Thursday, November 15, 2012

HAKUNA MKATO KATIKA MAISHA..



Ni kupambana,ni kutia mkazo ili jema la mtu likaja upande wake,maana lako ni lako,maana wewe ni mtu maalum,ikiwa kuna  wakati unaotofautisha maana na kuleta tafsiri tofauti,ukiwa unaishi fanya lile la kesho maana leo imeshatokea pengine ndiyo maana yapasa kujiandaa kabla ya safari,ikiwa kungalikuwa na uwezo wa kutokusafiri kwa kutumia muda basi wengi wasingechelewa,haina maana ya kupita mkato ama njia ndefu ili kuleta neno maisha,ya leo ukiyaacha utafahamu vyema kuhusu kesho,kivingine ikawa ni ufunuo,hakuna mkato katika maisha kwani kila mtu yapasa aishi yake.

Ikiwa kuna kufananisha  ndiyo kumeleta vitu na utofauti,ukitaka kuachia njia yako jaribu kukalili ulipoishia,maana unaweza ukawa hauelewi na kujikuta umeelewa vyema sana kwa kuwa ndiyo njia uliyotaka kupita,unaweza kurudia jambo mara nyingi na usijue ni kwasababu gani haujaweza fanya lingine,hayo yakiwa ni matendo katika maisha yako,jaribu kufikiri nini unataka,chukua hatua na jaribu kupata na kuyaelewa ya nyuma,sisi wote tuna namna moja ya kuishi,ikiwa unaweza kulichukulia jambo kiuhakika katika mlengo wako wowote,upe muda na njia zilizo sahihi,hata ikiwa haujafahamu nini usahihi wake lakini muda utakuonyesha njia,maana utafanya lile linalokusudiwa na muda.

Kama ukienda na kufikiria kila maisha ya mtu mmoja unaweza usione mafanikio maana ni lazima ujue nini unachohitaji katika muda sahihi,pengine yaweza kuwa tumbo linauma kwa sababu ya njaa,fikiri kama unaijua njaa kihalisia,maana hata ikawa gari bila mafuta ni sawa na kumpa baiskeli mtoto asiyeweza kutembea,yote yanawezekana,ikiwa unaweza kukubali kwa yale yanayokupitia maishani mwako.hakuna mkato katika kupika nyama bila maji maana utakuwa unachoma,jambo ni kujua.

Wednesday, November 14, 2012

DUNIA YA FURAHA..


Katika malengo yanayomfanya mwanadamu kuweza kuishi pengine ikiwa ni kwa muda fulani ama ki namna ilivyo kwa mtu akataka furaha iliyoje ndani ya maisha yake,na ikiwa mwanadamu unaishi na hutaki furaha kuna ulazima wa kuonekana kutokukamilika,kwani hata mahitaji pengine yasiwe yako,ikiwa tunapokutana tunafundi shana,leo ikaja zamu yako kwa kutokueleweshana na kesho akaja  mwanafunzi ili kumuelekeza,furaha haipimwi na mizani labda wanene wakawa na roho kubwa,ingawa maisha yako ni kile unachokifanya,kile kinachoonekana katika biashara yako,kazi zako ndiyo mtazamo wa maisha yako.

Unaweza kuwa na maana kubwa katika lile ulifanyalo,ikiwa hakuna kile kinachoweza kukamalika bila kujitoa/nguvu,kutoa nguvu inapasa kufanya kila mara,ikiwa kama mazoezi,mtu akaogopa kufanya lile lake kwa kuhofia mengine kwani unaweza ukawa unaishi maisha ya mwenzako,kila mshindi hushinda kwa kuonyesha njia,kila mshindwa hushindwa kwakuonyesha njia pengine ile ile,kila mtu anawakilisha zawadi ile aliyopewa na mwenyezi mungu,kwa kupita katika  majaribu,kulia,kucheka ,kuchekesha hata kunyamazisha,hayo yote yakiwa  ni madhumuni ya maisha yako,kusaidia watu na kusaidiwa hii ieleweke kuwa  ndiyo njia ya kupumua,ni njia ya kufikiri..njia ya kuishi,maana bila hivyo haikuwa na maana ya kuishi katika dunia ya furaha.

Inapasa kujua wapi ulipo katika maisha yako,furaha yako umeibeba mwenyewe,kila mtu anapaswa kufanya jambo ambalo kimsingi litapelekea mapenzi,na hii ikiwa inatupasa kuwapenda hata maadui zetu,unaweza usimchukie mtu lakini yeye akakuchukia,ikiwa kuna watu ndiyo wametufikisha hapa tulipo,kwa mapenzi ama uadui,maisha hayana uadui,wewe ndiyo adui wa maisha yako,wewe ndiyo mbaya wa maisha yako,kinachobadilisha mabaya kuwa mazuri ni matumizi na  muda wake,ikiwa kama mvumilivu hula mbivu,na siye vumilia si kwamba atakula mbichi,maana na furaha haipimwi kwa kilo.

Tuesday, November 13, 2012

RIDHIKI NI POPOTE...


Ridhika katika kufanya maisha yako yawe unavyotaka,maana nikasema mazuri pengine ndiyo mabaya kwa kulinganisha na yale mazuri ya wengine,maisha hayajawa mpira mpaka ikaja kuyapiga ikiwa kama dana dana,shida yapasa mtu kuzipata peke yako,ridhiki ikiwa yako haina unyang’anyi kwani kwa kile ulichokiandaa ndiyo hicho kitapendezea kulika,kuweka mezani chakula si kwamba ule hadi meza,maana njaa lazima itakuja,ikiwa kama ni ridhiki lazima chakula kitaandalika tena na endapo itakutwa meza haipo itastahiri kulika mpaka sahani zenyewe.

Maisha hayajawa mchanga mpaka yakafika namna ya kuchanganya watu pasipo kuelewa nini cha kufanya,wengi wakiwa wanatafuta ridhiki wakiamini pesa ndiyo tatizo la kulitatua tatizo husika pekee,ukiamini endapo ukiwa una pesa yote yanaweza kurudi mwanzo,ikiwa ni njaa,sahani Pamoja na meza yenyewe.maana unaweza kutokudhani baadaye kwa kutokujua unataka nini.ridhiki yako ikawa kama ni mnyororo uliojifunga maana hakuna wa kumuuliza nani aliyefunga.

Ridhiki haiokotwi bali inatafutwa,yakiwa saba bora kuchagua lile la mwisho maana usije kuridhika na moja wakati haba lipo,haipaswi kuchukia na hoja moja wakati ya wengine yanaonekana kama vioja,yaweza kuwa yako,unaweza kuwa wewe.ridhiki haimfuati mtu,ridhiki haichagui kabila wala mahala,ridhiki huenda pale kwake kuliko na usahihi,mwanadamu anapaswa kuwa makini ili kuelewa popote yake,ikiwa kama mdomo umekosa ridhiki kwa  kula basi hata pua zitanusa,pengine masikio yakasikia lile lililosemeka na vingine vikawa vile vilivyoungika.

NENDA UKIJIAMINI KATIKA MWELEKEO WA NDOTO ZAKO..ISHI MAISHA YALE ULIYOKUWA/UNAYO YAFIKIRIA.

Monday, November 12, 2012

NGUVU ZA LAZIMA.


Ikiwa Mungu ni kila kitu na wa kila mtu,mwanadamu amepewa uwezo wa kuweza kufanya maisha yake,kufanya maisha yako ikiwa siyo kujaribu,yaani kutokuwa na uhakika wa kile unachokifanya na baadaye ukaja muda ukasema unajaribu,hata ingali ikafika kipindi wakubwa watalazimika kufanya vya watoto na hii ni kwa sababu wakubwa waliwaambia watoto kwamba usifanye kile cha wakubwa.katika kufanya maisha hakuna kujaribu na ili ueleweke unaishi ni lazima kutumia nguvu za lazima.na wala siyo lazima kufanya ulazima huo ikiwa haina ubishani katika kila mtu anapofanya maisha yake

Haikuwa na maana kwa mtu mkubwa kavaa nguo za watoto,maana hii ni fashion,ama ikawe jitu kubwa linataka sifa za kitoto.maisha hayana ngoja wala subiri,leo ukiwa mahala fulani fikiri kama na jana ulikuwa hapo,jua mwisho wa maisha ni pale utakapo kuwa hau ishi tena,hakuna mtu wa kuweza kuishi maisha ya mwenzake,ikiwa chaguzi la mtu ili kueleweka ameishi siyo lazima awe na kile wewe unachokitaka,unaweza kutumia nguvu kulazimisha kuota ndoto uliyoota jana ya kuwa ilikuwa nzuri sana na kujikuta umechelewa kuota ya leo,unaweza sema yote hayo ya mungu ya kwako fikiri, fanya yanayotokana na maamuzi yako

Kumbuka umeletwa duniani ili uishi,umeweza fanya mengi kwa nguvu zako na baada ya kumaliza akatajwa Mungu hapo ikiwa uliweza,toa nguvu zako..jiamini wewe ndiyo wa kufanya lile la lazima,ikiwa furaha ya maisha yako ni wewe mwenyewe,hauwezi kunywa pombe na kuiomba ‘KILEVI’ kikuleweshe kidogo,unasahau pale unapoanza na kukumbuka mwishoni kwani utamu wa mwanzo huonekana pale nguvu zinapoisha,siyo lazima kulima ikaeleweka unanguvu nyingi na haujaja kujipaka rangi ili kuonekana umpendeza,maana utapaka rangi zote na kujikuta umekuwa na rangi ya kopo la kuchanganyia mara nyingi huwa inakuwa haieleweki.

NI WAZI KILA MTU ANAJUA,HIVYO KAMA UMESHINDWA KUELEWA VINGINE  FANYA UNAVYOJUA WEWE ILI KUSIWE NA LAWAMA.

Saturday, November 10, 2012

Makaya's Forum: SHUKURU KWA YOTE..

Makaya's Forum: SHUKURU KWA YOTE..: Hapa   akihusishwa mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake,inapaswa kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito umeifanya,ikiwa una uelewa ni ...

SHUKURU KWA YOTE.

Hapa  akihusishwa Mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake inapaswa    kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito umeifanya,Asante Mwenyezi Mungu.
Ukiwa una uelewa ni lazima kubaki katika njia ambayo wewe mwenyewe unaiona siyo ya mapumziko maana ni lazima kutoa nguvu  Pamoja na akili yako ukiwa umeamka na kuchagua kile ambacho wewe umetaka kukiangalia,ukichagua lile ambalo limekuja katika muda unaofaa kimaendeleo,ikiwa maisha ni sehemu inayofanya ndoto kukamilika,ki imani ikiwa kama ndoto ni jibu la tatizo.pale unapomaliza jambo yapasa kushukuru kwa kuwa linakuwa vile kidogo ya ulivyofikiri,huwa yanafanana lakini rangi tofauti na kuthaminisha kule/kile/vile ulivyofanya.

Kama una ndoto ya kuwa  na furaha ama vile katika hali isiyofahamika,kama unapofumba macho ukitegemea kuona chochote mengine yatapita yakiwa ni afadhali kwa kuwa yatastahiri kukuchanganya,shukuru kwa kuwa siyo yote unayoyategemea hutokea ,mengine yakiwa yameletwa maksudi ili mradi na wengine wakapata shukrani za lazima,lakini ikiwa kama mtu ameamua kufa kwa kujinyonga akipona hastahiri kushukuru kwani lengo lake halijatimia.

Pongezi kwa shukrani iliyomaliza jambo,hongera hutoka pale shukrani inapokuwa na jibu lake katika jambo husika,maana katika namna ya kuzaliwa kwa sisi waswahili zinaweza kuwa ni kejeli,ikiwa unataka kuona ni nini unachokifanya haistahili kuuliza bila ya kuulizwa,hapa itatakikana kuonekana mwisho ikiwa unakipaji chochote cha kufanya hakitaweza kulinganishwa na muangaliaji ama yule asemaye kwani mwishoni huja na kukuvisha taji.mawazo yako ndiyo mtaji shukuru Mungu wako alikuumba wewe. hata ungali muda bado kuisha.


Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS