Thursday, September 20, 2012

KATIKA KUJILINDA...

Hakuna kusamehe kama inakuja nakukumbushiana,maana bila ya kupata baadhi ya machaguzi pengine hata ingalikuwa ni kifo maana kwa vitendo vinavyotendeka yaweza kuonekana kama umeona kumbe ni swala la kukimbia majukumu na kukata tama katika yale unayoyafanya,mwanzo ukitegemea uwe mwisho pengine utasubiri sana kwani inapoisha huwa kama inapoanza,pengine tukiweka katika jambo lolote na  ya kuwa ni msamaha basi isiwe kama ni ugomvi,ili ikiwa ni mwanzo kweli mbio ziokoe taifa.
Mageni mengi ndiyo yanayotaka usaidizi ikiwa ni mwanzo wa kutaka kuelewa ama kutokuelewa kwa lolote,pengine mambo kwa walio na mengi ni bora kuanza na machache kwani katika kushugulika na mihangaiko ya huko kukutana na wengi,ya msingi yakiwa ni mengi kwani hayo ndiyo uliyonayo,siyo kwa mahesabu ama hata tukianzia enzi za mababu,kwa walio na usaidizi bora kupunguza maana ni sawa na kuleta inzi kwa kutaka mateso kuendelea.
Katika kujua ni zaidi ukajua kuweka ,maana utawekewa na usijue lolote,pengine ujue kuwekewa lakini si kuweka , kwa wengine utasikia karibu wakikupa chombo wakijua unajua,pengine isiwe katika namna ya kutengeneza na tukajaribu kutafuta maana kwa mpangilio uliopangwa unachanganya sana,pengine haikupangwa vyema,ama hujajipanga,na ili uwekwe katika ubora na kiwango ni lazima kushukuru kwa hofu zote maana zaweza jirudia usijue kama ulipitia.

INAPENDWA POCHI...


Pochi ni sehemu ya hifadhi katika yale mwanadamu anayoyaona anayaweza ikiwa katika kuweka ama umbile kwa namna ya kuleta muonekano mzuri,leo nasema ikiwa kwangu kesho kwako,maana kama itakuja leo kwangu,ikaungana na kesho kwangu basi jua zinazofuata ni zako tena mgawane maana hata katika pochi zimeisha,ikiwa za mfukoni hamzipendi kwani ni wazi sina usafiri na pengine ikawa ni chenji  katika mizunguko.
Napenda pochi kwa hifadhi langu nililonalo,wanaopenda pochi ni kwa nafsi zao walizonazo,maana wengine hawatembei na pochi lakini kwa namna ya wenzao wanavyozipenda pochi zao ni hali ya kushangaza kwa kushindwa na hata kubembelezana,mara nyingine ni vigumu kutoka kwa lazima zaidi ya vile ilivyoandaliwa,ukiwa hauna namna ya ubebaji katika hitaji kwani pengine tukajadiri dini,maana na pochi zetu zahitaji Baraka zake.
Tusije tupiana lawama kwa yale yaliyovuruga amani,maana kwa pochi za malengo huaribu sana sherehe.nakupenda hata usiku nakuwaza,tena kama ingalikuwa ni nyimbo basi ningekupigia hata nyingi kusambaza,maana katika kuelewa namna ulivyokuja na kuondoka ukiwa mfuko umetoboka basi kwa wabeba kubwa ,watufichiee na zetu ndogo humo.

SIMBA WA YUDA.


Akiunguruma wageni wakiwa kwa wingi maana wao wamechangia sana,na hapo zamani za kale kabla ya kuanza moja alikuwapo kueshimika simba wa yuda,ukaogopa ukali bila ya kujua matumizi na kwa yale na lile ulilopewa.machache yakaonekana ya shetani kumbe katika kiumbo bado haijafikirika,ikiwa unaweza kuchoka na kufutwa jasho tafuta kifutio,kikiisha bila ya kujua namna ya kufuta hapo shari,ingali hata kifutio huna ungesaidikika.majasho yana ishi.
Unaweza kulia kwa kufanana matendo na kusahau kushoto kiama,kwa sauti zitokazo zikiwa zinaimba ni namna ya mwituni akiwa wa yuda simba,leo akitaka majani yu radhi kupata ya kuwa anaunguruma,tena si katika namna ile ya kupokonywa majani hayo,ukilazimisha utamu wake.wachache wengine wakijaribu kufuga simba wao wanakuwa hawaungurumi ya kuwa wamefungwa koromeo,ni midomo ilionekana mwanzo,na ikaeleweka namna ya mwanadamu anavyoongea.
Leo nimekuja na nimepata mengi sana,ikiwa kuambiana kama hujasoma kwani kusoma nini?maana heli ya ubaya kuliko ubaya wa uzuri.Kheli aje simba wa yuda maana kwa mengi yasiyoeleweka kueleweka,ikiwa umesoma basi si vile ilivyo katika shulekusoma,maana yenyewe ina mengi ya kufundisha,kukicha kesho kubali kuwa umeelewa,ukitaka kujua umeelewa vipi,kujua namna inavyo unguruma.

Wednesday, September 19, 2012

MIMI SI KITU

Maisha yangu yameniweka kuwa kitu cha muhimu katika maisha ya watu wegine,hii hainipeleki kuwa kitu cha maana katika vile vingine na la mtu huyo mwingine,nikiamini uzima hauji kwa mmoja pekee,ingawaje tumeumbwa na tukaamini basi kila mtu akashike hilo analoliamini,ona malengo na namna ya kuweza kuyafanikisha kwani yale mema yanakuwepo ndani yako,tena lazima ujue mafanikio ni namna unavyofurahi kwa vitu unavyoviona.,lakini ikiwa  furaha yako ni kuweza kuungana pamoja katika kusafiri ndani ya dunia,yaani maisha tunayoishi,na kila kitu ndani yake vikiwa si kitu zaidi yetu.
Mimi si kitu,lakini katika safari hii kamilifu kama sio uharibifu ndipo unaanza kutokea kwani kwa wengine kitu cha ukamilifu ni uharibifu upande wake,fikiri kwa isiyo kuwa nzuri ikapendeze maana si lazima iwe nzuri pengine hata ikatakikana sana,kama ingalikuwa safari yangu ni sawa na jaribu japo la kufanya kubadili yale yaliyo wekwa kwa kudhani pengine ni ya hatari,kwa muda uliopo mdanganyifu basi nina mengi ya kufanya,mengine nikiwa siyajui nikiomba kwa mwenyezi japo nguvu za kushindana kuwapenda maadui.
Kila kitu kipo sawa,kila kitu kina maana ya kuitwa kitu,kama vile ulivyo wewe kwa mzazi wako,nani ukamwita baba na mwengine ukamwita mama,hiyo yote ukiwa unajua kuwa dada siyo mama,sisi ni kitu kimoja mimi na wewe,tunaumia pamoja na ingawa tusipokuwa kitu pamoja.furaha ya safari inapatikana ndani ya safari,hivyo tumai la maisha  lina ulazima kulitupia maishani yakiwa ni maisha  yakiafrica,maisha yaliyojaa uasili na  na hisia
inayotia ukakamavu machoni,ikiwa na maana ya nguvu. .

Friday, September 14, 2012

YANAWEZEKANA LEO.

Nilijua ilikuwa ni mara yangu ya mwisho kukuona na japo kukusabahi,maana pengine ilikuwa ni dakika za mwisho kwa lile lilotakikana jana likaja leo,hapo nikawa nimekuchelewa kwa kutokuwahi muda,maana itakuja kila siku na kuona kwamba yaliyopita ndiyo ndwele,hapo chululu tukitaka kujua maana,isisemeke na kujulikana kama imesahaulika kwani katika upendo unaweza kuwapo hata kwa adui yako,leo nikisema na kesho ntaweza kurudia,maana nikiwa na hitaji la kutokusahau.

Leo ikiwa imekuja haijaja kwa ahadi kwamba ndiyo imekuletea vizuri,gari,tunapenda sana magari kwa kutaka kusafiri na kuelekea kusikojulikana,kwa kijana ama kenda umri namna gani leo ikitakiwa kuwa ni siku ya nafasi,kwa vile vinavyopendeza vikashikana ili kuzuia mmomonyoko,si ya kuwa yakidondoka kwa uzembe wa kutokujua uongozi na kusahau kusubiri kesho wakati kuna leo,pengine tukifuatana na ya jana ili kuleta maana.

Unaweza kulaumu siku yako kwa kutokuona kesho inakuja,maana hiyo na hayo ni mafanikio tu,pale unapopenda una chukua muda ikiwa hakuna makosa na haina haja ya kulaumu,ama hapo ndiyo tuamke na kusema samahani,makosa mengine waweza yafahamu mwenyewe kwa kutokujua kulaumu kesho.ikiwa aliye na hitaji na kuishi na kufanya yeyote anayoyaweza bila kungoja kesho.

Thursday, September 13, 2012

VIPINDI...

Ukiwa ni mtoto,pengine ndiyo unazaliwa,ama vile ilivyo ,hapa nikiwa na maana katika maumbile na namna ya vile tulivyoumbwa,pengine wengine wakaumbika,kutokana na kile walichokipokea kwa kutazama kujua ama kutokujua,nyingine zikiwa kama ni sheria za kuishi,ikiwa unaweza kuzipenda ama kuzichukia,lakini hiyo itakuwa ni yako,pengine sababu katika kipindi chote kinachozunguka  maisha yako ,hapo ni lazima kujifunza,tena kujifunza hata kwa kulazimisha kipindi.

Hivyo ikiwa kama umejiunga katika shule,pindi tokea pale ulipozaliwa,katika kila siku ya mungu utapata nafasi ya kuweza japo kuelewa zaidi ni nini kinachofundishwa katika vipindi hivyo,tena kukiwa hakuna makosa ni vipindi tu,hapo ikiwa utavipenda,utavichukia pengine hata kutoa machozi kabisa,hapo ikiwa kuna kukua kwani ni jaribu la kosa na kile kifanyikacho kwa matendo.yale yanayofanyika kwa kushindwa pengine hutokea na kuwa kamili.

Vipindi huwa vinarudiwa mpaka vile ilivyo ieleweke,ikiwa kipindi hicho kimekuja katika namna ya kutaka watu welewe,na baada ya kumaliza ukaelekea katika kipindi kinachofuata.vipindi havina mwisho,hakuna maisha ya mwanadamu yasiyo kuwa na vipindi,kama uko hai basi jua kuna kipindi japo kimesomeka,hata wakati wengine wakiwa kama mahala ambapo kipindi hicho kitafanyika.

ANZA UPYA..

Ni katika kuanza mwanzo,pale ikiwa kuna makosa ama ni njia mpya,ikiwa unahitaji la kuwa peke yako ama kukaa gizani ikiwa jua litawaka kesho,hivyo ni lazima kufanya katika uwezo wako ili inayofuata ije vizuri,pale inapofika kipindi cha kuanza upya,moyo ukiwa na yake kama mistari ya rangi ikiashiria mvua kunyesha pasipo taarifa,ama ni kuzuia endapo italeta uharifu.miaka haita weza kuchukua vile ulivyofanya,ikiwa nafasi ya kuanza upya ni pekee kwa sasa,hivyo bado ndoto zitakuja kweli.

Ukiwa muda uwapo na upweke sio peke yako,njia yaweza kuonekana nyembamba ikiwa hata sauti hazisikiki,pengine sauti ndiyo zikatembeze nafsi,pale unapokuwa peke yako,hiyo ikiwa umeishia hapo unasubiri kile maisha itakuletea,katika kila maisha ikitakikana asubuhi njema,kwa mabaya ya maisha kuyaacha na kuchukua nafasi yako iliyo mpya,pengine ikiwa ni muda wa kufanya vile uvifanyavyo,yaani ipasavyo.

Magumu huwa yanaonekana baada ya kufanyika ikiwa haikueleweka mwishoni utasikia ‘nilijua’maana hata ya kushindwa yanajulikana,na hii ikiwa kwa kufahamu ama kwa vile ilivyo inavyoweza kwa makosa kuyafahamu,maana kwa kipindi kilichopo yahitaji kuwa kiongozi bora ndani ya maisha yako,ukiwa kijana anza kwa kuweza hata kuendeleza maana yote yanayokuja ni baadhi ya yale uliyoyafanya mwanzo.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...