Leo umetaka kuongozwa na nani maana inaashiria mfumo
unapajua unapoelekeza ,pengine ikawa
vyote ni vya kijani,kwani kwa vile vinavyosemeka vikiwa na lengo la kufanyika
hali kadharika ikawa ikifikirika tumbo la kila mmoja ili ikaeleweka
imependeza,maana kwa sasa usipofanya wewe utakufa masikini,hivyo watu wameamua
kunyanyuka na kusema nataka bila ya kujua shauku hasa la mioyo yao,maana siyo
kila njaa inahitaji chakula,fikiri umeijua njaa yenyewe?pengine hata na chakula
chenyewe kiwe tofauti basi.
Ni wazi zinalika,ni wazi utaifa unapotea kwa sisi
wenyewe.ikiwa ni kweli wananchi wapo makini,ikiwa ni kweli viongozi wapo
makini,hapa hakuna aliyemkosea mwenzake kwani hata Yule anayeongozwa afikirie
kuongozwa,zaidi ya kutaka kuongozwa vile unavyotaka ni kutaka kuwa
kiongozi.kama umelima mchele na umevuna mahindi jua shamba si lako,na kama uliweka alama ya kusema usipotee basi mshukuru mungu wako kwa maajabu ,maana
yatakuwa yamtendeka.la sivyo badili mfumo wa kulima.
Mashati hata tukishikana yatachanika na tutabaki watupu,bila
kuelewa mfumo haitawezekana kwenda mbele wala nyuma,wewe ambaye upo katika
mfumo ndiye utafahamu maana na mfumo wake unaweza kuwa umeelekea kule
unapouelekeza au ulipoelekezwa bila kujua kama unaendana na mfumo wako,maana
pengine kwa wengine ikawa ni lawama kwa namna ya hali ilivyo,hizi siasa
zinaweza kubadili hata mfumo wa maisha yako.Wenzetu wanatumia
lugha’system’kukiwa kuna kila aina ya maana ya neno hilo kutokana na yaliyopo.
BADILI MFUMO WAKO BADILI MATENDO YAKO
BADILI MFUMO WAKO BADILI MATENDO YAKO
No comments:
Post a Comment