Friday, August 10, 2012

NANE NANE


Sitashangaa kusikia moja moja,maana pengine imekuwa ni kama matokeo tu,tunapoonyeshwa hatuoni kwa kusema ona,maana na macho na yenyewe lazima yaambiwe ona,ikiwa kila sauti yanasikia maana tumeona vitu vya ajabu sana katika mikusanyiko yenu,mikutano ikiwa nane inaashiria kuendelea kufika kumi,tujue ya saba imetoka wapi basi.wananchi na nchi yao hawawezi kuwa wapumbavu kwa kushindwa kuelewa wanachoonyeshwa,hapa wanahitaji kuelekeza ikiwezekana kupewa semina,sijui tunaishije bila semina maana ndiyo yamekuwa maisha yetu,sijui unajifunza nini humo,sijui ndo hivi vya semina ama ni katika kufanya biashara.

Siku ikiwa ni ya nane ni kwa sababu ya saba jumapili,ndiyo maana ukasikia sabasaba,hawa watu wanapenda sana kupumzika ikiwa ni siku yao ya kuonyesha,si wanauza..!wewe ndugu yangu umelima lini jana tunasikia unalia njaa?au nini nisaidie ndugu yangu maana kila kitu siku hizi ni maonyesho ya sabasaba,wapeni watu uzalendo wa kuifikiria siku kuku,pengine mtu akiwaza shari kuzidi heri,sikunyingine zinakuja maana mpaka kumi kumi.ikiwa huduma zitaonekana kuwa duni.

Muda unatoka tofauti ya vile tulivyofundishwa,maana na wenyewe wanahitaji kufundishwa,kwa hilo ukiamua kusema kilimo kinaanza sio kama uzamini wa simba na yanga,hapa ni zaidi ya ‘madaruga’ na ‘mabarugaja’,ni zaidi ya kombati siku yake ya kumi inapofikia,maana hapa tutasema dunia imejaa mengi kwa bila kufikiri yale yamoyoni umeyaweka sana akilini,inaleta matatizo kubadili maana kwa kuonekana ikiwa kama ushahidi,angalia namna ya maisha uliyochagua kabla siku ya saba haijaisha maana hii ya nane utaingia shambani.

Wednesday, August 8, 2012

VIJANA MSILIE..



Haina haja ya kutoa machozi wakati unayeishi ni wewe mwenyewe,haikuwa na maana ya kutafuta na kufika mahala fulani,serikali ikiwa sio baba wala mama yako,serikali ukiwa ni wewe na unahitaji kusaidia wananchi wasiojiweza,msilie wale wa mbagala mabomu,msilie enyi wataifa kama wafuasi wa kibwetele,utamaliza nguvu zeko bure,maana anayetakiwa kusikia ameongeza sauti ya kutokusikia,ukisema umechoka kwa yale uliyoyalilia,ni baada ya kuwa magumu na ahadi wengi umewapatia.

Unakaukiwa maji mwilini na mabomba yamekatwa,ikiwa maisha ya chini ya mtanzania ni chini ya dora,yanashida sana kwa ajili ya kuongezeka kuwa mengi hapo wengine watalia wakitaka usaidizi bila kujua wamejijazia wenyewe,haitaleta maana.ukiwa mwalimu ni lazima utengeneze pesa kupitia mlango mwengine,swali linakuja ni unawezaje kutengeneza?maana yeye akafundishe kufanya biashara na asifanye,unawezaje kukaa na kuja na majibu mazuri ambayo yasikufanye ukalia,hapo ni swala la mwalimu kukubali kusoma yale ya duniani,kama umegundua kitu hakiendi ni heri kukiacha maana kitakuliza sana.

Duniani kuna lile la ukitaka kuwa na pesa ni lazima ukae katika mchezo wanaotengenezea pesa,hapa labda kimazingira maana kuna mahala pesa zinamwagika kama vile zinatengenezwa,yale ya msingi yakiwa bado hayajafanyiwa kazi,ukiwa nje tu utaskia pale ni pazuri,ni kwa sababu ya kuutambua uzuri,usiende na maisha yako na baadaye kuwapa watu lawama,kama ulishazaliwa na unakuwa jua wewe ni wewe,jitambue.hata ukitokwa machozi hutafutw, wachache sana,na ukisema hafadhari ya kwa heri,maana huko unakoelekea yaweza ukatoa machozi sana,kwa vile ilivyo hata haikutegemeka.

ASILI...


Hii ikiwa ni kama tabia lakini pengine hapa tukajumuisha wengi,
hapa ikawa ni mazoea kwa kuwa wengi huwa wanatumia kufanya hiyvo,sio ya kwamba wamekosa au hawajafuata maelekezo ni namna ya vile ya asili ya waliopo juu wanavyofanya maana hata katika nafasi ndogo ilibidi wafanye wale wa hali ya chini sasa wakubwa wanafanya,hivyo inaleta kulalama kwa kuwa hali ni ngumu,tulipotoka ni mbali wala haina haja ya kuyakumbukia labda tusubiri matokeo maana tulishalalamika kabla ya kufanya.

Tunapopaza sauti kwa kutaka kusikika ni namna ya vile kutumia nguvu kubwa wakati safari ni ndogo,
pale tunapohitaji kutulia na kufanya yale tunayoyaweza yanakuwa magumu yakuwa yalizoeleka ni mengine,
ikiwa asili imepoteza maana yake,na asili sio mtu zaidi ya mtu vile alivyo,maana kila mtu anafanya vile katika wakati na mlengo wake,tunapokuwa tunaheshimu asili zetu tunajua kile tunachokiwaza,
ikiwa ni mafanikio na maono ya kufika pale unapohitaji kwa undani na kukufanya ujiskie vizuri.

Maisha ya mwanadamu hayajaumbwa kwa shida,labda pengine tumechelewa,na hivyo ikiwa tunaishi tofauti na asili zetu,sio kwamba kujiskia vizuri ndiyo kuwa na asili nzuri,pengine asili haina maana kwa kuwa unaishi kwa namna unavyoishi,hapo ukiwa umechagua kufurahia maisha yako.

Sunday, August 5, 2012

MIPAKA..


Leo imefika tunagombana kwa yale tuliyoyashindwa jana,pengine haikuleta faida sana,ama hasara ikiwa endapo kama tunaweza kukaa na mali na bila ya kuziendeleza basi ni tumeshindwa kabisa,hii ikiwa mali zenyewe zinaendelezeka,inapofika mwisho wa jambo ni haki kuweka alama ikiwa ni kwako,hii haki..maana ni dhuruma kwa mwengine kuichukua.tusifikiri tumeishi zamani  na ya kutamani tutayaweza,zisije fikra zenyewe kwani wengine wameshasema wakijiandaa mapema.leo ikiwa mwisho kulipia haina maana ya kesho usilipe,ila kama ilichukulika bila ya malipo ya kuelewana kuna uwalakini wa kutokuelewana zaidi,hasa mzazi anapomwambia mwana mpaka wako wa kucheza ni mwisho hapa.

Ni wazi ya kuonekana hayafichiki,tuseme vingine vipo wazi lakini vinahitaji ubishi,maana kama kuna kukubari haraka haraka hata itakuja siku tuwakatae wazazi wetu,kama walivyo wengine tayari kuona mipaka yao kwa wazazi wao,maana  mmoja atasema huyu sio mama yangu na mwengine atasema wala baba.hapo tukivuka mipaka bila  ya kufahamu kama mwisho wa safari ndiyo mwanzo maana yapasa kujipanga upya.

Leo unaweza kugombana sana,pengine watakufa wachache na kwa wengine ikawa maana,
maana unaweza kujiuliza tangia siku zote hizo ulikuwa wapi?
hapa ikiwa  tunataka sababu.kama kwa mungu hakuna mipaka basi hakuna anayejua,
maana hii yetu sijui tumeitoa wapi ikiwa bado tutaendelea kung’ang’ania hata vile visivyo vyetu,mwishoni kueleweka mambumbumbu kwani hata na kuingia shuleni hakuna cha zaidi ya kufanyia tulichojua zaidi ya mipaka ya shule yenyewe,unapoambiwa uingie chumbani kwa baba sio uzungu ni muvi za video tu hizo,waache wakubwa wanaongea watafikia mwisho wa mipaka yao.

LIFETIME..

Life is undetermined, and this if most of us do not understand in what we call large percentage, not as we want to do our things that influenced by external objects, as well as finding that what it was in detail on positive thoughts about you, if its love, faith, and other things that surrounding us, we say and think that we loved because we never hated, if each one explains what he/she is feeling and will in the world through his/her lifetime. That will be a lifetime.

Fewer and much else seems in as one he/she saw, perhaps as a parent batters son hit, I do not know if the son he is considering on what, for such an error would have been told he would understand, even seventy times that at the time noted and thought well, maybe we know the parent is concerned about what after penalty therefore,the child would probably have restored? Or imagine how it can be unfortunately? Few here will understand that of large percentage..!!For those who choose to live in such a way to appreciate their lives as a smooth load.

Perhaps we will give judgment here in the world, when we have not understood why some of things happen in our lives, perhaps become we understand but not as most of it is, or its smaller than everyone understood as one suppose to understood him/her self, for should not understand other than you, because as was heard, 'A' another said, 'B', each one will tell us how he/she heard and say, or perhaps we should have learned abroad.

Saturday, August 4, 2012

KIALIMU ZAIDI...

Mwalimu kazi yake ni kufundisha,kama ilivyo kwa daktari kutibu,kwa meneja kutawala,ikawa na kwa muhasibu kuhesabu na vyovyote vingene inavyokuwa alimradi ni kazi ya mtu ameichagua,pengine kazi zote ni sawa kutokana na mahitaji ya mtu mwenyewe,imekuwa ni kwa kasi kubwa wale wasomi kutaka kazi tena zenye mishahara minono,hiyo ikiwa wametoka shuleni,wao wakidai wamepoteza muda mwingi wakiutumia kusoma sio kama vile wale waliobaki wakiamua kutafuta maisha yao katika namna wanavyoweza.na wao wanafanikiwa zaidi,hivyo ikawa isilete lawama kwa kuwa kama ni shule mtu umeamua kwenda mwenyewe,tena kama ni chanda kilikuwa kikicheza tu ni lazima tutafute namna ya walivyokuwa wanamchezesha,maana wengine wamejifunza vizuri ru.

Pengine leo hii utaambiwa sio haki yako,pengine ni wito,mwalimu anayeamua kufundisha kuanzia saa moja asubui hadi jioni huyo ametimiza wito wake,kwa maana ametaka watu kuelewa zaidi ya kile anachoridhika nacho,baba wa taifa alipata kuridhika na mali alizonazo na kama angegoma kufundisha watanzania mpaka sasa tungekuwa tunatawaliwa na mtindo tofauti sana,pengine hata tusingepata nafasi ya kugoma,tusifananishe maisha yetu ya kuwa hatuna uwezo wa kupigiwa simu saa nane za usiku kana kwamba kuna mwanafunzi amezidiwa kwa kuwa kesho na mtihani,kazi ni kufundisha,swala la kuelewa hilo hatuwezi kulazimishana..

Pengine ndugu zetu tuangalie na usalama wa nchi yetu,hata kama tunadai haki zetu.haya mengine machache tu na ikiwa umeona umeshindwa kuishi wewe,hata watoto wako wataishi tu,labda ikiwa haina maana ya kujipanga tena maana umeshachelewa,wengine tuendelee kukaza buti maana hili ni janga letu sote,kama tutagoma kula chakula tulichopika wenyewe hapa yapasa kusafirisha njaa, maana tusipoileta katika muda hata wa nyongeza,hapo tutaeleweka kama wanafunzi maana swala ni kuishi.

MAISHA YA KUTUMIKA..

Katika kutumika ni lazima kusafiri na kujua katika nafsi umeweza kufikia malengo fulani,umekuwa katika akili na yote kufanyika ikiwa kila mmoja amechukua nafasi yake,kufuta yale ya zamani pengine yanaweza kuwa mabovu,katika kufanya maisha yawe katika namna ya kutumika ni kuendelea na maisha yako katika mlengo wa maono na dhumuni ikiwa vyote sio kitu kimoja,na hapo ukafungue milango yetu ya kuelewa ili uweze kuelewa namna ya kuishi,tofauti ya vile unavyotamani.

kila maisha ya mwanadamu yana maana yake ikiwa sababu imeanza kwanza,hivyo mwanadamu anapaswa kufanya na kuingia katika mawazo ambayo yanaweza kumjenga ili yeye mwenyewe aweze kuelewa sababu yake,unaweza kuishi tofauti na kusema hiyo ni sababu moja wapo ya kuishi lakini sio ile moja ambayo kila mtu anayo ya kwake,pengine haikupaswa kuishi hivyo unavyoishi,ama ilikuwa ni chini sana na kutokana na juhudi zako umefika hapo,na hiyo ni kwa sababu ilisemwa lazima kufanya ili kusaidikika,pengine mengine yakiwa ya ziada na msaada basi unastahiri kushukuru kwa yote.

Bila kukubali katika maisha ya kutumika hapo hatutatumika,hapo hautajielewa vyema vile ulivyo kwa maana ya kutokujua uwezo wa kweli ulionao katika sababu ya kuishi humu duniani,pengine inakulazimu kujua yapasa muda mwingine kupata vile vya pembeni na hiyo ikiwa kila mtu ana asili yake ya kupata kile kilicho cha pekee kwake,pale unapotumika uangalie muda ya kuwa kuna kuharibika baada ya kukaa muda mrefu,na kama tutaharibika na kuendelea kutumika hapo utakuwa unajizika wenyewe ya maana kama wafu.Tuzitumikie nafasi zetu vile tunataka maisha yetu kuwa.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS