Machache yanakuwa ni ya kila mtu zaidi ya mwengine
aliyonayo,maana kuna kusikia ikiwa mmoja amefanya tofauti,namna ya kusema ilivyo
na kufanya huwa mbaya zaidi ya watu vile wanavyosema,ikiwa kiti cha mtu mmoja
ni makosa kukaliwa na watu wawili,hapo baadaye tukaja na kuambiana ilibidi
kufanya hivyo baada ya maongezi,na bila kudhani kabla mapema kama maongezi
hayakuwepo.kumbe siyo lazima mmoja kuona vile walivyoona wengine,hata katika
upande wako jua hayo ni ya kwako tu.
Ni makosa sana kumfundisha mtoto maswala ya kikubwa,ni
makosa sana hata kumwona mtoto akifanya mambo ya kikubwa,pengine hapa
tumeshindwa kuambiana ya kitoto ni yapi,na ya kikubwa ni yapi.pengine na watu
hao wakafahamike bila ya heshima ya umri maana na yenyewe imeleta ukubwa,kuna
wakubwa wanamambo ya kitoto na hayo ni makosa makubwa,pengine kwa upande
wangu,labda na watoto waachwe watende makubwa.
Inasemeka katika makosa ni namna ya kuweza kufanikiwa,na
wanofanikiwa ni wote ikiwa ni watoto na wakubwa,mafanikio hayana umri,pengine
ndiyo maana mwanadamu anaweza kufanikiwa katika umri wowote,hii ikiwa kama
atachelewa sana basi kuna makosa aliyafanya,pengine ni mipango tu.makosa sio ya
kumfaya mtu kukata tamaa ya maisha kwani ndiyo nguzo ya kufanikiwa,hata
mwanadamu asifanikiwe bila makosa,tunaweza kukosa vingi ikiwa ni pamoja na
pesa,afya na yetu mahitaji mengineyo.tukubari kukosa pale inapotokea ikiwa ni
nafasi pekee katika kuelekea kufanikiwa,lakini pale tunapojifunza kweli.