Maneno hayana pa kutokea kama sio mdomoni,ilivyo
maandishi kwa kuandikwa,pengine ukiwa unataka haraka kuelewa nini maana ya
ulimi kabla ya kuufahamu mdomo,kile kinachotoka katika ulimi kinapita mdomoni
pia,maana mdomo umejawa na yaliyo katika ndimi ni yanapita tu,
Ni maneno ya wasanii,wasanii wachache
wanaofundisha wakitaka kueleza,mimi ni mlinzi ya kuwa nalinda. na Yule
anayemuongoza mlinzi yeye sijui anafanyaje..naogopa kugeuza ulimi wangu,kwani
sijasema nimeshindwa kulinda.Haya hayajalambwa labda uyaone ya pembeni,
Vyovyote iwe ikataje kwa namna iliyozoea,naupenda ulimi wangu kwa
uvumilivu
wake,nikikumbuka mara ya kwanza nikipata pilipili,maana nao ulipokea
ukisema haya ni mafunzo,tena elewa..asikudandanye mtu hili limeshindikana,maana
ulimi unaweza kuwa umegeuka,hata usijaribu kugeuza ikiwa hautaki kusema tofauti,maana hata mpaka sasa umedanganywa sana na kuambiwa samahani ni ulimi tu..
Unapofanya meno yako yafurahi ni pale uunapoulaza ulimi
wetu,kweli hata mkafurahi wengine na wakapewe shida nyingine,maana ulimi kazi
yake kuleta maneno.wacha waseme ,watasema mchana usiku watalala,akianza kumung'unya tu ujue ulimi unaelekea maala pake.
ukikaa kimya inaeleweka umekubali,asikukubalishe mtu asijue ni kwa shida ama ni kwa raha tu.
Maana meno yamefanya kazi sana,hata wakasema wasisikike,tena ukifikiri
ni nini kama sio ni wewe mwenyewe umeamua,hapo unataka kusema kama unataka
kusema utakatwa ulimi,sijui ili meno yasichoke na vingine tunadanganyana
sana,vingine havina maana.
No comments:
Post a Comment