Tuesday, November 20, 2012

MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA..



Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi maana kwa kutokuyapenda na kujifanya unajua zaidi kujikuta unaumia bila faida,katika vitu na watu wanaoisukuma  dunia ni vile na wale wanaojifanya kujua kila kitu,unaweza ukawa unafanya sahihi na usikute lolote limefanyika,pengine hata nguvu za kusukumia zikawa hamna,kwa  kuwa mwenye nguvu umesahau kuangalia akiba,usipojua nini kupenda nini utafanya,wengine huwamo ni kwa sababu ya kuvaa,pengine nguo zikichanika hakuna jipya litakalo tokea,maisha ndiyo mapenzi na mapenzi ya mtu anayeishi yasikufanye mwanadamu kutokuujua wakati wako.

Hakuna mtu aliyekatazwa kupenda lakini fikiri kwamba utapenda nini au wangapi?wangapi umewapenda?je kile au yale mabadiliko unayoyataka yametimia?penda unavyoweza ukielewa unapenda ili uishi,maisha yaliyojawa na upendo ni maisha thabiti kama umeyaishi usijaribu kuyaacha zaidi ya kuongeza,ikiwa kumpenda mwenzako ni zaidi ya kujipenda wewe mwenyewe,haukatazwi kujipenda zaidi,ili mradi kwa mwenza kisiwe cha ukaidi.

Hautakiwi kuishi kwa taabu kwa sababu ya upendo,upendo hautafutwi kama inavosemekana,upendo umezaliwa kwa kila moyo wa mmoja wetu,unapochagua kufanya jambo fikiri kama umelipenda,fikiri endapo una uhitaji nalo ili inapowezekana kufuta baadhi ya uchafu,maana moyo ukiwa msafi hata uje msafi ,usafi utabaki pale pale,upendo ni asili ya mtu,jinsi ulivyo,usikimbie kimbia ya kuwa ni lazima kupenda,ili mapenzi yakatimie,maana unaweza kuisukuma dunia ya wengi na kuacha yako.hapa nasema umependa pasipo pendeka.

Sunday, November 18, 2012

MUDA WAKO…

Hakuna anayeelewa kwani wengine wanasubiri waelewe wengine ndiyo wanafanya, bila kujali muda yapasa kufikiri pengine kuwa na wazo, Tumetofautina namna ya kupanga muda wetu,  muda haungoji mtu, ukiwa na subira utapata,pengine hata ukiwa na subira na usielewe unasubiri nini, utakuwa umechezea muda wako , unapopanda ngazi usidhani ni mlima maana kwa kupanda na kushuka, korofi nyingine hazina maana ya kuleta kuongeleka, muda wako ukifika kitaeleweka.

Leo jambo na mambo yameongeleka, kwa yale uliyoyasikia machache ndiyo ya kuweza kuukamilisha muda uliobakia, pengine ikiwa hakuna muda uliobaki basi itapaswa kuongezwa, ikiwa kuna mgonjwa  hilo ni la pili maana wa kwanza hakujiweza, ukisema upo njiani lazima ujue unapoelekea, na uliyefika ulitumia njia gani ili ikiwezekana ukawe wa tofauti. Unapofikiri fikiri na utofauti uliopo, maana kwa kujifananisha unaweza kujiona Kenge wakati wewe ni Mamba.

Ikiwa umekubari kuwa mamba ni lazima ujue kuogelea nchi kavu, mwanadamu anayeishi katika maji huyo kazaliwa huko, na akija nchi kavu lazima aogelee mavumbi. kwa Yule anayeelewa mda wake ni lazima kuufanya si ya kuhofia mavumbi, maana kama kuchafuka unaweza  usitakatishe roho wakati wa kusuuza ila ukaja muda wa kuvaa na kusema mashine hazikufua  vyema, muda ndiyo unaotufanya kuzeeka, haipaswi kuustarehesha muda wako.

JITHAMINI.

Haina thamani kuuzungumzia ujuzi na wakati uwezo unao, Haitawezekana kuzungumzia ya zamani na wakati mapya yapo, uwezo unaoendana na wakati ndiyo unaohitajika, moja sitajidanganya kuwa nimechelewa kufanya ya pili hoja, watakataa sasa yakuwa haijulikani lakini thamini unachokifanya pengine yakupasa kuuliza  maana unaweza ng’ang’ana kujenga barabara na hujui mwelekeo, maisha yametofautiana yanaenda na wakati wake .

Hakuna aliyeumbwa hawezi labda yule asiyejua thamani  katika maisha yake Mabadiliko yanatokana na mtu mwenyewe, wakati mwingine inakupasa kuongea peke yako ikiwa yakupasa kujua yako kabla wengine hawajayajua, maana unaweza kujulikana ndiyo kumbe si hivyo, wapo wanaoteseka kwa kufanya yaliyo sahihi na kuonekana si sahihi kwa sababu ya kutokujiamini ama vile mwingine anavyokutathmini.

Usikate tamaa katika maisha  maana kesho  inakuja kukuletea thamani yako. Ngoja,jithamini jiamini itakuwa tu. Hakuna linalowezekana bila imani usipoijua imani utahukumiwa kutokana na uelewa wako, mabadiliko siyo mafanikio au yakafanye kuthaminiwa vile utakavyo, mtu anaweza kujibadilisha kwa  lengo la kupata jambo, ukikubari kubadilika rangi kama kinyonga haitashangazwa kuitwa kinyonga ila kubadilika tu ni ishara tosha ya kuwa kuna utofauti.



Saturday, November 17, 2012

AMUA YAKO.


Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa ulienda na ukasoma shule jua kuna maisha,hivyo shule ikusaidie kuishi,hata kama hujasoma Isiwe usijue nini maana ya gurudumu na wakati unaona linazunguka,ombea kuwa wa ndani maana ukionekana tu kipindi umechoka wenye raha zao watafanya maamuzi,maisha si unavyotaka mwingine wewe yawe kwa mwenzako,amua maisha yako leo kwa kufikiri sahihi,kubali kuwa haukuja duniani ili uishi tofauti na unavyopenda.

Hakuna mtu anayependa kulalamika au kumlalamikia mwenzake kwa kutokufanya jambo,ila ikitokea umechemsha kweli ni lazima kuzungumziwa na baadaye zikionekana lawama ni vile utakavyokuwa umeamua na ndiyo kujifunza,ukikubari kujifunza ni umejua,umeelewa maana yanayokuja ni mengi zaidi ya uliyoyapita,kumbuka mbele kama unaweza zaidi ya ilivyo huko nyuma,maana isije tokea ukasema kulikuwa na utabiri,inatokea wakati mtu kutofautiana kwa kutokuelewana ina weza wote tukawa na maana moja tatizo likaja kwenye kuelewa,isingewezekana kumwita mwenzako chizi bila kuujua uchizi,kuujua uchizi ni kuwai kuwa hata chembe hai zinazoelekea..😊

Hakuna uhitaji wa kuwa na haraka kwa kuogopa wasi wasi,maana imekuwa kama mbuzi anapoona majani ya miiba,ikiwa hayapatikani basi yakionekana adimu na kutakwa kwa sana,ukijisahau u adimu itakuja zamu yako utashindwa kuweza japo kwa kuamua maana fikra ndogo na maamuzi mengine hayahitaji ufahamu unaoujua wewe,hapo watakuja watu kukuamulia,tena ikiwa haukuamua vyema itaonekana maamuzi yako si bora kuliko ushauri unaouhitaji jua namna ya kufanya sahihi pale unapoamua,jua ulichokiamua juu ya maisha yako kamwe usiigilize.

Cheka na maisha yako.

Friday, November 16, 2012

MAISHA NI VITA.

 Uko vitani jina liko vitani,ili kudondoka karibu au halisi katika nyota liweke jina lako katika mwendelezo wa kuwa JUU pengine unaweza usifikiri kuyatilia maanani yale unayoyawaza kwa kudhani Mawazo yako si bora sana,ikumbukwe utofauti wetu kimwili,maungo maumbile na kadhalika upo hadi katika utajiri maana ni wewe unachagua ukiamua,pengine ukapendezwa na yana au yaliyotokea kutokana na kwamba hayajakupata wewe zaidi,huwezi kuyajua ya adui bila ya kupigana naye vita,pengine hasira haina ufahamu zaidi ya adui wenyewe wa pande zote mbili kujua tofauti zao maana umeumbwa katika namna hiyo ya utofauti

Haki ya kesho ni siku nyingine maana unaweza ifahamu kwanza,pengine mmoja akikupokonya chako hapo ndiyo unaweza jua kweli,pengine ikaja vita nakupigana,hapo bila ufahamu,unapopigana lazima ujue unapigania nini,ikiwa ni ya wengi lazima uangalie kama na yako umeyapigania,katika maisha uwongo ni sumu na kichecheo kikubwa sana cha vita kuliko kitu chochote kile,hapo ufahamu uongo ni nini,hapo mahala kwengine kwa moyo kukiwa wazi na kwengine kukiwa kunasaza,maana vita ni kama mzani.

Huwezi kuelewa mwenzako anapigana nini bila ya wewe kuamua kupigana,ingawa si lazima wote muwe katika vita,wengine hukasirika kwa kuambiwa huwezi kwa kuona unaweza na kuleta vita,wakiwa wachache wenye ufahamu ni wengi wanapoutumia ufahamu wao,maana baada ya kujua wengi ni wachache imekuja kuleta vita na kuondoa amani,ile nguvu ya kwenye ufahamu imekuwa nyingi kwa wengi.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...