda
tuseme tumeweza kuyafuatilia ya wenzetu na yetu tumeyaacha chumbani,haya mengi
sana yamechanganyika na ya watu..na hii ndio hufanya kushindwa,au hata kufauru
ikiwa lengo,asiyependa upumbavu ndiyo yule anayetaka maana,kile kinachoingia
hakiingii hivi hivi ni lazima kiwe na njia,na kama walisema tusikie na tukaziba
masikio yetu basi hatutaelewa vizuri kwani yaliyosikika si yale yaliyoonekana
mdomoni.
Katika kufanya ni kunatokea na kile unachokitaka
kitokee,kama hatutajua ni namna gani tumevifanya basi hata tunapovipata
tusiseme ni sisi tumefanya,maana wapo waliofanya ndio wakasema tugawane,kwa
yule aliyegawa..ikiwa anaye gawa anagawa chochote kilichomzidia,ikiwa tumemwita
mwenzetu mmoja na kibri ni lazima tuelewe kimetoka wapi,isije ikawa ni chetu
maana chuki hugawika kwa upendo,tukawapa wengine wasiwe na hatia na kwa uzito
tu ikawe kujibu kwa mitetemo,yule akaonekana muongo kwa kutetemeka,tuache
kufanya kufahamu herufi kabla ya maneno,maana hayo yakiunganika yatatuangamiza
zaidi.mwanadamu amependa basi amepata ikiwa alitafuta,tutafikiria yaliyo sahihi
na mabovu yataendelea kuharibika,kwani malengo yapo,na nani anaweza
kuyafuatilia,kwa kutokujua idadi maana tungesema ni mengi,au machache endapo
yangehesabika,hivyi vyote hata ikawa hakuna lolote yaani hakuna cha kuhesabu hata
vingi vikawa idadi,mwanzo ukigundulika mwishowe hueleweka,mtu anaposema pole sio
kaumia yeye,
Yale yaliyopatikana sasa ndio yaliyokosekana mwanzo,yakiwa
na ukosekanaji pale palipo na uhitaji,haya mengi sio ya kuyasumbukia labda iwe
imeeleweka hayo ni mengi kiasi gani,tutasaidiana sana lakini tutafikia tofauti
ikiwa usaidizi mwingine haufanyiki baada ya kusikilizwa,na ndio baadae tusiseme
yale ni ya Fulani na haya ni ya nani,vichwa vitauma endapo dawa zitaonekana,maana
bila hivyo tena wanaadamu watahitaji kula nyama ya mwanadamu mwenzao,tunaweza tengeneza njia ya
msitu wa miba,,haiwezi kuonekana njia ikiwa wale wengine walikataa
kusikia,hatutaweza kuyafikia ikiwa tu tumekaa na kushindwa kutembea,yule anaye tembea
anajua mengi,maana atakuja hata nyumbani akikwambia ana njaa,njaa haijatokana
na kazi za huko ya kuwa mwanadamu ni lazima ale.labda iwe na awe ameelelewa
hivyo.
Yawepo,yasiwepo yatatafutwa.
Lengo ni kuyapata!!
By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657.
Wednesday, February 1, 2012
LENGO NI KUYAELEWA.
Lengo ni mambo au vitu ambavyo mwana adamu anavyomiliki katika akili au fikra yake ikiwa ni katika kuyakamilisha yale ambayo yana kusudi katika upande wake,katika kuelewa mambo au vitu ni lazima tujue ni sababu gani au ni katika namna gani ambavyo hivyo vitu tunavyovihitaji vinaeleleweka,ndipo hapo inahitaji wote tupaswe kuelewa,hapa tuelewe,ni lazima tuelewe vile vilivyo katika malengo yetu.
Katika baadhi ya mambo kuna yale mabaya na mazuri zaidi mengi hasa pale lengo linapotimia,yale mabovu ndiyo haya mazima katika upande mwingine,na yale tunayoyasema ni magumu ndio hasa yanayohitajika,ikiwezekana.tunayoyafikiria ni mengi mno,ikiwa yamo yote hasa zaidi tunapoyasema nayo tukayajumuisha,
Hii yote ni katika kuweza au kuelewa jambo au mambo,kadri siku zinavyoenda wanaadamu tunapaswa kujua zaidi,ikiwa ni kuongeza ufanisi na uwezekano wa nafasi endapo hata ikatokea isiwe ni tofauti ya vile malengo yetu yalipo,hata kama bado hatujapanga tufikiri nini kitakacho tusaidia,
Angalau kwa sasa ili na baadae wakafanye wengine mazuri yale.Lengo sio kubishana,sio tu moja na likaeleweka,tuyatafute,tusiyafuate,tuyatende au wengine ndiyo watende,ikiwa tu kwa umoja imeshindikana,tuone kwa yale yanayoelezeka na yasiyo elezeka,lengo ni kuyaelewa,yote yanafanana ingawaje yote yakawa ni tofauti,vile vilivyoumbwa kwa mfano ndiyo vile vinavyoleta utofauti yaani vile vilivyopita katika mikono yetu sisi wanaadamu na tukavisema kwamba ni vyetu,
Tukiwa na maana halisi ya chanzo na mahala Fulani yalipotokea,kimsingi ili kukuchanganya ni lazima tuelewe ni wapi palituchanganya,ili mwalimu asiwe na kazi kubwa ya kurekebisha au hata kuacha tuangamie ya kuwa tumekuwa wagumu sana kuelewa.
Usitumie nguvu wakati uwezo unao,ninaposema usitumie nguvu sio kwamba usishinde njaa wakati ni wazi uwezo hauna,kwani ikawa hivyo ni dhambi za kuiba zitaongezeka,na ikiwa lengo ni kuyaelewa kwa wenye dhambi hufurahia majumuisho,kwani yaweza kuwa utajiri pia.
Usitumie nguvu wakati uwezo unao,ninaposema usitumie nguvu sio kwamba usishinde njaa wakati ni wazi uwezo hauna,kwani ikawa hivyo ni dhambi za kuiba zitaongezeka,na ikiwa lengo ni kuyaelewa kwa wenye dhambi hufurahia majumuisho,kwani yaweza kuwa utajiri pia.
Kushiba kwa moyo ni kuridhika,kuelewa ni pale akili inaposhiba vyake pia,pale aelewapo mmoja sio lazima na wa pili afuate hivyo,tuogope wengine wasije wakazidisha maana na wao ni furaha yao kucheka wengine,kama inavyokuwa hakuna njaa inayoshindikana kwa tumbo,kwani inapozidi na yenyewe huuma,hapo ikiwa inataka kutambulika kwa lengo lake.
Tujenge madaraja yaliyo imara,kwa upande mmoja wengine tutadhani tutapita sisi tu,wengine labda watajenga ya kwao,ikiwa na sisi tuliyojijengea hatuwazi tumejenga wapi,isiwe tumeelewa tu utofauti wa tumbo na moyo kiuhalisia,ni kama pale iwapo shida na raha ikatokea,pale baadhi wakidhani shida za mmoja ndiye raha zake,ikiwa kwa wao hizo zinaweza kuwa ni raha,lakini yote ni malengo tu,na labda tufahamu shida zipo tu labda iwepo kuna unafuu.
Kwa yale moyo uyapatayo ni rahisi zaidi kuliko haya mengine niyasemayo,tusifahamau pale tunapohitaji mabadiliko,fahamu ziwepo na hasa zikawe ni suluhisho pale mabadiliko yanapotokea kwani tuna haki ya kuyafahamu mabadiliko hayo kabla,tunapojua tunaelewa,kuelewa sio kufahamu,kufanya ya kuwa vile si hivyo,au hivi ilivyotakiwa lengo ni kuyaelewa,yote ni mambo,ule uzuri au ubaya ni utofauti,kama vile chafu na safi,au kueleweka ama sio kueleweka,chaguzi ni lako katika nzuri au tofauti,chafu au safi ikiwa ni kueleweka ama la.tufanye yataeleweka tu,kwa Yule aelewaye yawe yanaeleweka tu.
Kwa yale moyo uyapatayo ni rahisi zaidi kuliko haya mengine niyasemayo,tusifahamau pale tunapohitaji mabadiliko,fahamu ziwepo na hasa zikawe ni suluhisho pale mabadiliko yanapotokea kwani tuna haki ya kuyafahamu mabadiliko hayo kabla,tunapojua tunaelewa,kuelewa sio kufahamu,kufanya ya kuwa vile si hivyo,au hivi ilivyotakiwa lengo ni kuyaelewa,yote ni mambo,ule uzuri au ubaya ni utofauti,kama vile chafu na safi,au kueleweka ama sio kueleweka,chaguzi ni lako katika nzuri au tofauti,chafu au safi ikiwa ni kueleweka ama la.tufanye yataeleweka tu,kwa Yule aelewaye yawe yanaeleweka tu.
Lengo hili halikuwa langu,ikiwa limeonekana katika upande mwingine ni lazima uelewe maana usibishane ingawaje hatujaambiana,hili au lile liwe lengo letu tena tulilolikusudia,lengo letu linapokuwa moja si kwamba wewe utafanya vile mimi nitakavyo fanya,au tutafanya pamoja ikawe mwalimu akasema Fulani ame nakili kwa mwenza,tuyaelewe na tuone utofauti wa malengo yetu.
By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714 33 66 57.
By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714 33 66 57.
Tuesday, January 31, 2012
MENGI YAMEDONDOKA.
Ikiwa ni kutoka juu hadi chini,chini hadi chini kabisa au juu kwa juu huko huko,pale pasipo kuwa na uangalifu mzuri na mara nyingine ukaseme ni bahati mbaya,Yaliyokuwa yameshikiliwa ndio sasa yanahitaji msaada,maana hata wale walio kuwa na nguvu wameamua kuachia,yanayodondoka huwa hayasemi zaidi ya yale yanayoshindikana.Kwa nini kama kudondoka tusingedondokea juu huko huko,maana yule anayedondoka akiwa chini yeye hubaki pale,na kwa yule aliye juu ikawe ni mshangao mkubwa tena.
Ikiwezekana umesahau maneno yetu ulipokuwa mtoto tukiyasema na ndiyo maana imefika muda shikamoo zimezidi,sio kwa utani lakini muda umesogea,angalia tusije kuwa sisi ndiyo wazee,kwani watoto wanazo zao,na kamwe mtoto hawezi kulingana na mtu mkubwa ikiwa hata anaumwa,ukumbuke ile ngoma ya watoto inakesha kwa namna yake,yale ya zamani yamekuwa ya kisasa zaidi,hawakua na mambo ya ujana ambayo yapo katika kipindi hichi na yanamaliza nguvu ya taifa,ingawa ilikuwa ni kipindi cha ujana wao.
kwa sasa wazazi wanashindwa kufanya lolote na watoto kukua katika namna wawezavyo wao,hatukatai mtu kuwa mzungu,kuwa mwarabu,lakini ni lazima mtu anaye taka kuwa katika jamii tofauti na yake ajielewe yeye,ajitambue ya kuwa hakuna muda wa kufananisha zaidi ya kufanya,yakuwa mwanzo unaonyesha mwisho upo katika namna zipi,njia hufanya mwanzo kuwa mwisho mara nyingine,kwani inapaswa kuurudia kwa makosa machache yanayotusibu katikati ya safari yetu ya maisha kabla hatujayamaliza.
Wale wanaotembeza sio wale waliopendeza,ikiwa haikusemeka hivyo,uzuri kila mtu anao wake,tukiambiana watu ni wabaya basi itakuwa ni vita ya kuutaka uzuri kwa lazima,tukiwa tunatoka safari tuangalie mizigo yetu tusije kuisahau nje,maana na wachache tukaonekana tumependeza wanajua tunapesa,tumefanikiwa kumbe ni tumefanya ili kuweza kutembea vyema,maana wachache hawachelewi kukwambia umepungukiwa akili,ila wakifanya wazee si mbaya kwani ndiyo walivyokuwa navyo na walitembea hivyo.
Wale wanaotembeza sio wale waliopendeza,ikiwa haikusemeka hivyo,uzuri kila mtu anao wake,tukiambiana watu ni wabaya basi itakuwa ni vita ya kuutaka uzuri kwa lazima,tukiwa tunatoka safari tuangalie mizigo yetu tusije kuisahau nje,maana na wachache tukaonekana tumependeza wanajua tunapesa,tumefanikiwa kumbe ni tumefanya ili kuweza kutembea vyema,maana wachache hawachelewi kukwambia umepungukiwa akili,ila wakifanya wazee si mbaya kwani ndiyo walivyokuwa navyo na walitembea hivyo.
hata ikiwa akaja mgeni na kubisha hodi,mshikishe jembe huyo,mwambie ndani wasafiri walipaki vyao na wamelipia pesa nyingi ikiwa hawataki usumbufu,tukalime na hao wageni maana si wamekuja na majembe wenyewe?angalia unapofundishwa na mwalimu mgeni,kwani lazima ujiulize wa kwanza yupo wapi?kama kashindwa uangalie Yule aliyeweza,muda unapita na utakao fuata ndiyo wetu maana sisi ndiyo wazee,na usikubali kuacha mafao maana utasumbuliwa tu,taarifa za mbali zinaweza kuja zikiwa zinatuhitaji na lazima ujiandae kwani ni sisi wa kuongoza,umwangalie sana Yule mzazi wa mtu mwingine anapomwambia mwana wa mwingine kuwa hana adabu,ikiwezekana ijulikane kama adabu yake ni nzuri ili tuache za wazazi wetu.
‘sio kila kitu wazee’.
‘sio kila kitu wazee’.
By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com
NAMI NIWEMO.
Ikiwezakeana sura yangu iwekwe
kwa kaisari,kilichoniweza ni kile nilichokiongeza,cha kwanza nilikuwa nacho
mapema,ndiyo maana ya kuja na kusema,ni maongezi nikifikiria,pembeni haina haja
ya kukuitia,tuongee pamoja tuelewane tusije jutia,ni mjita wa suguti mara
musoma nimetokea,muda wote haina haja ya kuitajia,tumefanya vingine kwa
waliotofauti ikaeleweka,wale wachache..tusiotaka hongera kwa makosa yetu,kila
mtu anayafahamu ya kwake!! inanikumbusha kulee,kule kwenye sura yangu,angalau
basi tufikiriane ndugu zangu,labda nimesema hivyo hata nikiwa nina nia mbaya,wala
si uongozi wangu utakuwa mzuri,ubaya wangu hautadhuru lolote ni mimi na uongozi
wangu.Labda tufahamishane kwa hili,nikipata nafasi ya kupiga picha ntapiga kama
ile katika shilingi mia,moja ile ya upande fulani,muda unavyoenda tutachaguliwa
wake ,maana naona nguvu zetu zinaisha,viwili kwake chake,moja kwetu vyetu,hii
ni mbaya ikitokea kwetu,labda tusijue nini maana lakini ombi langu ni
hilo,moja..hili la sura yangu kuwapo pale,najua ntaweza ikiwa sijafika hapo
waje wawaambie,zikiwa kama hadithi kwa wale watakao chelewa sana.
Tusitake maisha ya kurudi utoto
bila kujua tutawarudishia wapi watoto wetu,maana tuwape na njia ili wale wenye
watoto wengi wengine wajisaidie,hata kama ni njia na zenyewe zimekuwa ni
nyembamba zikihitaji nguvu ili kupita,tukisema kukonda ili kupita vyema wao
wanasema tumepata ugonjwa wa mawazo na tukinenepa inakuwa vibaya kwa
mapitio,itabidi tutafute njia yetu.kilichozidi zaidi lazima kiwe na sifa yake
iliyoongezewa zaidi,ni kweli maisha yalikuwa ni magumu lakini hii iliyopo ni
zaidi,hakuna asiyejua kuishi labda asikuelezee,yale tunayoyataka yataleta
maafa,nikiwa sijui maana yake labda,niseme maswali ya dunia nakumbuka kauli hii
nilipoulizwa kwa nini maswali ya dunia jibu likaja ya kuwa hilo nalo ni swali
la dunia,hatuwezi kwenda na maswali huku majibu tumemwachia mwengine,maana kama ni
shule zimekuja hadi za lugha tofauti,hili si kosa kwani shule ni kujifunza na
endapo unataka kujifunza unatakiwa kujifunza kitu ambacho wewe unataka
kujifunza,haina mshangao ila ni ya kustaajabisha sana shule watu tumeenda za
nini?maana ionekanavyo tu wengi sana tumesoma na maswali yakiwa hayana majibu.
Labda kama sijamaliza lengo
lieleweke,maana inaweza kutoka picha tofauti na ndugu zangu wakasema 'tulijua
sisi' ,wengine humaanisha vyao daima,bila ya kumjali mlengwa,hakika matangazo
tunayaona,tumejitahidi kulemba sura zetu zikiwa na ujumbe mbalimbali
tofauti,hiyo yote ikiwa ni kushawishi,hapa napo tunashawishi lakini imekuwa ni
namna tofauti,kwani lengo hapa ni uwepo wa sura tu mahara pale,pengine hata nkikumbuka kwa kipindi kile waswahili ndugu zangu walikuwa na usemi juu ya
upendo ingawa unawezekana bado ukawepo,nakupenda sana nikinywa maji nakuona
kwenye glass,yaani mzungu hapa anakwambia ‘indeep’,huu ni undani..ingali bado
tunaendelea kuishi basi ukawe undani wangu mwingine.tumalize na hili...
‘Ikiwezekana sura yangu ikae katika shilingi’
By: Benson G. Makaya,
Tel: +255
714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com
NB: 10
Outfits Parents Love But Kids Hate
http://www.enannysource.com/blog/index.php/2011/12/11/10-outfits-parents-love-but-kids-hate/
http://www.enannysource.com/blog/index.php/2011/12/11/10-outfits-parents-love-but-kids-hate/
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
POPURAL POSTS
-
Makaya's Forum: HASIRA YAKO : Unakasirikia maisha yako wengine wakiwa na furaha,ikiwa lengo si kutaka kuijua furaha ya mwengine bali kuj...
-
Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...
-
We do and say a lot, being that it brings an understanding or misunderstandings within the community, it is likely that we have as y...
-
Think, do , receive.... many we receive thanks, Being after something done, If not assume thanks focused on how, whether for evil, b...
-
When I was a child, I saw how a magnifying glass could burn a piece of paper, when the rays of the sun were focused through it. The fir...
-
Katika malengo yanayomfanya mwanadamu kuweza kuishi pengine ikiwa ni kwa muda fulani ama ki namna ilivyo kwa mtu akataka furaha iliy...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Not to be laughed whatever somebody does...Doing, Without knowing what it is! If the executive is supposed to do beyond what would...
-
Choice lays with the person and his/her decisions, And when we include a person then it is his/her choice, The knowledge and ability,...
-
Hata usipozungumzia utaifa lakini kiwango cha maisha ya mtanzania ni kidogo sana,hapa nikiwa nazungumza na watanzania wale walio na nd...