Saturday, September 1, 2012

CHEKECHO...

Mafanikio ni kwa kila mwanadamu anayehitaji kuishi,ikiwa katika mipangilio iliyo na mlango maana katika kutoka kuuliza waliingia wangapi isiwe shaka,wasije kutoka wengi kuliko walioingia au pengine ikawe ni namna ya mtoko ya kuwa patapewa na jina kabisa,aliyeona mbali hasumbuliwi na wa mbali zaidi maana karibu ni ya Yule aliyeikaribia mbali yake,ukitangaza sifa kwa mbadala wa kujisifia maana tumedanganyika na  sifa zetu,leo utasemsemea twiga na huku kuku akitotolewa na mwanadamu,pengine uangalie hii namna ya uzungu,na hata vile vilivyo visafi kwa kuvaa nguo nyeupe ijulikane ndani yake,mwishowe ikiogopeka kuitwa rangi tuu ya kuwa imepauka.

Fikiri kubwa na dogo pia maana hata wateja wanataka nyongeza ya kupunguziwa bei,wakijisahau ni wauzaji wa bei kubwa,katika pambano la vita kifo ni rafiki wa siraha,kifo hakina huruma ya kuwa hakisemi,yaweza kuweka mipango lakini bado ikagonga mlango,maana ya mlango kugonga ni uwepo mzuri wa kizuizi,ukizuia dondora waliotoka kwenye mti wenyewe,maana hata harufu tu wanaijua,pengine njaa ikizidi sana hata harufu ya kinyesi haisikiki,hii ikiwa pua imechoka kunusa hata hewa,mazingira yote yakiwa  ni machafu,kwa waliotaka maji wakasingizia mifereji.

Linalomalizia katika mengi huwa ni la mwisho hivyo haina kusema namaliza,maana wakati unaanza 

haikutegemeka tena kuanza,labda kupitia mwisho wake,maana kama halikuisha vizuri basi ndiyo itakuwa limeendelea kuanzia hapo,maana huo nao huitwa mwanzo,wakati huo  ni mwisho pia,ni katika kuchagua maana swala utuonyeshe na yale magumu umeyafanyaje,maana yaliyokuwa marahisi yalitamkwa kwa kusema asante ili mradi hata waliopata japo kuona kusema kashukuru,sio kwamba hatujui maana kuna wale wenzangu bali ni katika namna ya kutafuta uzoefu.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...