Namna tunavyoweza kujitambua katika kufikiri
na vile ilivyo kwa kuona na kusikia.basi nafsi inaweza kuwa roho.Kuweza kujitambua ni kuwa na utambuzi,utambuzi
wenye mtazamo halisia na Yule mwenye nafsi.nafsi huru ndiyo ile inayofikiria
mema juu yake,ikiwa mema ni yale ya mtu mwenyewe hivyo tunafika na kuona namna
nyingi za kuifanya akili yako kuwa
katika mtazamo ulio bora kupitia nafsi.
Usichukulie vitu ki
mimi zaidi, hapa nikiwa nina maana ya
ubinafsi,wengi wetu hatulewi nini ushirikiano lakini ukitegemea kwa kutofanikiwa
kwa yale unayofanya peke yako,sijui ingekuwaje kwa jinsi ungevyomlinda Mungu kama ingelifahamika tu kila mtu amekuja peke yake na wake,yaani haieleweki
alipotokea ni mshtuko na kukutwa yupo akinyonya maziwa yaliyoshushwa
mbinguni,ingelikuwa ni hatari sana kumzidi kuweza kufikiri mmoja wapo asiyenyonya lakini si katika nafsi ya pili
na kuona katika jicho la tatu.
Sahau yako yaliyopita
yale ya zamani.ndwele,ikiwa sio mazuri au
mabaya kinachohitajika hapa ni kuweza kusahauika ,ni mengi zaidi yanayokuja
hasa tukiangalia na yenyewe yanahitaji akili na nafsi zetu hizi hizi ili kuwezakufikirika,binadamu ana aina ya matendo pale inapomkutia nafsi yake,sipendi
kumsingizia mungu lakini kwa mwanadamu lolote lina haki kutokea mbele yake
ikiwa ilipangwa kuishi hivyo inatupasa
kusahau inapobidi na zaidi ni kuweza kufikiri yanayobidi.
.
Kubali yale yasiyo
badilika kubali
kuna yale marahisi,kubali kuna yanayowezekana,ikiwa yamewahi kuwezekana kwako
basi kubali pia kuwa kuna yale yasiowezekana maana ingalikuwa hivyo tungefanya
vyote wote tena bila kujali,magumu mengi huchanganya wanaadamu hivyo kufanya hata
kuchanganyikiwa,hapa haina haja ya kuchanganyikiwa endapo utafahamu kuwa yapo
ambayo hayawezekani katika nafsi yako.
Kuwa mvumilivu…hatuwezi
kusema uvumilivu ndiyo kila kitu kwani hata tukiuvumilia moto mwishowe ni
kuungua tu,hata ukavumilie mazuri kwani mabaya ni yapi?uvumilivu unahitajika
katika watu pamoja na maeneo pia.huku akili timamu ikitangulia kutafuta majibu sahihi pakiwa na uhuru ndani ya yako,uvumilivu ni njia ya ushindi pale
unapotakiwa , unapaswa kuwa wavumilivu ili kuweza kujua hasa ni nini zaidi
ambacho kinapasa kuvumilika.
Kaa mbali na wale
wanaowaza tofauti na vile utakavyo wala hapa tusitengane wala haina haja ya kubaguana,la msingi zaidi ni kuweza
kuwaza ilivyo tofauti na vile wanavyowaza wachache wale wa tofauti,na lengo
liwe ni kutaka kuleta utofauti tu,na badaye kuwa bora katika utofauti huo,
maana
unaweza kuona kuwa Fulani yupo tofauti kumbe naye anaona swala hilo ni lipi na
upande wake kwako pia.
Nafsi yenye vita ina wivu..wanasema wivu
hudhihirika katika mapenzi ya ukweli,hapa upendo umeonekana ni bora zaidi maana unawezaje kuwaonea wivu wale watu unaowapenda?wivu hautakiwi kokote kwani ni
sumu,tunasema sumu ni sumu tu haina idadi ya kua ni nyingi ama ndogo hapo
matokeo ndiyo husema,na wivu usiwe mwingi,hapo utavuna mengi
zaidi.nafsi yako itadhurika
Usiweke na toa
kinyongo nafsini,Weka Nafsi yako huru..moyo unamengi sana
ya kufanyia kazi ,kipindi unaweza kukuta mwanadamu anataka kujiua hiyo
ikiwa ni namna ya mashambulizi aliyokumbwa nayo katika sehemu yake maana uwanja wa nafsi ni mmoja lakini namba tofauti.watu tupo tofauti.hivyo
katika yale ya kuumia zaidi iwe ki hasara ama faida yatupasa kuondokana nafikra
hizo chafu na nzuri katika upande wa mtu husika ili kuwa huru. katika mawazo uliyonayo.
Punguza muda wako
katika kuangalia tv na kusoma magaeti muda ulionao ni kwa kuwezesha mambo kwenda katika mtazamo ulio bora hivyo yapasa kuimarisha ubongo na sehemu
zake nyingine kwa kuweza hasa kusoma na kuangalia matukio na vitu mbali mbali
ambavyo kiharisia vina punguza kasi ya akili katika kufikiria mambo yasiyo
kuhusu na zaidi kujishugulisha na kwa nini sio mimi,hiyo ikiwa ni kama njia moja ya mafanikio binafsi maana akili njema hufuatana nayale inayoyafikiria.
Jishugulishe fanya
mazoezi.vile ilivyo maazoezi sio lazima kunyanyua vitu ambavyo ni vizito labda
lakini unawezakufanya mazoezi marahisi yatakayo weza kukufanya kuwa katika
mtazamo Fulani,
yaani ikawe unafanya mazoezi huku ukifikiri hayo mazoezi
katika kuujenga na kuimarisha miili yetu.
unapoimarisha mwili wako unaimarisha nafsi yako
Jifunze namna ya
kuweza kukaa kimya na kufikiri juu ya maisha yako.muda mwingi huwa tunakaa hasa
tukitafuta maisha lakini nafsi na akili zetu zikiwa baado hazina utulivu,hapa
tunashauriwa kutulia kwa muda na sio bila kuongea lakini pale inapobidi hii
itasaidia katika kujua yale mazuri kwa upande wako na yale mabaya pia.
By Benson G.Makaya