Tuesday, January 31, 2012

NAMI NIWEMO.




Ikiwezakeana sura yangu iwekwe kwa kaisari,kilichoniweza ni kile nilichokiongeza,cha kwanza nilikuwa nacho mapema,ndiyo maana ya kuja na kusema,ni maongezi nikifikiria,pembeni haina haja ya kukuitia,tuongee pamoja tuelewane tusije jutia,ni mjita wa suguti mara musoma nimetokea,muda wote haina haja ya kuitajia,tumefanya vingine kwa waliotofauti ikaeleweka,wale wachache..tusiotaka hongera kwa makosa yetu,kila mtu anayafahamu ya kwake!! inanikumbusha kulee,kule kwenye sura yangu,angalau basi tufikiriane ndugu zangu,labda nimesema hivyo hata nikiwa nina nia mbaya,wala si uongozi wangu utakuwa mzuri,ubaya wangu hautadhuru lolote ni mimi na uongozi wangu.Labda tufahamishane kwa hili,nikipata nafasi ya kupiga picha ntapiga kama ile katika shilingi mia,moja ile ya upande fulani,muda unavyoenda tutachaguliwa wake ,maana naona nguvu zetu zinaisha,viwili kwake chake,moja kwetu vyetu,hii ni mbaya ikitokea kwetu,labda tusijue nini maana lakini ombi langu ni hilo,moja..hili la sura yangu kuwapo pale,najua ntaweza ikiwa sijafika hapo waje wawaambie,zikiwa kama hadithi kwa wale watakao chelewa sana.

Tusitake maisha ya kurudi utoto bila kujua tutawarudishia wapi watoto wetu,maana tuwape na njia ili wale wenye watoto wengi wengine wajisaidie,hata kama ni njia na zenyewe zimekuwa ni nyembamba zikihitaji nguvu ili kupita,tukisema kukonda ili kupita vyema wao wanasema tumepata ugonjwa wa mawazo na tukinenepa inakuwa vibaya kwa mapitio,itabidi tutafute njia yetu.kilichozidi zaidi lazima kiwe na sifa yake iliyoongezewa zaidi,ni kweli maisha yalikuwa ni magumu lakini hii iliyopo ni zaidi,hakuna asiyejua kuishi labda asikuelezee,yale tunayoyataka yataleta maafa,nikiwa sijui maana yake labda,niseme maswali ya dunia nakumbuka kauli hii nilipoulizwa kwa nini maswali ya dunia jibu likaja ya kuwa hilo nalo ni swali la dunia,hatuwezi kwenda na maswali huku majibu tumemwachia mwengine,maana kama ni shule zimekuja hadi za lugha tofauti,hili si kosa kwani shule ni kujifunza na endapo unataka kujifunza unatakiwa kujifunza kitu ambacho wewe unataka kujifunza,haina mshangao ila ni ya kustaajabisha sana shule watu tumeenda za nini?maana ionekanavyo tu wengi sana tumesoma na maswali yakiwa hayana majibu.

Labda kama sijamaliza lengo lieleweke,maana inaweza kutoka picha tofauti na ndugu zangu wakasema 'tulijua sisi' ,wengine humaanisha vyao daima,bila ya kumjali mlengwa,hakika matangazo tunayaona,tumejitahidi kulemba sura zetu zikiwa na ujumbe mbalimbali tofauti,hiyo yote ikiwa ni kushawishi,hapa napo tunashawishi lakini imekuwa ni namna tofauti,kwani lengo hapa ni uwepo wa sura tu mahara pale,pengine hata nkikumbuka kwa kipindi kile waswahili ndugu zangu walikuwa na usemi juu ya upendo ingawa unawezekana bado ukawepo,nakupenda sana nikinywa maji nakuona kwenye glass,yaani mzungu hapa anakwambia ‘indeep’,huu ni undani..ingali bado tunaendelea kuishi basi ukawe undani wangu mwingine.tumalize na hili...

‘Ikiwezekana sura yangu ikae katika shilingi’

By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com


No comments:

ELEWA 2

  Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye na kukataa kuelekea hata kwa ku...