Saturday, June 9, 2012

HII KALI..

Maji ndiyo haya yanaitwa 'water',na 'man' sio neno bali ni kauli ya kuogopa,hapa tunataka uhai..hapa tunataka pumzi zisizo sio za kuogopa,tumechoka kuchokeshwa,hatujachoka kulalama,maana hata tukanyamaza leo wengine watasema,haina haja kumfikiria mwengine ikiwa hatujajifikiria,haitawezekana kwa wengine ikiwa hatujajimilikisha,sasa ni ndiyo sasa,sasa ndiyo hasa tunahitaji kujipiga msasa,pengine bila kujari zile za jana anasa.

Ndiyo tunafanya,ndiyo hatutakiwi kufanya,hapo ikawe hatujakatazwa bali ni hatari kwa afya yako,
hiyo ni kwa kila mtu,hasa kama hapa tunapozungumza pamoja,hapa tuangalie ya zamani,hapa tukajifunze kupitia hayo,maana hata hatuwezi kujifunza bila kujua vitu hivyo yaani hayo ya mwanzo,
na ikiwa pale mwisho unaeleweka,yaani upi ni mwanzo maana tukajisahau kuwa mwishoni na kuuweka mwanzo ikiwa ni sababu,tena baadaye tukasema kila jambo,tuangalie sana hapa,tuangalie sana tunakoelekea,hata tulipotoka ikiwa ni mwanzo huko,ikiwepo mwisho kwa mmoja basi yapasa kuonyeshwa mwanzo wake.

Hatutaki kupigana na yale yasiyo na maana bora,kwani kufanya jema lililo sasa ni kutengeneza kile kilichopo baadaye,haina haja ya kujisemea na wakati walishasema,watasema na sisi inabidi tuseme maana watakao sikia na wao watahitaji kusema pia

Tunahitaji mazoezi ili kujenga miili yetu,tunahitaji maongezi ili kujenga misingi yetu,tunahitaji maamuzi ili kujenga mbele yetu,maana likiwapo hakuna linalorudiwa,sio kwa kupotea bali halikufanyika,na hapa yapasa kurudia,sasa tusijerudia kazi za nyumbani,hizi ni kazi zisizo hitaji utani

Friday, June 8, 2012

NAMNA..

Tumeyachagua wenyewe,hapa machache yameongeleka lakini yasipigiwe vigeregere,
usiombe kusubiri,usiombe usubiri,
maana pengine mazoezi yatakuwa makali sana kipindi hicho,
yataongezeka kwa kulingana na muda,pale tukitaka kupumzika bila hitaji letu,

Tukataka kutulia na kupigiwa makelele majumbani kwetu,
pengine tukiwa hatutaki usumbufu,
pengine sisi ni wasumbufu sana,
hapa ni kuelewa,hasa kwa mmoja na mwenzake mwenye uelewa.

Yanayochagulika ndiyo hasa tuliamua kuyafanya,
maana hapo baadaye tukasema ziikuwa ni ndoto,tena tusijue tumeota wapi na lini?
bali tukafananisha si tunaijua jumamosi?ya kila mtu ndiyo iliyo ya kwake maana pengine ilipogeuzwa ilifanyika kwa namna ya kugeuka,

pale itakapogeuzwa zaidi itageuka na yenyewe,
maana muda unasema unataka kwenda na sisi ili na wenyewe ufurahi,
pengine ndiyo maana tunahadhibiwa kwa kutokuwa na muda.
Hapa mengine yaliyochagulika yakawa ndiyo hayo yaliyopita,
si kama imegeuka vilee..tumefikiri sasa bila kujua uzee wa mbao kabla ya msasa,
tutazeeka sana,kama tutapigana na bila  ya hamasa.

MOYO WAKO.

Inapofika wakati isiwe na maana ya kumchagulia mtu,pale inapokuwa imewezekana basi ndipo huwa yanaonekana ya maana,maana hatuwezi kusema usiku ni muda wa kulala na wakati watoto bado hawajala,tukitumia damu hatutaweza kujishafisha na dhambi zetu bila maelewano,na tukataka kuelewana ili hata kwa yule asiyeelewa akaelewe,

Wana jeshi wengi wametuzunguka,matapeli kweli tunawakumbuka,wakijifanya wakihasi hata kwa kuuchoma moyo mkuki,tungalitukitaka kujua jana fulani kasema nini basi ni lazima tukae chini tukumbuke,askari mmoja aliyemdhuru askali mwenzake,maana pale yaliyotoka yale ya moyoni,yalikuwa tofauti sana na vile ilivyokuwa katika kupigana,haikueleweka,pengine hawaelewei,mwanajeshi aliye bora hapigani,mwanajeshi waliye na moyo bora anapigana..ni anataka haki,na haki ya moyo hutenda kile kisichorudikana,hufanya kazi pale ikawepo imesemeka,na hata kufanyika pengine.


Jamani tufuatane,jamani tuungane,katika vigumu vya kuunganisha ni mioyo,iwepo mioyo tukapeana hadi wanaume,pengine ndiyo maana yapasa kuoa,yapasa kuwa na mtu wa karibu japo ya moyoni kabla ya mkuki tukayaskia,mioyo ikiunganika ndiyo pale kunakuwa na upendo,pale tukapendana hata kwa bila ya kuonana.

Moyo wako ukisema vizuri usikilize,maneno yako ukiyaone mazuri yasikilize..tunapotaka kuwa watu wazuri ni tunataka kuwa na moyo mzuri,tukumbuke damu imesambaa kwingi,imeingia akilini mwa watu na pasieleweke ikigombaniwa nini?kama ni pesa ni kuzitafuta na vile ilivyo furaha iyo ni ya mtu,furaha ya mtu anayo mwenyewe,kwa yule anayeitafuta furaha asipoifahamu yake tumwangalie asijeleta vita tukachomana mikuki.

DUNIA.

Walio na kusikia wasikie kwa jinsi dunia na mihimiri yake inavyojizungusha,kutoka pande moja na kuelekea kwengine,labda kwa lugha hii ndiyo itakuwa rahisi'kwani yule aliyeamua kuweka kulia na mwengine aliweka kushoto,wote wakiwa na maana ya kitu kuelekea ila kupasa kuonyesha utofauti na utofauti uliopo ni huo wa kushoto na kulia,hivyo mengine yatakuwa na maana moja,hivyo pegine tukaweza kuelewa kwa pamoja.

Tatizo lije pale chaguzi zinapoingiliana,matatizo yatakuja pale chaguzi zinapokuwa tofauti,ikiwa imechagulika vyema kwa kupatiwa maana yake,na nyengine ikaonekana sio njema kwa vile na chaguzi lake,hapa na pale mmoja akataka kushoto na mwengine akaelekea kulia,hivo ikiwa ilifikirika kwanza.

Katika  kuelekea kuna kuchanganya,katika muelekeo labda tupate njia zile zilizo pana,ili pa kupumzikia pasije pakawa na uhaba,ya kila siku yakatendeke yakiwa hata ikawa mara saba,tusameheane kwa hilo,tusameheane hata mara sabini,na ndiyo maana ya kuweka umahala,ndiyo maana pakawa pakawa.kote pamekuwa ni sahihi,fanya wewe,anza wewe.

Haja ya kulia na kushoto ni mengi,ya kati yale yanayosimama,kwani tunaweza kusimama kulia lakini katikati.kulia na kushoto ndiyo kumetofautisha,tufanye tuchukue vyote hata katika maumbo,hata tukalizungusha tukipeleka kulia na baadaye litakuja kushoto,hivyo ni kuwa makini hasa kwa pale tunapokuwepo,inazunguka na baadaye kushoto kukawa nyuma na kulia mbele,au kulia nyuma na kushoto mbele.
Tuelewe kwa mduara uliopo,maana hata ikaelekea kushoto yaweza kuelekea na kulia,inajizungusha..

Thursday, June 7, 2012

UOTO..

Tusitake ubishi kwa yaliyo matapishi,tusipende upishi kwa walio wabishi,tumeamka leo mapema ikaonekana ni wabishi,tumefanya leo jambo jema isije kuwa watishi,watoto chungeni wazazi wenu wanawaona,wakubwa jiangalieni madogo mumeyaona,tumetoka juzi kufanya bila kujua,tulifahamu juzi kwa watoto walitambua,mizigo  midogo vyombo vikubwa visije ungua,uadilifu mdogo tuyaangalie makubwa yatatuumbua..

Samaki mkunje akitaka akikatika amezeeka,samaki mbonye  akiweza kaoza,ona tumekuja leo bila kuzoza,wachache jitayarisheni mje kutuongoza,tumesubiri sana tusije kupuuza,watoto kaeni wazazi kuwatunza,wazazi kaeni chinjo wakubwa wamekuwa,tusiseme kwa sasa ya kuwa tumejipiga msasa,tusiseme ya sasa kwani yametungoja sana


Vichwa vitakuja na kuwa wangu mkia,watoto watakuwa bila ya salamu kuwatamkia,haki iacheni mwenyezi akatubarikia,mabaki yaacheni maana wasije kututapikia,wachache waacheni maana matusi watatutamkia,haki ya nani wa kwanza kashika mkia,haki ya Fulani wa mwisho atapaswa kutuamkia,adhabu hapewi mtu akafa akafia,adhabu hapewi mtu yakaja yakamfikia.

Tunaondoka tukienda tukisema,tunaenda tukiondoka tukihema,mazoezi yamekuwa mazito kwa watoto na kunena,mapenzi yamekuwa mazito kwa Fulani kunisema,haki hawa watoto wa vizito sio tukiwasubiri tutawasoma,haki wa kwa watu wenye vibito kwa foleni hawatagoma.mtoto subiri haya magali yamegoma,ingekuwa kiroboto asingesubiri kwa magodoro kuyachoma.

Ndoto zikamilike kwa watoto,uoto uelimike hata kwa viboko..

Wednesday, June 6, 2012

VIMO..?

Naamka baba nishike mkono,nimeshtuka maana tusije fika kikomo,wameshuka maana hawakulisoma somo,wamechemka kwa sababu ya kuwapo humo,pilika na mazoea yameibua mengine,birika na vya kuzolea yamekuwa mengine,tukaamke tukasahau iwapo kama ipo,tukatembee tukakumbuka kama yapo yapo,yakatembea tukawepo kama ya kukumbuka yapo,pengine ni namna kubwa sana,pengine ni asili kubwa sana,palipooza tupaache maana muda si mrefu patapasuka,embu tuone la pili hata la mwenza maana haya machache yamejichanganya na meupe.

Kinachokuwa na msingi nikuweka nakshi,kinachokuwa na mchuzi ni kuweka nazi,pengine tukaseme kama mwanzo ya kuijua minazi kuliko nafsi zetu,ikawe ni kwa yaliyojaa na mengine kushindwa kutoka,hata kumwagika maana na nafasi imekuwa ndogo hasa kwa wanaowakilisha tu,mbio zisiwepo maana hata nafasi yenyewe ni ndogo,kile kilichokatazwa ndiyo kwanza kinaanza.

Ya jana ndiyo yaliyoleta maana ya leo,ya jana ndiyo maana ikaja leo,muda wowote ni wa kulala hasa pale unapochoka,kwani kulala sio usiku kama sio kupumzika,basi hapa tutaoneana,ikiwa tutapangiana hata muda wa kulala,pengine tukafanye shuguli zetu usiku,hii ikiwa sio mabundi bali Yule aliyefanya mchana alichoka na kwenda kulala wakati mwengine Yule akiwa amelala.

Msingi ni mkubwa kuliko kitu,kuonekana kwa juu lazima tutafute kwa chini,tukainue hata yale yaliyopo majini,maana sasa yahitaji kufanya hayo yote ya ndani,tumejiziba sana tuangalie tusijepumulia mipira,tumejiziba sana tuangalie kwa wale walio na hira,kwani yaweza kufunulika na kutokuonekana kitu hiyo ikiwa walishachukua wataalamu.


Tuesday, June 5, 2012

JANA NA LEO.


Jana ikawa siku ya maandalizi na leo ndiyo leo,ndiyo ikawa na maana ya uangalizi pale la muhimu likawa matoleo,ikiwa kwa mara chache yakikaribia usoni huruma kwa mwenzio,ikiwa mara chache yakikaribia rohoni ya nini kwa mkeo,hakuna asiyependa maana maadui wapo,hakuna asiyechukia maana tunaopenda tupo,maisha yameharibu kuta kufanya nyufa na kuonekana leo,maisha yameharibu vitu kufanya watu na mahusiano yao,isiwe hatari ya mwenzako ikawe kinywani baada ya kileo,isiwe adhabu ya mwenzako ikawa samahani kwa leo

Pengine umechelewa kucheka,pengine umewahi kununa,maana ulipaswa kucheka jana na kununa leo,vile ikawa jana na leo,pengine hata mavazi ya jana yasionekane ni yaleo,tutasahauliana jamani tusijefanyiana ya haya ungeyafany a jana,usijeugua magonjwa ukasema yamekuja leo,ukitafuta sababu na kurudi jana na kusema walipasa,walileta wao.

Mengine haina haja ya kumwachia mungu,pengine haina haja ya kumsemea ndugu,ya leo uyaache ya jana kafanya nani uangalie usije vuna mabua ukaja fanana na nyani,ya dunia yameongezeka na hizi pilika kiu zikijaa vinywani.

Ya leo yamekuwa machache kwa imani ya wasio tamani,ya jana yalikuwa mengi kwa imani iliyotamani,maana umetaka uje sasa,maana umetaka ufike leo,kumbe ulitamani yale ya jana yaje leo,kumbe haujatamani kwa ya leo yakafika kesho,hapana haya ya leo kwa kweli yabaki hapa,yaishie hapa na kama yakitaka kuondoka yakaenda basi yarudi jana.

Kesho ije itatukuta vizuri,kesho ije kama ni kuta
umezipamba vizuri,

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...

POPURAL POSTS