Saturday, September 1, 2012

MUINGILIANO


Muingiliano wa kuongea imeletwa kupitia maneno yaliyoongelewa ikiwa  kwa uchache wa kuelewa ama kutokufikiri ikaleta namna iliyo tofauti ati kusema kwamba wachache walifikiria,na hapo ikiwa walishajipa maksi mapema ya kuwa wamekuwa haina haja hata ya kusema nani atakuuliza,maana kipofu asiyeiona si sawa na Yule anayeona asiyeona.pengine wasioona wakiwa wameona vyao na ili kuepusha muingiliano ni lazima kutambua katika nafasi uliyopo,ikiwa umepewa ya kuchangamkia,inamaana ya kumaliza mpaka mwisho ikiwa damu bado inachemka,na haki ikitakikana.

Katika nafasi ndogo iliyopo hakuna namna ya kusema ‘adjust’ hii ikiwa na samahani ndani yake,kwa maana ilivyo kwa kunenwa ,wengine wakija huja bila ruksa ati ni shemeji,shemeji mkeo maana ndugu zake ndiye wanakuita hivyo,kumbe shemeji ni heshima ilivyo kama baba,tena mkwe,maana wengine hawashangaliki zaidi kama wakitenda yao peke yao na wakitenda yao wakiwa na wakwe zao,hii inaashiria umungu katika kuhofia maana na nafsi ya mtu inabebwa na kile alichonacho,kama yangu katika maandishi yangu,pengine nakua nimesema japo nimeingilia kunena.

muda mwingine unaweza kuingia bila hodi kwani kuchangakiwa ni kama kuchanganya,yaani kuleta fulani ikaingiliana na fulani na matokeo yakajulikana yasipojulikana basi umechanganya zaidi.maana kama ili itokee juisi ni lazima kuweka sukari basi tulambe sukari yenyewe,ukaingiza hata visivyo tumika ali mradi ikaeleweka kwamba ni imepemdeza,ingawa sio yako lakini watu wanafanya hivyo,pengine ujaribu hivyo..ili kutokuingiliana.na kama inatokea basi inajulikana mapema.maana kama umeingia sasa hivi haukuwekewa nafasi,labda tuelezane kwa namna uliyokaa hapo.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...