Saturday, September 29, 2012

MADHALA...


Tusidhulike tena ya kuwa  mandhali zimetengenezwa,pengine ikiwa ni mipango tangia ya mababa zetu kwani ilivyo ki enzi za zamani babu anaweza asihusike sana,vingine vikija katika namna ya kusaidia kipato,vingine vikija katika namna ya kusema haya ni maisha tu,maana ikiwa kuna kujifariji ili ieleweke kwamba hakuna madhala ndani yake.

Mengi yanayopoteza muda huwa na muda wake wa kurudi.kwani mwanzo wa kitu ndiyo kuumbika kwake ikiwa haijatokea kuwa na mwelekeo wa kuleta madhala kwani kama ni mpofu wa macho basi atatengenezewa namna ya kutokudhulika ikiwa mtu mwenyewe umejua kudhulika,mambo na vitu vinavyoendelea ni mlengo wa wewe mwenyewe,kwani ikiwa kuna kufa haustahili kukaa karibu na madhala.

Pengine yafanyike taratibu,ikiwa tunajua kila starehe ina mtu wake basi  ni kama kumpongeza mwizi anapoiba vizuri,na kama ni mlevi basi aje atuimbie kwa maneno atayozungumza,pengine ataleta radha iliyo tofauti,imekuwa ni kama  kioo kwa vile watu kwenda na kujiangalia,yaani kuweza kuongea si namna ya kuongoza wanaoongea..isije onekana kujaribu wakati kuna uwezekano.pengine tusifanye ya kuwa tunataka kujaribu.

Wednesday, September 26, 2012

UKAMILIFU..


Kuna ulazima wa kuchagua wewe ni nani ikiwa unataka kukamilika,pengine ukiwa na malengo,mipango yako iliyokamilika na ikitakikana kufanyika ama imeshafanyika na wanadamu kuona namna ya vile ilivyotendeka ikiwa wao ndiyo huleta makamilifu ya sifa,chako ni chako,kichafu na kisafi ni vyote vilivyo kamilika ikiwa ni katika namna inayotakiwa,kwani pale anapopenda mmoja mwengine anaweza penda hapo ilipo ya kuwa ni katika kukamilisha matokeo.

Mabaya huwa ni mazuri kwa kuwa yameweza kuwa na uwezo wa kuwa mabaya .kukamilika ni namna ya kitu kilivyo,na endapo hakijakamilika ni lazima kupeana namna ili inapokuwa inataka kukamilika iweze kukamilika katika namna na maana ya vile ilivyo.pengine ni utofauti unaofanya mtu asiwe na ukamilifu,akiamini yeye ndiyo yeye,kwa kuweza jambo na wengine kushindwa.hayajawa mashindano maana hata muda wa mchezo wenyewe unapangwa na  wewe mwenyewe.

Maisha yanajengengeka na namna ya ukamilifu wako,ikiwa haujatimiza jambo na unahisi ya kwamba si mkamilifu basi jaribu kukamilika kwa kuweka kile unachokihitaji kukifanya kuwa kama ni baba au mama maana hakuna pengine pa kuwapata,si ndiyo ikawe fulani ni mtoto wa fulani na fulani,si vile ikawa haieleweki  kwa kutokukamilisha uzazi,na ki ubainadamu wengi hupenda kujikamilisha na kutokukamilisha ya wengine.wakijua yao yamekamilika.

UNAPOIANZA SAFARI


Kupitia kutumika ama ilivyo kama inasemekana kuishi ikiwa ni katika ngazi tofauti mwanadamu unapokuwa katika kuelekea mafanikio ya safari yako,mengi husemeka na wengi pale mwanzo unapoanza,ikiwa ni maisha yako inakupasa kabla ya kujipa tumaini la kujua kama ipo siku,kama mambo yalikuwa tofauti basi yataenda utakavyo,maana nzuri yangu mimi ndiyo inayoweza kutuletea ugomvi hasa ikaonekana kama nilipo ni mwanzo.

Kila mtu ana lake la mwenzako haipaswi kulinyemelea,safari ni yako hasa zaidi kama imetokea umeifanya bila kujua unashuka kituo gani ni bora kuuliza katika Yule unayeona umefanana naye kimaisha,pengine ukiwa unapata vyanzo vya kukufanya uweze lakini ‘kwa kuwa fulani kasema basi ile itakuwa mbaya’,na ubaya wa safari unategemea na kujiandaa kwako pengine ukiwa kama ulikuwa ni wakupanda milima alafu ukavaa suti,lazima kuonekane namna ya kutokufikiri sahihi,isipokuwa mlengwa usipojilaumu juu ya safari yako.

Mengi yanapotokea hutokea ya kuwa ni rafiki ama ndugu hawa wakiwa ni baadhi katika vile vinavyofanya safari ieleweke ipo katika namna gani,haraka hufanya ajari na ikawa hata unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako,hatari ya safari  imekuwa baada ya safari yenyewe kuanza,fikiri uwezo wako maana wanaokatisha tamaa ya maisha wapo karibu yako tena kila mtu akijifanya mjuaji,mtu unapojifanya unajua jua unajua ya kwako ya mwengine mwache aende nayo kwani kujilaumu kwa kukosa hupewa moyo na siyo mtu kaa mbali na kuwa makini na maisha ya mwenzako,kama huwezi jambo hakuna faida ya maneno na wakati muda unataka kusema yake.

Sunday, September 23, 2012

KWA MUDA MFUPI...


Ni wazi mandeleo ya mwananchi huletwa na nafsi yake mwenyewe,hii ikiwa ni katika kuamua endapo kuna  jambo lifanyike ama la..na ikiwa imechagulika na ieleweke,maana pengine  ni  kwa faida ya wananchi,na katika faida ni lazima isiwe na kudanganya toto,na endapo imekuwa bila ya kufahamika basi hiyo ni sahihi maana hata sisi wenyewe tunaishi kwa muda mfupi tu,na pengine kupitia wengine yaweza kuwa ni kwa faida yao tu,maana kama unajijua unakaa kwa muda mfupi ujenge ya nini?

Hapo kwenye kujenga yatasemeka mengi,maana kwa vingine ni lazima kufikiri endapo kuna tegemezi na hiyo ikaeleweke kama ni la muda mfupi ama kudumu,vinadumu vyote lakini si nafsi ya mtu mwenye mawazo mafupi,utanenepa kwa kuwa unakula,utakula na usinenepe kwa kuwa haujaridhika,tena maswala ya muda mfupi yakiwa yanakuchanganya.

Fikiri kwa muda mfupi ili kuweza kueleweka kwa kuwa wengi wanataka majibu,usikurupuke ya kuwa muda ni mfupi ikaja ndiyo sababu,hata yale yaliyofanyika ni namna ya kutaka sababu endapo yakauliziwa,kesho tutaendelea kulalama kwani wale wa kwanza muda wao unaelekea kuisha,tungalikuwa na thamini na yale yanayotutegemea,hakika hata  muda mfupi usingekuwa ni sababu.

MAISHA YAKO.


Unapofanya hivyo unasogeza namna ya kupokea vyema ikiwa katika muda mwema,na katika vitu vya kuzingatia katika maisha yako pengine ukatafuta mtu au watu mkawa mnashirikiana katika mambo mnayofanya na kukuta kuna kusema maana vizuri vinakatisha tamaa kwa kuwa mwanzo unasemeka ni mgumu,unapokuwa na lengo ni vyema kutumia na nguvu zako kwani katika baadhi nyingine ya kuamini ikiwa nikutafuta na kutaka kujua wewe ni nani na pengine nini kilichopo ndani yako.zile nguvu zako ndiyo zinaashiria undani wako.ikiwa ni kihalisia zaidi.

Leo utasema ya mwenzako lakini ya kesho ni yako,maana haukuyasema jana,hiyo ikiwa ni namna ya kunyimana,pengine isifahamike kwamba hata ile iliyo ndogo haipo,kwa iliyopo kuonekana kama ni nyingi kwani umejaribu japo kujipendezesha na uturi pia,kesho inayokuja ndiyo hiyo ya hukumu yako,maana wengi wametegemea samahani kutoka kwako.

Maisha yenyewe yako wapi?Ni usemi tumeusema,tumeuskia.hapo ukiwa umeona tofauti na kile halisia maana kama ulinyimwa na ni bora kusema pengine wengine walijisahau.ndiyo maaana ya kesho kuja na kusema samahani.unapojinyima una maana ya kutengeneza,ama pengine ukanyima na kukuta unafanya mbadala wa kutengeneza yaani kubomoa ,hapo ikijengeka chuki,Chuki ni kama upendo maana upo katika maisha ya kila mmoja wetu,asiyekuwa nayo sasa ni kwa sababu ya muda na maisha yake.maisha yako ni tofauti na ilivyo.ni swala la kutambua tu.

Friday, September 21, 2012

MTIHANI...

Jirani karibu maana ninatafakari kwa yale yaliyo ya mbali, Tukibadili lugha tutaelewana tu ya kuwa ni mtihani,na kama kuna kuishi ni lazima kuufanya,leo umekuwa mtihani baada ya kutaka machache yaliyo kwa wachache ,leo umejuaje kwani  mungu naye ameleta lake kwa kuwa pengine wengine wanaweza kushangaa kwa kuwa hata wale wa mbali waliweza kusema ni hiyo ili iliyo ndogo  ikaeleweka kuwa na muelekeo wa kusema kwamba mimi hii ni yangu ili kulainisha lazima.

Kiswahili ni lugha ambayo hata mwelewa akasema haleluya maana ni lugha ya dini katika utaifa wa namna yoyote,wale wa kwanza katika kuanza ni wale wanaotaka kuwa wa kuelekeza katika namna ya kuelekeza kwamba unaweza,maana kuweza kunahitaji uwezo wa mwendo wa kusimamisha ili kimo kikaeleweka .

Tunarudia na kusema,Kile nini unachokifanya katika maisha yako ni juu yako mwenyewe,kifahamike au la,pengine usiishi kwa kusema kwamba ukitaka maana,vingine vinavyokuwa tofauti ni tofauti zenyewe maana hata unapochanganya ni sawa na kuuleta ugumu wa tatizo katika tatizo lenyewe,ikiwa hata mwalimu anakosea kusahihisha,hapo kuna kujiona mjinga kana kwamba kama ni kazi basi wamefanya wengine kwa kupitia wewe.sio kukupitia bali ilikuwa ni mitihani tu.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...