Monday, July 23, 2012

KAMPUNI.


Maana wao wananunulika tu,hiyo ikiwa ni kama bidhaa,tena kwa noti mbili zenye thamani moja,hii kweli ni kioja..tufanye noti moja ikawa mfano wa kununulia bidhaa moja na tena ikaja noti nyingine na namna ile ilivyo na biashara kufanyika hapo tunasema kuna uharamu,tena uharamu mkubwa sana bila kugundua maana nitapenda kuelewa wageni wanapokuja kuingia kwenye kampuni mnatoa zipi,zile za kwanza ama hizi zilizofuata,maana pengine zikija za tatu tusiwe na mashaka na za pili,maana za kwanza si zilikuwepo.

Leo ndugu zangu makampuni yanaongezeka,watu wanauza watu na sio mali,maana kama hautataka kufanya kazi katika kiwango cha chini basi kafe njaa,wewe bisha kesho ikutokee maana usiiombee..kesho watoto wetu watakuja na hasira sana maana hata tukishindwa kuwa na kampuni,nchi imegeuka kuwa kampuni,ya nini nishindwe kuwa na nchi yangu,pengine ni wewe,pengine ni mimi  endapo tunakubali ,nina mengi sana kuhusiana na hapa na kama kuna mahala zilibaki basi na sisi tugawieni,maana mbona zipo nusu nusu..au mnasemaje wateja? 

Hapa ni mengi tu jamani mmeyamezea,sijui ni baba zenu wamewaambiaa?maana bora hapa vile viboko vya mchungwa,pale mchungaji anapokuwa hajui kuchunga..haya yamekuwa mateke ya kuambiwa’aya pangeni mstari..kila mmoja anakuja hapa anapigwa teke la tumbo moja moja anaenda zake kulala'..hapa kila mtu angebaki nyumbani kwake ‘kura’ ampigie nani?ndugu zangu muda huu wanosikia wachache sana,ila itakuja kueleweka,maana  hayo yatakuwa ya ‘kodi’ itabidi tuyamalizie ndani ya kampuni..

Sunday, July 22, 2012

DANGANYA TOTO

Kweli ikifahamika kweli itaumiza,maana wakubwa wamekuwa kama watoto,na watoto wanashindwa kuelewa maana wakubwa wamedanganywa na vile walivyotakiwa kudanganyia watoto ni mchanganyiko maisha magumu mtu anajiuza nafsi kwa kidogo kitu ni chakula ndiyo tena ukibisha sana utanunua hata kavu.siku hizi si kwa wanawake tu ndiyo maana hata ikaruhusiwa ndoa za jinsia flani,maana hata hawa hawa wanaume wananunuliwa na hii sielewi sijui ikiwa kununua na kuuza ni tofauti?maana Yule anayenunua danganya toto ili akadanganye toto naye kadanganywa na muuzaji,hapo baada ya kugundua mtoto amedanganganywa kweli..

Leo tunataka barabara ili tuendeshe magari yetu pale sebureni,watoto wakijinadi kwa wazazi si kuna yale magali ya ramani?samahani watoto wenzangu wa uswahili haya yanafuata yalipoelekezwa,pengine yalikuwa machafu basi yanaenda mtoni kuoshwa,na ikiwezekana huyo muoshaji anayehitaji atapata na mengine bure,ila lazima atie saini,sasa umepewa au mumebadilishana?maana watu wanakaa vyuo miaka saba mnataka muwashibishe na makaratasi..?hakuna mtu anayependa kula cha mwenzake,ndiyo maana kila mtu ana kwake,vile vya kwake kula na watoto wake,ili wasidanganyike..

Nani huyo asiyedanganyika maana wanaodanganya wanajua,kwani ile huwa ni tabia,pengine atakaa pembeni na kujifikiria baada ya kujua ukweli,pengine inauma sana ukifikiria ulipodanganywa kitoto toto,achana na hilo imakuwaje taifa zima kudanganyika?maana hapa bila kujua matokeo ya kile tunachokishangilia,tutakufa sisi na kubaki wao,tunaweza kukubali kudanganyika kwa kusema ni ‘Shida’bila ya kujua hata kama ulizaliwa kwa shida,kama kuna mtu alizaliwa kwa raha basi huyo ndiyo anawapa shida wengine..

Saturday, July 21, 2012

USALAMA..


Usalama wangu mnautisha,pengine isitokee kuwa salama,ama ikawa vile itakavyokuwa sihitaji kuyasema haya,maana pengine ni makubwa sana yatufaa kuogopa lakini iwe ni  kwa nini imefanyika hivyo tena isivyo kwa usalama,maana kama ni mlio basi ule wa puh.!ikiwa kimedondoka kikubwa,changanya watu wanakudanganya hali ya sasa si nzuri hata kwa wauza nyama na nyanya,maana wamelima wakajitahidi na kufuga lakini wa kununua nani?ama pengine wafe malishoni,na la kulaumu si jamii kimsingi tukifuatana na hii shilingi.

Maisha salama ni matunzo bora ya mwili,pale unapokubari umeridhika ndiyo hapo unakuwa na maisha salama,ni umelidhika na mazingira uliopo kwa yale unayoyaona,pengine bila kutaka kufikiria mengine,ama ikawe ni uvivu kwa sababu fulani na mida inannaniii..usalama wa maisha yako ni pumzi,maana usikubari ikate kwa kuanza kupungua,pengine kujitahidi iongezeke ikiwa inahitajika zaidi,kwani tunapokuwa na pumzi salama na maamuzi huwa yanakuwa salama,huwa kuna kuwa na subira.

Usalama wako unavuta kheri,maana ukiwa ukiendelea na subira kutokana na malengo yako,pengine unaweza kuwa na usalama katika maisha yako na usijue kama wewe ni nani,hapo ukichelewa watakuiba,maana hujui kitu..basi kubari kuwa wewe kwa usalama wako.maana haya ni maisha yako.Pengine kule mnaniskia maana lengo lenu hili ni salama,haikuwa mapema kumeanza kusikika kwa uvamizi wa fikra za watu,jaribu kufanya mambo yako salama,maana wewe ndiyo mkuu,hii ya kusikia a,a,a,a kila siku watu huchoka na hatimaye kuacha shule,pengine pia ilifananishwa a,e,i,o..na kivile tusingefika salama.

Friday, July 20, 2012

TABIA..

Leo ikiwa inatakiwa kujijua zaidi ya maana ya kujirudia,ingelikuwa ni mpya ningesema usihofu lakini haina maana ya kuingoja wakati ni bure muda unaenda,leo ndiyo siku ya kukwambia maana jana ilikuwa inaanza kujirudia,tena ikafahamike kwamba imerudi kwa ajili ya kuelewa,tena kufanya sahihi kwani ni tabia,tabia kila mtu anayo ya kwake,mwanzo ikaonekana ni makosa yaliyo na samahani kumbe hata wengine walikuwa wakitamani,si wanaujua ukweli,tena hakuna kubisha maana imejirudia. 

Unaweza kujaribu kuwa tofauti na ilivyo lakini mwishowe ni kukubali maelezo,tena ukahisi kuna usaidizi kwa kujulikana ni bahati mbaya lakini tabia yako imejulikana,maana ukionekana sijui ni vipi utasema haina maana,ya kuwa umegundua ni makosa,ni makosa makubwa sana  kwa kutokufanya lile usilokusudia,maana wakati mwingine unaweza kutenda jambo ukihisi umeweza bila ya kujiuliza yaweza kuwa unayarudia,tena yale yale..

Tabia yako chafu sana maana Ikiwa unajua kama unayoyatenda ni makosa alafu unatenda,sasa labda uitwe ni mpumbavu,maana kwa vile ya kutokujua ni mkosa baada ya kufanya kosa,ikiwa mwanzo lilipuuzika tu,hiyo ni tabia ya binadamu kuchagua njia zao katika kuelekea kifo pia,unachagua wenyewe,unajijenga wenyewe,maana kuna vitu unaweza kuishi navyo maishani mwako na usivifurahie,baadaye ukitegemea uvafurahie,inakuwaje usipofurahia milele?maana kwa hapo tu yanakuwa yamewezekana mengi sana..tena yale yale.

Inatakiwa kiingilio sasa katika kuwekeana tabia njema,hapo ukianza tangu utoto,hakuna Yule mwenye tabia nzuri kati yetu wote humu duniani zaidi ni wote tunayajua mema ni yapi na mabaya ni yapi,hapo haikuwa na maana ya kusema mimi,kizuri ni kile cha mtu chake maana mkubwa anasema ili mtoto afuate tabia fulani,tena ikiwa mkubwa amekuwa katika tabia fulani..uelewa ni swala tofauti na tabia,maana tabia ni wewe,ndiyo maana hakuna kama mungu,ni yeye lakini yu ndani yetu,yupo kama sisi,yamkini yeye ni mkuu.yeye anatabia zake..

Wednesday, July 18, 2012

POLENI WATANZANIA..


 
Poleni watanzania,wabishi na mimi nimo..!!maana kwa misiba mingi kufikia,pengine wengine wanasema mungu ametoa na mungu ametwaa vile tukafarijiane majumbani kwetu,muda huu huu wengine tumechelewa kufika eneo la tukio japo tukarusha kamba kuwaokoa wachache pengine ilitakiwa kutokuruhusu leo na kuwa kesho lakini ndiyo imetokea,haya ni majonzi yetu,hapa tunastahiki kushtuka,maana si kwa kutokuwa kawaida bali kuwa tumeuweka uongozi pembeni na kuweka ubinadamu,maana fikiri unaambiwa mtoto wako yupo humo,pengine je wewe ungekuwemo humo?haya ni kiimani zaidi,haya ni ya mungu.


Tusife moyo kwani japo tunarekebishana kidogo,tukumbuke hiace zote zimeacha kutembea mijini na sijui ni kwa sababu ya udogo,ajali ama foleni,pengine bahari imekuwa na mabonde,na madeleva wameshindwa kuendesha kwani walizoea tambarale,pengine ni wazi inahitaji kuvichunguza vyombo vyetu,maana ndiyo tulivyonavyo na kama watu ni wengi inapaswa kuwabeba ikiwa watu hao wanashughuri za kimaendeleo pande ya pili

Zanzibar ni kwetu ndiyo maana tuliungana,kama ingekuwepo sasa ni mimi na wewe,katika muungano kuna mengi humo,mwisho tunapata undugu,kutoka dare s salaam mpaka Zanzibar sio mbali kwa ndege lakini tumezoea meli,na boti huu ni usafiri unaotukidhi na maisha yetu,hivyo tunahaki ya kuwa makini na vyombo tulivyonavyo,ikiwa kama vinataka kuzeeka basi tunavifanya virudi katika ujana kwa maana kikizeeka sana hatuna budi kununua vipya,poleni sana ndugu zangu,poleni sana watanzania wenzangu..
Mungu alaze roho za marehemu pema..!!

HALI BADO NGUMU..


Maana bado inaendelea,hali kuwa ngumu.ikiwa kwa mara ya kwanza tulipoambiwa tukajifanya tumeelewa tena sasa tunaambiwa turudie tunashindwa kuelewa.tumekuwa bidhaa sasa mpaka tukashindwa kuzuia upepo,tunapelekwapelekwa tu,hatuna misimamo zaidi ya kugombania vyama,tunapumbazwa na sifa badala ya maisha yanayotuhusu,maana tunataka haki pasipokujua haki tunapata wapi zaidi na badaye ije tumlaumu mtu,eti aahh Yule hakuwa kiongozi bora,sasa tunataka nini,maisha bora,kiongozi bora,chama bora au wewe bora?hata nisifahamu maana kila mtu ana kujifahamu mwenyewe.

Kesho tuangalie tusije gombana,maana hivi tunavyoenda bila ya kuelewa hiyo inaashiria jambo bovu,maana tutaenda kinyume na maana ya mwongozo,hata kama ni mbovu.nzima ipi?hata hivyo hakutunga yeye..hamkujua ya kaisari anapaswa apewe nani?,sijui hata tutajengaje maana kila mtu atataka kuujenga mnara wake,ili uwe wake ndiyo ndiyo hapo tutatofautisha ujuzi na pesa,mwenye nguvu atajenga tu,kwani we hujui namna ya kufyatua tofali?haina maana ya kuitwa mtanzania kama ni mchina.

Haina maana kumkataza mgeni asiingie na wakati ni kwake,maana ameshanunua sasa tunataka kuwalipa mara mia au?mkubwa akielewa amekosa sio kumchapa mkubwa mwenzake,leo tunaondoka bila taarifa,samahani hivi bunge la nyumbani litaongozwa na nani?kama mama na baba wote wamechukia,na familia zenyewe zilivyo za kihindi kila mtu anataka aonyeshe hasira zake,rudini bungeni jamani..swala la kukaa chini na kuangalia ni nini kifanyike,maana tutagombea viti huku watu wanaendelea kuteseka,maana sijui mtueleze mnang’ang’ania nini na wakati mnashindwa kusaidia watu walio katika msaada,hapa mahala hapata kuwa sawa, hali bado inaashiria  vigumu.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS