Saturday, November 10, 2012
Makaya's Forum: SHUKURU KWA YOTE..
Makaya's Forum: SHUKURU KWA YOTE..: Hapa akihusishwa mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake,inapaswa kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito umeifanya,ikiwa una uelewa ni ...
SHUKURU KWA YOTE..
Hapa akihusishwa Mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake inapaswa kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito
umeifanya,Asante Mwenyezi Mungu.
Ukiwa una uelewa ni lazima kubaki katika njia ambayo wewe mwenyewe
unaiona siyo ya mapumziko maana ni lazima kutoa nguvu Pamoja na akili yako ukiwa umeamka na
kuchagua kile ambacho wewe umetaka kukiangalia,ukichagua lile ambalo limekuja
katika muda unaofaa kimaendeleo,ikiwa maisha ni sehemu inayofanya ndoto kukamilika,ki imani
ikiwa kama ndoto ni jibu la tatizo.pale unapomaliza jambo yapasa kushukuru kwa
kuwa linakuwa vile kidogo ya ulivyofikiri,huwa yanafanana lakini rangi tofauti na kuthaminisha kule/kile/vile ulivyofanya.
Kama una ndoto ya kuwa na furaha ama vile katika hali
isiyofahamika,kama unapofumba macho ukitegemea kuona chochote mengine yatapita
yakiwa ni afadhali kwa kuwa yatastahiri kukuchanganya,shukuru kwa kuwa siyo yote
unayoyategemea hutokea ,mengine yakiwa yameletwa maksudi ili mradi na wengine
wakapata shukrani za lazima,lakini ikiwa kama mtu ameamua kufa kwa kujinyonga
akipona hastahiri kushukuru kwani lengo lake halijatimia.
Pongezi kwa shukrani iliyomaliza jambo,hongera hutoka pale
shukrani inapokuwa na jibu lake katika jambo husika,maana katika namna ya
kuzaliwa kwa sisi waswahili zinaweza kuwa ni kejeli,ikiwa unataka kuona ni nini
unachokifanya haistahili kuuliza bila ya kuulizwa,hapa itatakikana kuonekana
mwisho ikiwa unakipaji chochote cha kufanya hakitaweza kulinganishwa na muangaliaji ama yule asemaye kwani mwishoni huja na kukuvisha taji.mawazo yako ndiyo mtaji shukuru Mungu wako alikuumba
wewe. hata ungali muda bado kuisha.
Friday, November 9, 2012
USIOGOPE,KUWA NA FURAHA…
Ni namna ya maisha yanavyokwenda,maana leo ikaja lakini siyo
kesho,ukawa na hofu ya leo maana ile ya jana nusu imeishia leo.. kama ilikuwa
ni chuki wazi ukawa na wasi wa kesho kuja na kukudhuru tena,usiogope kwa kuwa
haujui,na tena kuwa na furaha kwani ukijua hautaweza kuogopa,hivi muda
unavyokwenda unapelekwa na wewe,hivi kesho giza baadaye ujue unaileta
wewee...mwangaza wa kung’aa humulika mbali kwa kuwa huitaji kukumulikia,ikiwa
mazuri unayaogopa basi kuwa na furaha na mabaya ya baadaye.
Muda wa kutokuzungumza utafika,ile shule ya maisha yako
ukaja kuijua shuleni.tena ukajifunza mawili kwa kuogopa kujua lako moja,leo ukiwa
unajitahidi kesho utaweza maana njia ya mpita njia hueleweka yake kwa kuwa
hupita kila siku hapo kwenye njia yake,pengine ikiwa ni mara chache acha jina basi,maisha
mengine hayajulikani,hayo ndiyo maisha yako,pengine ukitaka kuyabadilisha ni
uyabadilishe hapo ulipo,ujibadilishe,ukaogopa kupangua kwa sababu ya uwingi wa kushindwa
kupanga tena jua unaidhurumu furaha yako,dhuruma mbaya maana hitaji lake wakati
wa kurudi ni FURAHA.
Sitaweza kuogopa kukwambia ukweli kwani naihitaji furaha
yangu baadaye,kwa Yule anayeogopa kwa kusema uwongo wakati ukweli upo,hafai
hata kujifunza jambo,maaana ataangamiza jamii kwa kutengeneza siraha inayodhuru
bila woga.pengine usiogope kusema utakavyo maana hautaishi tena,kama ikiwa ni katika namna tofauti,hata kama umewahi kusikia pale mtu akisifia “ahh yale
siyo maisha”..yapo yale yaliyo ni maisha pengine kama ulikuwa unaogopa kuuliza
ijue furaha yako.
Wednesday, November 7, 2012
MAZURI YANGALI KUJA.
Hapa nazungumzia nafsi ya kila mmoja,ikiwa hata wewe
leo ukaelewa iwe katika ndoa namna ya vile maisha yanavyokuwa iwe katika hali
ya kutokuwa katika ndoa na kukuta maisha yako vile vile jinsi yalivyo,maisha bado kwa wengine
yakiwa ya uadui tu,ikiwa unawaza kuanguka kamwe huwezi kuiona siku yako ya mafanikio.maana
mazuri huja baada ya kipimo chako cha kufanikiwa,pale ukaishi maisha mengi na yaliyo jaa
vingi,pale umetegemea mengi lakini hakuna katika yale uliyoyafikiria kutenda na kutokea,maana waweza
fanya mia leo na kesho kuja moja na kudhani yale mia yalikuwa ni kanuni,mazuri
yangali njiani,mazuri yangali kuja maana kama umefikiri sahihi lazima kuielewa
ile maana ya kwanza yaani sababu.
Kama yalikuja basi hongera maana pengine sijui mtu unaishi
ukifikiria nini,waweza kuota ndoto na kulazimisha kutokea,ikiwa umezani wewe ni
mkuu sana kwa nafasi uliyopo,ukijisahau kwa kuwa fikra zako ni zimekujaa wewe pekee,kumbuka hakuna
mtu anayemfikiria mwenziye katika namna mwenziye anavyomfikiria,ukiambiwa kuongea peke yako yapasa kuelewa hasa unaposikia ukidhani rahisi ama magumu yote.mazuri yangali kuja,hayo magumu ndiyo njia ya
kwenda kuzuri,ukiwa na furaha sasa jua ni yale marahisi yamewezakana,ikiwa mazuri yangali kuja.
Furaha ya mchizi ni kufurahi,pengine furaha ya mchizi ni
anaifahamu mwenyewe,ikiwa umeona mazuri siyo ya kwamba yamekuja ,angalia kesho
usijenuna na kupewa lawama,maana si furaha yako unaijua mwenyewe,anayeamini
anapata maana anakuwa ametaka akifikiri yatakayotokea,ikiwa mwanzo wa jambo basi una mwisho,wanaposema Mungu hamtupi mja wake siyo kila mtu ni mja wa Mungu,maana Mungu wa mmoja si mmoja yule wa amwaminie mwengine na pengine kesho ifikirike ili ya jana yakaonekana ni tofauti.
Mazuri yangali kuja...!!
Tuesday, November 6, 2012
MJUE WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.......
WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.. NI mshiriki wa EPIC BONGO STAR SEARCH ANAYETOKEA MBEYA,HIVI SASA AKIWA KATIKA FAINALI HIYO ITAKAYO FANYIKA DIAMOND JUBILEE IJUMAA TAREHE 9 MWEZI HUU..HAYA MACHACHE KUTOKA KWAKE MWENYEWE WALTER...
"Nashukuru sana watu
wangu, ni Maombi na Kura zenu tuu.. Nashukuru kuingia FAINALI na nakuomba
endelea na moyo huohuo kwa kunipigia kura kwa kuandika neno EBSS12 kwenda namba
15530".
Hiyo ni status aliyoiandika
Walter katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter jana baada ya kurushwa kwa
show yake ya nusu fainali iliyompelekea kuingia fainali itakayofanyika Diomond
Jubilee, Ijumaa ya tarehe 09/11/2012.
Pamoja na hayo Walter
aliongeza kuwa anamshukuru Mungu na watanzania kwa hatua aliyofikia kwani
haikuwa rahisi kihivyo.
Pia Walter ameongelea suala la
yeye kuwa amnatokea Mbeya kwani ni jambo lililokuwa linachanganya watu wengi.

"Mimi ni mzaliwa wa Mbeya na naishi huko na mama yangu na
wakati wa audition za EBSS nilikuwa nipo Dar katika michakato yangu na ndio sababu
nikasailiwa kama mshiriki kutoka Dar".
Aliongeza, "Naomba watu wangu waendelee na moyo huo huo wa
kuwa bega kwa bega na mimi na waendelee kunipigia kura kwani kura ndio kila
kitu hata kama nitapendwa vipi"
Walter ni mshiriki aliyeingia
FAINALI pamoja na wenzake wanne, hivyo washiriki wa EBSS waliobaki katika
fainali ni Walter, Nshoma, Nsami, Wababa pamoja na Guiter gira Salma...
Ili kumpigia kura Walter
Chilambo, andika neno EBSS12 kwenda namba 15530".
Monday, November 5, 2012
CHUNGA KAULI..
Hata zikiwa nyingi wachache hutaka moja tu kauli kuielewa,kwa kujua kwa
yale mengi hakuna wa kuyaweza naye.ukisikia kauli lazima uishike isiwe
kauli nyingine zikasahaulika,ama
ikaonekana vile walivyosema wengine,kwamba kauli ya mtoto kumwambia mkubwa yaweza
kuwa makosa ki heshima,lakini siyo ikawe mkubwa kwa mkubwa
mwenzake,ikawa si hekima,maana itaoneka dhambi kwa kujaribu kuyafanya ya juani wakati kauli
nyingine ni za gizani.
Ni wazi hakuna lililo sahihi zaidi yako Mungu,kwa Yule
anayebisha ni sawa na kufananisha ndiyo na hapana ,ukikaa na kukuwa bila
kuelewa utanawa sana kichwa kwa kupata moto tena hutaelewa nini cha kufanya pengine ukiwa haujafanya kitu hapo mwanzo lakini kauli zako zikakukuponza.
Ninatoa kauli yangu pale inaponibidi ikiwa nazijua haki zangu,akili yangu inajua cha ziada nje ya mwili kinachoendelea,hivyo kauli yako yaweza kukuliza ikiwa hujachukua dhamna ya kuyabeba majibu yatokanayo na kauli zako,ni mizigo ya ndani,wachache wanafunzi huelewa nini mwalimu anachofundisha,maana kila
mwanafunzi anaelewa yake pale inapokuwa nafasi na wakati wa kila mmoja kutoa kauli yake katika uelewa
Ni kweli kauli nyingine
ni makosa sana kutamkwa,si vyema kusema kitu usichokifahamu na kugeuza kauli yako ya kweli,ni wazi hata samahani isimaanishe kitu hata ikawe kwa mtu
kuuana na mwenziwe.kauli nyingine hazitakiwi kukumbukwa,kauli nyingine zina
maana ya kuleta kauli nyingine zisizo na maana.Chunga kauli.
Friday, November 2, 2012
NISHIKE..
Utawaza kushika maneno ya bwana mungu kwa kuwa yapo katika maandishi na kujifanya kujua kusoma,maana ni wazi kama angekuwa mbuzi sababu zingepigiwa mstari kwa kuwa ni sahihi,pengine ili kutokupigiwa mstari tukae ukinishika mkono kwa kunielekeza,maana pengine naona giza,huo mwanga siyo kama huu,huo nahitaji kushika kwa kunipendezesha,acha harufu kwani umepuliza wa kutosha sasa angarau nikaotee jua,najua japo nikishika moto pengine nitaotea kwa yale mema kuwa mabaya,kwa ule wema kuwa wa mbaya.
Ukishika bilioni lazima utakuwa billionea,ukishika maneno ya bwana mungu wako lazima utakuwa mtoto wa mungu wako,pengine ikiwa umeyashika kwa sababu ipi,ikiwa umeyashika unayoyajua wewe,kesho mwanafunzi anapofeli darasani aulizwe nini anataka ili afauru,pengine isipokuwa kwa kushika ramani ama kuleta amani.maana ikiwa umefeli umetaka kushitaki,haina maana kwa waliofauru kwa kutokwenda kushitaki.
Hapa kunaweza kuwa na chaguzi hasa zaidi katika yale mazuri na mabaya,yale ambayo mmoja akayaona kuwa ndiyo na mwengine akasema kwa mshituko kwamba siyo,kuwa na imani kwa lolote lile unalohitaji kulishika,imani ya kushika unapohitaji siyo ya kuthubutu endapo kukiwa na mahitaji,tabu zikamfanye mtu ajitambue zaidi yakuwa ameshika yale yaliyomletea taabu ama raha zaidi.ama tuyashike yale tuliyofundishwa zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...