Saturday, August 25, 2012

TENDA WEMA NENDA ZAKO..


Hulazimishwi kulia na wakati wewe unataka kufurahi na kucheka,swala la msingi ni kujua unapokatazwa kulia,hapa nikiwa sina maana ya kuhudhunika kwa lile linalokwaza,hakuna baya alitendalo mwanadamu zaidi ya Mungu mwenyewe kujua,maana imekuwa hata nafsi yenyewe ikajitendea mabaya ikiwa wema umezidi sana,maana binadamu umekua unayashika mabaya kuliko yale yaliyo mema ikiwa mabaya hayo yanahesabika ujiulizie mazuri ili ukayatende na uende zako,hapa mtu ukiwa na lengo la kutaka kujua,na sio kushabikia kwani unaweza kushabikia timu alafu ikawa inafungwa kila siku ni sawa na kumsaidia mtu kila siku alafu mwishoni anakufukuza kama mbwa,yakupasa kuacha kushabikia usivyovijua.

Adhabu zote yakupasa kuzitumikia kwani maumivu hujenga,lakini si katika namna ya kutaka kuishi na adhabu hiyo hata kama mema yanahitajika,mwanadamu kila siku anakuwa kwa kusikia na kuona pia unaambiwa maneno mengine siyo ya kuwaambia watoto wako wakiwa hawatakiwi kujua menigne yale,ingawaje ni vyema kumjuza mtoto ili naye akikuwa akatende yale tu yaliyo mema kwake na yakuwa wanadamu hatuna dogo yakupasa kutazama pande ya kule na huku alimradi ikufae.

Shukuru mungu yakuwa unapumua mengine ni ya dunia,songa mbele usikate tamaa kwa kwenda na bila kutenda,kwenda zako isichukulike hasira kwani kesho na kesho kutwa mjinga atafahamu kuandika na kusema shukrani,Mbinguni unaenda kwa ajili ya mazuri na mabaya yako,kama mtu unaamini kule atapata adhabu kwa mabaya yako basi ujue hayo ni ya Mungu asiyoyaruhusu wakati huu uliyasikia lakini hukuyafanyia kazi ama uliyafanyia kazi lakini si sahihi na vile ilivyotakiwa,ya binadamu yanaisha hapa hapa duniani,unapaswa kuwa mwema ili kufanikiwa vyema katika maisha yako na kuleta amani ya moyo na fikra iliyo na  mafanikio makubwa.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...