Tuesday, January 31, 2012

MENGI YAMEDONDOKA.


Ikiwa ni kutoka juu hadi chini,chini hadi chini kabisa au juu kwa juu huko huko,pale pasipo kuwa na uangalifu mzuri na mara nyingine ukaseme ni bahati mbaya,Yaliyokuwa yameshikiliwa ndio sasa yanahitaji msaada,maana hata wale walio kuwa na nguvu wameamua kuachia,yanayodondoka huwa hayasemi zaidi ya yale yanayoshindikana.Kwa nini kama kudondoka tusingedondokea juu huko huko,maana yule anayedondoka akiwa chini yeye hubaki pale,na kwa yule aliye juu ikawe ni mshangao mkubwa tena.

Ikiwezekana umesahau maneno yetu ulipokuwa mtoto tukiyasema na ndiyo maana imefika muda shikamoo zimezidi,sio kwa utani lakini muda umesogea,angalia tusije kuwa sisi ndiyo wazee,kwani watoto wanazo zao,na kamwe mtoto hawezi kulingana na mtu mkubwa ikiwa hata anaumwa,ukumbuke ile ngoma ya watoto inakesha kwa namna yake,yale ya zamani yamekuwa ya kisasa zaidi,hawakua na mambo ya ujana ambayo yapo katika kipindi hichi na yanamaliza nguvu ya taifa,ingawa ilikuwa ni kipindi cha ujana wao.

kwa sasa wazazi wanashindwa kufanya lolote na watoto kukua katika namna wawezavyo wao,hatukatai mtu kuwa mzungu,kuwa mwarabu,lakini ni lazima mtu anaye taka kuwa katika jamii tofauti na yake ajielewe yeye,ajitambue ya kuwa hakuna muda wa kufananisha zaidi ya kufanya,yakuwa mwanzo unaonyesha mwisho upo katika namna zipi,njia hufanya mwanzo kuwa mwisho mara nyingine,kwani inapaswa kuurudia kwa makosa machache yanayotusibu katikati ya safari yetu ya maisha kabla hatujayamaliza.

Wale wanaotembeza sio wale waliopendeza,ikiwa haikusemeka hivyo,uzuri kila mtu anao wake,tukiambiana watu ni wabaya basi itakuwa ni vita ya kuutaka uzuri kwa lazima,tukiwa tunatoka safari tuangalie mizigo yetu tusije kuisahau nje,maana na wachache tukaonekana tumependeza wanajua tunapesa,tumefanikiwa kumbe ni tumefanya ili kuweza kutembea vyema,maana wachache hawachelewi kukwambia umepungukiwa akili,ila wakifanya wazee si mbaya kwani ndiyo walivyokuwa navyo na walitembea hivyo.

hata ikiwa akaja mgeni na kubisha hodi,mshikishe jembe huyo,mwambie ndani wasafiri walipaki vyao na wamelipia pesa nyingi ikiwa hawataki usumbufu,tukalime na hao wageni maana si wamekuja na majembe wenyewe?angalia unapofundishwa na mwalimu mgeni,kwani lazima ujiulize wa kwanza yupo wapi?kama kashindwa uangalie Yule aliyeweza,muda unapita na utakao fuata ndiyo wetu maana sisi ndiyo wazee,na usikubali kuacha mafao maana utasumbuliwa tu,taarifa za mbali zinaweza kuja zikiwa zinatuhitaji na lazima ujiandae kwani ni sisi wa kuongoza,umwangalie sana Yule mzazi wa mtu mwingine anapomwambia mwana wa mwingine kuwa hana adabu,ikiwezekana ijulikane kama adabu yake ni nzuri ili tuache za wazazi wetu.
‘sio kila kitu wazee’.


By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...