Sunday, March 24, 2019
Makaya's Forum: BADILIKA.
Friday, November 18, 2016
SHIKA YAKO
Watu wanaona wanachowaza wao juu ya wenzao ni sahihi zaidi, yaani mtu anaamua kumwamulia mwengine kwakuwa tu labda wametofautiana katika hali zao hasa katika uchumi wa binafsi na pengine ikawe ni tabia na kujifanya nafsi ya mtu iko mikononi mwao.
Sibishani na mtu ili akapata faida,aliyetaka kuelewa aliuliza mapema kile kinachohitajika kufanyika na kikafanyika , hakuna haja ya kulazimisha kujulikana kama unajua na wakati haujui, anayefanya jambo moja huacha kutokana na mtu mwengine karibu kufanya jambo lile lile, na aliyeamua kufanya jambo hakatazwi kwa maneno ama kwa kile kilichofanywa,na akiacha isiwe kwa maneno maana kuna binadamu wanajua ya wenzao kuliko wenzao,wakijiweka wao bora zaidi ama tu kukuchafua kwa vile mpumbavu hachagui neno la kukusemea,
Tuesday, October 11, 2016
KUZA KIPAWA CHAKO NA KATAA KUSHINDWA.
Tuesday, September 27, 2016
YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU.
Yafanye
mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako
na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyiyale wanayoyategemea zaidi
ya kile kilichopo pasipo kufikiri ni kwanini mtu anajawa na msongo wa mawazo yanayokataza
kuishi ndoto zako.
Labda
kwa sababu ya watu na matendo yaliyopita yanaisumbua roho yako, watu
wengi wanaishi wakikimbilia wasichokijua kwa kuogopa nafsi zao kubaki nyuma na
baada ya kuangalia wanajikuta walichokifanya kilipaswa kufikirika kabla ya maamuzi
ya kutenda, hivyo kukuletea shida katika kufanikisha mambo pasipo kujua
wapi walianza.
Wengine wanaishi maisha yao kwa kujiona, kujiona kwamba ndiye yeye,ukijiona kwamba u tajiri na wakati bado ukihitaji msaada na kuuacha uhalisia, kwamba kila kitu kipo sawa katika malengo na yale unayoyahitaji huku unasahau maisha yanakutegemea wewe, kwa lolote unalolitafuta na lenyewe linakutafuta, ni kama nguvu ya mvutano.
Hivyo ni lazima kuwa nalo jambo, acha kufanya lile lisilo na tamanio kwako na fanya kile unachoweza maana na chenyewe kitafanana nawe, ukitembea sana katika maisha utakutana na kauli ambazo nyingine zinasimamisha na kurudisha nyuma nafsi yako, ikiwa lakini yako utaitumia vizuri ukiangalia ni wapi utawekeza akili yako na baadaye uyaache maamuzi yako yakikufata sambamba nawe.
Angalia katika njia ambayo unaweza
kuyatengeza maisha yako yakawa vile utakavyo kama vile ukaamini kwamba ipo siku maisha
yako yatakaa na kubadilika ukiamini unaweza kuyafanya maisha yako katika
yale utakayo yakakurudia ama kukupata upya, kama hauna kitu nyanyuka na ukafuate
kile unachokitaka.
Hutapoteza kile unachokitaka kipo na kinakusubiri wewe kama bado ulikuwa haujakipata,achana na mawazo ya kilichopotea maana unapoelekea ni mbele kupata maana amua sasa ili watu wengine waje wasome kupitia wewe.wengine wanasema hapana huku wakiwa hawajui kama wanakataa juu ya nini.
Nguvu iliyopo ndani yako ni kubwa,jiamini na safiri na nyota yako.
Sunday, September 25, 2016
FANYA LEO YAKO
Saturday, September 24, 2016
BADILIKA.
NIKIFANANISHA MAISHA KAMA MKONDO WA MTO, PENGINE UNAPOTILILISHA MAJI YAKE HAYACHAGUI NJIA YA KUPITA LAKINI YATAFIKA PALE YANAPOTAKIWA KUFIKA PALE NJIA ILIPOTENGENEZWA NA MAJI, HIVYO NJIA HALISI YA MABADILIKO ANATENGENEZA MTU MWENYEWE, UKIWA NA LENGO LA KUULETA UKWELI WA MAISHA YAKO.HIVI SASA KAMA ULIKUWA BADO UNAHITAJI LA KUFIKIRI NI NAMNA GANI UTAWEZA KUYABADILISHA MAISHA YAKO, MATATIZO KUWA STAREHE, NA KUJIPELEKA MWENYEWE KATIKA DARAJA LINGINE LA JUU ZAIDI ULIYOPO.JARIBU KUFANYA KILE UNACHOHISI NI MAENDELEO, KINACHOWEZA KUKUONGEZEA THAMANI NA NGUVU KATIKA MAISHA YAKO,FIKIRI YALE YALIYOFANYIKA MIAKA YA 70 NA SASA NI SAWA SAWA PENGINE WATU NI TOFAUTI,AU NI TOFAUTI NA WATU NI SAWA SAWA,USIKUBALI KUWA MTU YULE YULE,YULE WA SIKU ILE,FANYA MAZURI KWA WATU AMUA,BADILISHA NAMNA NA TEMBEA UKIJUA ULIPOTOKA,ULIPO NA UNAPOKWENDA
JAZA UBONGO WAKO NA YALE MAZURI, YALE YALIYO NA WELEDI WA KUWEZA KUUFANYA UBONGO UKAWEZA KUKUVUSHA KATIKA YALE MAGUMU,PANGA NA AMUA KUFANYA KATIKA KUELEKEA MAENDELEO INGAWA DUNIANI KUNA ATHARI NYINGI AMBAZO KIMSINGI ZINATUKABILI NA HIZO HUWA NI CHANGAMOTO KATIKA MAISHA,FUNGUA UBONGO WAKO NA KUYAFANYA MAISHA YAKO YAWE YENYE NGUVU NA MAANA,FUNGUO HIYO NI MAAMUZI YA KUJIAMBIA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU KUWA INAWEZEKANA,INAWEZEKANA KUBADILI KILE UNACHOKIFIKIRIA KWANI KUJUA KAMA INAWEZEKANA NI MABADILIKO TOSHA.
@Benson Makaya
Friday, September 23, 2016
MAAMUZI
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...