Tuesday, September 11, 2012

AGIZO LA NAFSI

Sitaki kuchekwa ya kuwa imekuwa nileo nkakosa usingizi,sitataka kuwa mwingine maana wa leo ameondoka akidai kurudi,sitaki ya jana maana yanakuwa na maksudi yake,hata ikiwa ivyo vilivyo ntaipigania na nikijua maana ya kutokujua  na maana ya kupatia ama kutokukosea,leo njoo hata na kesho nitakuita,hata akiwa mgeni basi nimwite mwenyeji ili mgeni asitetemeke,karibu sana mgeni na upumzike ya kuwa kesho ni leo yangu hata usingizi ukaupate.

Usipoangalia utakesha kwa kuwa maongezi ni mengi,usipotazama ukasinzia na kutouona  utofauti maana  na manguli ni wengi,ukasikia yaliyo ya ziada,ukaonyeshwa visivyofutika  haifai kuuliza kwanini,basi kile kilichofuta ni lazima kilikuwa na hitaji la lipizi,pengine ni agizo,umetazama kwa kuona yale yanayokaribiana,karibu sana mweusi maana wengine walishatangulia,walioitwa weupe wamejazwa na rangi ili kuchanganya ikaeleweke imerandana.

Karibu mgeni leo nimepika chakula kitamu kwa wale wasio kula pilau,na kesho ikija karibu tena niliyoyasikia jana sipendi kuyasikia na leo.usijezama kuwa tishio na kutikishika visivyo tishika,uzinguzi uje kwa mwanga maana leo imekuwa ni giza sana sijaona kama ya jana ama vilenipo pazuri likiwa fikra ya mmoja wapo pengine.

No comments:

Makaya's Forum: ELEWA 2

Makaya's Forum: ELEWA 2 :   Mateso ya moyo huudhoofisha undani wa mwili,unaweza kubadili mwelekeo hata ule uliotakiwa kuelekea baadaye n...