Sunday, January 29, 2012

HITAJI,,


Hitaji huwa linatokana na mtu mwenyewe,nafsi yake na mapendeleo ya kwake.Pale mtu anapohitaji liwe la ulazima ama si la ulazima katika mazingira yaliyo au yatakayo ya ulazima ikiwa na maana ya uwekezaji,yale ya hasara hakuna asiyeyapata labda tusikitike kwa kupoteza watu kwenda kuwa wafu na isiwe hasara,hiyo mitazamo inatokana na kile kilichomo kichwani na sio mwilini,maamuzi yanatokana na mtu pamoja na nguvu zake,pale nguvu zinapotumika tunaweza kusema maamuzi yalichukulika mahala Fulani,Ni wengi wetu tunaohitaji,hii haitokani na kwamba mahitaji ni ya lazima,mahitaji mengine ni yale yanayotupelekea kuhitaji.kuna kipindi mwanadamu hutenda katika mahitaji yake,hii inaweza ikawa ni kwa ulazima au ombi ikiwa mahitaji yako yamekulenga wewe mwenyewe.

Bidhaa zinapouzwa zinataka bei,ikiwa unahisi kulaliwa bei..usiuze,kwani yaweza kuwa matokeo unayoyahitaji siyo yenyewe.Isiwe lazima kumfanyia mtu mahitaji yasiyo kuwa na ulazima kwako.Kwa makusudi yapi sasa?pengine tunawaza tukiingojea samahani au itakuwa ndiyo mahitaji ya kutumia nguvu,maana lugha nyingine hutumika kurahisishia mambo,zikiwa pamoja na samahani,wachache tukatumia lugha hizo tukijua bado tunamahitaji mengi ndani yetu,pengine ikiwamo misemo hiyo tofauti inaendana na thamani ya kitu,tumekuwa wajanja saana katika kufanya mambo yetu,na hii inatupelekea mahitaji yetu kuwa ya kijanja janja tu,hatutafika mahala endapo tutahitaji kijanja,kwani tutapata kijanja hivyo ilivyo.

Pengine wengine hubaki pale jambo linapotokea,sio kukaa na kuwa nyuma bali kufikiri vyema mahitaji yao,ikiwa ni wao ndio wanataka kufanikiwa,mara nyingine tunapokuwa safarini tuwafikirie na wengine maana wao wamebaki huko,hatuna haki ya kupaita ni nyuma kwani kila mtu anahitaji lake,na ikiwa mlengwa amekuwa na malengo halisia.tusiseme tuna shida wakati wenye nazo wametulia,maana wao sijui ndiyo wamezizoea au ni mahitaji kama ilivyo kwa uhalisia,na tunaposema hitaji hilo linaweza likawa ni la mtu basi tusifikirie vibaya kwani iliyo nyeupe kwa mmoja si impendezayo mweusi anayependa hiyo,ni kama vile uongozi,ikawe pale tukajua ni nini maana ya uongozi na sio tukaenda na bado tukazidi tukidhania lengo letu,hapa watu watatushaangaa sana,ingawa uchache ndiyo uhalisi wa hitaji,vile vingi vinatafutwa baada ya kuona utamu,utamu wa jambo na wenyewe huja baada ya kutaka kuwa na miliki,tunapomiliki vitu vingine vinaweza visiwe katika mahitaji yetu,vingine vikawe kama ni mwongozo katika mahitaji yetu,Yule anayetaka kuyajua ni lazima akubari ,tena ikiwa kwa maelezo maana ujanja unaweza kuingia pia.

Pengine tuseme hakuna anayetaka kutangulia,na hili tusiliite hitaji,maana tumefanya kwa ulazima,kwa wale wanaojinyonga waliamua,hawakuonja kifo lakini walipaswa maana lilikuwa ni hitaji kwa muda huo,haina budi kushangaa kilichocheupe na wakati ni cheusi tukitafutacho nacho hatuna,labda tufikiri kabla ya matendo,matendo yetu yakatupelekee kuwa watu wenye mahitaji mazuri,kwa Yule anayelenga ni lazima apate na kama asipopata atakuwa amelengaje?labda tuseme lengo la mlengwa halikulenga malengo,matokeo ndiyo malengo ya mahitaji,katika kufeli hakuna kufauru ila tunaweza jitahidi zaidi tukafauru,hivyo basi tunaweza kufanikiwa kwa jambo lolote ikiwa tu tumelenga na kuwa na hitaji nalo.pengine imefika wakati tuyatangaze,maana wachache wameanza kununua,ingekuwa ni kuhama tungeshafika huko,au tukaupande ili uishe ikiwa ule ulio bora kabisa tusipewe ruksa,mambo ya msingi ndiyo haya yanayotupita kwa kusikia hata,kwani ikiwa kumbukumbu zimejaa na tusisahau pale hitaji linapofikia turudi tena tusimame kihisia pia,kwani walioweza walianza hawakuhusika ya kuwa kila mtu ana lake hitaji.

By: Benson G.Makaya,
Tel: +255714336657.
Email:bensonsmakaya@gmail.com

Saturday, January 28, 2012

SIO LAZIMA KUFANYA WAKATI WAKO.


Wakati ni muda,nafsi ndiyo hutofautisha miliki.Nikasema hivyo utofauti nitakao kuwa nao ni mkubwa zaidi ya fikra zile ukafikiria,unapotamani sauti kuu ni lazima uinue midomo na ikasikika kwani uo ndio unaweza kuwa wakati wako,watu wakataka kukusikia au kuiskia sauti yako wakati ule ndio halisi walikuwa na furaha yale ya mwanzo usiulize ni nani yule na labda hapa nawazungumzia wengine zaidi,inapofika wakati umetaka kujua ni wazi umeguswa kwa vile namna iliyo moja na nyingine,kama kazi ya baba ni Fulani basi mama afanye nyingine na yeyote kivingine ikiwezekana kwani ule wakati walivyooana uliweza kuwa sio wao,ni yanatokea tu labda ujue ni namna gani muda utakaa kwani na wenyewe huwa hautaki usumbufu kwa kusikiliza tu itasahaulika kwani na wengine sio wapenzi,ilivyo kwa watu wakachagua wamuabudu nani yule mwingine akawe na damu yake iliyotofauti na wengine,hilo nalo usibishe zaidi Kumshukuru yule aliyefanya hivyo,mimi naweza kuwa sijulikani kwako lakini Mungu kwa hapa yote ameweza yeye na uwepo wake ndio unakuwa katika nafsi za watu wengine pamoja na sisi.

Ikiwa Mungu ndiye mwalimu mitihani hii tunahaki kuifanya sisi,kwani hata ukakimbia ni unajisahihishia mwenyewe tatizo ni chaguzi yeye anaangalia nani amejisahihishia vyema ikiwa ni kwa uaminifu,na endapo  ni wewe na utakuwa ikiwa hata kiupendeleo huwa inatokea, ,maana njaa za kila siku hizi hazina mwelekeo maalum,ukiwa unajua nalo ni neno la aibu sana,kwani yule anayetegemea kuishi anataka kuishi ili aendelee kuishi sasa sijui tutaishi vipi,na wapi maana huko mbele ndio hakuna mwelekeo kabisa,wakati mara nyingi huwa unakuwa ule unaoweza kusemeka,sio wakati wa mateso ambao mtu anachagua mwenyewe,kila kichaguliwacho ndio kimekuja kufanya kile kitakacho tukia na mengine hutokea bila kuchaguliwa ni kwa sababu yanataka kuonyesha kama yapo yametokea wengine tunapofanya yale yetu tunayaweka nyuma ikiwa tunataka tuelewe yale mengine.

Haki Hata ukikimbia  haitakuja kwetu,ya kuwa utakuwa unamkimbia mwenyeji na ukizoeleka zoeleka kwingine watataka haki yao utatoboa mahala wengine watumbukie maana hata kwa uchache huu tunasumbuana dadi haitishi kitu maana kila mtu na wakati wake yaliyopo yapo na yaliwekwa ili uyatendee labda ubaki nao huu wakati ili usije ukawa wao wakaenda na wasirudi  nao.

By: Benson G. Makaya,
Tel: +255 714 33 66 57.
Email:bensonsmakaya@gmail.com
webbrogger:www.bensonmakaya.blogspot.com

Friday, January 27, 2012

UTAVUNA UNACHOKIPANDA.


Mavuno ni baada ya kupanda,mtu unapanda mbegu ukitegemea kuvuna mazao iwapo katika uchache ama wingi ndiyo pale unapoweza kusema mavuno ni mazuri au mabaya inategemea na lengo lako mpandaji.

  Unachokipanda mtu unakifahamu mwenyewe,labda isisemekane kama ni chema ama si hivyo,ikiwa wote tunamalengo,malengo ni yale kila mmoja akayatakia ikiwa mengine ni mipango au si hivyo tena,vile unavyosikiliza hivyo husikilizwa mara nyingi,kwani hata ukaomba ikaeleweka ni pale ulihitaji,umakini usio kuwa wa kusikiliza si pale ukimsikiliza mtu tu,nitasema hao wale ndio hawaelewi,sio yakuwa tu umefanya ndio ukajiona umeelewa vyema,kwani hata jinsi ulivyopanda si namna ya kuvuna vingi upande wa mwengine,kila mbegu ipo mahara pake na hakuna ziada la kuweza kuunganisha hayo,ili yawe mengi ni lazima kuungana,usisahau zile mbegu nono,maana hizo ndio zinakuletea matatizo muda mwingine,usije ukafanya kasoro kwa uwingi wa kuona,haina haja kutendeana kile mabaya.

Labda haukuelewa nini ilivyo kigeugeu,ikiwa aliyepanda mahindi akategemea kuvuna dagaa,hiyo itakuwa mbali sana na ukaribu utakuwepo kwa wale walioelewa moja kwa moja na usijue ni wapi haujaelewa,ambapo bado hujafanya haina haja ya kuuliza.Pale unapopanda upendo hata vurugu unaweza kuvuna,haya mengine sijui yanatokea wapi maana utayaacha mbali ukisema hautayafanya tena,hivi navyo hata vile.yule anayekaribishwa chakula akasema asante umuulize kama ana hamu ya kujua ni chakula gani anachokaribishwa,maana utatia aibu kwa yale machache tu yakusikia harufu ya chakula cha jirani na kutofautisha kile cha jana ulichokileta mezani na ukapelekana mezani wakati si kile dhabiti ya tumbo..jirani Yule akatake kuijua radha ya chakula,amalizapo unamwita mtoto  kwa kula kidogo na kikubwa hakikuwepo,utacheza sana mashambani ukililia mbolea na wakati uwezo wa kulima ni bustani,kumbe unachafua mazingira na hao wachache ndio wanaoelewa,ukiwamo haina shaka mazao mengine bora yakabadilishwa maana hayaeleweki bado katika mavuno.

Unaweza kupanda na kufika wakati mbolea isitoshe,na labda usiyazungumze ya jana,ikiwa tu kipindi kile njaa haikutisha labda uelewe wapi sasa haitatosha,yanayotokea yote yapo kama yale yaliyo na mwenendo ule wa kwao wenye mazao,mvua yenyewe imenyesha nyingi na utegemee kipindi furani tena,kwani hata hivyo ulivyokuwa unavitegemea vimefanya kuharibu vipya vinginevyo,zimebomoa kabisa hata yale waliyojenga wao,huu kumbe ni mda wa kupanda,ingawa wapo wale watakao vuna mavuno yatakuwa hayana nguvu,unapofanya kwa mmoja wa pili huwa anasogea,kwani mbele au nyuma ni kule aliko yeye ndio kutamtambulisha.

Muda bado unaenda.ikiwa umeelewa kwamba unahitajika kuvuna na kupanda mazao bora ni lazima ujue kama na hiyo mistari imenyooka,maana haitakuwa vyema pamoja ukaweka na visingizio,hapa usiite majina ya kiujumla.kumbe kunyoosha ni kuelekezwa,ikiwa shambani na ukaelekezwa upande vile natukapanda tofauti haitamaanisha kitu katika ukubwa wako,mtu na maamuzi yake ndiye akaamue sahihi kile cha kupanda,ili aje avune hicho,sio tegemezi ya kupandiwa mazao alafu ukalalama wakati wa uvunaji,eti na mpandaji usimwelewe alikuwa anafanyaje au mda wote huo alikuwa anategemea nini ikiwa wewe unasubiri,ingawa sio wote wakulima basi utajaribu kuwa hata mpandaji.maana itafutwa kwa yule angalau ameliona na kuligusa shamba,wengine wasifahamu mazao hayo yametoka mahala gani,wakasikia na wasielewe ya kuwa wapo mbali sana,vipindi huwa vinabadilika ikiwa ni shule utasoma hesabu,kiingereza na mengineyo yakiwa na maana..kama wakulima mwenyewe hujasoma na hujui kuhesabu sijui hizo biashara zinafanyaje kuendelea,ukatumia nguvu nyingi na zisiwe na maana katika malipo.


    Unapopanda upande mema,hata kama ni machache unavuna kwa namna hiyo iliyopo,na ni nani yule aliyepanda kichache akalalamika kuvuna hicho?labda usihesabu mavuno ukahesabu mbegu,na kila mbegu ije na vuno lake bora. 
      

By:Benson G.Makaya
Tel:+255714336657

Thursday, January 26, 2012

Makaya's Forum: HATA TUSINGEFIKA BILA MENGINE KUTOKEA.

Makaya's Forum: HATA TUSINGEFIKA BILA MENGINE KUTOKEA.: Kufika sio kuwahi,yaweza kuwa kuwapo ama kutangulia,na yale yanayotokea sio lazima kupanga kwani mara nyingi huwa hatupangi sisi zaidi ya m...

Makaya's Forum: UNAPOTAFUTA LAZIMA UTAMBUE UNATAFUTA NINI !!.

Makaya's Forum: UNAPOTAFUTA LAZIMA UTAMBUE UNATAFUTA NINI !!.: Kutafuta ni kuhitaji katika wakati Fulani pale mwanaadamu anapoihusisha nafsi yake kupitia mapendo ,tukisema watu wanaenda tu kutafu...

UNAPOTAFUTA LAZIMA UTAMBUE UNATAFUTA NINI.

Unapotafuta na kuhitaji kitu wakati Fulani pale mwanaadamu anapoihusisha nafsi yake kupitia mapendo ,nikisema watu wanaenda tu kutafuta maisha maswali yanaweza kuwa ni mengi tena isiwe ni kwenda tu baada ya kuulizwa unatafuta nini hata sielewi kama yalifichwa ila itakuwa ni ile sehemu iliyopo katika akili zako za kuweza kutafuta kitu kilichopo,kama ilivyo hesabu unaweza ukawa unajua majibu na usijue nini njia yenyewe,kila jibu linatokana na yale yaliyopo njiani pia ikiwa mtu ameishia gerezani kwa ajili ya kuiba si kwamba naye aliiba katika njia zake zote,yaweza kuwa alienda kwa sababu aliiba katika njia moja na watu wakapata kujua kuwa Yule ni mwizi,ni vigumu kuishi ukiwa unajua hupendwi,hata ikawa unapendwa basi chuki zikawa ndani ya watu wengine juu yako,hauwezi kujua wanaokuchukia bila ya wewe kuwa na chuki pia,ni kweli kwani hata ukamwona simba anapita barabarani kitakacho fuata ni kukimbia,na kama itakuwa wataamua wachache ndiyo wakaweze mdhibiti simba huyo,au useme vyovyote itatokea kwani matokeo huwa ni tofauti daima kama ilivyo kwa wanaotoa majibu na sio majibu yenyewe.katika maisha hakuna kujaribu zaidi ya majaribu

maisha yenyewe hayatafuti,yapo yamekaa yakiwa yana mengi mengine yapo mbali,yameonekana kwa walio lakini kwa wachache hawana budi kuinama uvunguni,kwani limeshakuwa sharti kwa kile cha uvunguni unachokihitaji kukiinamia,miguu haiji mikono bora endapo mikono ipo,na kama ungelizoea kula majani au miti nadhani juhudi za kupanda miti zingeongezeka,unatafuta pesa na hauelewi ununue nini,ikiwa unataka ununue.unatafuta pesa unakuwa na malengo ya kufanya vitu na vitu hivyo vinakuwa kama havikupangwa,kumbe pesa sio kitu  pekee kinachomuzesha mtu kufanya jambo,ikiwa unaweza kuwa na nia ya kutaka kufika mahala katiks maisha,unaweza kujua ni nini unahitaji  na tatizo sio kutafuta,sio nguvu,wala mtafutaji,ikiwa mtafutwa yupo na hata hizo sababu za kutafutia  zinaweza zisiwe na maana zaidi endapo mtafutaji  hajui pa kutafutia.

Ndugu yangu kwa chochote kinachotafutwa ni lazima kiwe na mlengo wa mafanikio,ndiyo hata watu walio na utajiri wamefanikiwa katika upande mmoja ya kuwa nao wana uwezo wa kupata kile wanachokitafuta,kumbe pesa ni daraja la mafanikio,na mafanikio ni mafaniko yenyewe.shabaha na mlengo unahitajika tena ikiwa mimi au wewe ndiyo unahitaji mafanikio,sijui itakuwaje ukipata unavyovitafuta,sijui unatafuta nini maana kwa kujua unachokitafuta utaweza kuelewa itakuwa ni namna gani pale utakapo pata,na ukipata ijulikane,maana kama ni pesa wengi wamezipata na wanazo ikiwa haujasikia mmoja wapo akisema nimezipata.lakini ya kuwa mtihani wanafanya wengine,wanasahihisha wengine na washangiliaji watakuwa wengine pia,kwa yule anayefanya mtihani ijulikane amelenga kupata maksi gani.

By:      Benson G, Makaya,

Wednesday, January 25, 2012

HATA TUSINGEFIKA BILA MENGINE KUTOKEA.


Kufika sio kuwahi yaweza kuwa kuwapo ama kutangulia,na yale yanayotokea sio lazima kupanga kwani mara nyingi tunasema hatupangi sisi zaidi ya Mungu.Yanayotokea mengi kwa sasa unayafanya kama historia ikiwa kwa muda wake umepita,mengine ndiyo yale yanayokupa sifa zaidi,ikiwa sisi nasi tunasema tumeyatenda hayo!!bila hao watendaji hata historia isingekuwepo kwani ingawaje yanatokea kwa sababu nyingine lakini ingeleta utofauti katika kuifikiria historia yenyewe,ulipo ndiyo hasa unapopahitaji,ikiwa hautaki kufanya historia basi ikaonekane imefanyika utakavyo,maana kama kweli isingefanyika hata kwa watakao kuwa pembeni wana haki ya kuonyesha kidole na kusema wale hawatafika,isipo kuwa endapo wao walitangulia na sio wale tuliopo katika safari moja,kimya maana yake kutokuwasiliana kwa hili sio ambalo limekusudiwa au lile lililotokea,unaweza kukaa kimya na kufika mahara halisi,hii ikiwa na maana sio wao tu unaweza kwa kufanya yale yaliyoandaliwa ikiwa unataka mafanikio,au kufika mahala Fulani ambapo moyo na fikra zinaweza kutulia.Kwa fikra unaweza kuwa mbali sana machache yanaweza kutokea na kuonekana kwamba yale yaliyokusudiwa hayataweza kutokea,yanayokusudiwa mara nyingi huwa ni mema mbele za mtu tena ukitaka Mungu ayabaliki ikiwa unahitaji mafanikio katika mambo uyafanyayo,kwa upande wa Yule anaeifikiria dhambi na akataka nayo imwokoe nina imani itamwokoa katika namna yake,kwani mvuvi ukimpa samaki ndiyo chema chake yaweza kuwa ni tofauti na maana na yanapotokea huwa ni halisi inapowezekana ni kuyakubali ndio matokeo.

Pengine unahitaji kuandaa pale ulipoandaliwa,kwa yale yaliyotukia ndio hasa nami nimepata ya kuyasemea,ingawaje utofauti upo lakini mara nyingi ukawe katika fikra kwani kila mtu anafikiria vyake yakuwa matokeo huja tofauti,na pale inapofika kipindi umegongana yaani upo katika namba moja ikiitwa sambamba sio kwamba ndiyo upo sawa katika yote kwa mwengine,ingawa ni kweli matokeo ndiyo hutoa majibu lakini sio majibu yote huwa sawa ndiyo maana mara nyingine unafanya vitu tofauti na ilivyo ikiwa unajua kabisa ni namna gani inaweza kutokea,labda ndiyo useme yatakuwa ni mawazo au fikra potofu lakini kila mtu ana njia yake na si lazima wote kupita njia moja bali lengo liwe moja,hili tunaposhindwa tusaidiwe na matokeo,kama ikiwa wanafunzi wamefeli sana basi mtihani ulikuwa ni mgumu, Mahala pazuri ndio wengi tunapenda tufike hapo,tena ukiwa na hamasa pia ya kufika huko,uangalie unaposikia maana hata dakika inapoamua kusogea mbele husogea hauwezi kuamua na kurudisha masaa nyuma zaidi utakuwa unajirudisha mwenyewe nyuma,na hayo yatakuwa matokeo yako ingawaje muda ulishaandaliwa ila wale wenye lengo na muda huo unaporudi nyuma watakuwa wamefanikiwa pia,na ikiwa kila mtu anayo yake basi kila mmoja akapate kuamini kile anachoweza swala la msingi ni kuweza kupata ushindi,na tukapongezane kwa ushindi huo,ikiwa mambo yatakuwa magumu tusikimbiane maana wengine bado watakuwa njiani,kama vile kabla ya mafanikio kuja na wengine wakiwa nayo hayo mafanikio
.
Maana hii isije kuleta vita tena vita itakayo nyong’onyesha viungo vya mwili,ingawaje vita inapokuja ni maelewano ndiyo yanayotakiwa,unaweza kuwa bora kwa kuyaangalia mengi lakini yasifike yote labda useme unaangalia machache na hii ikaeleweke ni kwa upande wangu maana kwa wengine wameonekana wakiwa na mambo mengi ni namna vile fikra zinavyotutuma,ili kupita baada ya makosa ni lazima kufikiri ikiwa unataka kupita mara ya pili,maana unatakiwa kuacha alama ili atakaye pita kwa mara ya pili aone,ukiwa amepita mara ya kwanza ukijitambue ndiyo ya pili ya wengine na ili usichanganyikiwe na maneno maana hayo huwa yanayumbisha hata kama yale yaliyotakiwa kutokea yalikuwa na ulazima bila shaka ndio maana umefika hapo.
MSHUKURU MUNGU kwa kila Jambo.

By: Benson G.Makaya

Tel: +255714 33 66 57.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS