Tuesday, April 23, 2019
Makaya's Forum: KATAA
Makaya's Forum: KATAA: unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa,ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekaa kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...
Saturday, April 20, 2019
BINADAMU UNAPOJIULIZA(usimwachie Ulimwengu)
Najiuliza umeniuliza kwanini Sitoi salamu nami huwa najiuliza pia kama huwa unaipata salamu yangu,ikiwa ubongo wa mwanadamu wa kila aliyeumbwa una swali la kujiuliza jiulize unaelekea wapi maana kila siku zinavyokwenda ulimwengu unaelekea na kuzidi kutoa maswali yanayoendana na technolojia ambayo haikukupa misingi yenye mizizi ya kina katika kujua mambo yaliyo duniani yanayoendana na maswali hayo katika kukabiliana na maisha ulimwenguni.
Jiulize kama umeshawahi kujiuliza kwa nini unafanya kile unachoweza kukifanya ama kwa nini unahitaji kufanya kile ambacho unahitaji kukifanya?je pengine ukifikiri kuna kuwa na uhakika wa kupata majibu ya maswali hayo au njia na majibu ya maswali hayo?maana aina nyingi za majibu yanayotokana na kuangalizia yanakuwa hayana maana iliyokiundani pale inapokuja mtoa majibu anapoangaliwa kwa umakini zaidi, utekelezaji wa waliotoa majibu huelekeza swali hilo lilimlenga nani,ikiwa kila mtu ana mtihani wake hivyo hata majibu ni tofauti pia.
Nimekuja kuishi duniani hivyo nina kila sababu ya kufanya hivyo iliyo vyovyote ili iwe, niishi. kutangulia sio kufika lakini sio katika kifo na hii mara nyingi hunipelekea kujiuliza naishije ama ntaishije ? sasa hili ni chaguzi ukizingatia Moyo nao hutaka kuamua yake pindi majibu yanapotoka hivyo bila kuuhusisha moyo wangu huwa nayavumilia majuto ikiwa pia nazingatia na muda nilioanza kupata wajukuu na kusoma hali zaidi kupitia hapo,
Nimekuja kuishi duniani hivyo nina kila sababu ya kufanya hivyo iliyo vyovyote ili iwe, niishi. kutangulia sio kufika lakini sio katika kifo na hii mara nyingi hunipelekea kujiuliza naishije ama ntaishije ? sasa hili ni chaguzi ukizingatia Moyo nao hutaka kuamua yake pindi majibu yanapotoka hivyo bila kuuhusisha moyo wangu huwa nayavumilia majuto ikiwa pia nazingatia na muda nilioanza kupata wajukuu na kusoma hali zaidi kupitia hapo,
Kama ndugu yangu pia una jiuliza swali kama hilo pia basi jaribu kuangalia na moyo wako unasemaje ili majibu yako yakahusishwe na wewe binafsi.Na inapofika kipindi humwelewi mwenzio ni bora ukauliza au ikiwa unataka kuelewa jinsi unavyoelewa basi kaa kimya maana mengine yanakuwa siyo yako.
Maisha yana mengi ni mtihani hivyo maswali mengine siyo yako ukiyajibu unakuwa kama unatumia akili yako vibaya,Kama utapenda kuyajibu na kuona umepata zaidi basi Mwalimu(Ulimwengu) ndiye atakayesema kweli kuzingatia na muda na ujue binadamu ameumbwa kupambana kila siku,
Maisha yana mengi ni mtihani hivyo maswali mengine siyo yako ukiyajibu unakuwa kama unatumia akili yako vibaya,Kama utapenda kuyajibu na kuona umepata zaidi basi Mwalimu(Ulimwengu) ndiye atakayesema kweli kuzingatia na muda na ujue binadamu ameumbwa kupambana kila siku,
Usijali kama swali la jana limebaki kuwa swali la nyumbani la leo inawezekana leo kulikuwa hamna swali pia jawabu ni kujipa moyo na kusonga mbele kwa kuangalia yanayofuata.
Friday, April 19, 2019
UNAPOWAZA
Eti kuwaza sana ni vibaya,nawaza sana nakuwa na mawazo nawaza sana yaliyo mema nawaza sana kuongeza kupata maisha sio kama ya fulani bali yale niliyoyawazia,wakati mengine yanapita Shukrani kwa muumba hazitaweza pita,Mwisho wa kuwaza unaelewa mwenyewe maana sio uwaze tu hata yasiyo na majibu,
Mbaya katika mtihani ni kuanza na swali gumu kuliko yote kumi utajikuta umefeli na kuyashagaa matokeo yakakupa mawazo tofauti yakuwa kabla ya kuingia katika mtihani uliwaza ukitoka utakuwa na mawazo tofauti zaidi ya yale uliyo kuwa nayo sasa,sijui niwaze nini nikufurahishe, nakusema siwezi ogopa ila muda haumdanganyi mwamuzi labda anayeamua akaamue.
Hivyo unachagua wewe,chagua wewe kuwaza nini mengine ni mazuri asikwambie mtu mawazo mabaya,ni kheri akakuongezee kwenye huo ubaya maana hata moto anaoupata yule anayechomelea na yule anayekaanga viazi ni tofauti nawaza tu,ukitaka kutokuwaza fanya starehe,ukifanya za kutosha na hautakuwa na mawazo ya kutosha,naposema starehe kila mmoja anayo katika mawazo yake unawaza kufanya starehe gani nasema hivyo maana kuna kauli inasema maisha ni mafupi sana hivyo inakupasa kuishi kwa thamani,matumizi yako yakaendane na mawazo yako ila pindi unapowaza kinyume huna budi kuwaza yaliyofanyika maana huo hua ni mwanzo wa mmomonyoko wa yale yanayofuata.
ukiwa unawaza yanayofuata ukawa hujui hasara yake maana kwa muda huo yanakuwa hayana mashiko na mmiliki yaani wewe uliyestarehe kwa mawazo yako kabla hujawaza sasa iliyopo ambayo ni baadaye.
Sikuwaza umri ni kama haya makubwa ninayoyawaza,wala kuna mengine sijawaza lakini yamekuja katika haya,mawazo ukiyaamini,yanakuletea imani yako inachokiwaza hata ukajiandae na utofauti ili kutokuyazidisha yaliyopo,maana nawaza sikufika hapa kama nilivyo wala sikuwa mimi kama nilivyo,sio tu kwa sababu ya nini ama fulani nikiwaza kwa mawazo yangu ni imani maana sikuijua kesho zaidi ya yule aliyeniambia niache kufanya ya kesho kwa kuwa hata usiku wa leo hayajafanyika.
Sikuwaza umri ni kama haya makubwa ninayoyawaza,wala kuna mengine sijawaza lakini yamekuja katika haya,mawazo ukiyaamini,yanakuletea imani yako inachokiwaza hata ukajiandae na utofauti ili kutokuyazidisha yaliyopo,maana nawaza sikufika hapa kama nilivyo wala sikuwa mimi kama nilivyo,sio tu kwa sababu ya nini ama fulani nikiwaza kwa mawazo yangu ni imani maana sikuijua kesho zaidi ya yule aliyeniambia niache kufanya ya kesho kwa kuwa hata usiku wa leo hayajafanyika.
Unapoona mengi kuna mengine yanakuwa sio makubwa yaliyowazwa zaidi ya kuonwa ikiwepo vingine nawe ukawaze hivyo,nikikiona nakielewa zaidi maana nikikiwaza ntakuwa kama nakiona,shida pale nawaza nisichokiona ninapowaza cha kesho na leo sijaimaliza hapa huwa naamua kufanya lililopo bila ya kuchelewa.
Kuna kucheleweshwa lakini aliyewahi kawai kesho ujifunze kuamka mapema ili kuyawahi mawazo kingafu ,maana kama mawazo yanaingiliana basi hata matendo pia,unapokufa wakisema utakumbukwa wengi ni kwa matendo yako,mengine waliyoyawaza husahaurika ,kufa leo uache mazuri yaliyotokana na mawazo yako na iwe kwa faida yako.
Nawaza ni kheri nizeeke muda mwingine ntakuwa nimepita mengi,nisionekane tu kwa mtu anayeona aonavyo bali nikajifiche kwa vile waonavyo,nilikaa na kuanza kuandika haya nliwaza mmoja atawaza yale ni mawazo tu,lakini kwa jinsi navyoona hata yule asemaye naye anataka kuonekana na mawazo bora,kuna vitu Mwenyezi Mungu amekupa na mwengine hana,Kama unaweza kufanya chochote bora fanya katika ubora uwazavyo.
Nawaza ni kheri nizeeke muda mwingine ntakuwa nimepita mengi,nisionekane tu kwa mtu anayeona aonavyo bali nikajifiche kwa vile waonavyo,nilikaa na kuanza kuandika haya nliwaza mmoja atawaza yale ni mawazo tu,lakini kwa jinsi navyoona hata yule asemaye naye anataka kuonekana na mawazo bora,kuna vitu Mwenyezi Mungu amekupa na mwengine hana,Kama unaweza kufanya chochote bora fanya katika ubora uwazavyo.
KATAA
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofauti na vile inavyoweza kusukumika,upepo unaweza vuma kuelekea kusini na yenyewe maisha yakataka uelekeo wa magharibi itakuwa na kueleweka vile inavyoonekana uelekeo ulivyo.
Unaweza ukawa umekatalika upande wa kushoto lakini kulia ukafanya kazi na kama vile ilivyo katika viungo vya mwanadamu,wengine wakatumie kufanya mambo yao kwa upande wa kulia na wengineo kushoto yaani pande zote na hiyo ikawe ni kulingana na mazingira ya jinsi ulivyoweza kuumbwa.
Unapokataa jambo ni lazima ujue kipindi cha kukubali pengine muda unaolikataa jambo ndiyo muda mdogo wa kusubiri na kupata jambo lingine likiwa ni lile lililokataa uelekeo ama ni jipya,yule aliyekataliwa jana na sasa anang'aa ni katika maisha ya mwanadamu huwa yanatokea,
Yote sio ya kumwachia Mungu Mengine hata yeye aliyakataa akaumba Amri ili uweze kujikataa katika nafasi uliyopo pengine ikiwa na mahitaji ya mabadiliko ama vinginevyo,ingawaje yaweza kupelekea kukataliwa na jamii na watu wanao kuzunguka lakini kataa kukataliwa kwa sababu ya maono ya watu,
Wengine wakadhani umejikataa lakini ni namna ya jinsi maisha yako umeyataka yawe,unapokaa chini ona waliokataliwa wakakata kutokukatalika,maana kuna vile vingine hukataliwa kwa sababu anafanya fulani.
Muda mwingine unaweza kudhani hata ulikosea kufanya kile unachokifanya au ulikosea kuoa,ulikosea kununua mashine fulani hata pengine ulikosea kumwambia mtu fulani jambo fulani na mengine mengi.Kile kinachosukuma mwelekeo kinatagemea uwiano wako na ukikataa kwenda kulia na msukumaji anasukuma kushoto basi jua utaenda kushoto tu.
Sio kila sikio linasikia kile chema kinachoweza kupitia mdomoni baadaye,midomo mingine hukataa kutoa tafsiri sahihi ya kile kilichokipokea kwa kuchelewa kufika taarifa ama kukataa kufikisha kile kilichotafsiliwa na kukifikisha kikiwa na maana tofauti inayoweza kukatalika.
Ingawaje hata kukataliwa kuna faida zake pia usijisikie wa chini pale unaposukumwa na mkatazo,kataa wewe kabla hujakataliwa,yule ajaye kakukataa atapata sababu baada ya wewe kujua kujikataa kwa faida.
Usijisikie hali yoyote katika kukataa,kukatalika,kujikataa ama kukataliwa pengine fikiria matokeo yake kwanza na ukajua leo yangu iliyokataliwa ni Nuru yangu kesho na hata kama kesho yako inaonekana kukataliwa kataa mawazo ya kuona kukataliwa.
Sunday, March 24, 2019
Makaya's Forum: BADILIKA.
Makaya's Forum: BADILIKA.: KUNA KIPINDI UNAWEZA FIKA NA KUSHANGAA NAMNA YA JINSI MAISHA YAKO YALIVYO,YAKIWA YAMESIMAMA AU KWENDA VILE AMBAVYO HUJATEGEMEA WEWE, KUMBUK...
Friday, November 18, 2016
SHIKA YAKO
Kamilisha mipango yako ukitilia maanani kwa kile chochote ukahitaji kufanya katika namna ya kukataa kujilaumu na kukwepa lawama,Utapatwa na mshangao kwa kuona Yale yanayotokea halisia sio kama vile ulivyofokiri, ukiwa na fikra zilizochanganyika na Mawazo ya aina nyingi yenye kujua lipi ni tusi na lipi ni shukrani.
Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwa Pumzi yako kwa vile utakalo wewe hutimia, nakumbuka mengi machache sio kama ya mwengine, Asante Nimekuja duniani nimekuja uwanjani pengine ni mchezo unaohitaji hasira na nikakasirike tofauti.
Watu wanaona wanachowaza wao juu ya wenzao ni sahihi zaidi, yaani mtu anaamua kumwamulia mwengine kwakuwa tu labda wametofautiana katika hali zao hasa katika uchumi wa binafsi na pengine ikawe ni tabia na kujifanya nafsi ya mtu iko mikononi mwao.
Watu wanaona wanachowaza wao juu ya wenzao ni sahihi zaidi, yaani mtu anaamua kumwamulia mwengine kwakuwa tu labda wametofautiana katika hali zao hasa katika uchumi wa binafsi na pengine ikawe ni tabia na kujifanya nafsi ya mtu iko mikononi mwao.
Maisha hayana uelekezi wa moja kwa moja yakakupa kanuni ili ufanye vile na ukafanane, binadamu tumetofautiana katika hali nyingi hasa ikiwa ya kwako umeyaweza Leo mwache kesho aweze mwengine unayemwona kashindwa Leo,haina haja ya kumsemea ikiwa kinachofanyika sio kosa kwake.
Ondoa wivu na roho ya kukunja katika lile jambo aliwezalo mwengine, ikiwa hujui ni bora kuuliza na kumwacha mwandishi aende na faida zake kuliko kusemea kitu kinachokuhusu wewe na kulinganisha na utofauti wa kile anachokifanya mwengine ya kuwa binafsi huna uwezo nacho.
Leo nikiangalia baadhi ya mambo yaliyoonekana na kusema hakuna aliyekamilika katika dunia hii yenye mengi, watu tumetofautiana chaguzi mmoja akaona kibaya ni kizuri na mwengine akaone kizuri ni kizuri hiyo yote ikiwa ni kutaka kuona mazuri na kuukataa uhalisia, au kuukubali katika namna yake.
Uhalisia huja katika pande zote lakini binadamu uufanya uhalisia wake pale anapopendezwa nao yeye, ni kheri kukaa kimya kuliko kusema kitu ambacho hakiwezi kufutika maana na kuleta uhalisia tofauti, kwani yanapokuja mabadiliko fitina na uwongo uliokithiri unaweza kuharibu picha na mtazamo wa maisha yanayokuzunguka.
Sibishani na mtu ili akapata faida,aliyetaka kuelewa aliuliza mapema kile kinachohitajika kufanyika na kikafanyika , hakuna haja ya kulazimisha kujulikana kama unajua na wakati haujui, anayefanya jambo moja huacha kutokana na mtu mwengine karibu kufanya jambo lile lile, na aliyeamua kufanya jambo hakatazwi kwa maneno ama kwa kile kilichofanywa,na akiacha isiwe kwa maneno maana kuna binadamu wanajua ya wenzao kuliko wenzao,wakijiweka wao bora zaidi ama tu kukuchafua kwa vile mpumbavu hachagui neno la kukusemea,
Sibishani na mtu ili akapata faida,aliyetaka kuelewa aliuliza mapema kile kinachohitajika kufanyika na kikafanyika , hakuna haja ya kulazimisha kujulikana kama unajua na wakati haujui, anayefanya jambo moja huacha kutokana na mtu mwengine karibu kufanya jambo lile lile, na aliyeamua kufanya jambo hakatazwi kwa maneno ama kwa kile kilichofanywa,na akiacha isiwe kwa maneno maana kuna binadamu wanajua ya wenzao kuliko wenzao,wakijiweka wao bora zaidi ama tu kukuchafua kwa vile mpumbavu hachagui neno la kukusemea,
Shika yako na mwache mwengine akiendelea zake.
Tuesday, October 11, 2016
KUZA KIPAWA CHAKO NA KATAA KUSHINDWA.
Vitu vinavyokuja kirahisi mbele yetu kama zawadi inaweza
kukupelekea katika sehemu nyingi chagua na kuwa na uzuri katika kila jambo, amua kutoka ndani ya mfuko
wa moyo wako na kuangalia nini unataka kufanya katika maisha yako ukitakiwa kuyandeleza maono na
mawazo yako.
Usijifiche bali fanya ni lazima kufanyia kazi kipawa chako ikiwa ni
nguvu na tabia ya mtu, amua kwamba utajisukuma ili kufika mahali Fulani kwa
nguvu zako mwenyewe,
Nguvu ya mwanadamu ni kubwa sana Zaidi ya ufikirivyo kile
ulichoamua hakuna mtu awezaye kukukataza, anza kuongeza na kuimalisha malengo
yako kwani mafanikio unayachungulia unayachagua wewe mwenyewe na kipaji chako kikufikishe
pale.
Kila siku yakupasa kutafuta nini njia ambayo utafika siku na
watu wakuulize na washangae umefikaje pale, maisha yanaweza kuwa ni silaha kwa
muda mwingine na vitu vingine watu hawafundishwi hivyo sio kila kile ufanyacho
ni mafanikio yakupasa kuwa na nguvu zaidi ya maisha yako yenyewe na namna
unavyoyapima mafanikio binafsi, kubali kwamba kuna watu wanaitafuta iyo nafasi
uliyonayo,
Hakikisha unatumia siku yako vyema haijalishi ukiwa na furaha ama
chukizo yakupasa kutambua kuwa ni wewe upo katika hiyo hali na nini kifanyike,ukiwa
unajua unachokifanya haikupasi kuwa na maisha ya katikati inakupasa kuvuka
vizuizi, usijaribu kuacha kupigana na kukata tamaa, jiamini na Pigania Maisha sio
leo wala kesho Kwani umekuja kuishi.
Tambua uko katika misheni ambayo inahitaji ukamilisho
wako, usijikatae kwa kukosea maana wengi waliofanikiwa wamekosea sana, utajifunza
kutokana na makosa bila kujali ni makosa ya aina gani maana mwenye makosa
ndiye anayetegemewa kufanikiwa, sema ndiyo kwa kila jambo linalohitaji kuendelea mbele, jaribu unapopata wewe ni lazima utambue
kuwa kuna nafasi nyingine katika maisha,
Kwa kile utakacho toa ndiyo hicho
utaingiza, usirudi nyuma kamwe muda wa kushindwa ulishapita,kipindi kigumu huwa kinapoteza vipaji vya watu
wengi na kujikuta wakibaki wakilalama na kufanya hakuna, funguo ya kufanikiwa ni
kujiamini kujifunza na kutenda kupitia makosa hayo hayo,
Toa sadaka yako leo kwa
ajili ya kesho nzuri inayokuja na utumie ubongo wako vizuri ili kukuendesha kuwa na furaha
na mafanikio unayoyategemea.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Makaya's Forum: ELEWA 2
Makaya's Forum: ELEWA 2 : Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...
-
Pengine ukawe umemaliza mambo yako,au ukawe upo katika njia ya kuutaka ufalme,kipindi kile cha ngamia kupenya kwenye tundu la sindano ...
-
Makaya's Forum: AMUA YAKO. : Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha kifo,maana wakiona taabu ndiyo utasikia Yule kachanganyikiwa kabisa...
-
Yafanye mapito yako kuwa nguvu inayokusukuma kwenda mbele ukitegemea kuishi ndoto zako na sio kile unachokiogopa na kuhofia,wengi hawafanyi...
-
Makaya's Forum: YAFANYE MAPITO KUWA ELIMU. : YAFANYE MAPITO YAKO KUWA NGUVU INAYOKUSUKUMA KWENDA MBELE UKITEGEMEA KUISHI NDOTO ZAKO NA S...
-
Duniani wengi humkimbia mtu kipindi cha shida,wanaoamini kufika darasani ni kuelewa zaidi ya maisha yalivyo wameelewa tofauti,ikiwa...
-
Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya...
-
Makaya's Forum: MAPENZI YANAISUKUMA DUNIA.. : Usipoelewa hautaweza kujua hata kama unashiriki vipi,maana kwa kutokuyapenda na kujifanya ...
-
Makaya's Forum: ONA KUSIKIA. : Mapema ni kheri kuona bila ya kusikia,maana haya machache tumeyasikia hapa kwa kuwa yalionekana mwanzoni,...
-
Unaweza ukawa unakataa mazingira uliyonayo,ukajikataa ukakataliwa ama ukakatalika hiyo yote ikaonekana kwa kuwa maisha yana msukumo tofaut...