Leo imefika tunagombana kwa yale tuliyoyashindwa
jana,pengine haikuleta faida sana,ama hasara ikiwa endapo kama tunaweza kukaa
na mali na bila ya kuziendeleza basi ni tumeshindwa kabisa,hii ikiwa mali
zenyewe zinaendelezeka,inapofika mwisho wa jambo ni haki kuweka alama ikiwa ni
kwako,hii haki..maana ni dhuruma kwa mwengine kuichukua.tusifikiri tumeishi
zamani na ya kutamani tutayaweza,zisije
fikra zenyewe kwani wengine wameshasema wakijiandaa mapema.leo ikiwa mwisho
kulipia haina maana ya kesho usilipe,ila kama ilichukulika bila ya malipo ya
kuelewana kuna uwalakini wa kutokuelewana zaidi,hasa mzazi anapomwambia mwana
mpaka wako wa kucheza ni mwisho hapa.
Ni wazi ya kuonekana hayafichiki,tuseme vingine vipo wazi
lakini vinahitaji ubishi,maana kama kuna kukubari haraka haraka hata itakuja
siku tuwakatae wazazi wetu,kama walivyo wengine tayari kuona mipaka yao kwa
wazazi wao,maana mmoja atasema huyu sio
mama yangu na mwengine atasema wala baba.hapo tukivuka mipaka bila ya kufahamu kama mwisho wa safari ndiyo
mwanzo maana yapasa kujipanga upya.
Leo unaweza kugombana sana,pengine watakufa wachache na kwa
wengine ikawa maana,
maana unaweza kujiuliza tangia siku zote hizo ulikuwa wapi?
hapa
ikiwa tunataka sababu.kama kwa mungu
hakuna mipaka basi hakuna anayejua,
maana hii yetu sijui tumeitoa wapi ikiwa
bado tutaendelea kung’ang’ania hata vile visivyo vyetu,mwishoni kueleweka
mambumbumbu kwani hata na kuingia shuleni hakuna cha zaidi ya kufanyia
tulichojua zaidi ya mipaka ya shule yenyewe,unapoambiwa uingie chumbani kwa
baba sio uzungu ni muvi za video tu hizo,waache wakubwa wanaongea watafikia
mwisho wa mipaka yao.
No comments:
Post a Comment