Wednesday, January 25, 2012

HATA TUSINGEFIKA BILA MENGINE KUTOKEA.


Kufika sio kuwahi yaweza kuwa kuwapo ama kutangulia,na yale yanayotokea sio lazima kupanga kwani mara nyingi tunasema hatupangi sisi zaidi ya Mungu.Yanayotokea mengi kwa sasa unayafanya kama historia ikiwa kwa muda wake umepita,mengine ndiyo yale yanayokupa sifa zaidi,ikiwa sisi nasi tunasema tumeyatenda hayo!!bila hao watendaji hata historia isingekuwepo kwani ingawaje yanatokea kwa sababu nyingine lakini ingeleta utofauti katika kuifikiria historia yenyewe,ulipo ndiyo hasa unapopahitaji,ikiwa hautaki kufanya historia basi ikaonekane imefanyika utakavyo,maana kama kweli isingefanyika hata kwa watakao kuwa pembeni wana haki ya kuonyesha kidole na kusema wale hawatafika,isipo kuwa endapo wao walitangulia na sio wale tuliopo katika safari moja,kimya maana yake kutokuwasiliana kwa hili sio ambalo limekusudiwa au lile lililotokea,unaweza kukaa kimya na kufika mahara halisi,hii ikiwa na maana sio wao tu unaweza kwa kufanya yale yaliyoandaliwa ikiwa unataka mafanikio,au kufika mahala Fulani ambapo moyo na fikra zinaweza kutulia.Kwa fikra unaweza kuwa mbali sana machache yanaweza kutokea na kuonekana kwamba yale yaliyokusudiwa hayataweza kutokea,yanayokusudiwa mara nyingi huwa ni mema mbele za mtu tena ukitaka Mungu ayabaliki ikiwa unahitaji mafanikio katika mambo uyafanyayo,kwa upande wa Yule anaeifikiria dhambi na akataka nayo imwokoe nina imani itamwokoa katika namna yake,kwani mvuvi ukimpa samaki ndiyo chema chake yaweza kuwa ni tofauti na maana na yanapotokea huwa ni halisi inapowezekana ni kuyakubali ndio matokeo.

Pengine unahitaji kuandaa pale ulipoandaliwa,kwa yale yaliyotukia ndio hasa nami nimepata ya kuyasemea,ingawaje utofauti upo lakini mara nyingi ukawe katika fikra kwani kila mtu anafikiria vyake yakuwa matokeo huja tofauti,na pale inapofika kipindi umegongana yaani upo katika namba moja ikiitwa sambamba sio kwamba ndiyo upo sawa katika yote kwa mwengine,ingawa ni kweli matokeo ndiyo hutoa majibu lakini sio majibu yote huwa sawa ndiyo maana mara nyingine unafanya vitu tofauti na ilivyo ikiwa unajua kabisa ni namna gani inaweza kutokea,labda ndiyo useme yatakuwa ni mawazo au fikra potofu lakini kila mtu ana njia yake na si lazima wote kupita njia moja bali lengo liwe moja,hili tunaposhindwa tusaidiwe na matokeo,kama ikiwa wanafunzi wamefeli sana basi mtihani ulikuwa ni mgumu, Mahala pazuri ndio wengi tunapenda tufike hapo,tena ukiwa na hamasa pia ya kufika huko,uangalie unaposikia maana hata dakika inapoamua kusogea mbele husogea hauwezi kuamua na kurudisha masaa nyuma zaidi utakuwa unajirudisha mwenyewe nyuma,na hayo yatakuwa matokeo yako ingawaje muda ulishaandaliwa ila wale wenye lengo na muda huo unaporudi nyuma watakuwa wamefanikiwa pia,na ikiwa kila mtu anayo yake basi kila mmoja akapate kuamini kile anachoweza swala la msingi ni kuweza kupata ushindi,na tukapongezane kwa ushindi huo,ikiwa mambo yatakuwa magumu tusikimbiane maana wengine bado watakuwa njiani,kama vile kabla ya mafanikio kuja na wengine wakiwa nayo hayo mafanikio
.
Maana hii isije kuleta vita tena vita itakayo nyong’onyesha viungo vya mwili,ingawaje vita inapokuja ni maelewano ndiyo yanayotakiwa,unaweza kuwa bora kwa kuyaangalia mengi lakini yasifike yote labda useme unaangalia machache na hii ikaeleweke ni kwa upande wangu maana kwa wengine wameonekana wakiwa na mambo mengi ni namna vile fikra zinavyotutuma,ili kupita baada ya makosa ni lazima kufikiri ikiwa unataka kupita mara ya pili,maana unatakiwa kuacha alama ili atakaye pita kwa mara ya pili aone,ukiwa amepita mara ya kwanza ukijitambue ndiyo ya pili ya wengine na ili usichanganyikiwe na maneno maana hayo huwa yanayumbisha hata kama yale yaliyotakiwa kutokea yalikuwa na ulazima bila shaka ndio maana umefika hapo.
MSHUKURU MUNGU kwa kila Jambo.

By: Benson G.Makaya

Tel: +255714 33 66 57.

1 comment:

Makaya Forum said...

may God bless you leaders..

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...