Saturday, November 10, 2012

SHUKURU KWA YOTE..


Hapa  akihusishwa Mungu kwanza maana kila mtu anayajua yake inapaswa kushukuru kwa kuwa ni kazi nzito umeifanya,Asante Mwenyezi Mungu.
Ukiwa una uelewa ni lazima kubaki katika njia ambayo wewe mwenyewe unaiona siyo ya mapumziko maana ni lazima kutoa nguvu  Pamoja na akili yako ukiwa umeamka na kuchagua kile ambacho wewe umetaka kukiangalia,ukichagua lile ambalo limekuja katika muda unaofaa kimaendeleo,ikiwa maisha ni sehemu inayofanya ndoto kukamilika,ki imani ikiwa kama ndoto ni jibu la tatizo.pale unapomaliza jambo yapasa kushukuru kwa kuwa linakuwa vile kidogo ya ulivyofikiri,huwa yanafanana lakini rangi tofauti na kuthaminisha kule/kile/vile ulivyofanya.


Kama una ndoto ya kuwa  na furaha ama vile katika hali isiyofahamika,kama unapofumba macho ukitegemea kuona chochote mengine yatapita yakiwa ni afadhali kwa kuwa yatastahiri kukuchanganya,shukuru kwa kuwa siyo yote unayoyategemea hutokea ,mengine yakiwa yameletwa maksudi ili mradi na wengine wakapata shukrani za lazima,lakini ikiwa kama mtu ameamua kufa kwa kujinyonga akipona hastahiri kushukuru kwani lengo lake halijatimia.


Pongezi kwa shukrani iliyomaliza jambo,hongera hutoka pale shukrani inapokuwa na jibu lake katika jambo husika,maana katika namna ya kuzaliwa kwa sisi waswahili zinaweza kuwa ni kejeli,ikiwa unataka kuona ni nini unachokifanya haistahili kuuliza bila ya kuulizwa,hapa itatakikana kuonekana mwisho ikiwa unakipaji chochote cha kufanya hakitaweza kulinganishwa na muangaliaji ama yule asemaye kwani mwishoni huja na kukuvisha taji.mawazo yako ndiyo mtaji shukuru Mungu wako alikuumba wewe. hata ungali muda bado kuisha.

Friday, November 9, 2012

USIOGOPE,KUWA NA FURAHA…


Ni namna ya maisha yanavyokwenda,maana leo ikaja lakini siyo kesho,ukawa na hofu ya leo maana ile ya jana nusu imeishia leo.. kama ilikuwa ni chuki wazi ukawa na wasi wa kesho kuja na kukudhuru tena,usiogope kwa kuwa haujui,na tena kuwa na furaha kwani ukijua hautaweza kuogopa,hivi muda unavyokwenda unapelekwa na wewe,hivi kesho giza baadaye ujue unaileta wewee...mwangaza wa kung’aa humulika mbali kwa kuwa huitaji kukumulikia,ikiwa mazuri unayaogopa basi kuwa na furaha na mabaya ya baadaye.

Muda wa kutokuzungumza utafika,ile shule ya maisha yako ukaja kuijua shuleni.tena ukajifunza mawili kwa kuogopa kujua lako moja,leo ukiwa unajitahidi kesho utaweza maana njia ya mpita njia hueleweka yake kwa kuwa hupita kila siku hapo kwenye njia yake,pengine ikiwa ni mara chache acha jina basi,maisha mengine hayajulikani,hayo ndiyo maisha yako,pengine ukitaka kuyabadilisha ni uyabadilishe hapo ulipo,ujibadilishe,ukaogopa kupangua kwa sababu ya uwingi wa kushindwa kupanga tena jua unaidhurumu furaha yako,dhuruma mbaya maana hitaji lake wakati wa kurudi ni FURAHA.

Sitaweza kuogopa kukwambia ukweli kwani naihitaji furaha yangu baadaye,kwa Yule anayeogopa kwa kusema uwongo wakati ukweli upo,hafai hata kujifunza jambo,maaana ataangamiza jamii kwa kutengeneza siraha inayodhuru bila woga.pengine usiogope kusema utakavyo maana hautaishi tena,kama ikiwa  ni katika namna tofauti,hata kama umewahi kusikia pale mtu akisifia “ahh yale siyo maisha”..yapo yale yaliyo ni maisha pengine kama ulikuwa unaogopa kuuliza ijue furaha yako.

Wednesday, November 7, 2012

MAZURI YANGALI KUJA.

Hapa nazungumzia nafsi ya kila mmoja,ikiwa hata wewe leo ukaelewa iwe katika ndoa namna ya vile maisha yanavyokuwa iwe katika hali ya kutokuwa katika ndoa na kukuta maisha yako vile vile jinsi yalivyo,maisha bado kwa wengine yakiwa ya uadui tu,ikiwa unawaza kuanguka kamwe huwezi kuiona siku yako ya mafanikio.maana mazuri huja baada ya kipimo chako cha kufanikiwa,pale ukaishi maisha mengi na yaliyo jaa vingi,pale umetegemea mengi lakini hakuna katika yale uliyoyafikiria  kutenda na kutokea,maana waweza fanya mia leo na kesho kuja moja na kudhani yale mia yalikuwa ni kanuni,mazuri yangali njiani,mazuri yangali kuja maana kama umefikiri sahihi lazima kuielewa ile maana ya kwanza yaani sababu.

Kama yalikuja basi hongera maana pengine sijui mtu unaishi ukifikiria nini,waweza kuota ndoto na kulazimisha kutokea,ikiwa umezani wewe ni mkuu sana kwa nafasi uliyopo,ukijisahau kwa kuwa  fikra zako ni zimekujaa wewe pekee,kumbuka hakuna mtu anayemfikiria mwenziye katika namna mwenziye anavyomfikiria,ukiambiwa  kuongea peke yako yapasa kuelewa hasa unaposikia ukidhani rahisi ama magumu yote.mazuri yangali kuja,hayo magumu ndiyo njia ya kwenda kuzuri,ukiwa na furaha sasa jua ni yale marahisi yamewezakana,ikiwa mazuri yangali  kuja.

Furaha ya mchizi ni kufurahi,pengine furaha ya mchizi ni anaifahamu mwenyewe,ikiwa umeona mazuri siyo ya kwamba yamekuja ,angalia kesho usijenuna na kupewa lawama,maana si furaha yako unaijua mwenyewe,anayeamini anapata maana anakuwa ametaka akifikiri yatakayotokea,ikiwa mwanzo wa jambo basi una mwisho,wanaposema Mungu hamtupi mja wake siyo kila mtu ni mja wa Mungu,maana Mungu wa mmoja si mmoja yule wa amwaminie mwengine na pengine kesho ifikirike ili ya jana yakaonekana ni tofauti.

Mazuri yangali kuja...!!

Tuesday, November 6, 2012

MJUE WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.......


WALTER CHILAMBO SPEECHWISE.. NI mshiriki wa EPIC BONGO STAR SEARCH ANAYETOKEA MBEYA,HIVI SASA AKIWA KATIKA FAINALI HIYO ITAKAYO FANYIKA DIAMOND JUBILEE IJUMAA TAREHE 9 MWEZI HUU..HAYA MACHACHE KUTOKA KWAKE MWENYEWE WALTER... 


"Nashukuru sana watu wangu, ni Maombi na Kura zenu tuu.. Nashukuru kuingia FAINALI na nakuomba endelea na moyo huohuo kwa kunipigia kura kwa kuandika neno EBSS12 kwenda namba 15530".
Hiyo ni status aliyoiandika Walter katika ukurasa wake wa Facebook na Twitter jana baada ya kurushwa kwa show yake ya nusu fainali iliyompelekea kuingia fainali itakayofanyika Diomond Jubilee, Ijumaa ya tarehe 09/11/2012.
Pamoja na hayo Walter aliongeza kuwa anamshukuru Mungu na watanzania kwa hatua aliyofikia kwani haikuwa rahisi kihivyo.
Pia Walter ameongelea suala la yeye kuwa amnatokea Mbeya kwani ni jambo lililokuwa linachanganya watu wengi.

            

"Mimi ni mzaliwa wa Mbeya na naishi huko na mama yangu na wakati wa audition za EBSS nilikuwa nipo Dar katika michakato yangu na ndio sababu nikasailiwa kama mshiriki kutoka Dar".

Aliongeza, "Naomba watu wangu waendelee na moyo huo huo wa kuwa bega kwa bega na mimi na waendelee kunipigia kura kwani kura ndio kila kitu hata kama nitapendwa vipi"
Walter ni mshiriki aliyeingia FAINALI pamoja na wenzake wanne, hivyo washiriki wa EBSS waliobaki katika fainali ni Walter, Nshoma, Nsami, Wababa pamoja na Guiter gira Salma...
Ili kumpigia kura Walter Chilambo, andika neno EBSS12 kwenda namba 15530".

Monday, November 5, 2012

CHUNGA KAULI..

Hata zikiwa nyingi wachache hutaka moja tu kauli kuielewa,kwa kujua kwa yale mengi hakuna wa kuyaweza naye.ukisikia kauli lazima uishike isiwe kauli  nyingine zikasahaulika,ama ikaonekana vile walivyosema wengine,kwamba kauli ya mtoto kumwambia mkubwa yaweza kuwa makosa ki heshima,lakini siyo ikawe mkubwa kwa mkubwa mwenzake,ikawa si hekima,maana itaoneka dhambi kwa kujaribu kuyafanya ya juani wakati kauli nyingine ni za gizani.

Ni wazi hakuna lililo sahihi zaidi yako Mungu,kwa Yule anayebisha ni sawa na kufananisha ndiyo na hapana ,ukikaa na kukuwa bila kuelewa utanawa sana kichwa kwa kupata moto tena hutaelewa nini cha kufanya pengine ukiwa haujafanya kitu hapo mwanzo lakini kauli zako zikakukuponza.

Ninatoa kauli yangu pale inaponibidi ikiwa nazijua haki zangu,akili yangu inajua cha ziada nje ya mwili kinachoendelea,hivyo kauli yako yaweza kukuliza ikiwa hujachukua dhamna ya kuyabeba majibu yatokanayo na kauli zako,ni mizigo ya ndani,wachache wanafunzi huelewa nini mwalimu anachofundisha,maana kila mwanafunzi anaelewa yake pale inapokuwa nafasi na wakati wa  kila mmoja kutoa kauli yake katika uelewa

Ni kweli kauli nyingine ni makosa sana kutamkwa,si vyema kusema kitu usichokifahamu na kugeuza kauli yako ya kweli,ni wazi hata samahani isimaanishe kitu hata ikawe kwa mtu kuuana na mwenziwe.kauli nyingine hazitakiwi kukumbukwa,kauli nyingine zina maana ya kuleta kauli nyingine zisizo na maana.Chunga kauli.


Friday, November 2, 2012

NISHIKE..


Utawaza kushika maneno ya bwana mungu kwa kuwa yapo katika maandishi na kujifanya kujua kusoma,maana ni wazi kama angekuwa mbuzi sababu zingepigiwa mstari kwa kuwa ni sahihi,pengine ili kutokupigiwa mstari tukae ukinishika mkono kwa kunielekeza,maana pengine naona giza,huo mwanga siyo kama huu,huo nahitaji kushika kwa kunipendezesha,acha harufu kwani umepuliza wa kutosha sasa angarau nikaotee jua,najua japo nikishika moto pengine nitaotea kwa yale mema kuwa mabaya,kwa ule wema kuwa wa mbaya.

Ukishika bilioni lazima utakuwa billionea,ukishika maneno ya bwana mungu wako lazima utakuwa mtoto wa mungu wako,pengine ikiwa umeyashika kwa sababu ipi,ikiwa umeyashika unayoyajua wewe,kesho mwanafunzi anapofeli darasani aulizwe nini anataka ili afauru,pengine isipokuwa kwa kushika ramani ama kuleta amani.maana ikiwa umefeli umetaka kushitaki,haina maana kwa waliofauru kwa kutokwenda kushitaki.

Hapa kunaweza kuwa na chaguzi hasa zaidi katika yale mazuri na mabaya,yale ambayo mmoja akayaona kuwa ndiyo na mwengine akasema  kwa mshituko kwamba siyo,kuwa na imani kwa lolote lile unalohitaji kulishika,imani ya kushika unapohitaji siyo ya kuthubutu endapo kukiwa na mahitaji,tabu zikamfanye mtu ajitambue zaidi yakuwa ameshika yale yaliyomletea taabu ama raha zaidi.ama tuyashike yale tuliyofundishwa zaidi.

SAHAU.


Kuna muda yapasa kujifanya kutokujua kwa kusahau pengine ikiwa ni makusudi ama vile ikawe ni mpango wako mwenyewe,kama ungejulishwa lile lililo katika ndoto zako ndiyo ukweli hakika ungeamini yako,sasa unaweza kuwa umesahau,muda huu unaweza ukawa kama siyo yale uliyokuwa unayaota kwa kuwa ni haki ukweli upo,pengine ukiwa unaamini yako kwa kuwa ndoto hazikusema,ama zimesema lakini umesahau kwani mambo na yenyewe ni mengi mno kwa kujichanganya na nafsi.

Utasikia huyu mimi simpendi,hapo akiwa ameshindwa yeye kukupenda,ikapita dakika kwa yanayofahamika ni lazima kuwa wazi,maana pengine unaweza kutega kwa kusahau,ukijiuliza umesahau yapi kama siyo unayoyajua,maana mapya na yenyewe yanapokuja huleta utofauti na yale ya mwanzo,hawa wa kwanza wakiwa wamekula sana,ikiwa siyo wa kwanza kabisa wao hawakula na wakijifanya wamesahau,na kwa muda unavyokwenda hawa waliokuwa hawajui imekuja kujua,maana kujitambua.

Kesho sahau sema jana nilisahau,usisubiri kukumbushwa maana wengine wanakusahaulisha kwa lazima,wakitaka kukamilisha kauli ile ya kutokupenda mengine yamekuja baada ya wengine nao kuota tofauti,wakiamini kusherehekea ndoto za wenzao kuliko yale ya kwao,unaweza tangaza vita kwa kupotelewa na siraha  bila ya kujua kama ulikuwa hujui matumizi yake,nisisahau mimi Siraha,Nisisahau mimi siku za vitani.

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...