Thursday, July 5, 2012

ITAKAVYOKUWA.

Na kama ni ndani ya familia iwe ni mzazi ama mtoto ndiye anayemwambia mmoja wapo hapo ujue kuna namna,ile iliyokuwa kama vile katika namna,mtanisamehe sana ndugu zangu kwa kuwarudisha nyuma,maana huko mbele vyovyote itakavyokuwavyo sawa tu,sio kwa wazazi ama kwa watoto,vyovyote vile..

Mara nyingine usisema ni kauli gani wakati hautajua ni kwa sababu gani,maana hata ya kusema ni ile ya namna gani tu,uliporudi nyuma uliwakuta mababu zako wakikuambia,maana ulisikia,kwa yale yote yaliyo mabaya ni yale waliyoyasemea,walisema mengi ndiyo maana haina haja ya kuwaambia nyinyi,wale walio watoto maana muda si wake,unaposema itakavyokuwa si ni ile ile ni  iliyopo inayoendelea kufika mahala Fulani,hapo useme umepita muda mrefu sana sijalisikia swala lile.ndiyo itakavyokuwa hivyo

Ngoja ngoja itakavyokuwa ikaumiza matumbo,kama samaki mkunje angali mbichi akitaka kunyooka mwache kwani atainama kukiokota kilicho sharti,maana kipo chini,lazima kurudi mwanzo,maana kama utaendelea kunyooka utakiuka waliyosema,sio ya kijinga yale,yalikuwa ni kwa ajili yako,uchambue yaliyopo maana mengine yanaelekea kuoza,yasije kufanya na yale mabichi mengine kushindwa kukunjika.

ukisema kwani imekuwaje ndiyo ilivyokuwa,na mara nyingine haiwezi kuwa bila nyingine kuwako,kwa hiyo vile ilivyo ndiyo vile itakavyokuwa,uangalie muda tu,muda unaenda sana,siku hazijirudii ndiyo maana haiwi tena ,nyingine namna tu,na hata sijui kwanini zimekuwa haba kwa namna ilivyo,maana ingepasa kila mtu kuwa na siku yake,na kama ipo basi neno itakavyo kuwa lisingekuwepo,ungetamani siku yako ije tu,na utatamanije kila siku?itakavyokuwa ndiyo hivyo hivyo..maana wengine wameshaelewa ilivyokuwa.

MDUNDIKO..!!


Mpira unapodunda sana,maana hata control zikakushinda,umekuwa kitenesi hata katika namna ya kukidaka ikawa mzozo,pengine kwa ajili ya hawa unaowaona,hata ikawe hujui umeona nini namna gani ipi yaani mpaka ikaeleweka ile ni kwa nguvu na nyenzake kwa akili,ikiwa hatujui imedunda ama imepaa maana nguvu ya juu hutegemea na ya chini vile ilivyo kwa kipimo cha akili yakiwa yanashirikiana katika kuyasogeza marefu na mapana.

Vingi vinapaa lakini hatuelewi vinapaaje pengine ndiyo vinavyotembea hivyo,vinadunda yaani,ilivyo muda usemekao zamani watu walikuwa wakitembea miondoko Fulani ya mdundiko walionekana wahuni,muda huu imezoeleka kwani unajidundia mwenyewe,wee dundaa na badaye utaeleweka maana ndiyo itajulikana nguvu zako ulikuwa unazitumia katika upande gani,hakatazwi mtu mara mbili asipoelewa ni aendelee na yanayompa nguvu kuyafanya kwa wakati huo

Hata kumbe mipira mengine siyo yakuitumia hiyo wanasema inachezeka hata mchangani,sijui kwa nini isingekuwa haiwezekani,kurudi ni kufuta maana iliyopo ikiwa  nguvu iliyotumika katika kudunda kwa mara ya kwanza na kushindwa kufikia mara ya pili kujaribu tena hapo unakuwa umefuta,sio adhabu ni mazoezi ya kuweza kumbe hata mpira unapojaribu kudunda hutafuta mahala panapoleta maana,hapo utasikia ule umetoboka,basi hapo ujue kuna mtu kakosa lengo.

Dunda ndugu usiogope uwanja wako,maana makelele tumeyasikia na pengine yangekuwa kiburudisho hivyo vingine uviite kukua kwa lugha maana ukafikiri yametokea kwenye nguvu ama pasipo tumia akili ,kwa sababu ya kudunda huanza chini ikiwa na lengo la kuelekea juu au huanza juu ikiwa na lengo la kuelekea chini.Chagua namna unaweza,fanya vile unaweza.

Sunday, July 1, 2012

CHAPA NG’OMBE.


Ni kauli vile mchungaji akimwambia mwanafunzi wake,maana sio kila mchungwaji anachungwa na mchungaji mwema,wengine si katika maovu bali ikiwa bado kutokujua kuelekeza,yaani wewe ng’ombe usipite hapo ni lazima na viboko?maana bora hata Ukamsukuma pengine mnaweza kusikia yaliyo karibu naye akalalamika tu,mnachapa sana ngombe hawa hii ikiwa ni historia ya kwamba ni bora akawa anachapwa chapwa hapo ukiwa unataka ngozi ,yeye yule sasa akiwa ameumbwa kama mwanadamu,ya kuwa na kizazi,yaani wote ni binadamu..sishangai pale unawaita watoto mbwa,ni mbwa pekee anayeweza kumzaa mbwa.

Labda utafute madawa ya kukaushia ngozi,maana ng’ombe wameskika wakilalama sana,ingali na viboko hivyo imekuja hata wanyonyaji,hata muda wa malishoni kwa ngombe imekuwa taabu,fikiri mchungaji anapolala hulala na usingizi upi na Yule ngombe alotoka machungoni kwa viboko?maana hilo la mchungaji sijui ndiyo kuendeleza nchi ama ni kutengenezana baadaye wakapata maziwa ndani yake,hutajua maana ya kiboko cha mgongo ni uelekeo wa wapi zaidi ya kutia maumivu.

Katika lile linalomuumiza mwanadamu ndiyo lile au yale yaliyotukia na furaha,maana hata mwisho wa sukari ni uchungu,pengine mchungaji utuulize kuhusu utamu wa viboko hivi,maana si kulalama,ila isemekanavyo maumivu yakizidi umwone daktari,sasa kama daktari amegoma  haya maumivu yanatokea wapi ikiwa yule daktari ni mwanafunzi,angelikuwa mwalimu asingekubali kuikosa heshima yake uelekezani,maana ni wito huo na mchungaji punguza namna ya nguvu zitumikazo kuchapia ng’ombe wako,maana kuna wale wenye vichaa,wakiruka kile cha kukanyaga  ni kesi yako mwenyewe,maana utaelezea imekuwaje hata viboko ukashindwa kuchapa,au vilichapwa kwa namna ya utofauti yaani yakaanza maumivu na kichapo kikaja baaadaye.

UCHUNGU


Uchungu wa uzazi aujuae mzazi,tena ikiwa Yule anayeujua uchungu katika kuzaa,hapa isiwe nazungumzia uzazi,pengine tukafikiri ni namna  gani pale ikaeleweka Fulani ana machungu..si ya kuwa kwa kwengine ikajulikane namna hiyo,bali Yule aujuae uchungu,akauelewe kwa vile uumavyo,kumbe ni maumivu,kumbe uchungu unauma,haya si mambo ya Kiswahili,pengine tusitake ya kizungu ila yakawe yanaeleweka basi..nakubali katika lile mtu asemalo,kwani kweli yake ipo humo,humo anakuwa ameamua yeye maana ni mahala,kama ilivyo pale,yaani ndani humo,pengine ni duniani,yakuwa machungu yameonekana kuwa mengi,duniani kuna maumivu..!!

Sikatai hakuna kulalama,pengine tukawaruhusu wezi kutuibia,maana kama hatutasikia machungu basi wezi endeleeni kuiba….maana ifike wakati hatujaelewa kwa nini wanaiba,maana hayo si ndiyo maovu..mengine machache lakini si yote hata hili moja linatosha sana,katika kifo cha mwizi kinatia uchungu sana,sijui Yule anayaekufa huwa anasikia maumivu gani?ikiwa hatujaelewana nitafanya kurudia,lakini tukubari na machungu yatakayo tujia,maana tunyoshe mikono haya tumeyashindwa,na tusiposema hivyo lazima tuulizwe yaliyopitwa…hapo ndiyo tutaona machungu,maana yalipitwa na imepasa kuyarudia,’ni kazi kubwa kuirudia adhabu’

Kila ya jana yanaisha ninapoamka asubuhi,hii ikiwa nimeamka,nafsi yangu ikiwa inaniambia kufanya kile kizuri cha jana kilichobaki,maana ndiyo kitaleta kesho,hapo nikiwa naogopa machungu,sasa huyo sio mimi na mimi nitasema machungu yangu yapi?ama iwe mimi wa sasa ndiyo kama mimi..hapa nimezunguka sana,baadaye itaitwa mizunguko,maana ikinyooka wanaita minyooko labda iwe na majungu,yakifikirika kinamna yoyote tofauti na msemaji hayo ni majungu,,maana si vile kila mtu ana machungu yake naye afanye yake,ikiwa kila mwanadamu hapendi kulia uvunguni.

Friday, June 29, 2012

MKUTANONI..


Mara kwingi ninapotoka ninakutana na watu wazuri,wakiwa wao ndiyo wao hasa ndiyo ikawe hata maana ya kukutana,pengine tukimaliza mkutano upate japo neno jema kwamba karibu kwenye mkutano,sijui ikiwa imetendeka nini ndani humo,maana kabla tulisema bila kujuana,pale ikaenda kimeisha kikao tupeane karibu,hizi zikiwa na maana ya sijapenda ulichokifanya na vile karibu sana,maana utasisitizwa hata siku nyingine,hapa sio kujua kwa kuwapo,ni kujua kwa kuelewa,tumejuana kwa kukutana.

Pengine sio bahati mbaya ila ni nzuri iliyokuwa na ubaya,kama vile jamaa alisema kuhusu mwongo ya kwamba ” Kuna mtu anauongea uongo si kwasababu amedhamiria ila ni kwasababu anajua huo ndio ukweli huyu hawezi kuwa mwongo, bali huyu haujui ukweli”.kwa kweli sio kosa la kukutana,bali ni vyema tumekutana ili kuelezana,pengine kila mtu awe na lake ili kuweza  maana,pengine ili kucheka zaidi ama kununa,maana ya kununa siijui zaidi yake,pengine ni kufa tu..

Sasa si italeta ugomvi,tena itakuwa ni bahati mbaya,maana kuna watu wanajua kununa kweli kweli,hapo bila ya kujua wanapoteza namna ya kucheka,kutabasamu..maana maisha ya mwanadamu aliyefanikiwa kiroho na namna awezavyo ni kucheka,hata kutabasamu maana ni mwanzo wa kucheka.

Hakuna maana ya kusema wewe ni nani wakati wewe ni nani,maana inahitaji uje kwa adabu tena ukitaka kusema wewe sio nani,maana hakuna aliyekutilia maanani,’hapo mwanzo alikuwepo sungura na fisi’,hadithi hizi hatuzitaki siku hizi.asante sana kwa kukutana maana imefika kipindi nimekueleza hata yale ya jana,ngoja kesho ije tutafayaje kama sio kusikiliza ya jana?kama umeyaacha mawili kayachukue,ikiwa haiwezekani ingia hivyo hivyo mkutanoni.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...