Friday, October 5, 2012

CHAGUA MOJA..

Chagua,chagua vizuri maana unaposogeza unafikiri,unafikiria vizuri ikiwa Yule anayeweza ameweza,akiwa na jinsia pengine namna yake ama iwe katika idadi,pesa sio kuishi,unaishi ikiwa unapesa,unapochagua unajua ya kuwa unataka,unapotaka sio kiraka kwani ikiwepo jua kama ulivyotaka,pengine kilitokea bahati mbaya,maana ya mmoja mwengine ikiwa ni tofauti na yako,nguvu hazimmalizi mwenye nazo zaidi ya Yule anayeziangalia maana kwa hofu isiwe kujitetea unaweza kuhofia.
Unapoona umechagua mahala na mwelekeo wa kuelekea alafu kuona hauelekei jua ulikuwa hauelekei,hakuna atakayeweza kukusaidia zaidi ya wewe mwenyewe,nguvu zako ndiyo zitakufikisha unapotaka,pengine usipofika basi jua hazikuwa ni nguvu zako,leo haitasomeka na wengi ya kuwa’ ukweli unauma’kesho usipokuja watakuja wa maana,ikiwa katika kuelewa imeeleweka ni zaidi.
Usikubari kusema basi,ikiwa walianza zamani mpaka sasa wapo,ikiwa alianza zamani mpaka sasa yupo,wewe siyo huyo bali ni Yule maaana itasemeka kwamba ulikuwapo,fikiri nyuma maana mbele kunakusubiri,angalia mbele maana sasa meza imegeuzwa,miguu ikiwa juu kichwa chini siyo tofauti,ni namna ya kufanya kichwa kiwe kama miguu,unapotembea jaribu kuangalia mbele,ikiwa sijui unaangalia wapi maana kila mtu ana yake chaguzi,usihofu yakiwa mengi maana hiyo ni moja yako.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...