Saturday, July 14, 2012

HESABU...


Ni kama pale tunapowapa watoto wetu usaidizi wa kuweza kupata hesabu ali mradi wasikosee,hesabu hizi ni namna inayomfanya mwanafunzi kuona kama anaweza,hiyo ikiwa kama mtihani maana haina haja ya kuhesabu kitu bila lengo maalumu,tutaeleweka wehu kwa kuhesabu tu tena tutakuwa tunahesabu ili iweje?maana katika hesabu kuna kutaka kugawanya,kutoa,kujumlisha,na kuzidisha,na hii yote ikiwa inafanywa kwa hatua kwa hatua kwani kinachomaanisha katika yote ni idadi baada ya kutoa hesabu hizo,labda leo tujiulize sijui tupo wangapi katika nchi yetu,au haina maana ya kuwapo...?

Yaweza isiwe na maana ya kuwapo kwani tutahesabu nini wakati pesa ya matumizi imeshatoka..?la msingi ni kuingia sokoni kwa namna iliyopo na tutakavyo rudi navyo isije kuwa lawama,maana baadaye itaonekana kama watu hawakuhesabu vizuri, ni kwa sababu mwalimu alishatoa majibu yake mapema kumbe naye alikosea,kwani hakupiga mahesabu kwa yaliyopo,maana kama tutakosea kwa yaliyopo haina haja ya kufanya hesabu za mbele.

Wageni karibuni tu nyumbani chakula kipo,tumepewa pesa ya matumizi nyingi na bila ya kujua nani atazitumia,hii ni hatari kwani imeonekana hatukujua mtihani kama utakuwa na mahesabu ya kuzidisha,tutachanganyana sana hapo mbeleni,maana yaweza mzawa kukosa kula ikiwa hata mgeni naye amejiandaa na pesa zake huko alikotoka,tutalala njaa sana  na haina haja ya kulalama kwani tumeipokea vyema .

Hizi ni propaganda,tusiseme watu wamekuwa wazembe kwa kukosa kula na maendeleo finyu, baada ya hesabu washindi wakionekana wengi hapo tutajua nini cha kuwapa.

Thursday, July 12, 2012

NGOJA NGOJA...


Ngoja ngoja huozesha matumbo kwani yameuma mara ngapi?maana si kwa sumu wala vyakula tunavyokula, leo utasikia hatuwezi kula vile mazingira yake mabaya,mwengine akiwaza anapata wapi kula kwa namna ile kutokana na yake matakwa,mwengine akisubiri tumbo kuoza maana hata angali kuozesha na kile kichafu ingalikuwa hafadhari,haki ya  athumani aende nayo maana yakibaki tutachafua hali ya hewa kwa kuwa na uozo usioeleweka ukiwa unangojwa kupelekwa  jalalani.sijui unangoja nini wakati hayafai hata kutamani.

Nimengoja sana kusubiria basi kituoni,sijui ni hii foleni ama ni namna ya askari wetu barabarani,maana ilisikika wakitaka leseni,ya mkwezi mwachieni,maana na kungoja kote huku..!sijui ikiwa imeeleweka hatuwezi kupanda minazi ama ni kwa sababu taa wameamua zisifanye kazi,maana shida kwa tulio wagonjwa wa matumbo,na shida hizi zimejaa sio tupu kwa namna hiyo zifikiriwavyo

Kesho tunapumzika tumechoka sana,maana hata tulichokifanya jana hakina maana,bora kungoja tukijua itapatikana,bora kuonja kwani na mazingira yenyewe haya hayaruhusu kwa basi kutungojea tusijeachana,kipindi hichi cha maana haina haja ya kungojeana bali kila mtu kungojea yake ya  maana,maana cha mtu chake,cha mwengine mavi,hayo ndiyo unaweza mpa mwingine na sio chako,labda muwe mnangojea pamoja..hii ikiwa atakaye pata wa kwanza aweze wa pili ajue kwamba wa kwanza kapata.

Matumbo hayajengwi na kile kilichopo tumboni tu,ukiwa na nia utashiba,wewe ngoja ngoja tu!

Wednesday, July 11, 2012

ELIMU MTAANI..

Elimu ni kuweza kukua katika uelewa,hapo nikitaka wengi ama waliokusudika kufika mahala wanapopapenda,kwa namna iliyo moja hadi nyingine ikiwa ni yoyote,kwa chochote kinachoweza kutokea  kulingana na mazingira yaliyopo ama vile nikayaita hayo yenyewe mazingira ni elimu,elimu mtaani ni ‘experience’ tosha,inatosha kwa kusoma haya yaliyopo mtaani maana ndiyo mwongozo ,kwani Yule anayekosa hukosa wapi?umetaka kufundishwa shuleni ukasahau makosa,umejifunza usiyoyajua na kuacha usiyotakiwa kuyajua,hatutakiwi kutenda makosa

Mtaa kwani wa nani?hivi wengine hatupiti mitaa ile maana kuna wakabaji sana,imeitenga halisi kwa kutaka vya rahisi,leo kabeni na mkiongezeka japo siku ifike arobaini na tano,maana arobaini zinapita sana,siku zinabadilika,yale yaliyomtaani kufahamika kama si ya kihalali,ikiwa watu hawana kwa kula wala kulala mahali,siwezi kuuliza ni lini itakuwa ‘graduation’ ya elimu yetu ya mtaani,kwani kumekuwa na mafanikio,yasiyohitaji cheti.

Leo mitaa imejaa sana.tena hapa haijatofautishwa kwa vile wale ni wazee ama ni vijana,au watoto imetutaka kusoma pamoja maana kinachofanyika ni kile kimoja na haina haja ya kukosea kwa kufanya vile ilivyo tofauti na mkubwa wako,maana tofauti hiyo ni ‘experience’jaribu uone ili kufikisha taarifa katika mitaa,maana sio kuonekana tu hadi kufikirika,utakuwa ni mtu wa hivyo maana ikawa unatofautisha mtu aliye na 'certificate' na Yule asiyenacho,elimu mtaani haina mwisho,elimu mtaa haijali muda wala umri hata mzee wa miaka mia anaweza kuwa darasa la kwanza,ni kwa sababu madarasa hupanda na kushuka,leo kwako na kesho kwangu.


Tuesday, July 10, 2012

ULIMI..


Maneno hayana pa kutokea kama sio mdomoni,ilivyo maandishi kwa kuandikwa,pengine ukiwa unataka haraka kuelewa nini maana ya ulimi kabla ya kuufahamu mdomo,kile kinachotoka katika ulimi kinapita mdomoni pia,maana mdomo umejawa na yaliyo katika ndimi ni yanapita tu,

Ni  maneno ya wasanii,wasanii wachache wanaofundisha wakitaka kueleza,mimi ni mlinzi ya kuwa nalinda. na Yule anayemuongoza mlinzi yeye sijui anafanyaje..naogopa kugeuza ulimi wangu,kwani sijasema nimeshindwa kulinda.Haya hayajalambwa labda uyaone ya pembeni,

Vyovyote iwe ikataje kwa namna iliyozoea,naupenda ulimi wangu kwa uvumilivu
 wake,nikikumbuka mara ya kwanza nikipata pilipili,maana nao ulipokea ukisema haya ni mafunzo,tena elewa..asikudandanye mtu hili limeshindikana,maana ulimi unaweza kuwa umegeuka,hata usijaribu kugeuza ikiwa hautaki kusema tofauti,maana hata mpaka  sasa umedanganywa sana na kuambiwa samahani ni ulimi tu..

Unapofanya meno yako yafurahi ni pale uunapoulaza ulimi wetu,kweli hata mkafurahi wengine na wakapewe shida nyingine,maana ulimi kazi yake kuleta maneno.wacha waseme ,watasema mchana usiku watalala,akianza kumung'unya tu ujue ulimi unaelekea maala pake.
ukikaa kimya inaeleweka umekubali,asikukubalishe mtu asijue ni kwa shida ama ni kwa raha tu.

Maana meno yamefanya kazi sana,hata wakasema wasisikike,tena ukifikiri ni nini kama sio ni wewe mwenyewe umeamua,hapo unataka kusema kama unataka kusema utakatwa ulimi,sijui ili meno yasichoke na vingine tunadanganyana sana,vingine havina maana.


Monday, July 9, 2012

NASHANGAA.!


Nashangaa kuona watu wanashangaa,maana sijui kipi ni kigeni,ama mimi ni nani,wewe je?pengine tusifikiri utamu wa sukari tukasahau wa asali,wengine watasema si yale yale tu lakini ile kuandika nyingineyo yenye maana mbadala bila kujua kama kuna maana tofauti hapo hatutaelewana ,hapa nafsi zitatutoka zana baada ya kuja kushangaa kama kweli ya fulani ndiyo ya kweli,ukisahau anaendelea kuishi kwa nini tusimkataze utapeli wake,maana zaidi utaingia kwa watoto wetu hapo inakuwa ni jasusi na mtutu.hatutashangaa vifo hapo,yamkini uwepo tu.

Karibu nyumba ya pili kuna sherehe,kumbe hapo mgeni kamkaribisha mgeni,hapo mwenyeji kaingiliwa na mgeni,haya mengine ni baadhi ya furaha katika yale machache yanayokuja,pengine tusijekushangaa hata yaliyopita,hapo yatupasa kuyarudia na sijui mageni ni yapi..?zamani ndiyo watu walikuwa wanashangaa mataa kwa sababu walikuja kwa ajili hiyo,siku hizi hata vijijini kuna mataa..kila mtu anatafuta lake,kila mtu anasiri yake moyoni..kila mtu na kitu vipo hivyo kwa sababu hiyo.

Tunakuja kustaajabu haya ya musa sasa,naona tunashangaa jua kuwaka mpaka jioni,maana yawekuwa nastahili la kuzama,kaisari kama unataka nipe ila kama unaitaka chukua,maana lipi limekuwa bora kama sio la kuambiwa?angalia hayo yote ni kwa sababu ya kaisari,mwanangu angalia pengine usisahau kusali.nashangaa kuona nilitaka kuandika mengi na nimeishia hapa,hili geni sasa,hili jipya akilini pengine linatoka ama linaingia,kumbe kwa geni yastahiri..

YAACHE YAENDE..!!


Maana mengine yamekuja kama tishio,mengine yamekuja ili yakionekana yaonekane ya kileo,wanajua wachache wale wanaoitwa walevi,maana kila mtu anajiona yeye mwema,katika kuishi maisha yale mtu akaishi anavyotaka,maana hata ukahamia kaburini nahisi utasikia wachache wakinong’oneza,maana wao si hawajawahi…!!hawajui nini maana ya kuona pale,ama kufika pale,pengine yale ni mengine yaache yaende,pengine yale ni mengine waache watende,

Muda huo unapofika ndiyo unakuwa wakati wangu,maana pengine ndiyo wako sasa,kama vile tunamcheka Yule anayecheza kipindi kifupi bila ya kujua urefu ukoje,mengine ni ya lazima kuelewa pale inapotakiwa kufanikiwa,maana kila mtu na mwenzake wanataka kufanikiwa,wakiwa  na tegemezi na kwenda nayo yale waliyo nayo na kama ni maadui basi kheri waongezeke,hapo wakiwa wawili pamoja na Yule mshamba,maisha sio kuelewa sana sana ya kutaka kuelewa sana,maana hapo tutakuwa tunaelewa tu,labda kukumbuka,na wala haina haja ya kuyakumbukia wacha yaendee..

Kesho tutalia zaidi ilivyo ya leo,maana hichi cha leo tulikijua tu,pengine tumezoea sana ili kutaka kueleweka,akiyafuata  Yule mjinga na mwenzake atamcheka,hapo tutapigana na kukumbuka umoja wetu usioeleweka,kuna Yule amepata kitu na asijue nini kile zaidi ya Yule anayepata kitu na kujua nini hiki,hiki kinatumika,zaidi ya vile ikafikirika maana kwa mwengine anaweza kuwa hafikirii mmoja unapofikiria,pengine sio wengi,pengine sio mengi,haya mengine tuyaache yaende tu!!

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...