Saturday, April 7, 2012

KALALE PEMA,TUNAJUA ULIPOELEKEA...!!


Kama lilivyoneno lenyewe,
ikiwa tutasema tumejiandaa labda tunaweza kueleweka tukiwa na maana ile ile ya kumbu kumbu,
kwa walio tangulia mbele wanaweza kurudi nyuma ikiwa ni kimaawazo au kiharisia,
kusema maneno ambayo umeshawahi kusema,
kufikiri kama ulifikiri vile kwa mara ya kwanza,
ikiwa tunakumbuka lazima tulifikiria kwanza,
tulipotoka mahala pale basi tukaelekea na kwengine,
kwa kumbukumbu zilizo kwa mtu mwingine ndiyo pale tukaja sema ni mawazo,
yaweza ni lengo la kuweza kuelekeza pale mwanzo yaani kukumbushia.

Kumbukumbu zile mtu anazo ikiwa ni nzuri kuwafanya watu kutabasamu na kununa,
au hata zikawe mbaya basi tabasamu pia na kununa tena,
ikiwa ni kwa sababu ya kila mtu anavyowaza,
mengi mazuri hufanya watu,
walio wafu hata walio na  pumzi,
tusijebishana kwa wafu wenye pumzi maana tulisikia tu.
matendo hayana wafu maana kila mtenda hutenda lake,
swala ni kuelewa labda hapa tukumbuke kwa kupiga simu,
kutuma email tena tukifurahia kwa yale ya jana yaliyotendeka kwani yalichekesha sana.

Wengine watakuja wanafurahia maana kwa kuwa jana walikosa kula basi angalau mpaka mazishi itakuwa hafadhari,
maana ndiyo na bajeti itajulikana hapo.
na ndiyo pale hata sielewi maana ya mlala hoi,
kwa mimi nikimaanisha mlala bila pesa.
yaliyopita yabaki huko labda sasa tuenzi,
tukijua hata kama ni adui yako ameaga dunia yastahiri kulia,
maana utapigana na nani?
au uliletwa kwa  ajili ya kuleta vita tu.?
tusikumbuke kizembe,
tena tusiwe tunakumbuka..!!

Tusizushe mengi kwa kuwa alikuwa ni ‘mkuu’,
ni lazima tutashangaa ya kuwa “hatukuufukiria ukuu”,
pengine haikuwa muda wake,
labda ‘amewahi sana’,
au kwa nini hakufanya hivyo?
ni maswali mengi yatakayo toka hapo asije kulia mkeo ukadhani naye alikuwamo,
maana tumekuwa na wivu kama tairi na gari,
maana hata likipata pancha gari linasimama ndiyo ije lichomoke?
tuseme na vingine kwa wao wanaoyajua magari vizuri,
inatakiwa tufike safali za kila mmoja wetu,
inatakiwa tutimize yale tuliyoagizwa na baba zetu yale waliyotuambia,
tufanye kile kilichofanana hata kutakiwa na ikitokea ibaki kueleweka,
alisema yesu ntarudi…
alijua mtamuhitaji..!!
zile ndiyo cement zenye kujenga daraja gumu,
lile linalozaa vidaraja,
itakuwa mvua inanyesha kwako tu.

Hongera kwa wafu si marufuku,
furaha kwa mfu si kitu,
labda tuseme tunasikitika,
hivi tunasikitikika ndiyo nini?
maana wengine wanacheka wengine wanalia..
jibu litakuwa kulia kwa majonzi sasa kwa nini lisiwe ndo neno mbadala wa kusikitika,
kaka,dada,mama,na baba mzazi kwa waliotangulia na kuacha chao ama kuondoka nacho muende kwa kheri..
mema hakika mmetenda kwa watu tofauti,
hakika tofauti..
hakika tofauti
 ‘..haki mkuu kujiita mkuu,maana ameujua ukuu”

Ded:
Missing you/badboys/Aliyaah-BIG

By:Benson G.Makaya SJR
Tel:+255714336657/0769556559
Email:bensonsmakaya@gmail.com

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...