Mawazo Chanya.

MAWAZO CHANYA.


Sunday, November 18, 2012

MUDA WAKO…


Hakuna anayeelewa kwani wengine wanasubiri wengine ndiyo wanafanya,bila kujali muda yapasa kufikiri pengine kuwa na wazo,muda haungoji mtu,muda sahihi si ule unaofanya kitu,ukiwa na subira utapata,utapata nini na wakati hakuna subira?pengine hata ukiwa na subira na usielewe unasubiri nini,maisha hayadanganyi,unapopanda ngazi usidhani ni mlima maana kwa kupanda na kushuka,korofi nyingine hazina maana ya kuleta kuongeleka,muda wako ukifika kitaeleweka.

Leo jambo na mambo yameongeleka,kwa yale uliyoyasikia machache ndiyo ya kuweza kuukamilisha muda uliobakia,pengine ikiwa hakuna muda uliobaki basi itapaswa kuongezwa,ikiwa kuna mgonjwa na asiye jiweza hilo ni la pili maana wa kwanza alishatangulia,ukisema upo njiani lazima ujue unapoelekea,pengine kwa uliyefika ulitumia njia tofauti.unapofikiri fikiri na utofauti uliyopo,maana kwa kujifananisha unaweza kujiona kenge wakati wewe ni mamba,tena wa mto wa kijiji,ukikaa vibaya wanakijiji watakumaliza maana mto unaelekea kukauka.

Ikiwa umekubari kuwa mamba ni lazima ujue kuogelea nchi kavu,mwanadamu anayeishi katika maji huyo kazaliwa huko,na akija nchi kavu lazima aogelee mavumbi.kwa Yule anayeelewa mda wake ni lazima kuufanya si ya kuhofia mavumbi,maana kama kuchafuka unaweza  usitakatishe roho wakati wa kusuuza,ili ukaja muda wa kuvaa na kusema mashine hazikufua  vyema,muda ndiyo unaotufanya kuzeeka,ikiwa starehe ndiyo zikamuweke mtu mzee,haipaswi kuustarehesha muda wako.

No comments: