Tuesday, January 31, 2012

MENGI YAMEDONDOKA.


Ikiwa ni kutoka juu hadi chini,chini hadi chini kabisa au juu kwa juu huko huko,pale pasipo kuwa na uangalifu mzuri na mara nyingine ukaseme ni bahati mbaya,Yaliyokuwa yameshikiliwa ndio sasa yanahitaji msaada,maana hata wale walio kuwa na nguvu wameamua kuachia,yanayodondoka huwa hayasemi zaidi ya yale yanayoshindikana.Kwa nini kama kudondoka tusingedondokea juu huko huko,maana yule anayedondoka akiwa chini yeye hubaki pale,na kwa yule aliye juu ikawe ni mshangao mkubwa tena.

Ikiwezekana umesahau maneno yetu ulipokuwa mtoto tukiyasema na ndiyo maana imefika muda shikamoo zimezidi,sio kwa utani lakini muda umesogea,angalia tusije kuwa sisi ndiyo wazee,kwani watoto wanazo zao,na kamwe mtoto hawezi kulingana na mtu mkubwa ikiwa hata anaumwa,ukumbuke ile ngoma ya watoto inakesha kwa namna yake,yale ya zamani yamekuwa ya kisasa zaidi,hawakua na mambo ya ujana ambayo yapo katika kipindi hichi na yanamaliza nguvu ya taifa,ingawa ilikuwa ni kipindi cha ujana wao.

kwa sasa wazazi wanashindwa kufanya lolote na watoto kukua katika namna wawezavyo wao,hatukatai mtu kuwa mzungu,kuwa mwarabu,lakini ni lazima mtu anaye taka kuwa katika jamii tofauti na yake ajielewe yeye,ajitambue ya kuwa hakuna muda wa kufananisha zaidi ya kufanya,yakuwa mwanzo unaonyesha mwisho upo katika namna zipi,njia hufanya mwanzo kuwa mwisho mara nyingine,kwani inapaswa kuurudia kwa makosa machache yanayotusibu katikati ya safari yetu ya maisha kabla hatujayamaliza.

Wale wanaotembeza sio wale waliopendeza,ikiwa haikusemeka hivyo,uzuri kila mtu anao wake,tukiambiana watu ni wabaya basi itakuwa ni vita ya kuutaka uzuri kwa lazima,tukiwa tunatoka safari tuangalie mizigo yetu tusije kuisahau nje,maana na wachache tukaonekana tumependeza wanajua tunapesa,tumefanikiwa kumbe ni tumefanya ili kuweza kutembea vyema,maana wachache hawachelewi kukwambia umepungukiwa akili,ila wakifanya wazee si mbaya kwani ndiyo walivyokuwa navyo na walitembea hivyo.

hata ikiwa akaja mgeni na kubisha hodi,mshikishe jembe huyo,mwambie ndani wasafiri walipaki vyao na wamelipia pesa nyingi ikiwa hawataki usumbufu,tukalime na hao wageni maana si wamekuja na majembe wenyewe?angalia unapofundishwa na mwalimu mgeni,kwani lazima ujiulize wa kwanza yupo wapi?kama kashindwa uangalie Yule aliyeweza,muda unapita na utakao fuata ndiyo wetu maana sisi ndiyo wazee,na usikubali kuacha mafao maana utasumbuliwa tu,taarifa za mbali zinaweza kuja zikiwa zinatuhitaji na lazima ujiandae kwani ni sisi wa kuongoza,umwangalie sana Yule mzazi wa mtu mwingine anapomwambia mwana wa mwingine kuwa hana adabu,ikiwezekana ijulikane kama adabu yake ni nzuri ili tuache za wazazi wetu.
‘sio kila kitu wazee’.


By:Benson G.Makaya,
Tel:+255714336657
Email:bensonsmakaya@gmail.com

NAMI NIWEMO.




Ikiwezakeana sura yangu iwekwe kwa kaisari,kilichoniweza ni kile nilichokiongeza,cha kwanza nilikuwa nacho mapema,ndiyo maana ya kuja na kusema,ni maongezi nikifikiria,pembeni haina haja ya kukuitia,tuongee pamoja tuelewane tusije jutia,ni mjita wa suguti mara musoma nimetokea,muda wote haina haja ya kuitajia,tumefanya vingine kwa waliotofauti ikaeleweka,wale wachache..tusiotaka hongera kwa makosa yetu,kila mtu anayafahamu ya kwake!! inanikumbusha kulee,kule kwenye sura yangu,angalau basi tufikiriane ndugu zangu,labda nimesema hivyo hata nikiwa nina nia mbaya,wala si uongozi wangu utakuwa mzuri,ubaya wangu hautadhuru lolote ni mimi na uongozi wangu.Labda tufahamishane kwa hili,nikipata nafasi ya kupiga picha ntapiga kama ile katika shilingi mia,moja ile ya upande fulani,muda unavyoenda tutachaguliwa wake ,maana naona nguvu zetu zinaisha,viwili kwake chake,moja kwetu vyetu,hii ni mbaya ikitokea kwetu,labda tusijue nini maana lakini ombi langu ni hilo,moja..hili la sura yangu kuwapo pale,najua ntaweza ikiwa sijafika hapo waje wawaambie,zikiwa kama hadithi kwa wale watakao chelewa sana.

Tusitake maisha ya kurudi utoto bila kujua tutawarudishia wapi watoto wetu,maana tuwape na njia ili wale wenye watoto wengi wengine wajisaidie,hata kama ni njia na zenyewe zimekuwa ni nyembamba zikihitaji nguvu ili kupita,tukisema kukonda ili kupita vyema wao wanasema tumepata ugonjwa wa mawazo na tukinenepa inakuwa vibaya kwa mapitio,itabidi tutafute njia yetu.kilichozidi zaidi lazima kiwe na sifa yake iliyoongezewa zaidi,ni kweli maisha yalikuwa ni magumu lakini hii iliyopo ni zaidi,hakuna asiyejua kuishi labda asikuelezee,yale tunayoyataka yataleta maafa,nikiwa sijui maana yake labda,niseme maswali ya dunia nakumbuka kauli hii nilipoulizwa kwa nini maswali ya dunia jibu likaja ya kuwa hilo nalo ni swali la dunia,hatuwezi kwenda na maswali huku majibu tumemwachia mwengine,maana kama ni shule zimekuja hadi za lugha tofauti,hili si kosa kwani shule ni kujifunza na endapo unataka kujifunza unatakiwa kujifunza kitu ambacho wewe unataka kujifunza,haina mshangao ila ni ya kustaajabisha sana shule watu tumeenda za nini?maana ionekanavyo tu wengi sana tumesoma na maswali yakiwa hayana majibu.

Labda kama sijamaliza lengo lieleweke,maana inaweza kutoka picha tofauti na ndugu zangu wakasema 'tulijua sisi' ,wengine humaanisha vyao daima,bila ya kumjali mlengwa,hakika matangazo tunayaona,tumejitahidi kulemba sura zetu zikiwa na ujumbe mbalimbali tofauti,hiyo yote ikiwa ni kushawishi,hapa napo tunashawishi lakini imekuwa ni namna tofauti,kwani lengo hapa ni uwepo wa sura tu mahara pale,pengine hata nkikumbuka kwa kipindi kile waswahili ndugu zangu walikuwa na usemi juu ya upendo ingawa unawezekana bado ukawepo,nakupenda sana nikinywa maji nakuona kwenye glass,yaani mzungu hapa anakwambia ‘indeep’,huu ni undani..ingali bado tunaendelea kuishi basi ukawe undani wangu mwingine.tumalize na hili...

‘Ikiwezekana sura yangu ikae katika shilingi’

By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com


Monday, January 30, 2012

Makaya's Forum: TUBADILISHANE KILE TUNACHOKIFANYA,NA SIKU !!

Makaya's Forum: TUBADILISHANE KILE TUNACHOKIFANYA,NA SIKU !!: Yanayofanyika ni matendo,kwa mtenda ndiyo ikafahamike haswa,ikiwa naye mtendwa akifaahamu zaidi kutoka kwa mtenda,yaani ilikuwaje?sio mawazo...

TUBADILISHANE KILE TUNACHOKIFANYA NA SIKU


Yanayofanyika ni matendo,kwa mtenda ndiyo ikafahamike haswa,ikiwa naye mtendwa akifaahamu zaidi kutoka kwa mtenda,yaani ilikuwaje sio mawazo haya ya kila siku uliyonayo lakini ndio baadhi yanayopelekea kutenda,yote ni matendo tu,ikiwa siku zinaenda wengi wetu ukiendelea kufanya vile unavyovifanya ili mradi siku ikapita,ikawe ili mradi sio tu ndiyo yapite bure,bure isiyo ya pesa,bure ikawe ya kutokufanya jambo kwa siku hiyo,kwani kama unabadilishana vinaenda wapi?yaani hivi vibovu na yale mazuri kwani kuyafikia na yenyewe yanahitaji siku iwe nzuri,itakavyo kuwa ndiyo jinsi ya kuelewa ielewekavyo,

Utasumbuka endapo ukitaka kubadilisha mazuri yawe mabaya,kwani ni uadui utakuwepo hapo,usije kosea na kubadilishana hewa,ili kesho ukapumue na wakati unazo tokea kuzaliwa,kipindi na cha kukifahamu ili ukabadilishane na vile vizuri,maana kipindi hichi kimekuja kinamna nyingine,siku hizi sio kama za zamani,wale wa zamani wanajua hilo yaweza kuwa nao hawaelewi kipindi chao,maana siku zao walibadilishana vyema,ikawe mbuzi kwa ng’ombe,naye mfanyabiashara akalizika kwani alitafuta mbuzi ili abadilishane na ng’ombe.

Ikiwa ni leo sijui kesho kutwa itaitwaje,maana mabadiliko yaliyofanyika ni ya leo tu,kesho ilisemekana watakuja wengine,lakini nao bado hawajaandaliwa ikiwa nao wakija wataanza yao,hata ukawa ni upepo ni lazima ujue unavumia wapi,ikaja hadithi uwahadithie ulikuwa unatokea pande ya kulia na kuelekea kushoto,zote ni pande nzuri labda iwe ujiamini leo na kesho,hapa ukitaka kufahamu ubora mwingine ulio wa zaidi ya leo na kesho.

Siku ni muda,kesho ni siku ya pili,muda huu ukauite wa kwanza ikiwa unategemea wa pili uje ukiwa umejiandaa kwa muda huo au useme muda wowote,usifike mbali wakati mwanzo unaonekana,ikiwa anayeanza hufikiri mwanzo bora iyo ikawe siku,maana hata kesho ikija itakuwa na yake,yale uliyoyapanga na haya mengine yatakayokuja,lazima yaje kwani wengine wanakufikiria kwa yale ya kesho na sio leo,utatafutana huko na usipokuwepo watakutafuta wakufunike,kwani hata walizani wao wamelala wakaandaa na mashuka kumbe yalikuwa ni yetu,unaposhindwa kurudia mema na kusahau mazuri ni kama pale unapofikiria yale maovu yaliyotuumiza siku za nyuma,yule anayefanya kazi bila kuomba mshahara anategemea kulipwa mengi,ikiwapo na mshahara wake mwenyewe.maana hakuupata,na hakuna kazi isiyo na mshahara,labda siku zipite ili ujue nini haja ya mshahara,tena sijui umekujaje baada ya kufanya kazi.

Wanaopaka ina wakiwa na yetu majina ,siku zimepita nyingi mengine yafutike,ikiwa mengine sio ya kuyatendea,utajiuliza kama ni kweli zimepita,bila kukanana pengine huwafahamu wasichana,kwa urembo wazee kuonekana vijana,hata ya jana yasingewezekana,muda mwingine inakuwa ni kujifunza kwa kuchanganyana,siku za zamani watoto ndio walieleweka kutokujua,maana nyingine hata hizo zilizopita zinaweza zisifike kwa wale wenye watoto kujisifu ikiwa ni wana wazazi kama wao,siku zinavyozidi kwenda utafahamu tu,labda uchelewe lakini ni lazima ufahamu ingawaje mpaka sasa umechelewa.

Lengo ni siku kupita,iwe imeeleweka kinamna yeyote.yule anayesema ameelewa vile aiambie siku yake,maana ndicho kitakuwa cha muhimu kwake..

By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
email:bensonsmakaya@gmail.com

Sunday, January 29, 2012

HITAJI,,


Hitaji huwa linatokana na mtu mwenyewe,nafsi yake na mapendeleo ya kwake.Pale mtu anapohitaji liwe la ulazima ama si la ulazima katika mazingira yaliyo au yatakayo ya ulazima ikiwa na maana ya uwekezaji,yale ya hasara hakuna asiyeyapata labda tusikitike kwa kupoteza watu kwenda kuwa wafu na isiwe hasara,hiyo mitazamo inatokana na kile kilichomo kichwani na sio mwilini,maamuzi yanatokana na mtu pamoja na nguvu zake,pale nguvu zinapotumika tunaweza kusema maamuzi yalichukulika mahala Fulani,Ni wengi wetu tunaohitaji,hii haitokani na kwamba mahitaji ni ya lazima,mahitaji mengine ni yale yanayotupelekea kuhitaji.kuna kipindi mwanadamu hutenda katika mahitaji yake,hii inaweza ikawa ni kwa ulazima au ombi ikiwa mahitaji yako yamekulenga wewe mwenyewe.

Bidhaa zinapouzwa zinataka bei,ikiwa unahisi kulaliwa bei..usiuze,kwani yaweza kuwa matokeo unayoyahitaji siyo yenyewe.Isiwe lazima kumfanyia mtu mahitaji yasiyo kuwa na ulazima kwako.Kwa makusudi yapi sasa?pengine tunawaza tukiingojea samahani au itakuwa ndiyo mahitaji ya kutumia nguvu,maana lugha nyingine hutumika kurahisishia mambo,zikiwa pamoja na samahani,wachache tukatumia lugha hizo tukijua bado tunamahitaji mengi ndani yetu,pengine ikiwamo misemo hiyo tofauti inaendana na thamani ya kitu,tumekuwa wajanja saana katika kufanya mambo yetu,na hii inatupelekea mahitaji yetu kuwa ya kijanja janja tu,hatutafika mahala endapo tutahitaji kijanja,kwani tutapata kijanja hivyo ilivyo.

Pengine wengine hubaki pale jambo linapotokea,sio kukaa na kuwa nyuma bali kufikiri vyema mahitaji yao,ikiwa ni wao ndio wanataka kufanikiwa,mara nyingine tunapokuwa safarini tuwafikirie na wengine maana wao wamebaki huko,hatuna haki ya kupaita ni nyuma kwani kila mtu anahitaji lake,na ikiwa mlengwa amekuwa na malengo halisia.tusiseme tuna shida wakati wenye nazo wametulia,maana wao sijui ndiyo wamezizoea au ni mahitaji kama ilivyo kwa uhalisia,na tunaposema hitaji hilo linaweza likawa ni la mtu basi tusifikirie vibaya kwani iliyo nyeupe kwa mmoja si impendezayo mweusi anayependa hiyo,ni kama vile uongozi,ikawe pale tukajua ni nini maana ya uongozi na sio tukaenda na bado tukazidi tukidhania lengo letu,hapa watu watatushaangaa sana,ingawa uchache ndiyo uhalisi wa hitaji,vile vingi vinatafutwa baada ya kuona utamu,utamu wa jambo na wenyewe huja baada ya kutaka kuwa na miliki,tunapomiliki vitu vingine vinaweza visiwe katika mahitaji yetu,vingine vikawe kama ni mwongozo katika mahitaji yetu,Yule anayetaka kuyajua ni lazima akubari ,tena ikiwa kwa maelezo maana ujanja unaweza kuingia pia.

Pengine tuseme hakuna anayetaka kutangulia,na hili tusiliite hitaji,maana tumefanya kwa ulazima,kwa wale wanaojinyonga waliamua,hawakuonja kifo lakini walipaswa maana lilikuwa ni hitaji kwa muda huo,haina budi kushangaa kilichocheupe na wakati ni cheusi tukitafutacho nacho hatuna,labda tufikiri kabla ya matendo,matendo yetu yakatupelekee kuwa watu wenye mahitaji mazuri,kwa Yule anayelenga ni lazima apate na kama asipopata atakuwa amelengaje?labda tuseme lengo la mlengwa halikulenga malengo,matokeo ndiyo malengo ya mahitaji,katika kufeli hakuna kufauru ila tunaweza jitahidi zaidi tukafauru,hivyo basi tunaweza kufanikiwa kwa jambo lolote ikiwa tu tumelenga na kuwa na hitaji nalo.pengine imefika wakati tuyatangaze,maana wachache wameanza kununua,ingekuwa ni kuhama tungeshafika huko,au tukaupande ili uishe ikiwa ule ulio bora kabisa tusipewe ruksa,mambo ya msingi ndiyo haya yanayotupita kwa kusikia hata,kwani ikiwa kumbukumbu zimejaa na tusisahau pale hitaji linapofikia turudi tena tusimame kihisia pia,kwani walioweza walianza hawakuhusika ya kuwa kila mtu ana lake hitaji.

By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Saturday, January 28, 2012

SIO LAZIMA KUFANYA WAKATI WAKO.


Wakati ni muda,nafsi ndiyo hutofautisha miliki.Nikasema hivyo utofauti nitakao kuwa nao ni mkubwa zaidi ya fikra zile ukafikiria,unapotamani sauti kuu ni lazima uinue midomo na ikasikika kwani uo ndio unaweza kuwa wakati wako,watu wakataka kukusikia au kuiskia sauti yako wakati ule ndio halisi walikuwa na furaha yale ya mwanzo usiulize ni nani yule na labda hapa nawazungumzia wengine zaidi,inapofika wakati umetaka kujua ni wazi umeguswa kwa vile namna iliyo moja na nyingine,kama kazi ya baba ni Fulani basi mama afanye nyingine na yeyote kivingine ikiwezekana kwani ule wakati walivyooana uliweza kuwa sio wao,ni yanatokea tu labda ujue ni namna gani muda utakaa kwani na wenyewe huwa hautaki usumbufu kwa kusikiliza tu itasahaulika kwani na wengine sio wapenzi,ilivyo kwa watu wakachagua wamuabudu nani yule mwingine akawe na damu yake iliyotofauti na wengine,hilo nalo usibishe zaidi Kumshukuru yule aliyefanya hivyo,mimi naweza kuwa sijulikani kwako lakini Mungu kwa hapa yote ameweza yeye na uwepo wake ndio unakuwa katika nafsi za watu wengine pamoja na sisi.

Ikiwa Mungu ndiye mwalimu mitihani hii tunahaki kuifanya sisi,kwani hata ukakimbia ni unajisahihishia mwenyewe tatizo ni chaguzi yeye anaangalia nani amejisahihishia vyema ikiwa ni kwa uaminifu,na endapo  ni wewe na utakuwa ikiwa hata kiupendeleo huwa inatokea, ,maana njaa za kila siku hizi hazina mwelekeo maalum,ukiwa unajua nalo ni neno la aibu sana,kwani yule anayetegemea kuishi anataka kuishi ili aendelee kuishi sasa sijui tutaishi vipi,na wapi maana huko mbele ndio hakuna mwelekeo kabisa,wakati mara nyingi huwa unakuwa ule unaoweza kusemeka,sio wakati wa mateso ambao mtu anachagua mwenyewe,kila kichaguliwacho ndio kimekuja kufanya kile kitakacho tukia na mengine hutokea bila kuchaguliwa ni kwa sababu yanataka kuonyesha kama yapo yametokea wengine tunapofanya yale yetu tunayaweka nyuma ikiwa tunataka tuelewe yale mengine.

Haki Hata ukikimbia  haitakuja kwetu,ya kuwa utakuwa unamkimbia mwenyeji na ukizoeleka zoeleka kwingine watataka haki yao utatoboa mahala wengine watumbukie maana hata kwa uchache huu tunasumbuana dadi haitishi kitu maana kila mtu na wakati wake yaliyopo yapo na yaliwekwa ili uyatendee labda ubaki nao huu wakati ili usije ukawa wao wakaenda na wasirudi  nao.

By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com
webbrogger:www.bensonmakaya.blogspot.com

Friday, January 27, 2012

UTAVUNA UNACHOKIPANDA.


Mavuno ni baada ya kupanda,mtu unapanda mbegu ukitegemea kuvuna mazao iwapo katika uchache ama wingi ndiyo pale unapoweza kusema mavuno ni mazuri au mabaya inategemea na lengo lako mpandaji.

  Unachokipanda mtu unakifahamu mwenyewe,labda isisemekane kama ni chema ama si hivyo,ikiwa wote tunamalengo,malengo ni yale kila mmoja akayatakia ikiwa mengine ni mipango au si hivyo tena,vile unavyosikiliza hivyo husikilizwa mara nyingi,kwani hata ukaomba ikaeleweka ni pale ulihitaji,umakini usio kuwa wa kusikiliza si pale ukimsikiliza mtu tu,nitasema hao wale ndio hawaelewi,sio yakuwa tu umefanya ndio ukajiona umeelewa vyema,kwani hata jinsi ulivyopanda si namna ya kuvuna vingi upande wa mwengine,kila mbegu ipo mahara pake na hakuna ziada la kuweza kuunganisha hayo,ili yawe mengi ni lazima kuungana,usisahau zile mbegu nono,maana hizo ndio zinakuletea matatizo muda mwingine,usije ukafanya kasoro kwa uwingi wa kuona,haina haja kutendeana kile mabaya.

Labda haukuelewa nini ilivyo kigeugeu,ikiwa aliyepanda mahindi akategemea kuvuna dagaa,hiyo itakuwa mbali sana na ukaribu utakuwepo kwa wale walioelewa moja kwa moja na usijue ni wapi haujaelewa,ambapo bado hujafanya haina haja ya kuuliza.Pale unapopanda upendo hata vurugu unaweza kuvuna,haya mengine sijui yanatokea wapi maana utayaacha mbali ukisema hautayafanya tena,hivi navyo hata vile.yule anayekaribishwa chakula akasema asante umuulize kama ana hamu ya kujua ni chakula gani anachokaribishwa,maana utatia aibu kwa yale machache tu yakusikia harufu ya chakula cha jirani na kutofautisha kile cha jana ulichokileta mezani na ukapelekana mezani wakati si kile dhabiti ya tumbo..jirani Yule akatake kuijua radha ya chakula,amalizapo unamwita mtoto  kwa kula kidogo na kikubwa hakikuwepo,utacheza sana mashambani ukililia mbolea na wakati uwezo wa kulima ni bustani,kumbe unachafua mazingira na hao wachache ndio wanaoelewa,ukiwamo haina shaka mazao mengine bora yakabadilishwa maana hayaeleweki bado katika mavuno.

Unaweza kupanda na kufika wakati mbolea isitoshe,na labda usiyazungumze ya jana,ikiwa tu kipindi kile njaa haikutisha labda uelewe wapi sasa haitatosha,yanayotokea yote yapo kama yale yaliyo na mwenendo ule wa kwao wenye mazao,mvua yenyewe imenyesha nyingi na utegemee kipindi furani tena,kwani hata hivyo ulivyokuwa unavitegemea vimefanya kuharibu vipya vinginevyo,zimebomoa kabisa hata yale waliyojenga wao,huu kumbe ni mda wa kupanda,ingawa wapo wale watakao vuna mavuno yatakuwa hayana nguvu,unapofanya kwa mmoja wa pili huwa anasogea,kwani mbele au nyuma ni kule aliko yeye ndio kutamtambulisha.

Muda bado unaenda.ikiwa umeelewa kwamba unahitajika kuvuna na kupanda mazao bora ni lazima ujue kama na hiyo mistari imenyooka,maana haitakuwa vyema pamoja ukaweka na visingizio,hapa usiite majina ya kiujumla.kumbe kunyoosha ni kuelekezwa,ikiwa shambani na ukaelekezwa upande vile natukapanda tofauti haitamaanisha kitu katika ukubwa wako,mtu na maamuzi yake ndiye akaamue sahihi kile cha kupanda,ili aje avune hicho,sio tegemezi ya kupandiwa mazao alafu ukalalama wakati wa uvunaji,eti na mpandaji usimwelewe alikuwa anafanyaje au mda wote huo alikuwa anategemea nini ikiwa wewe unasubiri,ingawa sio wote wakulima basi utajaribu kuwa hata mpandaji.maana itafutwa kwa yule angalau ameliona na kuligusa shamba,wengine wasifahamu mazao hayo yametoka mahala gani,wakasikia na wasielewe ya kuwa wapo mbali sana,vipindi huwa vinabadilika ikiwa ni shule utasoma hesabu,kiingereza na mengineyo yakiwa na maana..kama wakulima mwenyewe hujasoma na hujui kuhesabu sijui hizo biashara zinafanyaje kuendelea,ukatumia nguvu nyingi na zisiwe na maana katika malipo.


    Unapopanda upande mema,hata kama ni machache unavuna kwa namna hiyo iliyopo,na ni nani yule aliyepanda kichache akalalamika kuvuna hicho?labda usihesabu mavuno ukahesabu mbegu,na kila mbegu ije na vuno lake bora. 
      

By:Benson G.Makaya
Tel:+255714336657

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...